Wednesday 19 October 2022

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA WABUNIFU MAJENGO NA WAKADILIAJI JENGO

...
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha alipotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Jengo yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Mhe.Atupele Mwakibete akipata maelezo kutoka kwa Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha alipotembelea banda la TBS kwenye Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Jengo yaliyofanyika leo Oktoba 19,2022 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

**********************

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeshiriki katika Maonesho ya Wabunifu Majengo na Wakadiliaji Jengo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika Maonesho hayo leo Oktoba 19,2022 Jijini Dar es Salaam, Afisa udhibiti ubora wa TBS Bw.Tumaini Chimangha amesema TBS limeshiriki kwenye Maonesho hayo ili kuwapatia elimu ya viwango wabunifu Majengo na Wakadiiliaji jengo ili majengo ambayo wanayabuni yawe bora na yenye viwango.

Amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wabunifu majengo kuelewa na kufuata taratibu za viwango vya matumizi ya vifaa vya kupimia majengo ambayo wamekuwa wakiyabuni na kuondoa kasoro ambazo zingeweza kuleta athari kwenye majengo ambayo yatajengwa.

Aidha amesema ushiriki katika maadhimisho hayo ni mkuwa kwani wabunifu mbalimbali wa majengo wameweza kutembelea banda la TBS na kupewa elimu juu ya matumzi sahihi ya viwango.

Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger