Friday 18 September 2020

Vilio Vyatawala Kuagwa Kwa Wanafunzi Waliokufa Kwaajali Ya Moto, Dr.bashiru Awaongoza Waombolezaji

...

Na  Allawi Kaboyo Kyerwa.
Mili ya wanafunzi 10 waliokufa kwa ajali ya moto uliounguza bweni la wavulana katika shule ya msingi Byamungu iliyopo wilayani Kyerwa mkoani Kagera imeagwa leo na kukabidhiwa kwa wanafamilia tayari kwa mazishi.

Zoezi hilo limefanyika leo septemba 18,mwaka huu katika viwanja vya shule hiyo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  Dkt.Bashiru Ally Kakurwa kwaniaba ya Rais Magufuli pamoja na ummati mkubwa wa waombolezaji pamoja wanakyerwa kwaujumla.

Akiongea katika hadhara hiyo Dkt. Bashiru amewapa pole wafiwa na jamii nzima iliyoguswa na msiba huo ambapo amewasihi wafiwa kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo huku akiitaka serikali pamoja na vyombo vya usalama kuendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

Dkt.Bashiru ameitaka serikali na viongozi wa mkoa wa Kagera kusimamia maagizo aliyoyatoa Rais Magufuli alipokuwa Bukoba na kuwataka wamiliki wa shule kuendelea kutoa ushirikiano pale watakapohitajika.

‘’Rais magufuli ameniagiza nije hapa kuwapa pole kwa msiba huu mkubwa lakini ameniagiza pia kuweka msisitizo wa maagizo yake aliyoyatoa ya kuhakikisha mazingira ya watoto wetu wanapokuwa shuleni yanakuwa salama.’’ Amesema Dkt. Bashiru.

Kwaupande wake Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesema kuwa serikali imekuwa bega kwa began na wanakyerwa na hasa wafiwa kwa kuhakikisha marehemu wanahifadhiwa vizuri pamoja na majeruhi wanatibiwa ambapo amesema kuwa tayari zimeundwa kamati za uchunguzi kwenye shule zote za boading mkoani humo kwaajili ya kuangalia miundombinu.

Gaguti ameongeza kuwa kwenye msiba huu serikali imegharamia gharama zote za mazishi ya wanafunzi waliofariki na gharama za kusafirisha mili pamoja na kuwagharamia majeruhi waliopo hospitalini.

‘’Sisi kama serikali tayari tumeshaanza kuchukua hatua, wapo majeruhi 6 ambao wapo hospitalini ambapo watano wapo Bugando Mwanza na mmoja yupo hapa hospitali ya mkoa, majeruhi hao watatibiwa kwa gharama za serikali na kwa familia zilizopoteza wapendwa wao serikali inatoa ubani wa laki mbini na elfu hamsini kwa kila familia.’’ Amesema Gaguti.

Wilbroud Mutabuzi ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (MNEC) awewasihi wanakyerwa na wafiwa kutokutumia nafasi hii ya msiba kuanza kuzushiana na kuleta maneno ambayo kwayo yanaweza kulta uvunjifu wa amani.

Amesema kuwa katika janga hili wazazi na wafiwa hawatakiwi kumnyoshea kidore mmiliki wa shule kwani amekuwa akiishi na watoto wao kwa upendo mkubwa hivyo ajali hiyo imetokea kwa bahati mbaya kama majanga mengine.

Sheikh wa mkoa wa Kagera Alhaj Kharuna Kichwabuta amesema kuwa hali hii wanadamu wanatakiwa kuipokea kwakuwa mpangajiwa kila ajali na tatizo kwa mwanandamu ni Mwenyezi Mungu na hivyo wafiwa wanatakiwa kuwa nasubira ambapo mmiliki wa shule hiyo Abdu Bushagama amemshukuru Rais Magufuli kwa huruma zake kwa kuamuru aachiwe ili kushiriki kuwaombea watotoaliowalea kwa upendo na kuongeza kuwa miongoni mwa waliokufa yumo pia mjukuu wake.

Usiku wa kuamkia septemba 14 mwaka huu ilitokea ajali ya moto katika shule ya msingi Byamungu ambapo bweni la wavulana kwenye shule hiyo liliuungua na kusababisha vifo vya watoto 10 na wengine kujeruhiwa.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger