Monday 21 September 2020

Serikali yaongeza muda wa maombi ya ajira za ualimu

...

Ofisi ya Rais - TAMISEMI imepokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali juu ya changamoto za upatikanaji wa mtandao zilizojitokeza mara baada ya mfumo wa kupokea maombi ya ajira ya walimu kufunguliwa rasmi tarehe 07 Septemba, 2020.

Tunapenda kuwataarifu wadau kuwa kwa sasa changamoto hizo zimetatuliwa na mfumo wa maombi ya ajira ya walimu umeongezewa uwezo na unapatikana kwa urahisi zaidi.


Ili kufidia kipindi ambacho kulikuwa na changamoto ya upatikanaji wa mtandao katika mfumo wa maombi ya ajira ya walimu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI inapenda kuutangazia umma kuwa imeongeza muda wa kupokea maombi ya nafasi za ajira ya walimu wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na mafundi sanifu wa maabara za Shule za Sekondari kutoka
tarehe 21 Septemba, 2020 hadi tarehe 30 Septemba, 2020.

Hivyo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI inawatangazia waombaji wenye sifa kuendelea kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia kiunganishi cha https://ift.tt/3iPsolz (Online Teacher Employment Application System - OTEAS) hadi tarehe 30 Septemba, 2020.

Sifa na vigezo kwa waombaji vitakuwa sawa na tangazo lililotolewa tarehe 07 Septemba, 2020.


Imetolewa na:
KATIBU MKUU
Ofisi ya Rais - TAMISEMI
18 Septemba, 2020



Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger