Friday 18 September 2020

Diva atangaza kuacha kazi rasmi Clouds media

...

Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM, Diva the Boss ametangaza rasmi kuacha kazi katika kituo hicho baada ya kukitumikia kwa miaka 11 mfurulizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diva ameandika; “Mashabiki wangu wa #AalaZaRoho mambo vipi? Mimi mwenyewe kwa akili zangu binafsi maamuzi yangu binafsi nachukua nafasi hii kuwaaga, nitawa-miss sana.

“Tumekuwa wote kwa miaka 11, worth it, natoa shukran zangu kwa uongozi wa Clouds FM kwa kunilea, Im forever thankful, shukrani kwa Joseph Kusaga na familia yake for making My Journey, ntakushukuruni sana.

“Positively nimeamua mwenyewe kuacha kazi Clouds FM leo (jana) mchana huu kwa mdomo wangu mbele ya HR na shahidi wake nilipotamka maneno hayo ya maamuzi ambayo toka natoka nyumbani nilisema nitafanya sababu ya vitu vingi tu ambavyo sitasema.

“Nashukuru sana sana sana, I’v been raised to be honest and speak up no matter what, sababu ya kusimamia ukweli wangu nimeamua fanya maamuzi ambayo nahisi ni sahihi kwangu… By saying That Life has a lot to offer Mungu yu Mwema… tutajuzana zaidi my next destination, love You all 💕,” ameandika Diva.


Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger