Wednesday, 27 March 2019

Picha : AGAPE YAENDESHA WARSHA KWA WASIMAMIZI WA SHERIA KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA SOKONI

...
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola.

Shirika la Agape AIDS Control Program la mkoani Shinyanga limeendesha warsha kwa Wasimamizi wa Sheria ili kutambua haki za binadamu kwa lengo la kuondoa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko ya Manispaa ya Shinyanga. 

Warsha hiyo ya siku mbili imeanza leo Machi 27,2019 katika ukumbi wa Katemi Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja wasimamizi wa sheria wakiwemo polisi,migambo,maafisa masoko,maafisa maendeleo ya jamii,wenyeviti wa kamati za masoko na wafanyabiashara sokoni. 

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola alisema warsha hiyo ni sehemu ya kutekelezaji wa Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaofadhiliwa na shirika la UN WOMEN kupitia Shirika la kitaifa la Equality for Growth (EfG). 

“Agape tunatekeleza huu katika Manispaa ya Shinyanga,katika warsha hii tumekutana na wasimamizi wa sheria na wafanyabiashara kutoka masoko kwenye masoko sita tunakotekeleza mradi ambayo ni Soko Kuu Mjini Shinyanga,Kambarage,Nguzo Nane,Ibinzamata,Ngokolo Mitumbani na Majengo Mapya”,alisema Myola. 

Kwa upande wake,Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo wasimamizi wa sheria ili waende wakasaidie kutokomeza ukatili wa kijinsia unaotokea kwenye masoko yaliyopo katika Manispaa ya Shinyanga. 

“Tafiti mbalimbali zimekuwa zikionesha kushamiri kwa matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana wafanyabiashara sokoni,mfano wanatolewa lugha chafu,wanadhulumiwa,wanabaguliwa katika nyadhifa za uongozi sokoni lakini pia kufanyia mashambulio ya aibu ikiwemo kushikwa shikwa bila idhini yao”,alieleza Isabuda. 

“Baada ya kutoa elimu kwa wasaidizi wa sheria pia tutatoa elimu kwa wasaidizi wa sheria sokoni ambao watakuwa na kazi ya kutoa elimu kwa wafanyabiashara,kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili sokoni na kutoa rufaa kwa wahanga wa ukatili na usuluhishi”,aliongeza.

Kwa upande wao wafanyabiashara sokoni walikiri kufanyiwa vitendo vya kikatili kama vile  kudhulumiwa malipo,kubaguliwa katika uongozi kwenye masoko,kutukanwa na wateja,wasichana kutongozwa kwa lazima na kushikwashikwa ovyo.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola akifungua Warsha ya siku mbili kwa Wasimamizi wa Sheria ili kutambua haki za binadamu kwa lengo la kuondoa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko ya Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde - Malunde1 blog.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola akiwasisitiza wasimamizi wa sheria kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye masoko unatokomezwa.
Wasimamizi wa sheria wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Agape,John Myola.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akielezea lengo la Mradi wa “Mpe Riziki Si Matusi” unaolenga kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wafanyabiashara kwenye masoko.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akizungumz wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Meneja Miradi wa shirika la Agape, Mustapha Isabuda akisisitiza umuhimu wa kushirikiana ili kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye masoko.
Mwanasheria Martha Masalu kutoka ofisi ya Masalu Law Attoneys akitoa mada  ya 'Uelewa wa Jumla wa Kisheria kuhusu haki za wanawake na wasichana'.
Warsha inaendelea.
Mwanasheria Martha Masalu akiendelea kutoa elimu kuhusu sheria mbalimbali.
Mwanasheria wa Agape Felix Ngaiza akifafanua jambo wakati wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Warsha inaendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger