Wafuasi wengi wa dini za kikristo katika bara la Afrika wamezidi kushikilia msimamo mkali wa kuwataka wahubiri na mapadri/kuhani kuzingatia maadili na mafunzo ya biblia ndipo waweze kuwaelekeza kondoo wao kwa njia inayofaa.
Kinyume na matarajio yao, kuna dhana kuwa wengi wa wahubiri hawa wameasi njia hiyo na kuchagua ma maadili watakayofuata na kuacha yale wanahisi hayawafai katika maisha yao ya kila siku.
Mchungaji Jide Macaulay kutoka nchini Uingereza, ambaye amejianika waziwazi kama shoga, amewatangazia wafuasi wake wa mtandao wa Instagram kuwa, hivi karibuni ataapishwa rasmi kama kuhani/Kasisi kwenye ujumbe aliounakili katika ukurasa wake.
Mhubiri huyo mwenye asili ya Nigeria, alifichua kuwa sherehe hiyo itafanyika katika kanisa la Uingereza mwezi wa Juni, 30 2019, huku hata akiwaalika wafuasi wake kuhudhuria hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment