Sunday 30 April 2017

TETESI:WAHITIMU WA SUA ELIMU YAO HATIHATI BAADA YA WALIMU WAO WENGI KUWA NA "VYETI FEKI"

...
 Image result for sua tanzania
Baada ya Rais Kupokea ripoti ya watumishi wa serikali wenye vyeti Feki,Wasiwasi umetokea kwa wanafunzi na wahitimu waliosoma Chuo kikuu Sua kutokana na kufundishwa na walimu ambao majina yao yametajwa kama ni watumishi wenye vyeti feki.


Mfano wa watumishi na walimu wa Sua waliopo ktk list ya watumishi hewa ni Mwalimu ajulikanae kwa jina la KIZITO MWAJOMBE(PHD) ni kati ya watumishi waliopo chuo kikuu SUA ambae amefundisha wanafunzi wengi zaidi kuliko mwalimu yoyote yule kutokana na ukweli kwamba kozi ambayo anaifundisha ni karibia kila mwanafunzi lazima aisome,maana nyingine ni kwamba huwezi kumaliza SUA bila kupita kwenye mikono ya mwalimu huyu ambae amepatikana katika orodha ya watumishi wenye vyeti Feki.

Baadhi ya wahitimu wameanza kuwa na wasiwasi kuwa walichokuwa wakifundishwa na walimu hawa, kuwa yawezekana walikuwa wakipotosha wanafunzi kwa sababu hata wao ameonekana kwamba wamefoji vyeti.

MASWAYETU BLOG tumebisha hodi chuo kikuu SUA na kuongea na mmoja ya watumishi waliopo katika sekta ya utawala na kuhoji swala hili ,je wanafunzi waliofundishwa na walimu hawa ambao wamefutwa kazi na Rais kutokana na kufoji elimu yao,je digrii zao pia ni feki?wametujibu kwamba swala hilo litajadiliwa kiungozi na kutolewa maamuzi sahihi.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger