Monday 10 April 2017

Mbinu Za Kupata Wafadhili Kutoka Nje Ya Nchi, Ili Kuitekeleza Fursa Yako

...

Wiki moja iliyopita niliacha ahadi yangu ya kuwa makala ijayo nitakueleza namna ya kupata wafadhili katika fursa yako. Na nilipokea barua pepe nyingi na ujumbe mfupi wa maandishi kwamba wanasubiri kwa hamu. Basi bila shaka siku uliyoingojea kwa hamu ndiyo hii. Kaa mkao wa kulisha ubongo kisha twende sawa ili niweze kukata kiu yako.

Enzi za utoto ndiko kulikonifanya niweze kujua ukweli juu ya jambo hili. Unajua ni kwanini? Wakati tupo wadogo pale kijini kwetu palikuwa na kanisa ambako watoto wengi tulikuwa tunapenda kwenda zaidi hasa pale walipokuwa wanakuja wazungu. Wengi tulikuwa tunapenda kwenda katika kipindi hicho wakija wageni hao kwa sababu walikuwa wanakuja na vitu vizuri kwa ajili yetu na kuweza kutugawia watoto wote ambao tulikuwepo siku hiyo. Walikuwa wanatugawia vitu kama saa, nguo, baiskeli na vitu vingine vingi ambavyo wakati huo vilikuwa vinatuvutia sana.

Nafikiri kwa kisa hicho kama utakuwa miongoni wa waliokuwa wanapata zawadi hizo nitakuwa nimekukumbusha mbali sana. Lakini kwa kipindi hicho hakuna aliyejali kwamba wale wazungu wamepajuaje kanisani petu pale kijijini zaidi ya kufurahia zawadi zao! na wakati hawajawai kufika hata siku moja katika bara letu hili! Kadri nilivyozidi kukua nikazidi kufanya uchunguzi ambao ulikata kiu yangu, naamini pia utakata kiu yako. Kumbe ukweli ni kwamba kuna njia ambazo huwa zinatumika mpaka kuweza kuwapata wafadhili ambao wapo nje ya nchi na wakaweza kukusaidia katika kutekeleza jambo lako.

Jambo ambalo huzingatiwa zaidi katika kupata wafadhili , wao huangalia mtu ambaye amekwisha kuanza kulitekeleza jambo lake kwa kiwango fulani. Kama nilivyokueleza mfano wa kanisa hapo juu ili wawaze kukufadhili ni lazima uwe umeshalianzisha kanisa hilo. Usiwatafute wafadhili kwa kupiga ‘stori’ tu bila kuwa na kitu maana kuna usemi unasema mwenye nacho huongozewa. Je, unataka kufahamu ni njia zipi za kutumia ili kuwapata wafadhili?
Zifuatazo ndizo njia za kupata wafadhili katika mradi wako;

1. Intaneti/wavuti (website)
Hii ndio njia ya kwanza ambayo kiukweli itakufanya ambayo hata wewe ukiweza kuitumia leo utakwenda kunufaika zaidi. Ikumbukwe ya kwamba kuitumia intaneti vizuri ni pesa mkononi ambayo itakufanya utengeneze pesa zaidi. Namna ya kutumia njia hii ni kwamba, ingia ‘google’ ile sehemu ya kuandika jambo ambalo unalihitaji, kisha andika jambo lako. Kwa mfano unacho kituo cha kulelea watoto yatima na unataka kupata hao wafadhiri.

Unaweza kuandika hivi (Organization supporting orphan children) baada ya hapo, ‘google’ itafunguaka kurasa mbalimbali zenye matokea zaidi hata ya elfu tano. Tuliza akili yako na uanze kufungua moja baada ya nyingine. Ukifungua nenda sehemu ya ‘home ya page’ hiyo kisha tafuta sehemu ya ‘contact page’ , baada ya kuipata sehemu hiyo zichukue namba zao za mawasiliano na uanze kuwasiliana nao watu hao. Huenda pia wakawa hawajaweka namba ya zao za simu au e-mail zao ila kukawa na sehemu ya wewe kujaza taarifa zao zijaze kisha utaona ni jinsi gani mtakavyoweza kuwasiliana nao.

2. Kujitolea na kujipendekeza.
Baada ya kutembelea hizo kurasa zao anza sasa na kujitolea na kujipendekeza kwa kutuma mawazo yako chanya, tuma picha mbalimbali za huku afrika ikiwemo vivutio tulivyonavyo, tuma shughuli unazofanya kama ni kilimo, biashara na vitu vingine baada ya hapo anza kutuma picha za jambo lako ambalo unalitaka ufadhili kama ni kituo cha kulelea watoto yatima tuma majengo yake kama tayari kimeanza kutoa huduma tuma picha mbalimbali.

Kufanya hivi kutawafanya wafadhili hao waweze kupenda kuja kukutembelea na kuona hivyo vitu vya utalii vilivyomo katika nchi yako. Hakikisha ya kwamba huwaombi fedha wafadhili hao mwanzoni tu mwa mawasiliano yenu maana watakuona wewe ni tapeli.

3. Jifunze kwa watu ambao tayari wana wafadhili.
Kwa kuwa kuna watu tayari wamekwisha wapata wafadhili ni muda wako muafaka wa kuwauliza waliwapata vipi wafadhili hao? Kufanya hivyo kutakufanya uweze kuwapa wafadhili katika jambo lako. Pia kama utakuwa hajaweza kuwapata wafadhili wa kutoka ya nje unaweza kujua namna ya kuwapata wafadhili wa ndani ya nchi ambao nao wana mchango mkubwa katika kukufanikisha jambo lako kwa muda sahihi. Kuwa ni mtu wa kutaka kujifunza zaidi kwa kufuatalia mwenyewe kwa ndani kuliko kusikia tu.
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger