Monday 27 March 2017

MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI AWAMU YA KWANZA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO MBALILMBALI KATIKA KOZI ZA CHETI NA DIPLOMA MARCH INTAKE 2017/18

...

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)


TAARIFA KWA UMMA
UTEUZI WA WAOMBAJI WA UDAHILI WA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA)
KWA AWAMU YA MACHI/APRILI, 2017 KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi liliratibu zoezi la udahili kwa waombaji wa kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) kuanzia tarehe 23 Februari, 2017. Zoezi la maombi ya udahili lilifungwa rasmi tarehe 06 Machi 2017 ili kuruhusu uteuzi wa kwa waombaji wa kozi hizo.

Baraza linapenda kuwaarifu waombaji wa kozi za Astashahada na Stashahada; na umma kwa ujumla kuwa, matokeo kwa waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali yametangazwa tangu tarehe 25 Machi 2017 kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) uliotumika kufanya maombi ya udahili. Waombaji wanashauriwa kutembelea kurasa zao (profiles) za kuombea udahili kupitia CAS ili kuona kama wamechaguliwa.

Ili kutembelea ukurasa wako, waweza pia kubofya hapa.


Imetolewa na
Ofisi ya Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
Tarehe: 26 Machi, 2017
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger