Sunday 19 March 2017

JPM Kuzindua Ujenzi wa Barabara za Juu Ubungo

...
Image result for fly over ubungo
Rais John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (interchange), katika makutano ya Ubungo tarehe 20 Machi, 2017.
Rais wa Benki ya Dunia Mheshimiwa Dkt. Jim Yong Kim anatarajiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la ‘interchange’ ya Ubungo.
Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Ubungo utagharimu takribani shilingi bilioni 188.71.
“Una lengo la kupunguza msongamano wa magari katika barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma,” ilisema taarifa hiyo
Mradi huu ni sehemu ya mradi wa uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania.
Chanzo: Mwananchi
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger