HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM

TANGAZO LA NAFASI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA YA
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA KIPINDI
CHA MWAKA 2015 - 2020
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wakazi wa Dar es
Salaam wenye sifa, kutuma maombi ya nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya
Ajira ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kipindi cha Mwaka 2015
- 2020.
SIFA ZA MWOMBAJI:
1. Awe Raia wa Tanzania, Mkazi wa kawaida wa Jiji la Dar es Salaam na mwenye umri usiopungua miaka Arobaini na tano (45).
2. Awe na taaluma katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
- Menejimenti ya Rasilimali Watu (Human Resources Management), Utawala na Uongozi (Public Administration au Sheria (Law).
3. Asiwe Mwajiriwa wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
4. Awe na uzoefu mkubwa katika masuala ya Rasilimali Watu na Utawala.
5. Awe Mwadilifu.
MAELEKEZO
1. Waombaji wote watume barua zao za maombi zikiwa na viambatisho vifuatavyo:-
- Cheti cha kuzaliwa.
- Vivuli vya masomo na Taaluma (Certified).
- Barua ya Utambulisho toka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa ikiwa na picha ndogo ya hivi karibuni.
- Wasifu (CV).
2. Barua toka kwa wadhamini wawili (2) zikiwa na anuani kamili
3. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 30 Septemba, 2016
4. Barua zote za maombi zitumwe kwa anuani ifuatavyo:-
Mkurugenzi wa Jiji,Halmashauri ya Jiji,Ukumbi wa Jiji,1 Barabara ya Morogoro,S.L.P. 9084,11882 – DAR ES SALAAM.

Sipora J. Liana
MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment