Waziri wa Ulinzi na JKT, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema, kuanzia mwaka huo JKT huchukua vijana 5,000 hadi 7,000 kwa madhumuni ya kuwapa stadi za kazi na kuwajengea uzalendo.
Akizungumza katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa na Televisheni ya Shirika la Utangazaji Taifa (TBC1), Dk Mwinyi alisema kuanzia mwaka 2010 vyombo vya ulinzi na usalama viliacha kuajiri kutoka uraiani, bali vijana waliopitia mafunzo hayo ambapo zaidi ya vijana 2,000 wamekuwa wakiajiriwa kwa mwaka.
Alisema pia kwa sasa kuna taasisi nyingi zimeanza kuchukua vijana waliopitia mafunzo hayo kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) na kampuni binafsi za ulinzi.
0 comments:
Post a Comment