Monday 19 April 2021

WAZIRI MKUU AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA FEDHA WA WAKALA WA MABASI YA MWENDO KASI 'DART'


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Fedha wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Suzana Steven Chaula baada ya kutoridhishwa na utendaji wake.

Akizungumzia kuhusu Mtendaji Mkuu wa wakala huo, Mhandisi Ronald Rwakatare, Waziri Mkuu amesema suala hilo atalikabidhi kwa Mamlaka ya uteuzi.

Waziri Mkuu amechukua hatua hiyo leo (Jumatatu, Aprili 19, 2021) wakati alipotembelea kituo cha Kikuu cha DART-Gerezani ambapo alionesha kutoridhishwa na utendaji wa viongozi hao.

“Tangu Mtendaji Mkuu ameingia DART ana miaka mitano hakuna hata basi moja alilonunua, na anasema hana fedha kwani abiria hawasafiri si kila siku wanapigania kule Kimara na wote wanalipa unasemaje hakuna fedha ya kununulia magari”.

Waziri Mkuu amesema kuwa tangu mradi huo ulipoanza mabasi yamekuwa yakipungua kutoka 140 hadi 85. “Watendaji wapo tu wamekaa ofisini wanapigwa na AC (viyoyozi) wananchi wanaumia. Hatuna sababu ya kumbakiza mtu kama hafanyi kazi”.

Amesema wakala huo ulianzishwa na Serikali kwa ajili ya kuondoa adha ya usafiri kwa wananchi lakini viongozi hao wameshindwa kusimamia vizuri na hivyo kusababisha mradi huo kutoendelea vizuri.

Waziri Mkuu amesema mapato mengi ya Serikali yamekuwa yakipotea kutokana na uendeshaji wa wakala huo. “Kwa nini ukatishaji wa tiketi haufanyiki kwa njia ya kielektroniki kwa asilimia 100? Tiketi zinauzwa kwa vifurushi.”

“Haiwezekani watu wanafanya ujanja ujanja tu wakuja na tiketi zao za mfukoni alafu wakimaliza anauza za POS (Mashine ya Kielektroniki ya Kukusanyia Mapato) na wasimamizi wapo tu Mkurugenzi wa Fedha yupo tu ameshindwa kusimamia hili na lipo mikononi mwake”.

“Kwa nini mnauza tiketi kwa vifurushi hamtumii mashine kukata tiketi. Mnaua wakala huu kwa sababu wauzaji wa tiketi wanakuja na tiketi zao na nyingine mnazileta nyinyi. Hamuwezi kusimamia mradi huu wa kimkakati”.

Pia, Waziri Mkuu ametembelea karakana ya UDA ya Kurasini, Dar es Salaam na ameshuhudia baadhi ya mabasi ya wakala huo yakiwa mabovu na alipouliza yanakabiliwa na changamoto gani Mhandisi Rwakatare alisema yanatatizo la mfumo wa gia (Gearbox).

Hata hivyo Mheshimiwa Majaliwa alibaini kuwa magari hayo yanachangamoto nyingine na siyo gearbox pekee kwa sababu baadhi yake yalikuwa yameondolewa baadhi ya vipuri, viti pamoja na matairi.

“…Unanidanganya gearbox ndiyo imeharibika wakati magari chakavu hivi yameharibika kabisa, kama gearbox ndio tatizo mbona kwenye magari mengine mmetoa hadi viti na matairi?

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemuagiza Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Njaule Mdendu ahakikishe mzigo ya wateja katika bandari hiyo inatoka kwa wakati. Ametoa agizo hilo alipotembelea Kituo cha Forodha Bandari Kavu iliyopo Ubungo mkoani Dar es Salaam.

(Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
Share:

KOCHA JOSE MOURINHO AFUKUZWA KAZI



Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepigwa kalamu baada ya kuisimamia timu hiyo kwa miezi 17 pekee.

Raia huyo wa Ureno alichukua mahala pa Mauricio Pochettino kama mkufunzi wa Spurs mwezi Novemba 2019 na kuiongoza klabu hiyo kuwa katika nafasi ya sita katika ligi ya Premia msimu uliopita.

Kwa sasa Spurs wako katika nafasi ya saba, baada ya kuvuna pointi mbili kutoka mechi tatu zilizopita na waliondolewa katika Ligi ya Europa mwezi Machi. Spurs inatarajiwa kukabiliana na Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao siku ya Jumapili.

Msimu huu, Tottenham chini ya usimamizi wa Mourinho imeshapoteza michezo 1. Rekodi ya kupoteza michezo mingi hivyo ni ya mara ya kwanza kwa Mourinho katika kazi yake ya ukufunzi.

Hakuna klabu ya ligi ya Premia iliopoteza pointi nyingi kutoka kwa klabu zinazofanya vizuri msimu huu zaidi ya Spurs ambao wamepoteza pointi 20.


Siku ya Jumapili , Tottenham walikuwa miongoni mwa timu sita za ligi ya Premia kutangaza kwamba walikuwa wanajiunga na ligi mpya ya Ulaya ya Superleague.


Mechi ya mwisho ya Mourinho akiisimamia timu hiyo ilikuwa sare ya 2-2 dhidi ya Everton siku ya Ijumaa.

Chanzo - BBC Swahili
Share:

TIC YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SARUJI CHA TANGA CEMENT JIJINI TANGA

MENEJA wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda wa pili kulia akisisitiza jambo kwa  Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema leo wakati walipotembelea na kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanywa na Kiwanda cha Saruji cha Tanga Cement kilichopo Jijini Tanga kulia ni Nestory Kissima na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha fedha kwenye kiwanda hicho Issac Lupokela

 

Mkuu wa Kitengo cha fedha wa Kiwanda cha  cha Tanga Cement,Isaac Lupokela akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo katikati ni Mhandisi Benedict Lema akifuatiwa na
MENEJA wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda na Nestory Kissima
Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akizungumza jambo wakati wa ziara hiyo

Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo
Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda
Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo kulia ni Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda



TANGA

MENEJA wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Daudi Riganda leo ametembelea na kujionea shughuli za uzalishaji zinazofanywa na Kiwanda cha Saruji cha Tanga Cement kilichopo Jijini Tanga huku akieleza kuridhishwa na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na kampuni hiyo kwa kuchangia kiasi kibwa katika maendeleo ya nchi.

Meneja huyo wa TIC,Daudi Riganda amefanya ziara leo Jumatatu Aprili 19,2021 akiwa ameambatana na Nestory Kissima.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali kwenye kiwanda hicho, Bw. Riganda alisema mwekezaji wa Kampuni ya Tanga Cement ni miongoni mwa wawekezaji mahiri waliosajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania na kupewa hadhi ya wawekezaji mahiri.

Bw. Riganda alisema wamefika kiwandani hapo kuangalia uwekezaji uliofanyika na kuangalia mkataba “Performance Contract” uliosainiwa baina ya Serikali na Wawekezaji hawa ni namna gani ulivyotekelezwa na kila upande. 

 

Katika ziara hii, TIC wamejionea uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 147.65 uliofanywa na kampuni hii, huku ajira zipatazo 330 za moja kwa moja na 677 zisizo za moja kwa moja zikitengenezwa kupitia uwekezaji huu. Kampuni ya Tanga Cement ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza katika kulipa kodi katika Kanda ya Kaskazini. 

Aidha Alisema imeonekana kwamba kuna matokeo makubwa yaliyopatikana upande wa teknolojia ambazo zimeingizwa nchini kupitia mradi huo huku akieleza kufurahishwa zaidi na namna kampuni hiyo ilivyofanikiwa kuajiri idadi ndogo ya wafanyakazi wa kigeni huku idadi kubwa ikiwa ni wafanyakazi wa Kitanzania, wengi wao wakiwa ni vijana wa kitanzania.

“Wapo wafanyakazi wa kigeni hawazidi watano na idadi kubwa walioajiriwa kwenye mradi huu wakiwa  ni vijana wa Kitanzania kwa hakika hili limetufurahisha sana “Alisema

Meneja huyo alisema suala lingine ambalo limewafurahisha ni jinsi suala la mazingira na usalama kazini yalivyozingatiwa tokea unapoingia getini mpaka unapotoka kiwandani.

Hata hivyo, imebainika kuwa Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kupitia mkataba walioingia na wawekezaji hawa hasa katika kipengere cha msamaha wa kodi ya zuio “withholding tax” kwenye mkopo wa kigeni ulioingizwa na kampuni hii kutoka nchini Afrika ya Kusini kwa vile serikali ilipaswa kutoa notisi kwenye Gazeti la Serikali kuruhusu msamaha huo kitu ambacho hadi hii leo hakijafanyika.

Kutokana na dosari hii maafisa wa TRA waliwaandikia kuwataka kulipa kodi yote kama inavyopaswa na pale walipotoa maelezo walijikuta wakifungiwa akaunti zao za benki, kitu kilichowafanya kuanza kulipia kodi hiyo.

Bw. Riganda aliahidi kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha mamlaka za serikali zenye dhamana ya kuhakikisha mikataba inayoingiwa baina ya Serikali na wawekezaji inasimamiwa kama ilivyosainiwa.

Meneja huyo alisema wao kama Kituo cha Uwekezaji watawasilisha malalamiko hayo kwa mamlaka za serikali kupitia Mkurugenzi wao wa kituo cha Uwekezaji ambaye atazungumza na Waziri wa Uwekezaji ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu kuangalia namna gani mikataba hiyo baina ya wawekezaji mahiri na serikali inaheshimika ili kuepusha changamoto ambazo zinaweza kuwapata wawekezaji nchini.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkazi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Benedict Lema alisema huo ni mradi mpya wa laini ya kuzalisha Clinka uliogharamu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 147 na walisaini mkataba huo na TIC.

“ Lakini mpaka sasa haijatangazwa na Gazeti la Serikali na hivyo  kuifanya Serikali kuonekana haijatimiza wajibu wake kulingana na mkataba ulioingiwa na pande hizo mbili, kitu kilichosababisha usumbufu kwa wawekezaji hasa kwenye masuala ya kodi ambazo TRA inawadai”, alisema.

Kampuni ya Tanga Cement ilikuwa na mpango wa kufungua kiwanda kingine cha saruji mkoani Arusha jirani na eneo la uwanja wa ndege wa KIA, mradi ambao ulikadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Kimarekani Milioni 50,hata hivyo wawekezaji hao wamesitisha mpango huo ambao ungetengeneza ajira na mapato zaidi kwa serikali, hadi hapo suala hili la kimkataba “performance contract” litakapopata suluhisho na kodi hiyo kusamehewa kama ilivyobainishwa kwenye mkataba.

Share:

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI JIONI HII


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali leo Aprili 19,2021.
Share:

MPINA AMVAA CAG HASARA ATCL

 

Mbunge wa Kisesa Mhe. Luhaga Mpina

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina ametilia shaka ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa namna ilivyoripoti hasara ya sh. bilioni 60 kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na kusababisha mkanganyiko mkubwa kwa wananchi.

Mpina amesema kwa mujibu wa Taarifa ya CAG inaonesha kuwa Kampuni ya ATCL ilipata hasara ya sh. bilioni 60 mwaka (2019/20), sh. bilioni 23 (2018/19) na kwamba sababu ya hasara hiyo iliyotajwa na CAG ni matumizi yanayohusisha usafirishaji wa abiria na mizigo kuongezeka kwa asilimia 45 kutoka sh. bilioni 133.6 mwaka 2018/2019 hadi kufikia sh. bilioni 193.6 mwaka 2019/2020.

Pia ripoti hiyo ilieleza mapato yaliongezeka kwa asilimia 41 kutoka sh. bilioni 116 hadi sh. bilioni 157.6 lakini cha kushangaza sababu za kuongezeka kwa matumizi hayo hazikuwekwa kwenye ripoti ya CAG licha ya kuwa zinafahamika wazi na kusababisha mkanganyiko mkubwa kwa wananchi.

Mpina amesema sababu hizo ni pamoja na kutokea mlipuko wa Covid-19 katika kipindi cha mwaka 2019/2020 na kuathiri usafiri wa anga ambapo hapa nchini ndege zilikuwa zinafanya kazi kwa asilimia 20 tu.

Kampuni ya Air Tanzania iko kwenye mageuzi makubwa ambapo katika mwaka 2019/2020 ndege mpya 2 aina ya Boeing na Bomberdear zilinunuliwa na ndege zingine zilinunuliwa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2018/2019 na hivyo kupelekea gharama za uendeshaji na utunzaji kuongezeka.

Pia ndege zinazotumiwa na Shirika la  Air Tanzania zimekodiwa kwa Wakala wa Ndege za Serikali na hivyo Kampuni inalazimika kulipa gharama ya ukodishaji kwa wakala huyo.

Kutokana na kuongezeka kwa ndege Shirika limelazimika kuajiri marubani na watumishi wengine ili kukidhi mahitaji ya utoaji huduma .

Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 Shirika liliongeza kituo kipya cha nchini cha Mpanda na kufungua kituo nje ya nchi cha Mumbai India, Pia shirika liliongeza miruko katika  vituo vya Dodoma, Mwanza na Kilimanjaro.

Pia Kampuni ya ATCL ina deni la miaka ya nyuma la sh. bilioni 217 ambapo inalazimika kulipa riba kila mwaka  na mwaka huu wa 2019/20 shirika limelipa riba ya deni sh. bilioni 12.5 ikilinganishwa na malipo ya riba ya sh. bilioni 8 ya mwaka 2018/2019.
Kampuni ya ATCL imeanza mageuzi ya uwekezaji miaka miwili tu iliyopita na hivyo sio rahisi kupata faida leo.

Pia amewatoa wasiwasi wananchi kuwa Kampuni yetu ya ATCL inazidi kuimarika na kuwataka wanaobeza kwa namna moja au nyingine waache na badala yake wapende vitu na mafanikio ya nchi yao.

Mpina amebainisha ushahidi wa kampuni yetu kuimarika na mafanikio yaliyopatikana kwani kabla ya hatua hizi kuchukuliwa na Serikali ya awamu ya tano  shirika lilikuwa halina uwezo wa kulipa watumishi wake mishahara hivyo Serikali ililazimika kulipa mishahara yote kwa 100% lakini tunapozungumza leo Shirika letu linajitegemea kulipa mishahara ya watumishi wake kwa 87%.

Katika kipindi cha ukaguzi shirika lilikuwa na ukwasi wa bilioni 17.5 huu ni ushahidi kuwa kampuni yetu inaendelea vizuri
Kampuni imeajiri marubani waliofikia 80 na wote ni wazawa wakiwemo marubani wanawake ambao wote tunawaona wakirusha ndege zetu kwa umahiri mkubwa.

Pia kwa kufanya ulinganifu na makampuni mengine ya kigeni  mfano Kenya Airways (KQ) ambapo Kampuni ya KQ toka mwaka 1977 inaendelea kupata hasara kila mwaka lakini Serikali yake inaendelea kuwapa fedha za kuendesha shirika hilo kwa kutambua kuwa faida za usafiri wa anga ni mtambuka.

Kuongezaka kwa idadi ya watalii nchini ni ushahidi mwingine wa mafanikio ya shirika letu ambapo watalii wameongezeka kutoka milioni 1.1 (2015) hadi milioni 1.5 (2019) na mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.9 (2015) hadi Dola za Marekani bilioni 2.6 (2019).

Huduma za biashara na uwekezaji nchini zimekuwa na ufanisi mkubwa najua watanzania hawajasahau abiria, bidhaa na mizigo yote kutoka nchini kwetu ilitegemea ndege za nje mfano. Mbogamboga, Maua, Samaki, Mabondo, Nyama kwenda masoko ya nje najua hatujasahau na hatutasahau.

Faida nyingine ni kuwahisha wagonjwa kupata matibabu ndani na nje ya nchi kwa gharama ndogo baada ya kununua ndege zetu mfano zamani mgonjwa alitakiwa kupelekwa India lazima apitie kwanza Dubai kuunganisha ndege za India kwa gharama kubwa na kutumia muda mrefu lakini baada ya kununua ndege zetu na kuanzisha ruti ya India gharama ya usafiri imepungua kwa asilimia 40 na muda umepungua kwa kiwango kikubwa na hivyo kuwahi kwenye huduma.

Kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Shirika la ndege Tanzania ni Mpina ameshauri watanzania wenzetu wanaobeza Kampuni yetu ya ATCL waache mara moja.

Pia Serikali ilipe deni la nyuma la ATCL la sh bilioni 217, Serikali iendelee kuwekeza kwa kuongeza idadi ya ndege za abiria na mizigo, kupanua na kujenga viwanja vipya vya ndege, kuongeza safari, marubani na kukarabati miundombinu muhimu mingine muhimu hii ni pamoja na  ujenzi wa uwanja mpya wa ndege Mkoa wa Simiyu.
Share:

WAKAMATWA WAKIIBA SIMU MECHI KATI YA SIMBA SC NA MWADUI FC IKIENDELEA...RPC ATAKA WALIOIBIWA WAKAZICHUKUE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawashilikilia wanaume watatu kwa tuhuma za wizi wa simu za mkononi wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Mwadui Fc na Simba Sc ikiendelea katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema wamewakamata watuhumiwa hao jana Jumapili Aprili 18, 2021 majira ya saa kumi jioni huko katika uwanja wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga.

Kamanda Magiligimba amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Amos Shija (38) na Gerald Abdallah (18) wakazi wa Majengo pamoja na Rashid Hamis (25), mkazi wa Tabora ambao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Akielezea kuhusu tukio hilo, Kamanda Magiligimba amesema askari wakiwa katika majukumu ya kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati wa Mechi ya Ligi Kuu kati ya Mwadui Fc na Simba Sc ikiendelea waliwakamata watuhumiwa hao wakiwa wameiba simu tano.

“Tuliwakamata watuhumiwa wakiwa na simu tano ambazo ni Iphone 5 aina ya s7+ rangi nyeusi, Infinix hot 08, Sony xperia, Itel ndogo na Tecno rangi ya silver”, amesema Kamanda Magiligimba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga anaomba wananchi walioibiwa simu zao siku ya tarehe 18/4/2021 ndani ya uwanja wa CCM Kambarage kufika kituo kikubwa cha polisi Shinyanga ili kubaini simu zao.

Katika mechi hiyo, bao pekee la Nahodha John Raphael Bocco liliipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Bocco alifunga bao hilo dakika ya 66 kwa kichwa akimalizia mpira uliounganishwa kwa kichwa pia na beki Mkenya, Joash Onyango kufuatia kona ya winga Mghana, Bernard Morrison kutoka upande wa kulia.

Ushindi huo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 52 baada ya kucheza mechi 22 na kurejea nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi mbili na Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.
Share:

WANAUME WAWILI WAANGUKA NA KUZIMIA BAADA YA KUIBA NGURUWE WA BIBI

Kumetokea tukio la aina aina yake huko Shinyalu, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya baada ya wanaume wawili wanaodaiwa kuiba nguruwe wa ajuza mmoja kuanguka na kupoteza fahamu. 

Afisa Mkuu msaidizi wa polisi eneo la Shisembe Mike Shivanda amethibitisha kisa hicho kulingana na ripoti ya OB iliyowasilishwa katika Kituo cha Polisi cha Shinyalu kwamba nguruwe hao waliibiwa Aprili 17,2021 majira ya saa nne asubuhi.

"Iliripotiwa na Mike Shivanda, chifu msaidizi, eneo dogo la Shisembe, kwamba wanaume wawili walianguka na kupoteza fahamu ndani ya kijiji cha Munyolo katika eneo la Murhanda takriban kilomita sita kaskazini mwa kituo hicho. 

"Maafisa walitembelea eneo la tukio na kupata wanaume wawili, ambao ni; Nicholas Abung'ana, mwanaume wa Luhya mwenye umri wa miaka 50, na Alexander Savala, wa kiume wa Luhya mwenye umri wa miaka 50 wakiwa wamelala katika nyumba zao, hawawezi kuongea au kuamka," ripoti ilisema.

Mwanamke mzee ambaye nguruwe wake waliibwa alitambuliwa kwa jina Doris Achitsa, 65, ambaye anadaiwa kuwa mwajiri wa Abung'ana.

 Achitsa ni binamuye Savala, ambaye ni mmoja wa washukiwa ambaye alipatikana amepoteza fahamu. 

Kulingana na ripoti ya polisi kwenye kitabu cha matukio (OB), mwanamke huyo ambaye alionekana mwenye masikitiko makubwa alitafuta huduma za mganga mmoja Kaunti ya Bungoma ambaye alimtembelea nyumbani kwake majira ya saa 12 jioni na kufanya ibada zake kabla ya kuondoka ambapo ilipotimia saa 1 usiku, wanaume hao wawili walianguka na kupoteza fahamu.

 Mfuasi huyo alikuwa ameacha maagizo kwamba mtu yeyote atakayeathiriwa asichukuliwe hospitalini bali aachwe katika hali yoyote aliyokuwa nayo hadi asubuhi atakaporudi. 

Ndugu zao walisisitiza kwamba maagizo ya mfuasi wa ibada yazingatiwe. 

Ripoti ya maendeleo ya kesi ya PUI ifuatwe," iliongeza.

SOMA ZAIDI <<HAPA>>




Share:

NIMEACHANA NA WAKE WAWILI KISA SIJIWEZI KITANDANI MWANAUME…..NIMETUMIA NJIA HII KUONDOA AIBU

Mimi ni mwanaume ambaye naheshimu na kujaldi mwanamke yoyote katika dunia hii.Naheshimu sana jinsi ya kike kwa sababu Baba yangu mzazi alimuacha mama yangu nikiwa bado mdogo kabisa. Mama yangu alijitahidi kadri awezavyo kuhakikisha napata chakula,mavazi na elimu bora na leo hii nina nafasi kubwa katika serikali yetu. Asante sana mama.

Mwaka 2015 mwenyezi Mungu alinijalia nikapata mke wa kwanza. Kulingana na malezi ambayo nilipata kwa mama yangu mzazi hivyo nilimuheshimu, kumpenda na kumjali mke wangu.

Nilifanya kila kitu niwezacho kumfurahisha mke wangu ila hayo yote mke wangu kipenzi mwaka 2016 aliniacha bila sababu yoyote.

 Kulingana na kazi yangu niliyokuwa nayo sikuweza chelewa kupata mwanamke mwingine, ilipofika 25/10/2016 nilipata mwanamke mwingine kutoka mkoa wa Mara.

Pia nilimpenda mke wangu wa pili kadri niwezavyo hadi ilifikia hatua mke wangu ananikosea nashindwa kusema kisa naogopa aibu endapo akiondoka kama mke wangu wa kwanza.

Maisha yaliendelea pole pole ila baada ya miezi sita mke wangu akaanza tabia ya kutoka nje ya ndoa.

Nilimkalisha chini na kumuuliza kitu gani amekosa kwangu hadi anaanza kutembea na wanaume nje na kunivunjia heshima ndipo kwa kinywa chake akasema kuwa kitandani sijiwezi hivyo mwili wake kuna kitu unakosa ndiyo maana yeye analala na wanaume wengine nje. 

Moyo wangu uliumia sana ila sikuweza kataa kwa sababu kuna muda hata mimi nilikuwa nahitaji kumridhisha mke wangu ila uwezo wa mashine yangu kukaa uwanjani nilikuwa siwezi kabisa. Nilikuwa najikuta kwa wiki naweza kuwa uwanjani mara mbili na kutoka na bao mbili tu.

Zaidi nilimuomba mke wangu anivumilie,lakini mke wangu kipenzi alifikia hatua ya kuondoka japo Mungu alinisaidia niliweza kupata mtoto mmoja kutoka kwake. 

Kwa kuwa nilikuwa nimeshapata mtoto kutoka kwa mke wangu wa pili hivyo sikuweza kuwa na mawazo ya kutafuta mwanamke mwingine zaidi ya kumhudumia mtoto wangu.

Maisha yangu yalienderea vizuri ila kila siku moyo wangu ulikuwa unaniuma sana haswa nilipokuwa naalikwa katika sherehe tofauti na kadi yangu inakuja imeandikwa kuwa naitajika pale nikiwa na mwenza wangu.

Mwanzo nilichukulia kawaida, nilikuwa nachukua hata binti mmoja tunaenda wote ila kwa upande wangu nilikuwa naumia sana japo mabinti ambao nikienda nao walikuwa wanafurahi na kunishukur.

 Kulingana na heshima niliyokuwa nayo katika jamii na kazini kwangu pia kitendo cha kutokuwa na mwanamke ni jambo ambalo lilikuwa la kushangaza.

Siku moja nikiwa nimetoka ofisini na rafiki yangu ambaye sitataja jina lake kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ilibidi nimueleze kisa kinachosababisha wanawake kuniacha.

Ndipo rafiki yangu akaniambia kuwa kuna Dokta ambaye anamfahamu anaweza kunisaidia ila yupo nchi jirani ya Kenya.

Niliomba mawasiliano ya Dr. Kiwanga akanipa namba ya simu : +254 769404965 Email : kiwangadoctors@gmail.com Website : www.kiwangadoctors.com.

Kwa haraka sana niliongea na Dr. Kiwanga kisha nikamuomba kuwa nahitaji kufika ofisini kwake. Dokta alinipatia siku maalumu ambayo naweza kuonana naye.

Nilifika ofisini kwake kisha nikapewa dawa na kurudi kwetu Tanzania.Nilitumia ile dawa kwa siku kumi na nne tu. Ndani ya hizo siku mashine yangu kila mara ilikuwa inaitaji kuwa uwanjani kwa ajili ya mpira. 

Sikuweza kuchelewa zaidi ya kupata mwenza wangu. Siku ya kwanza kuingia uwanjani kweli hata mimi nilikubali maana tangu nizaliwe nilikuwa sijawai kuwa uwanjani kwa dakika 90 na zaidi kuweza kucheza mechi 4 just single night.

Kiwangadoctors walinieleza kuwa wanashughulika na mambo tofauti hasa yanayotokea katika jamii zetu kila siku kama kurudisha mpenzi aliyekuacha,kupata mpenzi wa ndoto zako,kusafisha nyota yako na kurejesha furaha,upendo na amani katika familia. 

Niliweza pata ata matibabu ya ugonjwa wa sukari na pressure na leo hii sina hilo tena.Wasiliana na Kiwangadoctors kwa namba +254 769404965 kwa maelezo zaidi au tembelea website yao www.kiwangadoctors.com utafahamu mengi kuhusu Kiwanga Doctors



Share:

RAIS SAMIA AMUAPISHA YUSUPH TINDI MNDOLWA KUWA BALOZI


Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Yusuph Tindi Mndolwa akila Kiapo cha Uadilifu pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao eGA Bw. Benedict Benny Ndomba mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 18 Aprili 2021.
Yusuf Tindi Mndolwa akila Kiapo cha kuwa Balozi katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 18 Aprili 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocol) katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Yusuph Tindi Mndolwa kuwa Balozi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma leo tarehe 18 Aprili 2021.
PICHA NA IKULU
Share:

JAJI MSTAAFU DKT. BWANA AKERWA NA BAADHI YA WAAJIRI NA MAMLAKA ZA NIDHAMU KUTOFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU

Share:

MASHUA YA KWANZA DUNIANI KUTENGENEZWA KWA TAKA ZA PLASTIKI FLIPFLOPI ILIVYOTUA DAR

Mnamo mwaka 2016, Ali A. Skanda kutoka Lamu nchini Kenya, pamoja na wenzake wawili kwa waliungana na kutengeneza mashua waliyoiita Flipflopi kwa kutumia taka taka za plastiki zilizokuwa takribani tani kumi (10) na kuifunika kwa ndala elfu thelasini (30,000), ambapo mpaka kukamilika kwake 2018, mashua hiyo ilikuwa na uzito wa tani 8, na ndicho chombo cha kwanza cha majini duniani kutengenezwa kwa takataka za plastiki.

Tarehe 15.04.2021 mashua hiyo ilitua Dar es Salaam ikiwa imebeba ujumbe wa kuhimiza usafi wa mazingira ya Fukwe za Bahari, Maziwa pamoja na mito kwa kwa ajili ya usalama wa viumbe wanaoishi humo na afya kwa wanadamu.

Jumamosi tarehe 17.04.2021 ujumbe huo wa Flipflopi pamoja na wenyeji wao wa Nipe Fagio waliungana kufanya usafi katika ufukwe wa Minazi Mikinda Kigamboni, na kuweza kukusanya zaidi ya mifuko 90 ya takataka.

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Nipe Fagio kutoka Tanzania kwa kushirikiana na projecti ya Flipflopi pamoja na wakazi mbalimbali wa Dar es Salaam wakiwa katika usafi wa kusafisha ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni wakati ujumbe wa projecti ya FlipFlopi ulipotua Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa Mazingira ya Bahari hasa kupambana na taka za plastiki pamoja na taka taka zengine ambazo ni hatari kwa viumbe hai wa Baharini.
Mashua na Boti ya FlipFlopi zikiwa katika Bahari ya Hindi eneo la Kigamboni Dar es Salaam

Muonekano wa Dampo ambalo sio rasmi, linalosabisha uchafuzi mkubwa wa ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni ambapo walioshiriki wa kufanya usafi walifanikiwa kupunguza taka hizo kwa kiasi kikubwa.
Zoezi la uchambuzi wa taka likiendelea baada ya kuokotwa kutoka ufukweni mwa Bahari, zoezi hilo hufanyika ili kuweza kufahamu idadi ya taka zilizopatikana na kufahamu makampuni ambayo yanazalisha bizaa hizo zinazopelekea uchafuzi wa mazingira ya Bahari, katika zoezi la usafi Zaidi ya viroba 80 vya taka vilikusanywa, taka zilizokusanywa ni Pamoja na plastiki, nepi za Watoto, vifaa vya umeme, nguo, viatu, ndala, nyavu za Samaki, vifungashio vya vyakula na aina zingine mbalimbali.
Muonekano wa Ufukwe wa Bahari eneo la Minazi Mikinde Kigamboni kabla na baada ya kufanyiwa usafi.
Maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazotokana na urejelezaji wa Taka rejeshi

Picha na Fredy Njeje - Mpiga picha wa picha za Mazingira

Share:

MREMBO AUAWA BAADA YA KUMTOSA SPONSA WAKE....JAMAA AKIRI KUUA HASIRA YA KUACHWA

Catherine Nyokabi enzi za uhai wake
Catherine Nyokabi akiwa na mpenzi wake
Gari ambamo mwili wa Catherine Nyokabi ulikutwa 

Ukizitazama picha maridadi za mrembo mwenye miaka 25, Catherine Nyokabi ambaye ameuawa kinyama na mpenzi wake, utatambua kwamba alikuwa mja mchangamfu.

Alikuwa mwanamke mchanga ambaye ndoto zake zilikatizwa ghafla na mpenzi wake baada ya mapenzi kugeuka shubiri.

 Mama huyo wa mtoto mmoja, amepatikana ameuawa ndani ya gari eneo la Witethie, Kiambu nchini Kenya na mwili wake kukatwa vipande Jumatano, Aprili 14,2021.

Mpenzi wake Evans Karani ambaye ni mwanaume mwenye familia amekiri kumuua kwa sababu alikasirika kwamba marehemu alitaka kumuacha.

Marehemu alikuwa mama wa mtoto mmoja na kulingana na swahiba wake Ann Wanja, uhusiano huo ulikuwa umeanza kuyumba na wakati wa mauti yake, wawili hao walikuwa wamekutana kutatua tofauti zao. 

Wanja alisema Nyokabi alikuwa amempenda sana Karani na kujitolea vilivyo.

 Familia ya Nyokabi ilikuwa inafahamu uhusiano wake na mume wa mtu kwani Karani alikuwa amewajuza mipango yake ya kumuoa kama mke wa pili.

“Nilikuwa nawafahamu kama wapenzi kama tu uhusiano mwingine, walikuwa na tofauti zao ambapo niliwasaidia kutanzua," alisema baba yake mrembo huyo Gitonga Njogu.

Makachero wa DCI wamemtia mbaroni jamaa mwenye umri wa miaka 38 kuhusiana na kifo cha mpenziwe, 25.

Kulingana na ripoti ya DCI, Evans Karani anazuiliwa kuhusiana na kifo cha aliyekuwa mpenziwe Catherine Nyokabi.

 Mwili wa Nyokabi ulipatikana kwenye gari lake katika barabra moja eneo la Juja ukiwa umekatakatwa na kuchomwa kwa tindi kali. 

Polisi wanashuku Karani alikuwa kwenye safari ya kuenda kuutupa mwili huo kichakani wakati gari lake lilikwama kwenye matope lakini mpango wake ulitibuka wakati gari lake lilikwama na kumfanya kukimbia.

Mvua ilikuwa imenyesha na kufanya barabara ya Bob Harris Juja kuwa mbaya na hivyo gari hilo likaingia matopeni.

 Tayari Karani anaripotiwa kukiri kwa maafisa wa polisi kuwa alitekeleza mauaji hayo baada ya tofauti za kimapenzi. 

Babaake Nyokabi aliambia gazeti la Standard kuwa alimjua Karani kama mpenzi wa mwanawe na walikuwa na mzozo wa kimapenzi.

"Niliwajua kama wapenzi. Na kama vile mahusiano mengine ya kimapenzi walikuwa na mizozo hapa na pale. Wiki mbili zilizopita, msichana wangu alianiambia walikuwa wametofautiana.

 "Aliniambia walikuwa wameachana na nikamwambia ni sawa kwani hakuna haja ya kuwa kwenye uhusiano ambapo kuna masaibu," alisema mzee huyo.

 Mshukiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji Jumatatu Aprili 19,2021.

Kulingana na taarifa kutoka kwa majirani, Nyokabi aliondoka nyumbani na kusema ameenda kukutana na mpenziwe.

 Nyokabi amemwacha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita huku familia yake ikiomba haki itendeke katika suala hilo.

CHANZO - TUKO NEWS

Share:

ULOMI FC WAIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, WAPEWA ZAWADI YA MBUZI


Mwakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Aaron Nyanda akikabidhi Mbuzi kwa Kiongozi wa Timu ya Ulomi FC Francis Richard, baada kuibuka washindi wa mashindano ya Kombe la Kichangani Bodaboda Football kupinga ukatili wa kijinsia kwa kuifunga timu ya Kontena FC bao 1-0 ,mashindao hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Kunguru-Goba mkoani Dar es Salaam.Pichani wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gender Action Tanzania (GATA), Neema Makando na kushoto ni Frank Mwanga-Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Mbezi Kati
Timu ya Ulomi FC ikifurahia kwa pamoja na zawadi yao ya Mbuzi waliokabidhiwa kwenye mashindano ya Kombe la Kichangani Bodaboda Football kupinga ukatili wa kijinsia baada ya kuifunga timu ya Kontena FC bao 1-0 .
Mwakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Aaron Nyanda akikabidhi zawadi ya Vizibao vyenye kuakisi mwanga (Reflekta) kwa Kiongozi wa Timu ya Ulomi FC Francis Richard, baada kuibuka washindi wa mashindano ya Kombe la Kichangani Bodaboda Football kupinga ukatili wa kijinsia kwa kuifunga timu ya Kontena FC bao 1-0 ,mashindao hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Kunguru-Goba mkoani Dar es Salaam.Pichani kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gender Action Tanzania (GATA), Neema Makando.
Mwakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Aaron Nyanda akikabidhi zawadi ya Vizibao vyenye kuakisi mwanga (Reflekta) kwa Kiongozi wa Timu ya Kontena FC, baada kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya Kombe la Kichangani Bodaboda Football kupinga ukatili wa kijinsia,mashindao hayo yamefanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Kunguru-Goba mkoani Dar es Salaam.Pichani wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gender Action Tanzania (GATA), Neema Makando.
Picha ya pamoja na Waandaaji wa mashindano hayo,kulia ni Bi Julieth Nzugika-Afisa Maendeleo Jamii Mbezi Juu,kabla ya mechi kuanza
Baadhi ya Mashabiki ambao ni Madereva wa Bodaboda wakifuatilia mchezo huo kwa utulivu
Golikipa akiokoa mpira wa hatari kutoka kwa mchezaji wa timu ya Ulomi FC
Gooooo....! Timu Ulomi FC ilipojipatia goli la kwanza dhidi ya timu ya Kontena FC
Mpambano ulikuwa mkali,kila timu ilionesha uwezo wake uwanjani
Afisa Maendeleo Jamii Mbezi Juu Bi Julieth Nzugika akizungumza jambo kwa wachezaji mara baada ya mechi kuisha.

***

TIMU ya Ulomi FC wameibuka washindi wa mashindano ya Kombe la Kichangani Bodaboda Football kupinga ukatili wa kijinsia baada ya kuifunga timu ya Kontena Bodaboda FC bao 1-0 na hivyo kuchukua zawadi ya mbuzi.

Mashindano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Kunguru uliopo Goba jijini Dar es Salaam na timu zilizoshiriki ni Wagwani FC ,Ndambi Bodaboda FC,Kontena Bodaboda FC na Ulomi Bodaboda FC.

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya Mbuzi kwa bingwa wa mashindano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Gender Action Tanzania (GATA) ambao ndio waandaji wa mashindano hayo kwa timu za waendesha bodaboda, Neema Makando amesema lengo ni kuendelea kuhamasisha jamii kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii na kupitia mashindano hayo yatasaidia kufikisha ujumbe kwa jamii.

Amesema kwamba kikubwa ambacho GATA wanahimiza ni jamii kuacha masuala yanayohusu ukatili wa kijinsia ambapo ameweka wazi michezo imekuwa sehemu mojawapo ya kuunganisha watu na kuleta upendo."Katika michezo hakuna magomvi na sote tunatambua magomvi ni chanzo cha ukatili wa kijinsia na sisi hatutaki kuona ukatili wa kijinsia unaendelea kutokea."

Makando amesema kwamba mashindano hayo ni mwanzo wa kuelekea katika ratiba ya Marathon ya kupinga ukatilii ambayo itafanyika Mei 9 mwaka huu huku akisisitiza mkakati uliopo baadae ni kuwa na timu nyingi za mpira wa miguu ambazo zitashiriki pamoja na michezo mingine,lengo kuendelea kutoa elimu kwa jamii kutambua umuhimu wa kukomesha matukio ya ukatili wa kijinsia katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) Aron Nyanda aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo amewapongeza GATA kwa kuandaa mashindano hayo kwa waendesha bodaboda kwani ni kundi kubwa na muhimu katika jamii ambalo likishirikishwa kwenye mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia ni rahisi kufanikiwa.

Amesema kwamba jamii ya waendesha bodaboda kwake anaiona kama taasisi rasmi na imekuwa ikitoa mchango mkubwa katika jamii hasa ya kusafirisha watu pamoja na bidhaa na hivyo wamekuwa wakipita sehemu mbalimbali na iwapo wataona tukio la ukatili wa kijinsia ni rahisi kutoa taarifa kwa viongozi wa Serikali ya mtaa.

"Unaweza kupita sehemu ukakuta mtoto anapigwa isivyokawaida, hivyo sio lazima uchukue hatua hapo hapo lakini unaweza kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa ambaye atafuatilia kujua kuna nini,"amesema Nyanda.

Katika mashindano hayo washindi wa pili ambao ni Ulomi Bodaboda FC wao wamepewa zawadi ya Vizibao vyenye kuakisi mwanga (Reflekta) ambapo Nyanda ambaye amewahi kuwa mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam amesema kwenye.michezo amani na upendo hutawala na anaamini hata Mbuzi huyo supu yake itanywewa na timu zote.

Aidha amesema TFF inajisikia faraja wanapoona wadau mbalimbali wanajitokeza kuandaa mashindano ya mpira wa miguu ambapo ametumia nafasi hiyo kuzungumzia nidhamu katika michezo ni lakini akaendelea kusisitiza umuhimu wa kupinga ukatili wa kijinsia kama lengo la mashindano hayo yanavyohamasisha.
Share:

RAIS SAMIA AKERWA MJADALA WA WABUNGE KUMLINGANISHA NA MAGUFULI


Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na mijadala inayoendelea bungeni ya kumlinganisha na mtangulizi wake, hayati John Magufuli.

Mjadala wenyewe ambao umeonekana kumkera Rais Samia Suluhu Hassan wa ni miongoni mwa wabunge wa chama kinachoongoza dola, CCM. Wabunge ambao wamegawanyika katika makundi mawili, wanaotetea rekodi ya rais aliyepita John Magufuli na ambao wanaoonekana kukosoa baadhi ya mambo ya utawala huo.

Akizungumza Jumapili Aprili 18, 2021 katika kongamano la viongozi wa dini, Samia amesema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na anaendeleza kazi iliyofanywa na mtangukizi wake huyo aliyefariki dunia Machi 17, 2021 kwa ugonjwa wa moyo.

''Inasikitisha sana kuona kwamba watu wanapiga ngoma mitandaoni, lakini ngoma ile inachezwa bungeni, kwa kulinganisha watu na sio kulinganisha ajenda za kitaifa, ajenda ya kitaifa ni moja, mnalinganisha Magufuli na Samia hawa watu ni kitu kimoja''.

''Awamu ya sita haikutokana na uchaguzi, haikutokana na chama kingine cha siasa, imetoka ndani ya chama cha Mapinduzi, imetokana na uongozi uliokuwepo wa awamu ya tano.'' Alisema Rais Samia.


''Awamu ni maneno tu , lakini mambo ni yaleyale.

Share:

SERIKALI YAANZISHA KITUO CHA KIMATAIFA CHA KUENDELEZA VIPAJI VYA MICHEZO.



Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo Omari (kushoto), akiwa naa liyewahi kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF na Kocha wa Timu ya Taifa Stars, Ami Ninje (katikati) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Dkt. Richard Masika wakikagua eneo la chuo kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa chuo hicho ili kujenga Kituo cha kuendeleza vipaji vya michezo.

Timu ya wataalam mbalimbali wa michezo na ardhi ikipitia ramani ya maeneo ya ujenzi wa madarasa na hosteli.

Timu ya wataalam ikiangalia eneo la ujenzi wa madarasa wa Kituo cha kuendeleza vipaji vya Michezo

 



Na John Mapepele, Dodoma

 

Serikali inatekeleza mradi wa  kupanua eneo la  Chuo cha  Maendeleo ya Michezo Malya ikiwa ni  mkakati  maalum wa kuanzisha Kituo cha Kuendeleza Vipaji vya Michezo  ili kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamichezo hapa nchini.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusuph Singo Omary ameyasema haya  wakati alipokuwa na  Timu ya wataalam walipotembelea na kukagua eneo  hilo hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kufanya maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kitakuwa na hadhi ya kimataifa.

 

“Niseme tu kwamba  kukamilika kwa kituo  hiki kutaifanya  nchi yetu kusonga mbele kwenye  Sekta ya Michezo kwa kuwa  vipaji vya wanamichezo wetu vitaibuliwa na  tutaweza sasa  kushindana  na mataifa mengine duniani sasa” amefafanua Mkurugenzi Omary

 

Amesema Tanzania ina hazina kubwa ya vipaji kilichokuwa kinakosekana ni kituo maalum cha michezo cha kuwanoa wachezaji na kwamba kukamilika kwa kituo hiki ni suluhisho la kudumu la changamoto hiyo.

 

Awali, Katibu Mkuu wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema  Wizara imeendelea  kufanya mageuzi makubwa ili kutimiza ahadi  za Serikali na matarajio ya wananchi kwa ujumla.

 

Amesema Wizara  inatekeleza kwa kwa kasi  masuala yote  yaliyobainishwa kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka  2020-2025 ikiwemo ibara125(a)-(h) kwa Sekta ya Habari, ibara239 (a)-(m) kwa Sekta ya Utamaduni, ibara 249 (a)-(j) Sekta ya Sanaa na ibara 243(a)-(k) kwa Sekta ya Michezo.

 

Akihutubia kwenye kikao cha Wafanyakazi wa wa Wizara hiyo hivi karibuni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema tayari Wizara yake imeshakamilisha agizo la Serikali la kuanzisha Mfuko wa Sanaa na Utamaduni ikiwa pia ni mkakati wa kukuza sekta ya Michezo nchini.

 

“Wizara imekamilisha agizo hili kwa kuhuisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni ambao umetengewa shilingi bilioni 1.5. 

Mfuko  huu kwa  mwaka ujao wa fedha utajikita katika ujenzi wa miuondombinu muhimu ikiwemo jengo la SANAA HOUSE hapa Dodoma, pia utaendelea  kutengewa fedha zaidi kwa lengo la kutekeleza  majukumu mawili adhimu; kuwajengea uwezo wanatasnia hizo za Sanaa na Utamaduni kupitia mafunzo na  kuwawezesha kupata mikopo na ruzuku katika kazi zao” amesisitiza Waziri Bashungwa

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger