Monday 19 April 2021

KOCHA JOSE MOURINHO AFUKUZWA KAZI

...


Kocha wa Tottenham Jose Mourinho amepigwa kalamu baada ya kuisimamia timu hiyo kwa miezi 17 pekee.

Raia huyo wa Ureno alichukua mahala pa Mauricio Pochettino kama mkufunzi wa Spurs mwezi Novemba 2019 na kuiongoza klabu hiyo kuwa katika nafasi ya sita katika ligi ya Premia msimu uliopita.

Kwa sasa Spurs wako katika nafasi ya saba, baada ya kuvuna pointi mbili kutoka mechi tatu zilizopita na waliondolewa katika Ligi ya Europa mwezi Machi. Spurs inatarajiwa kukabiliana na Manchester City katika fainali ya Kombe la Carabao siku ya Jumapili.

Msimu huu, Tottenham chini ya usimamizi wa Mourinho imeshapoteza michezo 1. Rekodi ya kupoteza michezo mingi hivyo ni ya mara ya kwanza kwa Mourinho katika kazi yake ya ukufunzi.

Hakuna klabu ya ligi ya Premia iliopoteza pointi nyingi kutoka kwa klabu zinazofanya vizuri msimu huu zaidi ya Spurs ambao wamepoteza pointi 20.


Siku ya Jumapili , Tottenham walikuwa miongoni mwa timu sita za ligi ya Premia kutangaza kwamba walikuwa wanajiunga na ligi mpya ya Ulaya ya Superleague.


Mechi ya mwisho ya Mourinho akiisimamia timu hiyo ilikuwa sare ya 2-2 dhidi ya Everton siku ya Ijumaa.

Chanzo - BBC Swahili
Share:

0 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger