Wednesday, 12 August 2026

BITEKO: TANZANIA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA AJENDA YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA


📌 Asema wajibu wa kila Mtanzania ni kuhakikisha mafanikio yanakuwa endelevu

KIZIMKAZI, ZANZIBAR

Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila Mtanzania kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanaendelea kuwa endelevu.

Dkt. Biteko amesema hayo wakati akishiriki mjadala kuhusu “Uongozi wa Kimkakati wa Tanzania katika Kuharakisha Mabadiliko ya Nishati Endelevu na Jumuishi”, uliofanyika katika Mdahalo wa Nishati Safi ulioandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF), Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Amesema uwepo wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia ni sehemu ya jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuipa msukumo ajenda hiyo katika ngazi mbalimbali za uongozi wake na kuifikisha hadi katika majukwaa ya kimataifa.

Dkt. Biteko amesema umuhimu wa kuendelea kuipa kipaumbele ajenda hiyo unatokana na ukubwa wa athari za matumizi ya nishati isiyo safi ya kupikia, ikiwemo uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi ya kuni na mkaa, ambapo takribani hekta 470,000 za misitu hupotea kila mwaka nchini.

Aidha, amesema zaidi ya watu 33,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusishwa na uchafuzi wa hewa wakati wa kupika, hali inayoonesha umuhimu wa kuongeza kasi ya mpito kuelekea matumizi ya nishati safi.

Ameongeza kuwa matumizi ya nishati isiyo safi yana athari za kijinsia, hususan kwa wanawake ambao hutumia muda mwingi kutafuta kuni badala ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi.

Amesema athari hizo pia zinawagusa watoto, ambapo baadhi yao hukosa muda wa kutosha wa kuhudhuria masomo kutokana na kulazimika kusaidia familia zao kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.

Katika mjadala huo, Dkt. Biteko amesisitiza umuhimu wa kufanya tathmini za mara kwa mara ili kubaini kiwango cha uendelevu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia, hususan baada ya wananchi kuwezeshwa kupata teknolojia na miundombinu husika.

Amesema tathmini hizo zitasaidia Serikali na wadau kubaini changamoto zilizopo, kupima matokeo yaliyofikiwa na kuweka mikakati madhubuti zaidi ya kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Pia, Dkt. Biteko ameipongeza Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) kwa kuwa miongoni mwa taasisi zinazochangia utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia shughuli mbalimbali, ikiwemo kusaidia upatikanaji wa miundombinu pamoja na kuendesha midahalo inayowakutanisha wadau kujadili namna bora ya kuharakisha matumizi ya nishati safi, salama na endelevu nchini.



Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO AGOSTI 12,2026



magazeti















Share:

Tuesday, 11 August 2026

UCSAF YABORESHA MINARA 431 ILI KUCHOCHEA MAENDELEO


Meneja wa kanda ya Ziwa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) Fredy Kandonga, akizungumza kwenye semina hiyo.
Meneja wa kanda ya Ziwa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) Fredy Kandonga, akizungumza kwenye semina hiyo.
Meneja wa kanda ya Ziwa wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote(UCSAF) Fredy Kandonga, akizungumza kwenye semina hiyo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza(MPC) Edwin Soko akizungumza kwenye semina hiyo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mwanza(MPC) Edwin Soko akizungumza kwenye semina hiyo.
Ofisa Mawasiliano Mwandamizi wa UCSAF Celina Mwakabwale, akizungumza kwenye semina hiyo
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo.
Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya Ziwa wakifuatilia mada mbalimbali katika semina hiyo.


Na Mwandishi wetu

Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) umeongeza kasi ya huduma ya intaneti Kanda ya Ziwa baada ya kubadilisha minara 431 kutoka teknolojia ya 2G kwenda 3G/4G, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kupata huduma za intaneti zenye ubora zaidi na kuwaletea maendeleo.
Share:

TUME YABAINISHA MATAMANIO YA SERIKALI KULINDA AFYA NA USALAMA WA WATUMISHI WA UMMA

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, akifungua mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa wakaguzi wa Tume hiyo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama naAfya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa lengo la kuwajengea uelewa wakaguzi hao wenye jukumu la kukagua uzingatiaji wa sheria na miongozo mbalimbali katika sekta ya umma.

******************

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Utumishi wa Umma imesema serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha watumishi wa umma wanakuwa salama na wenye afya njema na hivyo kutekeleza wajibu wao wa kuwahudumia wananchi ipasavyo.

Kauli hiyo imeelezwa na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda, alipofungua mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa wakaguzi wa Tume hiyo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa lengo la kuwajengea uelewa wakaguzi hao wenye jukumu la kukagua uzingatiaji wa sheria na miongozo mbalimbali katika sekta ya umma.

Amesema serikali inatamani kuona kila mtumishi wa umma anakuwa salama dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi ili aweze kutoa mchango wake kikamilifu katika kutekeleza majukumu ya serikali.

“Sote tunafahamu kwamba kinga ni bora kuliko tiba, Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi inaelekeza maeneo yote ya kazi kuwa na mifumo madhubuti ya kuwalinda wafanyakazi dhidi ajali na magonjwa yatokanayo na kazi. Serikali inaamini kwamba watumishi wakiwa na afya njema, utendaji wao utaimarika na tayari ina chombo chake mahsusi cha kusimamia hilo ambacho ni Taasisi ya OSHA,” ameeleza Katibu wa Tume.

Amebainisha kwamba si wajibu wa Tume kusimamia utekelezaji wa Sheria bali Tume hiyo ina jukumu la kuhakikisha waajiri wanatekeleza sheria hiyo pamoja na miongozo mingine inayotolewa na OSHA ili kulinda afya na usalama wa watumishi wa serikali.

“Kutokana na umuhimu wa rasilimali watu, Serikali kupitia Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ilisisitiza Tume kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria ya usalama na afya mahali pa kazi ili kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi katika mazingira bora na hivyo kuwa na ufanisi,” amesisitiza Katibu Kipanda.

Aidha, amewataka wakaguzi wa Tume kuwa na uelewa wa kina kuhusu Sheria ya Usalama na Afya mahali pa kazi ili waweze kufanya tathmini sahihi ya utekelezaji wa sheria hiyo na kushauri maboresho stahiki.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija Mwenda, ameipongeza serikali kwa kudhihirisha nia ya dhati ya kuwalinda watumishi dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi kupitia utekeleza wa sheria na miongozo ya usalama na afya mahali pa kazi.

“Napenda kutoa shukrani zangu kwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuonesha nia ya dhati ya kuhakikisha kwamba nguvukazi ya nchi inalindwa katika sekta zote za umma na binafsi ambapo kupitia maelekezo yake masuala ya usalama na afya yamejumuishwa katika kanuni za kudumu za utumishi wa umma,” amesema Mwenda na kuongeza:

“Tunaishukuru Tume kwa kutushirikisha ambapo tumeweza kuandaa mafunzo ya kuwajengea uelewa wakaguzi wake ili wakienda kukagua wajue ni maeneo gani muhimu ya kuyafuatilia na wametuahidi baada ya ukaguzi tutakuwa na kikao cha pamoja kwa ajili ya kupata mrejesho.”

Baadhi ya Wakaguzi wa Tume wameyaelezea mafunzo hayo kama nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mafunzo haya yametupa uelewa mpana sisi kama wakaguzi utakaotuwezesha kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi,” ameeleza Rose Silayo.

“Kipekee ninashukuru kwa mafunzo haya ambayo yatatuwezesha kukagua na kushauri ipasavyo uzingatiaji wa masuala ya usalama na afya ili kulinda afya za watumishi wa umma,” ameelezaDavid Shombe.

Mwaka 2022, Tume ilifanya maboresho ya mfumo wa ukaguzi wa masuala ya kiutumishi ili kuendana na sera, sheria na mazingira ya wakati husika ambapo maeneo sita ya kiutawala yaliongezwa katika maeneo saba yaliyokuwa yakikaguliwa awali. Eneo la usalama na afya kazini ni miongoni mwa maeneo yaliyoongezwa.


Mkurugenzi wa Mafunzo, Tafiti, Takwimu na Uhamasishaji wa OSHA, Bw. Joshua Matiko, akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizoibuliwa na washiriki katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa Wakaguzi wa Tume ya Utumishi wa Umma yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).

Meneja Mafunzo wa OSHA, Mhandisi Shaban Mkindi, akiwasilisha mada katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa Wakaguzi wa Tume ya Utumishi wa Umma yaliyoandaliwana Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).

Mkaguzi wa Tume ya Utumishi wa Umma, akipitia Jarida la OSHA katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa Wakaguzi wa Tume ya Utumishi wa Umma yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda (Katikati) akiwa na viongozi wenzake katika meza kuu wakati wa mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa wakaguziwa Tume hiyo.

Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Nolasco Kipanda (Katikati) akiwa na viongozi wenzake wakifuatilia mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA kwa Wakaguzi wa Tume hiyo.

Afisa Mafunzo Mwandamizi wa OSHA, Bw. Simon Lwaho, akiwasilisha mada katika mafunzoya usalama na afya mahali pa kazi kwa Wakaguzi wa Tume ya Utumishi wa Umma yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).

Wakaguzi wa Tume ya Utumishi wa Umma wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) kwa lengo la kuwajengea uelewa juu ya masuala ya usalama na afya mahali pa kazi.



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger