Thursday, 7 May 2026
WAZIRI RIDHIWANI AWASHA MOTO AAPAM, AIPA HONGERA TEMESA KWA BOSI MPYA

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb), leo tarehe 6 Mei, 2026 amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma (AAPAM), unaowakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Waziri Ridhiwani alisisitiza umuhimu wa wataalamu wa Rasilimali watu katika kuimarisha utendaji na ufanisi wa taasisi za umma ambapo alibainisha kuwa mchango wao ni muhimu katika kufanikisha utoaji wa huduma bora ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kiutawala na kiteknolojia.
Aidha, alieleza kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wataalamu hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
.jpg)
Katika ziara yake katika mabanda ya maonesho yanayoambatana na mkutano huo, Mhe. Ridhiwani alitembelea banda la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), ambapo alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hiyo pamoja na maboresho ya huduma zake.
.jpg)
Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma TEMESA Bi Martha Joachim akimkabidhi zawadi Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb)
Akiwa katika banda hilo, aliipongeza TEMESA kwa kumpata Mtendaji Mkuu mpya, nakusema hatua hiyo imeashiria fursa ya kuimarisha zaidi uongozi, kuongeza ubunifu na kuleta matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa umma.
“TEMESA kwanza nawapongeza kwa kupata mtendaji mpya naamini mabadiliko haya yataleta chachu ya kiutendaji na utoaji wa huduma bora hongereni sana.” Amesema Mhe. Ridhiwani.

Mkutano huo wa siku nne umebeba kaulimbiu isemayo: “Kufikiri upya utoaji wa huduma kwa umma: Jinsi Serikali inavyoweza kutumia teknolojia kuanzisha huduma bora na zinazomlenga mwananchi, kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na changamoto za mazingira.”
Wednesday, 6 May 2026
BLUE TICKS, RED FLAGS & BARIDI YA JIONI: SOMO KUTOKA GORDON’S & TONIC

Na Mwandishi Wetu
Katika ulimwengu wa mahusiano ya kisasa, wengi wanakubaliana na jambo moja: dating si burudani tena—imekuwa kama kazi ya muda wote isiyo na mkataba wala masharti ya wazi.
Asubuhi unapambana na majukumu ya kikazi, jioni unapambana na hisia. Leo unapokea ujumbe wa “good morning babe,” kesho unajikuta umeachwa kwenye blue ticks kana kwamba uliwasilisha ombi la kazi lisilopata majibu. Hakuna mrejesho, hakuna maelezo—hata ile heshima ya “seen” haipo.
Hali hii imewaacha wengi wakijiuliza: tatizo liko wapi? Kadri mtu anavyojaribu kutafuta majibu, ndivyo uchovu wa kihisia unavyoongezeka.
Ukweli unabaki kuwa mahusiano si jambo jepesi. Na consistency—kile kitendo cha kuwa thabiti—kimekuwa kama bidhaa adimu. Watu hubadilika, hisia hubadilika, na mara nyingi kinachobaki ni mkanganyiko pamoja na maumivu yasiyoelezeka kirahisi.
Hata hivyo, katikati ya hali hiyo, kuna vitu vidogo vinavyoweza kutoa nafuu. Mfano ni utulivu wa jioni ya baridi baada ya siku ndefu, au ladha ya kwanza ya kinywaji kilichotengenezwa kwa ustadi.
Hapo ndipo bidhaa kama Gordon’s Premix Cocktail inaonekana kuleta tofauti. Kwa watumiaji wake, kinywaji hiki kinatoa uzoefu ulio thabiti—ladha ile ile kila wakati, bila kubahatisha. Hakuna maswali ya “leo itakuwaje?” wala mshangao usiotarajiwa.
Tofauti na baadhi ya mahusiano ya binadamu yenye mixed signals, hapa hakuna mkanganyiko. Baada ya siku ndefu ya barua pepe zisizoisha na jumbe zisizojibiwa, wengi wanatafuta kitu kisichohitaji kufikiria sana—kitu kinachofanya kazi kama kilivyoahidiwa.
Hakuna kusubiri tonic iongezwe. Hakuna visingizio. Unachofungua, ndicho unachopata.
Na pengine hapo ndipo somo linapopatikana, hasa katika msimu huu wa baridi na mvua. Consistency si kelele wala ahadi nyingi zisizotekelezwa. Ni ule utulivu wa kujua, hata bila kuuliza, kwamba mambo yako sawa.
Wakati mwingine, maisha na mahusiano yanaweza kuwa magumu kuliko inavyopaswa. Lakini si kila kitu kinahitaji juhudi kubwa kiasi hicho. Vingine vinafanya kazi kwa urahisi—kama vile cocktail iliyo tayari kunyweka.










.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)








