Sunday, 30 January 2022

MHESHIMIWA YAKUBU AIPONGEZA UDSM KWA MIKAKATI YA KUKUZA VIPAJI KUPITIA SANAA NA UBUNIFU

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu akimkabidhi hundi ya Shilingi Milioni moja (1,000,000/=) kwa mshindi wa kwanza wa Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu akimkabidhi hundi ya Shilingi laki saba (700,000/=) mshindi wa pili wa Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu akimkabidhi hundi ya Shilingi Laki tano (500,000/=) kwa mshindi wa tatu wa Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu akikabidhi vyeti kwa washiriki wa Mashindano ya Muziki kwenye Tamasha la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu akizungumza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),Prof.William Anangisye akizungumza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022.Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam-UTAFITI Prof.Benadeta Killian akizungumza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. Mkuu wa WWilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James akizungumza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. Mmoja wa wasanii wa nyimbo za kinyaturu mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitumbuiza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022.Mmoja wa wasanii wa nyimbo za kisukuma mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitumbuiza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022.Mmoja wa wasanii wa nyimbo za kimakonde mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitumbuiza katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. Kwaya Kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakitumbuiza katika katika Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. Wanamuziki Farid Kubanda (Fid Q) pamoja na Hamis Mwijuma (Mwana FA) wakifuatilia Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakifuatilia Shindano la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho yaliofanyika UDSM tarehe 29/01/2022. NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James( wa pili kushoto), Makamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof.William Anangisye (wa pili kutoka kulia) na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam-UTAFITI Prof.Benadeta Killian wakiimba wimbo wa Taifa katika Tamasha la Muziki la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha dar es Salaam kwenye Maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa,Tamaduni na Michezo Mhe.Said Yakubu amekabidhi zawadi ya washindi wa Mashindano ya Kuimba Chuo kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Chuo hicho.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe.Yakubu ameupongeza uongozi wa Chuo hicho kuendeleza na kukuza vipaji vya muziki kwa vijana wa Chuo hicho kwa kuwapatia fursa kuoneshesha vipaji vyao na kuvikuza.

Amesema matamasha kama haya matumaini yake yawe endelevu ili kuendelea kuibua fursa kwa vijana kupitia sanaa ya muziki kwani sanaa ni ajira kwasasa.

"Kukuza matamasha kama haya ili kuibua vipaji kwa vijana na pia kuwa sehemu ya kuwa daraja kwa watu ambao wanahitaji kuonesha na kuvikuza vipaji vyao". Amesema Mhe.Yakubu.

Kwa Upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM),Prof.William Anangisye amesema Chuo kiliandaa Tamasha la Muziki la Wanafunzi ambao hushindana na kuibua vipaji

Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika taifa kwakuwa ni kitovu cha Utafiti, ufundishaji na ujifunzaji.

"Wahitimu wengi wameajiriwa Serikalini, katika Sekta binfasi na mashirika ya Kimataifa kutokana na ubora wa wahitimu katika kufikiri, kuchanganua mambo na kutatua changamoto mbalimbali katika vituo vya kazi, jamii na taifa kwa ujumla". Amesema.

Mshindi wa kwanza wa Tamasha hilo amekabidhiwa kitita cha Shilingi Milioni moja za Kitanzania, Mshindi wa Pili akikabidhiwa shilingi Laki saba na mshindi wa Tatu akiondoka na kitita cha Shilingi laki tano.

Mshindi wa kwanza ambaye aliondoka na kitita hicho Moses Selestin, mshindi wa pili ni Rodhey Rutashwotwa na mshindi wa tatu ulienda kwa Calum Aloyce.
Share:

KATIBU CCM :TARIME SIYO YA MCHEZO ITAKUPANDISHA CHEO,ITAKUSHUSHA ITAKUONDOA


Katibu wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Tarime mkoa wa Mara Valentine Maganga

Na Dinna Maningo, Tarime

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Tarime mkoa wa Mara Valentine Maganga amesema kuwa watu wa wilaya ya Tarime ni majasiri si waoga na hawana aibu kumkosoa mtu.


Akizungumza na Malunde 1 blog Katibu huyo alisema kuwa wananchi wa Tarime wako tayari kumkosoa mtu yeyote na hawana mambo ya kona kona kwa kuwa ukosoaji kwao ni utamaduni.


"Tarime siyo ya mchezo ni wilaya ya kuwapima viongozi ukiletwa Tarime ujue kuna kupanda cheo au kushushwa,watu wake ni majasiri hawana aibu, kukukosoa kwao ni jambo la kawaida ni watu wasio na kona kona ukikosea hawaogopi kusema kwa sababu ndiyo utamaduni wao" amesema Maganga. 


Maganga amewaomba viongozi wa Chama na Serikali walioko Tarime kushirikiana katika maendeleo na kutatua changamato zinazowakabili wananchi kwakuwa hitaji kubwa la wananchi ni kusikilizwa na kutatuliwa kero zao.



Wakizungumza na Malunde 1 blog kwa nyakati tofauti,Baadhi ya wananchi wameunga mkono kauli hiyo,Mwita Ryoba mkazi wa kijiji cha Matongo-Nyamomgo anasema kuwa wilaya hiyo hutizamwa kama mahali pa kuwapima viongozi utendaji wao wa kazi.


"Tarime ndiyo kipimo cha viongozi maana sisi watu wa Tarime hatuna uoga wala kumvumilia kiongozi anayekwenda kinyume tunapenda haki na hatupendi uonevu na tuna ujasiri ambao unatusaidia kutoogopa kumkosoa mtu yeyote hata kama ni kiongozi wakurya ndiyo tuko hivyo hata akija mgeni akiishi Tarime naye anakuwa jasiri", anasema Ryoba.


John Mseti mkazi wa kijiji cha Turugeti kata ya Bumera anasema" Tarime ni kipimo cha matendo ya watu hasa viongozi tumeshuhudia baadhi walioletwa kufanya kazi Tarime wakashushwa vyeo na wengine kuondolewa kwenye nafasi za kazi"


"Wapo waliokuwa DC Tarime walitumbuliwa ,wapo walioletwa kuwa RPC wamepanda kutoka kuongoza wilaya mbili za kipolisi Tarime/Rorya sasa wanaongoza mikoa,wapo waliokuwa OCD hapa Tarime leo ni RPC,wapo watendaji waliokuwa nafasi za kawaida na wamepanda vyeo  huko Serikalini na kwenye vyama" anasema Mseti .

Chacha Marwa mkazi wa mtaa wa Sabasaba anasema kuwa watu wa Tarime si wakorofi kama inavyodhaniwa bali ni watu wanaojiamini,wenye msimamo,wanapenda haki na hawapendi kuonewa.

Rhobi Marwa mkazi wa Rebu anasema kuwa faida ya mtu kuwa jasiri inamsaidia kutokuwa na uoga katika kufanya maamuzi sahihi na kwamba kumkosoa mtu ni kumsaidia kujua tatizo lake ili ajisahihishe.

Muhiri Chacha Mkami mkazi wa kijiji cha Nyangoto kata ya Matongo anasema"Watu wa Tarime usiwaone hivyo ukija kama wewe ni kiongozi huwa hawana papara watatulia kwanza we utaona hawasemi jambo kumbe wanakupima kwanza matendo yako,siku wakikuamria hutoboi.


"Hata kwenye siasa ukipewa uongozi alafu ukaichezea nafasi uliyopewa kukubadilikia ni dakika moja ndiyo maana utaona Tarime inaongozwa na CCM na Chadema wao hawaangalii chama wanaangalia mtu atakayefaa bila kujali anatoka chama gani,ukifanya vizuri watakusema kwa mazuri ukifanya vibaya utasemwa kwa mabaya" anasema Muhiri.


Lucy John anasema kuwa watu wa Tarime ni wachapa kazi si tegemezi na ujituma kuhakikisha wanajiinua kiuchumi wakiwemo wanawake na hata uchumi ukiyumba hawakati tamaa kutafuta pesa.

Share:

DC SHEKIMWERI ATAKA JAMII KUKOMESHA MAUAJI, WIZI

 Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akiongea na wananchi wa kata ya Kikuyu(hawapo pichani)ambapo amewataka kukemea vikali vitendo viovu.

*****

Na Dotto Kwilasa Malunde 1 blog- DODOMA.

MKUU wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kukubali kusimamia ulinzi na usalama wao kwa kushirikiana kuwabaini watu wenye viashiria vya vitendo viovu hali itakayopunguza mauaji yanayotokea mara kwa mara.


Aidha ameuagiza uongozi wa Kata ya Kikuyu kwa kushirikiana na Kamati ya ulinzi na usalama kusimamia suala la usalama kutokana na kuibuka kwa vitendo vya wizi pamoja na mauaji katika eneo hilo.


Shekimweri ametoa maagizo hayo jana Jijini Dodoma wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Kikuyu Kusini wakati walipokuwa wakitoa kero mbalimbali zilizopo katika eneo hilo.


Aidha ametaka pia Viongozi wa dini kuhubiri suala la kuwajenga kiroho wananchi ili kuwa na hofu ya Mungu kwani hivi sasa kumekuwa na matukio ya ajabu ambayo yanatishia usalama wa maisha ya watu.


"Naomba Viongozi husika mkae mjadili haya masuala ya usalama kama ajenda wapi wakristo wanaenda kwenye jumuiya hebu muongelee na masuala ya upendo mnapokutana haiwezekani watu wanafikia hatua ya kutoana uhai suala hili halikubaliki,"amesema


Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya  amemtaka Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kuhakikisha anatekeleza kero za wananchi hao hasa suala la fidia ya viwanja kutokana na  mashamba yao kuchukuliwa na Serikali kwa ajili ya maendeleo.


Pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kuzingatia suala usafi wa mazingira ili kuhakikisha Jiji linakuwa na hadhi ya Makao Makuu.


"Hapo baadae nitakuja na Sheria nikikuta mazingira yako ni machafu tutakutoza faini wala hakutakuwa na mjadala na katika kuonyesha kuwa tupo makini na hilo tayari tumeajiri migambo wa Jiji kutekeleza hilo,"amesema.


Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ,Joseph Mafuru ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa wapo katika mchakato wa kuwapatia viwanja wananchi ambao mashamba yao yamechukuliwa kama fidia.


Alisema jumla ya wananchi  328 wa Kata ya Kinyambwa wa Jijini hapa watapatiwa viwanja kama fidia  kwa  mashamba yao yalichukuliwa na Jiji kwa ajili ya uendelezaji wa Jiji hilo.


Mafuru  alisema mpaka hivi sasa tayari wameshatoa viwanja 25 kati ya 328 ambapo zoezi la upimaji linaendelea ili kuweza kukamilisha haraka na kugawa viwanja hivyo.


Awali baadhi ya wakazi hao wameeleza kero zinazo wakabili wamesema waliahidiwa na Jiji hilo kupewa viwanja mbadala baada ya kuwachukulia mashamba yao lakini mpaka sasa  bado hawajapewa.


"Mheshimiwa Mkurugenzi tunaomba uliangalie  suala hili kwa umakini kwani imekuwa ni muda mrefu sasa hatuoni kinachoendelea kuhusiana na suala hili la kupatiwa haki zetu,"walisema.


Pia wamelalamikia kitendo cha baadhi ya watu  kutupa taka ovyo katika maeneo ya makazi ya watu bila kuchukuliwa hatua na kutaka suala hilo kutatuliwa kwani ni kero kwao inayoweza kusababisha maradhi ya magonjwa ya mlipuko.


"Huu ni msimu wa mvua ,hali ya uchafu imezidi kuwa mbaya zaidi,takataka kila kona,tunaomba Mkurugenzi utusidie suala hili la sivyo magonjwaya mlipuko yatatumaliza,"wamesema baadhi ya wananchi hao.


Share:

TPC YATAKIWA KUBUNI HUDUMA MPYA ZA WATEJA KWA KUTUMIA MFUMO WA ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI

 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, mawasiliano na Teknolojia ya habari Teddy Njau akiongea wakati wa mafunzo ya uelewa wa mfumo wa anuani za makazi Jijini Dodoma.

*****


Na Dotto Kwilasa Malunde 1 Blog,DODOMA.

SHIRIKA la Posta Tanzania (TPC) limetakiwa  kutumia mfumo wa anuani za makazi na postikodi kubuni huduma mpya kwa wateja ili utekelezaji wa mfumo huo utakapokamilika uweze kutumika ipasavyo kufikisha huduma na bidhaa kwa wateja.

 

Hayo yameelezwa na jana Jijini hapa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Teddy Njau wakati akifungua semina ya mafunzo ya kujenga uelewa kuhusu mfumo wa anuani za makazi na postikodi kwa Mameneja wa Mikoa ya Shirika hilo wa Tanzania Bara na Zanzibar.

 

Njau amewataka washiriki hao kuweka anuani za makazi kwenye maeneo yao; kwa wateja wao na kubuni huduma mpya zitakazotumiwa na wateja kupitia mfumo wa anwani za makazi utakapokamilika utekelezaji wake kwa kuwa Shirika hilo lina mtandao mpana nchi nzima na ni wadau wa msingi wanaotakiwa kutumia miundombinu hiyo.

 

“Kila mmoja wetu ana jukumu la kuhakikisha anuani za makazi zinawekwa na kutumika nchi nzima, leo mnapatiwa mafunzo ya kujenga uelewa ili mkasimamie na kushiriki utekelezaji wa mfumo huu kwenye mikoa yenu Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuwa ninyi ni wadau muhimu na ni wajumbe kwenye kamati za kitaalamu,” amesisitiza Njau

 

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano wa Wizara hiyo, Caroline Kanuti amesema kuwa mfumo wa anuani za makazi utakuwa wa kidijitali ili kutoa fursa kwa Serikali kutekeleza majukumu ya sensa ya watu na makazi ili anuani zijumuishwe kwenye sensa inayoanza mwezi Agosti mwaka huu.


Ameongeza kuwa utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi utafanyika kwa miezi mitano nchi nzima kwenye kata na wadi 4,174; halmashauri 196 na mikoa 31 ili zoezi hili likamilike ipasavyo na taarifa zake ziwekwe kwenye tovuti maalum na zitumike kwenye simu za mkononi ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi

 

Naye Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Macrice Mbodo amesema kuwa Shirika lake ni mdau muhimu katika anuani za makazi na postikodi ndani na nje ya nchi kwa kuwa posta zote duniani zina jukumu la kutoa anuani zinazotambulika na muundombinu huu utakapokamilika Shirika litatumia anwani za makazi kusafirisha huduma na bidhaa kwa wananchi mpaka nyumbani kwa kuwa tayari tuna duka mtandao.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 30,2022

Share:

Saturday, 29 January 2022

VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU VYENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 70 VYATEKETEZWA

Zoezi likiendelea la kuteketeza vipodozi viambata sumu vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga. Zoezi likiendelea la kuteketeza vipodozi viambata sumu vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga. Mkaguzi wa TBS Kanda ya kaskazini Bw.William Mhina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuteketeza vipodozi viambata sumu vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga.


*******************


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza vipodozi vyenye viambata sumu katika dampo la Muriet jijini Arusha vyenye uzito wa Tani moja na thamani ya millioni 70 ambavyo vilikamatwa katika kaguzi mbalimbali zilizofanywa hivi karibuni na TBS katika mikoa ya kanda hiyo ambayo ni Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga.


Akizungumza katika zoezi hilo mapema hii leo, Mkaguzi wa TBS Kanda ya kaskazini Bw.William Mhina amesema katika kuhakikisha kuwa maeneo yanayojihusisha na uuzaji wa vipodozi yanasajiliwa na Shirika yapo salama na yanafaa ni pamoja na ukaguzi wa bidhaa zinazouzwa katika maeneo hayo.


"Ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Kanda imepelekea kukamatwa na kuondolewa sokoni kwa bidhaa za vipodozi zilizopigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu kwani yana viambata sumu ambayo huweza kudhuru afya ya mtumiaji".Amesema.


Aidha amesema bidhaa zilizokamatwa zenye viambata sumu ziko za aina tofauti tofauti na zinatoka nje ya nchi.


Pamoja na hayo amewaasa wananchi kuacha kutumia vipodozi vilivyopigwa marufuku kwani huleta athari kwa nguvu kazi ya Taifa pindi mtu anapoathirika hulazimika kutumia gharama kubwa kujitibu na muda mwingi hupotea na kushindwa kujenga Taifa.


"Kila mtanzania awe mkaguzi wa bidhaa hizi,tunasisitiza ukaguzi uanzie ndani mwetu sisi wote". Amesema


Amesema orodha ya vipodozi vilivyopigwa marufuku inapatikana kwenye tovuti ya Shirika www.tbs.go.tz, pia wanasambaza vipeperushi kwenye maeneo yote yanayojihusisha na uuzaji wa vipodozi, lengo ni kuhakikisha elimu inafika kwa kila mwananchi.
Share:

DKT. KIJAJI: TANZANIA INATAKA KUONA MKATABA WA AfCFTA UNAKUWA CHACHU YA KUONGEZA FURSA ZA KIBIASHARA NA UWEKEZAJI KWA NCHI ZA AFRIKA.


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiongea kuhusu nia ya Tanzania kuona Mkataba wa AfCFTA unakua chachu ya kuongeza fursa za kibiashara na uwekezaji wakati akishiriki Mkutano wa Nane wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika, uliofanyika Accra, Ghana tarehe 28-29 Januari 2022.

..................................................

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) kwa niaba ya Serikali amelithibitishia Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) nia ya Tanzania kuona Mkataba wa AfCFTA unakuwa chachu ya kuongeza fursa kwa nchi za Afrika kupanua zaidi biashara baina yao na kukuza uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya Bara la Afrika.

Waziri Kijaji ameyasema hayo alipokuwa akishiriki Mkutano wa Nane wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara barani Afrika, uliofanyika Accra, Ghana tarehe 28-29 Januari 2022. Waziri Kijaji aliongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki katika Mkutano huo

Mkutano huo unaofuatia hatua muhimu ya Tanzania kuridhia na kujiunga katika Mkataba wa Kuanzisha Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kupitia Azimio la Bunge la Tanzania la Septemba 9, 2021 nakuifanya Tanzania kuwa nchi ya 40 kuridhia na kuwasilisha Hati ya Kuridhia Mkataba huo kwenye Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC). Amesema Waziri Kijaji.

Aidha, Mkutano huo uliohudhuriwa na nchi wanachama wa AfCFTA umejadili masuala muhimu yaliyosalia kuridhiwa ili kuwezesha biashara baina ya nchi za Afrika kuanza kufanyika chini ya Mfumo wa Eneo Huru la Biashara Afrika. Masuala hayo muhimu ni pamoja na ufunguaji wa biashara ya bidhaa, ufunguaji wa biashara ya huduma, vigezo vya uasili wa bidhaa, hakimiliki na bunifu, uwekezaji, pamoja na sera ya ushindani.Amesema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji ameeleza kuwa Baraza hilo la Mawaziri limeridhia kwa kauli moja mapendekezo ya hatua mbalimbali zilizopendekezwa ili kuharakisha mchakato wa kukamilisha majadiliano katika maeneo hayo yaliyobakia ili kutimiza kiu ya wadau wengi, hususan Sekta Binafsi barani Afrika kufaidika na uanzishwaji wa Eneo hilo lenye walaji takriban bilioni 1.3 linalotarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi, kibiashara na kijamii barani Afrika.

Wakati huo huo, Akiwa Ghana, Waziri Kijaji amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Viwanda na Biashara wa Ghana Mhe. Alan Kyeremanten ambapo wamejadiliana namna ya kuanzisha mahusiano ya kimkakati ya kibiashara kati ya Tanzania na Ghana ili kuhakikisha uhusiano mzuri wa kisiasa na kihistoria uliopo baina ya nchi hizo mbili unakuwa na manufaa ya kiuchumi kwa wananchi wa Tanzania na Ghana.

Aidha, Katika kikao hicho Mawaziri hao walikubaliana pia kuchukua hatua za makusudi kuwaunganisha wadau wa Sekta Binafsi pamoja na wafanyabiashara wa nchi hizo mbili kwa kuanzisha makubaliano rasmi na kuratibu ziara za mara kwa mara za kibiashara na kubadilishana utaalam na uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Vilevile, Waziri Kijaji alipata fursa ya kukutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA Mhe. Wamkele Mene, ambapo Katibu Mtendaji huyo alimpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa sekta muhimu ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na kuahidi kuendeleza ushirikiano wa Sekretarieti katika kuhakikisha maslahi ya Tanzania yanazingatiwa kikamilifu katika mchakato wa kukamilisha uanzishwaji wa Eneo hilo Huru la Biashara Afrika.
Share:

MKAKATI WA KITAIFA WA ELIMU JUMUISHI WA MIAKA MITANO WAZINDULIWA JIJINI DODOMA


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akizungumza wakati akizindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Kamishina wa Elimu Tanzania Dkt.Lyabwene Mtahabwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia Dkt.Magreth Matonya,akielezea lengo la mkakati huo wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Kimataifa Dkt.Daniel Baheta,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Wanafunzi walioshiriki uzinduzi wakifatilia Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Wadau mbalimba wakifatilia Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka (hayupo pichani), wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia Dkt.Magreth Matonya kabla ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akizindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa na wadau pamoja na wanafunzi wakionyesha vitabu vya muongozo mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika leo Januari 28,2022 jijini Dodoma.

............................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imezindua mpango mkakati wa kitaifa wa elimu jumuishi wa miaka mitanto (5) unaolenga kutoa fulsa sawa ya elimu kwa makundi yote bila kujali kikwazo cha aina yotote au mazingira.

Akizindua mpango huo leo Januari 28,2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Eliamini Sedoyeka amesema mpango huo ni wa tatu na umelenga kwenda kuboresha utoaji wa elimu katika ngazi zote bila kujali kikwazo cha aina yoyote katika fulsa ya upataji wa elimu kwa watoto.

"Kama Serikali tulikuwa na mipango mbalimbali na huu tunaozindua ni wa tatu ambao unakwenda kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu kwa usawa bila kujali hali ya mtoto toka ngazi ya awali, msingi, sekondari, ualimu, vyuo vya ufundi, maendeleo ya wananchi, elimu ya nje ya mfumo, na elimu ya juu” amesema. Prof. Sedoyeka.

Amesema mkakati huo unalenga kuwa na mfumo wa elimu unaotoa fulsa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kupata elimu bila vikwazo kimtazamo, mazingira, kiuchumi na kitaasisi katika ngazi zote.

“Mkakati huu unatoa fulsa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kusoma masomo ya ufundi tangu wakiwa darasa la awali lengo kuwajengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi kwa kuwa na uchuzi” amesema.

Ameongeza kuwa “mkakati huu pia utatekelezwa katika ngazi za vyuo vya ufundi, vyuo vya maendeleo ya wananchi ambako wananchi watapata umahiri katika fani mbalimbali zikiwamo za ujasiliamali na TEHAMA kuwaimarisha kiuchumi” Amesema.

Amesema mkakati huo umechapishwa kwa kuzingatia ujumuishi kwa kuwa na nakala za maandishi ya kawaida, maandishi yaliyokuzwa na maandishi Braille kwa ajili ya watu wenye uoni hafifu na wasioona.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Maalumu Dkt Magreth Matonya amesema mpango mkakati huo umeboreshwa na wanaamini utaendana na mahitaji ya sasa na ili kuhakikisha unafanya vyema mpango huo utakuwa ukifanyiwa tathmini kila baada ya miezi sita ili kuona utendaji kazi wake na matokeo.

“Mkakati huu utatupa dira ya wapi tuelekee katika utekelezaji wa elimu jumuishi, utasaidia upatikanaji wa taarifa za upatikanaji wa taarifa za utelelezaji wa elimu jumuishi ili kurahisisha ufanyikaji wa tathmini” amesema Dkt. Magreth.

Amesema mkakati huo umelenga kurekebisha sera ya elimu iendane na elimu jumuishi, kuimarisha upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika ngazi zote, kuongeza uandikishwaji na ushiriki wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika ngazi zote za elimu.

Nae Kamishna wa elimu hapa nchini Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema kuzinduliwa kwa mkakati huo ni lengo la kumfanya kila mtoto wa kitanzania anapata elimu bora na kwa usawa kwa maendeleo ya taifa na jamii kwa ujumla.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger