Sunday, 29 March 2026

KISA CHA MTOTO NELSA CHAREJEA: MAPENZI YA SIRI, FEDHA ZA MICHANGO NA TASWIRA MITANDAONI


Kisa kilichowahi kugusa mioyo ya Watanzania kinarejea tena mezani, kikichorwa upya na mvutano mpya:Mtoto Nilsa enzi za uhai wake (Mungu amrehemu) akiwa pamoja na Baba yake, Simon Bryson Mnyola wanashughulika na mjadala mkali kuhusu matumizi ya fedha za michango ya watanzania na namna taswira ya mtoto inavyo tumika mitandaoni.


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Kisa kilichowahi kugusa mioyo ya Watanzania kuhusu mtoto Nilsa, aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichwa kujaa maji na baadaye kufariki dunia, kimerudi tena katika mjadala wa umma kufuatia kuibuka kwa tuhuma mpya kutoka kwa mama mzazi wa mtoto huyo Jesca.

Kwa mujibu wa maelezo ya mama huyo, aliyewasiliana na chombo hiki kwa njia ya simu, anadai kuwa aliyekuwa mume wake Simon Bryson mnyola (baba nilsa)

alitumia kisa cha mtoto wao kama fursa ya kujipatia fedha kupitia michango ya wananchi, huku akijenga taswira ya kuwa mzazi mwenye upendo mkubwa mitandaoni, jambo ambalo anadai halikuwa halisi.

Jesca anadai kuwa wakati wa ugonjwa wa mtoto, baba huyo alimchukua mtoto na kupiga naye picha ambazo baadaye zilisambazwa mitandaoni kwa lengo la kuibua huruma kwa umma na kuchochea michango ya matibabu.

Kutokana na hali hiyo, Watanzania wengi waliguswa na kuanza kutoa misaada ya fedha.

Hata hivyo, mama huyo anasema baada ya kifo cha mtoto, jumla ya fedha zilizopatikana zilifikia takribani shilingi milioni 17, ambapo anadai alipewa kiasi cha shilingi milioni tatu pekee kwa ajili ya kulipia madeni ya matibabu, huku fedha zilizobaki zikibaki chini ya usimamizi wa baba huyo bila ushirikishwaji wa pamoja.

Aidha, anaeleza kuwa baada ya tukio hilo, mawasiliano kati yao yalivunjika na juhudi zake za kuomba msaada zaidi hazikupata ushirikiano.

Badala yake, anadai kuwa baba huyo ameendelea kutumia jina la mtoto huyo kujitangaza katika shughuli zake za kibiashara mitandaoni.

Katika hatua nyingine, mama huyo anadai kuwa kulikuwa na jitihada za kuonyesha hadharani kuwa wana uhusiano mzuri, ikiwa ni pamoja na kupiga picha pamoja na kuchapishwa mitandaoni, jambo ambalo anasema lilifanyika kwa shinikizo ili kulinda taswira ya baba huyo mbele ya umma.

Wakati huo huo, uchunguzi wa maoni ya mitandaoni unaonyesha kuwepo kwa mgawanyiko wa mitazamo miongoni mwa wananchi, ambapo baadhi wanaendelea kumuunga mkono baba huyo, huku wengine wakianza kuibua maswali kuhusu uwazi wa matumizi ya fedha za michango pamoja na nafasi ya mama mzazi katika mchakato mzima.

Hata hivyo, jitihada za kumpata baba anayehusishwa na tuhuma hizo ili kutoa ufafanuzi wake hazijafanikiwa hadi wakati wa kuchapishwa kwa habari hii.

Hapo chini nimekuwekea baadhi ya maoni ya waliokuwa mashabiki wa Nilsa kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonesha hisia zao moja kwa moja









Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MACHI 29,2026


Magazeti







Share:

Saturday, 28 March 2026

PROF. SHEMDOE AWAASA WALIMU 150 KUZINGATIA MAFUNZO NCHINI INDIA ILI KUWA MAHIRI NA KULETA MAGEUZI YA ELIMU NCHINI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka walimu 150 wa Amali za Kihandisi wanaokwenda India kuongeza umahiri kuhakikisha wanajifunza kwa bidii ili watakaporejea wawajengee uwezo walimu wengine, na hatimaye kutoa mchango utaokuwa na tija katika kuharakisha mageuzi ya elimu nchini.

Prof. Shemdoe ametoa wito huo Machi 26, 2026 kwa walimu hao waliopata fursa ya kwenda nchini India kuongeza umahiri, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu hao iliyofanyika Jiji Dar es Salaam.

“Nendeni mkajifunze kwa bidii na nidhamu, mkazingatie maadili, jifunzeni mbinu mpya na muwe tayari kuzitumia mtakaporejea, hivyo tunatarajia mtakaporejea mtakuwa nguzo ya kuboresha elimu ya amali katika shule zenu na chanzo cha maarifa kwa walimu wengine,” amesisitiza Prof. Shemdoe.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesisitiza kuwa mpango wa mafunzo hayo ni utekelezaji wa sera ya elimu ya lazima ya miaka 10, unaolenga kujenga umahiri wa ufundishaji na kuandaa kizazi cha wataalamu wenye ushindani wa kimataifa, huku akiwataka walimu hao kutambua nafasi yao kama daraja kati ya sera na utekelezaji darasani.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia walimu hao fursa ya mafunzo, akisisitiza kuwa ni ishara ya dhamira ya dhati ya kuendeleza mageuzi ya elimu, huku akipongeza mshirikiano wa viongozi wa wizara za kisekta katika kulitekeleza kwa ufanisi.

Wanufaika wa mafunzo hayo, akiwemo Mwalimu Judith Faustine wa Uhandisi Ujenzi katika Shule ya Sekondari Mwadui Ufundi na Mwalimu Jacob Mwalyego wa fani ya Uashi katika Shule ya Sekondari ya Ufundi Mbogwe, wameishukuru Serikali kwa kuwapatia nafasi hii ya kipekee. Wamesema ni heshima kubwa na fursa ya kuongeza maarifa yatakayowawezesha kuendeleza mageuzi ya elimu nchini.

Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa ameeleza kuwa mafunzo hayo ya mwezi mmoja yamewahusisha walimu kutoka mikoa yote 26 ya Tanzania Bara na viongozi wa ngazi ya elimu mkoa kutoka mikoa tisa, hivyo
kuiwezesha Tanzania kuandika ukurasa mpya katika historia ya elimu ya ufundi kwa kupeleka walimu 150 wa Amali za Kihandisi nchini India ambao  wakirejea watasimamia kikamilifu uendelevu wa mafunzo nchini.








Share:

Friday, 27 March 2026

SERIKALI YA TANZANIA YASAINI MAKUBALIANO YA UFADHILI WA SAMIA SCHOLARSHIP NA CHUO KIKUU CHA LIMERICK


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Limerick cha nchini Ireland wamesaini hati ya makubaliano ya utekelezaji wa ufadhili wa Samia Scholarship Extended, utakaowawezesha wanafunzi 32 kusoma katika chuo hicho.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo Machi 26, 2026 jijini Dar es Salaam, yakishuhudiwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda pamoja na ujumbe kutoka ubalozi wa Ireland nchini na viongozi wa chuo hicho.

Akizungumza katika hafla hiyo, Profesa Mkenda amesema ufadhili huo ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha elimu kwa kuandaa wataalamu wa sayansi na teknolojia watakaoendana na mahitaji ya dunia ya sasa.

Amesema ushirikiano huo umefanyika wakati muafaka ambapo Tanzania inaendelea kujenga uchumi unaotegemea maarifa na ubunifu, huku ukilenga kuwawezesha vijana kupata elimu bora, uzoefu wa kimataifa na ujuzi wa kisasa.

Aidha, chuo hicho kimetoa punguzo la ada kwa asilimia 50 kwa wanafunzi watakaojiunga kupitia mpango huo.

Profesa Mkenda alibainisha kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mpango wa Samia Scholarship katika fani za Sayansi ya Data, Akili Unde (AI) na taaluma zinazohusiana, ikiwa ni mkakati wa kuwajengea vijana uwezo katika teknolojia mpya.

“Tayari tumewapeleka wanafunzi 34 nchini Ireland, ambapo 32 wanasoma katika Chuo Kikuu cha Limerick na wawili katika Chuo cha Cork,” amesema.

Ameongeza kuwa wanafunzi hao ni sehemu ya ufadhili wa wanafunzi 50 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita, huku wengine 16 wakiwa tayari wamejiunga na vyuo vikuu nchini Afrika Kusini.

Kwa upande wake, Balozi wa Ireland nchini, Nicola Brennan, amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu bora ili kukidhi mahitaji ya ajira kwa idadi kubwa ya vijana inayotarajiwa kuongezeka kufikia mwaka 2050.

Amesema Tanzania ina rasilimali watu yenye nguvu na mazingira ya utulivu yanayowezesha maendeleo, lakini uwekezaji mkubwa katika elimu ni muhimu ili kuendana na ongezeko la watu.

Naye Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Limerick, Colin Fitzpatrick, amesema chuo hicho kinajikita katika mafunzo ya vitendo na kuwapatia wanafunzi uzoefu kupitia ushirikiano na kampuni kubwa za kimataifa.

Amesema hatua hiyo itawasaidia wanafunzi kutoka Tanzania kupata ujuzi wa nadharia na vitendo katika mazingira halisi ya kazi, hasa katika sekta ya teknolojia inayokua kwa kasi duniani.
Share:

Thursday, 26 March 2026

ALIKUWA AKIONEKANA KAMA TAKATAKA MBELE YA WANAWAKE, SASA HIVI ANADUNDA NA MKE MREMBO!


Naitwa Ramadhani, kijana ambaye kwa miaka mingi nimekuwa nikifanya kazi ya utingo wa malori hapa jijini Tanga. Licha ya kuwa ni kazi halali na ya jasho langu, niliishi maisha ya kunyanyasika sana upande wa mahusiano.

Kwa zaidi ya miaka kumi na miwili, nimekuwa nikitafuta mwanamke wa kutulia naye na kuanzisha familia, lakini kila niliyemfuata alikuwa ananitazama kwa dharau na kuniambia mimi siyo “level” yake.

Share:

Wednesday, 25 March 2026

MREMBO ALIYEFUNGWA KUTOOLEWA AANIKA SIRI YA KUPATA MUME WA KIZUNGU

Maisha ya hapa mjini Dar es Salaam yana mambo mengi, lakini kwa upande wangu, yalikuwa ni mfululizo wa maumivu na masikitiko. Jina langu ni Neema, mkazi wa Tabata. Kwa miaka zaidi ya kumi, nilikuwa mwanamke wa kuonja na kuachwa. Kila mwanaume aliyekuja kwangu alikuwa akiahidi ndoa, lakini baada ya muda mfupi, walikuwa wakitokomea kama moshi.

Nilijaribu kila mbinu; nilijiremba, nilivaa vizuri, na hata kutumia gharama kubwa kutafuta mvuto, lakini wapi! Nilikua nikishuhudia wadogo zangu na rafiki zangu wakiolewa, huku mimi nikibaki kuwa mpambe wa maharusi (bridesmaid) kila kukicha.

Share:

TIB HOSTS EADB DELEGATION, EYES EXPANDED PARTNERSHIP


By Staff Writer

The Tanzania Development Bank (TIB) has welcomed the new Country Manager of the East African Development Bank (EADB), Ms. Angela Muga, on an official visit aimed at strengthening cooperation between development finance institutions in the East African region.

The visit underscored the commitment of both institutions to fostering sustainable economic growth, sharing experiences, and promoting regional integration.

During her visit, Ms. Muga was accompanied by a delegation from EADB, led by Mr. Stephen Wambura, the EADB Resident Manager for Tanzania. The delegation took the opportunity to visit Pipes Industries, a key beneficiary of joint financing from TIB and EADB. Located in the Vingunguti Industrial Area in Dar es Salaam, Pipes Industries is a leading manufacturer of plastic pipes and other plastic products essential for infrastructure development.

Pipes Industries received a loan of approximately TSh 28.65 billion, which has significantly contributed to expanding its production capacity and enhancing its operations. This financing has enabled the company to increase the production of vital plastic products, including pipes crucial for water supply infrastructure in urban and rural areas. The investment has yielded important development outcomes, including job creation for Tanzanians, increased government revenue through taxes, and improved access to water infrastructure equipment.

The project aligns with Tanzania's broader strategy of industrial development, aimed at boosting domestic production and reducing dependency on imported goods. By supporting industries like Pipes Industries, TIB continues to play a pivotal role in strengthening the private sector and enhancing economic resilience.
Speaking during the visit, TIB's Chief Executive Officer, Mr. Deogratius Kwiyukwa, emphasized the importance of collaboration between regional development finance institutions in mobilizing long-term capital for transformative projects. "It is a great pleasure to officially welcome Ms. Angela Muga, the new Resident Manager of EADB Kenya, to our offices. Our partnership spans over 10 years, during which TIB, through EADB, has financed projects worth over TSh 80 billion across various sectors, including agriculture, health, education, industry, mining, and tourism," Kwiyukwa said.

He added, "Through this collaboration, over TSh 28 billion has been invested in the expansion project of Pipes Industries co Ltd in Vingunguti, Dar es Salaam, resulting in increased production of plastic products like water pipes, job creation for young men and women, and the growth of the industrial sector in Tanzania."

Ms. Angela Muga, EADB's Country Manager, highlighted the significance of cooperation among development finance institutions.

"Collaboration among DFIs is crucial for unlocking large-scale capital for regional transformation. By pooling our resources, we can accelerate industrial growth, strengthen regional integration, and deliver sustainable outcomes for East Africa," she said.

She further noted that the partnership between TIB and EADB exemplifies the growing trend of development finance institutions working together to mobilize long-term capital for impactful projects in Tanzania and the broader East African region.

The collaboration between TIB and EADB underscores the growing role of regional financial institutions in driving economic development. By providing patient, long-term capital, these institutions are building value chains that continue to yield positive outcomes long after the financing period ends.

TIB is a government-owned development bank focused on catalyzing domestic investment, particularly in priority sectors such as infrastructure, agriculture, industry, mining, tourism, and small and medium enterprises (SMEs). The bank also plays a key role in managing development funds and supporting project preparation to unlock investments that drive sustainable economic growth in Tanzania.

EADB, established in 1967, is a regional development bank owned by Kenya, Uganda, Tanzania, and Rwanda, along with other development and commercial financial institutions. Its mandate is to promote sustainable socio-economic development and regional integration in East Africa by providing financial and related services to companies in its member states.

The visit concluded with both parties reaffirming their commitment to deepening their partnership and exploring new avenues for collaboration in support of Tanzania's development agenda.

Share:

Tuesday, 24 March 2026

DENI LILOMSUMBUA MFANYABIASHARA KWA MIEZI TISA LILIISHA GHAFLA BAADA YA TUKIO LA AJABU LILILOBADILISHA HATIMA YAKE!





Kuna deni linalokunyima usingizi. Unaamka nalo. Unalala nalo. Kila simu ikiita moyo unashtuka ukidhani ni mkopeshaji. Hivyo ndivyo maisha yalivyokuwa kwa Samuel, mfanyabiashara wa vipuri vya magari kutoka Industrial Area, ambaye alijikuta akizama katika deni la zaidi ya laki saba baada ya biashara kuyumba ghafla.

Samuel alikuwa amechukua mkopo kupanua duka lake. Mambo yalikuwa mazuri mwanzoni. Lakini ushindani uliongezeka, wateja wakapungua, na mzigo wa marejesho ukaanza kumlemea. Kila mwisho wa mwezi ulikuwa vita.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger