Saturday, 11 October 2025

SHUWASA YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, WANANCHI WAIPONGEZA KWA HUDUMA BORA


Na Michael Abel.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kufanya hafla maalum katika ofisi zake, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wafanyakazi wake na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi. 

Hafla hiyo imefanyika leo Ijumaa Oktoba 10 2025, katika ofisi za SHUWASA Shinyanga Mjini na kuudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ambapo mali na mengi yaliyofanyika, mfanyakazi bora amezawadiwa zawadi kwa kujituma na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na ubunifu.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amewataka watumishi wa SHUWASA kuendelea kutoa huduma zenye ubora na kuwaheshimu wateja, akisisitiza kuwa serikali inatambua umuhimu wa huduma bora kama nguzo ya maendeleo na ustawi wa wananchi, na kuwa mamlaka za maji zinapaswa kuwa mfano wa nidhamu, uwajibikaji na ubunifu katika kuhudumia jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopora, amewapongeza wafanyakazi wote kwa kujituma katika kazi na kutoa huduma bora, huku akiwashukuru wananchi kwa kuendelea kuiamini mamlaka hiyo. Amesema SHUWASA itaendelea kuboresha miundombinu na mifumo ya utoaji huduma ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa wakati wote.

Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wameipongeza SHUWASA kwa huduma bora na utayari wa kushughulikia changamoto kwa haraka, Wamesema mamlaka hiyo imekuwa mfano wa uwajibikaji na imechangia kuboresha maisha ya wakazi wengi kupitia upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi wa mazingira, hali inayoongeza imani kwa wananchi kuendelea kushirikiana nayo.

<<<TAZAMA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI>>>









Share:

Friday, 10 October 2025

MR. BLACK NA UONGOZI WAKE WAFANYA ZIARA YA KIDIPLOMASIA NCHINI RWANDA


Mr. Black akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Gallus Kambanga katika ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda
Mr. Black akiingia katika Bunge Tukufu la Rwanda kwa shughuli maalumu

Kigali, Rwanda – 9 Oktoba 2025

Peter A. Frank Lugumi, anayejulikana pia kama Mr. Black, ambaye ni Mkurugenzi wa The BSL Investment Company Limited pamoja na BSL Schools Tanzania na Rwanda, na pia ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi kwenda Vijana (CCM Shinyanga Mjini), ameendelea na ziara yake ya kidiplomasia na uongozi nchini Rwanda.

Ziara hii inafuatia matembezi yake katika Ikulu ya Uganda tarehe 8 Oktoba 2025, ambapo leo Oktoba 9, 2025, amepata fursa ya kutembelea Bunge Tukufu la Rwanda kwa lengo la kuimarisha mahusiano na kuitangaza zaidi Tanzania kidiplomasia.

Katika hatua nyingine, Mr. Black amepokelewa rasmi katika Ubalozi wa Tanzania nchini Rwanda, ambako amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mhe. Dkt. Habib Gallus Kambanga, pamoja na Afisa Uwekezaji wa Ubalozi huo, Ndugu Mosses E. Mosses.

Mazungumzo yao yamejikita katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, elimu na uwekezaji kati ya Tanzania na Rwanda.

Vilevile, Mr. Black amepata nafasi ya kufanya mazungumzo na viongozi wa Bodi ya Uwekezaji ya Rwanda (RDB), hatua ambayo imezaa mafanikio kadhaa katika kukuza fursa za biashara na uwekezaji kwa nchi zote mbili.

Akiwa nchini Rwanda, Mr. Black ametembelea pia maeneo mbalimbali ya kihistoria kwa lengo la kukuza na kuendeleza historia ya Afrika Mashariki, pamoja na kuhamasisha utalii ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kupitia muendelezo wa ziara hii, Mr. Black ameendelea kuwasisitiza vijana wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kulinda amani, kuheshimu historia ya mataifa yetu, na kuendeleza mshikamano wa kikanda.
Share:

Thursday, 9 October 2025

MAGANGA ATEMBELEA BANDA LA OFISI YA WAZIRI MKUU KWENYE MAONESHO YA WIKI YA VIJANA MBEYA





Na Mwandishi wetu, Mbeya

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bi. Mary Maganga, ametembelea mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, ikiwemo banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Uhindini jijini Mbeya, leo tarehe 9 Oktoba 2025.

Maadhimisho haya yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.”



Share:

MRADI WA EACOP WANYANYUA UCHUMI WA TAIFA

Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) umewezesha kukua kwa uchumi haswa katika mikoa ambayo imepitiwa na bomba hilo.

Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhe. Balozi Ombeni Sefue.

“Mradi huu umekua na manufaa makubwa katika nchi yetu kwanza tumeona mradi umelipa fidia nzuri hii ikijumuisha nyumba, viwango vizuri vya pesa, chakula na elimu ya kilimo na ufugaji pamoja na pembejeo”, amesema Mhe. Balozi.

Mhe. Sefue amefafanua zaidi kuwa kwa sasa maisha ya wananchi yameimarika na wanaendesha shughuli zao za kilimo na ufugaji kwa ufanisi zaidi.

Aidha Mhe. Balozi amebainisha kuwa pamoja na ustawi wa uchumi, mradi umefanikiwa kuweza kufuata misingi bora ya utunzaji wa mazingira na kwa sasa ni moja ya miradi bora duniani katika utunzaji wa mazingira.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Batilda Burian amethibitisha mchango mkubwa unaofanywa na EACOP katika kujenga uchumi na ustawi wa mkoa wa Tanga.

“Sisi Kama Mkoa wa Tanga kwanza tunashukuru sana na kupongeza serikali yetu kwa kuwezesha mradi kuwa nchini lakini unionize TPDC kwa usimamizi bora wa mradi kwakweli mradi umeijenga Tanga”, ameeleza Mkuu wa Mkoa.

Mhe. Batilda amefafanua kuwa moja ya sehemu ambayo imekua kwa kasi kutokana na mradi huu ni ukuaji wa Shughuli za Bandari ambapo kwa sasa tunapokea Mel zaidi ya 50 kwa mwezi.

Mhe. Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa kwa sasa mradi unashirikiana na TANESCO Ili kuweza kusambaza umeme kwenye vijiji ambavyo havina umeme katika maeneo yaliyopitiwa na bomba hilo.

Aidha katika masuala uwajibikaji wa Jami ‘CSR’ mradi unatarajia kujenga kituo bora cha afya ili kuboresha huduma za afya kwenye mkoa wa Tanga.

Baada ya kumalizia kikao na Mkuu wa Mkoa wa Tanga walipata wasaa wa kutembelea shughuli za ujenzi wa mradi katika eneo la mto Sigi ambapo bomba linapitishwa zaidi ya mita 15 chini ya sakafu ya mto kwa kutumia teknolojia ya HDD.

Pamoja na ujenzi wa bomba katika Mkoa wa Tanga, mradi unajenga matenki ya kuhifadhia mafuta, kituo kituo kikuu pamoja na ghati.

Share:

KAULI YA ZITTO KABWE KWENDA KULETA MABADILIKO KUPITIA SANDUKU LA KURA YAUNGWA MKONO!

Na Mwandishi wetu
Kumekuwa na maoni tofauti Mtandaoni, mengi yakiunga mkono kauli ya  mmoja wa viongozi wa upinzani Zitto Kabwe ya kuwataka watanzania kupuuza wanaotoa wito wa kutopiga kura Oktoba 29.

Katika klipu ya moja ya hotuba zake katika kampeni akiwa Songea, Zitto anatoa wito wa wananchi kuwafikiria wanaohimiza kutopiga kura kama watu wenye walakini ingawa wengine anawaheshimu.

 Zitto Kabwe  anayetokea ACT Wazalendo na mgombea ubunge Kigoma, alisisitiza watu kutoka kwenda kupiga kura kwani kutofanya hivyo ni kama kununuliwa na chama tawala kukiacha kifanye kinavyotaka.

Zitto anasema watu wanaohimiza wengine wasishiriki katika kupiga kura wana walakini vichwani mwao kutokana na umuhimu wa zoezi hili.

Kauli ya Zitto inachagiza ukweli kuwa kura si tu haki, bali ni mamlaka ya kuajiri viongozi wa nchi. Kauli ya Zitto imelenga kuwaamsha Watanzania wachanga kutokubali kupuuzia mchakato huu. 

Umuhimu wa uchaguzi unasisitizwa kwa data za vitendo kwani taifa linatakiwa kuendelea kusonga mbele kijamii na kiuchumi kutoka katika msingi uliowekwa.

Serikali  ya sasa imewekeza mabilioni ya shilingi katika miundombinu ya kisasa kama vile Mabasi ya Mwendokasi (BRT), ujenzi wa Hospitali mpya 50 za wilaya, na upanuzi wa vituo vya afya.

Kwenda kupiga kura Oktoba 29 ni fursa ya kuajiri Msimamizi: Kura inakupa wewe uwezo wa kuhoji na kuchagua viongozi watakaoweza kulinda na kusimamia urithi huu wa Taifa, na kuhakikisha huduma bora za afya, elimu, na usafiri zinasonga mbele.

Aidha ni fursa ya Kudai Uwajibikaji: Vijana wanahimizwa kuhoji wagombea kwa kutumia sanduku la kura kuhusu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakiwa miongoni mwa wanajamii.

Matusi na uharibifu wa mali za umma (kama vile mabasi ya BRT na vizimamoto) hauna nafasi katika siasa ya karne ya 21. Kura yako ni ya ustaarabu na ndiyo njia pekee ya kulinda urithi wa Taifa.

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI OKTOBA 9,2025


Magazeti






Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger