Friday 28 June 2024
TBS KANDA YA KUSINI YATEKETA TANI 3.5 ZA BIDHAA HAFIFU
Video Mpya : TOTO KHAN x SLYVEPO - POMBE
Thursday 27 June 2024
ORYX GAS, VIGOR GROUP WAZINDUA BOHARI YA KUHIFADHI NISHATI YA GESI ZANZIBAR
TANZANIA YASHINDA TUZO YA UBUNIFU KOREA KUSINI
Na Mwandishi wetu, Korea
Tanzania yashinda Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Ubunifu bora katika huduma za umma kupitia mfumo wa e-Mrejesho.
Tuzo za Umoja wa Mataifa za Ubunifu katika Huduma za Umma 'UN Public Service Innovation Awards' zimetolewa leo Juni 26 mwaka huu, nchini Korea Kusini kwenye Kilele cha Wiki ya Huduma kwa Umma ya Umoja wa Mataifa 'UN Public Service Week'.
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 72 zimeshiriki ambapo mifumo 400 iliwasilishwa na mifumo 15 ilishindinda tuzo ukiwemo wa e-Mrejesho.
Kutoka Afrika nchi zilizoshiriki na kushinda tuzo hizo ni Tanzania na Afrika Kusini pekee.
Wiki ya Huduma kwa Umma ya Umoja wa Mataifa ni tukio la kila mwaka linaloadhimishwa kimataifa, kwa lengo la kusherehekea thamani na umuhimu wa huduma ya umma kwa jamii.
Tukio hili linasisitiza kutambua mchango wa watumishi wa umma na kuhamasisha vijana kuchagua kazi katika sekta ya umma.
Wiki hii kwa kawaida hujumuisha matukio, sherehe za tuzo, na majadiliano kuhusu jinsi ya kuboresha ufanisi wa utoaji huduma kwa umma duniani kote.
Mfumo wa e-Mrejesho unawawezesha wananchi kutuma kero au malalamiko, maoni, maswali, na pongezi kidijiti kwenda katika taasisi yoyote ya umma na kisha kupata mrejesho wa utekelezaji wake kidijiti mahali walipo.
Mfumo huu umetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Mfumo wa e-Mrejesho unapatikana kwa njia tatu ambazo ni kupitia simu ya mkononi kwa kubofya *152*00# na kisha kuchagua namba 9 na kisha namba 2, njia zingine ni kupitia simu janja kwa kupakua Aplikesheni tumizi (Mobile App) ya e-Mrejesho inayopatikana kwenye Play Store na Apple Apps Store, na kwa njia ya Tovuti ya e-mrejesho.gov.go.tz.
RAIS DKT. SAMIA ANAGUSWA NA KUJALI MAISHA YA WAFANYAKAZI
*Amenyanyua kikokotoo, Ndejembi asema huo ni mwanzo tu
Nukuu za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi- Bungeni
"Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo tunaenda kuipitisha inaonyesha ni namna gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaguswa na maisha ya wafanyakazi wa nchi hii. Tangu aingie madarakani mwaka wake wa kwanza alipandisha madaraja yaliyokwama kwa miaka mingi, wafanyakazi waliokuwa hawajapandishwa maradaja kwa miaka Tisa (09), alipandisha zaidi ya watumishi 222,000" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Mheshimiwa Rais aliguswa sana na madeni kwa watumishi wa Umma, alitoa fedha kwaajili ya kulipa madeni hayo ya watumishi" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Julai 2022 kuna mabadiriko ya Kikokotoo yalifanyika, waliokuwa watumishi wa Umma walitoka kulipwa mkupuo wa Asilimia 50 na kushuka Asilimia 33. Waliokuwa Asilimia 25 walipanda kwenda Asilimia 33. Ilikuwa ni kilio kwa watumishi ambao mishahara yao ni ya chini na husubiria mkupuo wa fedha hizi kuanza maisha yao wanapokuwa wamestaafu" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Wizara ya Fedha mwaka wa fedha 2024/2025 wameweka Shilingi Bilioni 155 kwaajili ya kulipa Kikokotoo kunyanyua kutoka Asilimia 33 kwa waliokuwa Asilimia 50 kabla ya Julai 2022 kwenda Asilimia 40. Waliokuwa Asilimia 25 wamekwenda Asilimia 35" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Wabunge wengi mmezungumzia suala la kuangalia kiwango kiendelee kunyanyuka kurejea kilipokuwa Asilimia 50. Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri wameshukuru Asilimia 40 lakini wanaomba iweze kurudi Asilimia 50. Huu ni mwanzo mzuri ndiyo maana Asilimia 7 imewekwa" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Serikali itazidi kuangalia ni namna gani itarudi katika Asilimia 50 ya Kikokotoo. Wanaoenda kulipwa siyo tu wanaokwenda kustaafu kuanzia 01 Julai, 2024. Wanaenda kulipwa wote hata wale waliostaafu kuanzia Julai 2022" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Watumishi 17,068 toka Julai 2022 wanaenda kulipwa mapunjo yao ya Asilimia 7 waliyostahili kupata. Waliokuwa wanapata Asilimia 33 kwenda Asilimia 35 watalipwa mapunjo yao ya Asilimia 2. Tunatarajia kuona wengi wakija kudai mapunjo ya mafao yao" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi