Wednesday, 28 February 2024
WAFANYAKAZI WA BARRICK BULYANHULU NA NORTH MARA WALIVYOSHIRIKI KILIMANJARO MARATHON 2024
WADAU SEKTA YA AFYA WAKABIDHI VITENDEA KAZI VYA THAMANI YA MILIONI 800 KWA SERIKALI
`
Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea vitendea kazi vyenye thamani ya Milioni 800 kutoka kwa wadau wa CDC kupitia THPS kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI na Kifua Kikuu katika Mkoa wa Tanga.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amepokea vitendea kazi hivyo leo Februari 23, 2024 Mkoani Tanga ambavyo ni pikipiki 50, friji 72, Centrifuges 56, Compyuta 50, UPS 50 na printa 50 ambavyo vitendea kazi hivyo vitaimarisha huduma za Afya katika Mkoa huo.
Aidha, wakati akipokea vitendea kazi hivyo Waziri Ummy amewataka wote watakaokabidhiwa vifaa hivyo kuvitumia Kama ilivyo elekezwa ikiwa ni pamoja na kuwafikia wateja wanaoishi katika mazingira magumu na mbali na vituo vya kutolea huduma za Afya ili kuwafikishia huduma.
“Lakini pia tunaamini kwamba mtaongeza idadi ya huduma mkoba ‘outreach services’, kuwafikia wateja walio katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa ugonjwa wa UKIMWI na kuwapatia huduma za kinga zikiwemo kinga dawa na kusafirisha sampuli kwa ajili ya kupima wingi wa Virusi vya UKIMWI.” Amesema Waziri Ummy
Pia, amewataka kutunza vifaa hivyo na kunifanyia matengenezo ya mara kwa mara ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kutimiza lengo la kudhiiti UKIMWI na VVU ambapo ametoa onyo kwa yeyote atakae fanya kinyume na maelekezo hayo kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Pia, Waziri Ummy ameyataka mashirika yote ya kiraiya yanayofanya kazi katika Sekta ya Afya kuzingatia ya ( katika fedha zote wanazozipata angalau watenge kiasi kisichopungua asilimia 10 kwa ajili ya ya kuajiri watumishi wa Afya katika vituo vya kutoa huduma za Afya ngazi ya msingi
“Tunaposema kupambana na masualaya ya UKIMWI lakini kuna upungufu wa wauguzi, hakuna madaktari, hakuna watu wa maabara, hakuna wafamasia, angalau ajiri wauguzi wawili na watumishi wengine wa mikataba.” Amesema Waziri Ummy
AIBU! MAMA MKWE HADI ANASHAURI NITUMIE NJIA GANI YA UZAZI WA MPANGO!
Jina langu ni Happy kutokea Tabora nchini Tanzania, ni mama wa watoto wawili kwa sasa, mwaka 2018 niliolewa na kijana ambaye kila jambo ilikuwa ni lazima amshirikishe mama yake.
Sikua na shida na hilo jambo, ingawa ukaribu wao ulikua kidogo umezidi kusema kweli, hata kabla ya kuanza naye mahusiano kumbe mama yake alinitathmini kwanza ndio akampa ruhusa ya kuanzisha hayo mahusiano.
Nilikuja kuambiwa baadae kuwa ndio kawaida yake, nilishangaa sana kwa sababu ndio ilikuwa mara ya kwanza kuona jambo hilo ingawa niliwahi kusikia kuwa kuna mambo kama hayo.
Yaani ilikua hata tukikubaliana jambo, ikitokea tu mama yake akatoa mawazo ya tofauti basi makubaliano yetu yote yalikuwa yanatupiliwa mbali.
Kilichonishtua sana ni pale alipokataa nitumie kipandikizi kwa sababu mama yake amemuambia sio njia sahihi. Hili halikuniingia akilini kabisa kwa sababu sisi kama wanandoa, haya ni maamuzi ya faragha inakuwaje anamshirikisha mama yake?.
Mwisho wa siku nilichoka, nikamueleza jirani yangu Mama Mage kuhusu tabia hiyo, akaniambia dawa ya huyo mama mkwe wangu ni ndogo tu, akanipatia namba za Kiwanga Doctors (+254 769 404965) na kuniambia atanisaidia.
Niliwasiliana na Kiwanga Doctors na kumueleza changamoto hiyo ya kifamilia, basi alinifanyizia dawa yake na tangu wakati huo ukawa ndio mwisho wa mama mkwe kuingilia ndoa yetu.
Kuna siku nilipata habari za chini chini kuwa mama mkwe anasema kwa sasa nimemshika vibaya mtoto wake kiasi kwamba hamshirikishi tena mambo yetu kama ilivyokuwa mwanzo, hapo nikajua kuwa dawa ya Kiwanga Doctors imefanya kazi yake.
Siku zote kumbuka Kiwanga Doctors anatoa huduma kama kusafisha nyota, kusuluhisha migororo ya ndoa, mahusiano, mapenzi na familia, kumfunga mume au mke asitoke nje ya ndoa, anatoa tiba kwa wanaotafuta watoto.
Vilevile anatoa huduma ya kukusaidia kupata kazi au ajira, kupandishwa cheo na mshahara kazini, kuwasaidia wenye urahibu wa dawa za kulevya, sigara na pombe, kwa wanaotafuta mume au mke pia anawasaidia tena ndani ya siku chache.
Anatibu magonjwa kama kisukari, msukumo wa damu (BP), upungufu wa nguvu za kiume, miguu kuwaka moto n.k, pia anaweza kuisadia biashara yako kunawiri, na huduma zote hizi unaweza kuzipata bila kufika ofisini kwake.
Basi chukua hatua ya kuwasiliana na Kiwanga Doctors kwa namba; +254 769 404965.
Mwisho.
Tuesday, 27 February 2024
DK. NCHIMBI AMJULIA HALI MWENYEKITI ALAT TAIFA
KIWANDA CHA ELSEWEDY PELEKENI SOKO LA EAC, SADC NA AFCFTA
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme pamoja na transfoma cha Elsewedy alipofanya ziara katika Kiwanda hicho kilichoko eneo la Kisarawe 11, Kigamboni Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zao
.....
Serikali imekishauri Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme pamoja na transfoma cha Elsewedy kuhakikisha inapeleka bidhaa zake katika masoko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na hata katika Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) ili kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameyasema hayo alipofanya ziara katika Kiwanda hicho kilichoko eneo la Kisarawe 11, Kigamboni Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zao
Alisema kiwanda hicho kilifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kinazalisha bidhaa mahsusi kwa ajili ya kwenda nchi za Kenya, Rwanda, Afrika Kusini na hata Demokrasia ya Kongo jambo ambalo lina mafanikio makubwa kwa Watanzania.
“Mmeanza kwa nchi tatu tuu bado kuna ziada, ukifika Burundi wanaendelea kujenga sana nchi yao, tushirikiane tufikie hata soko la Uganda tupeleke bidhaa zetu kwa pamoja,” alisema Dkt Kijaji.
Alisema katika kufanikisha hiko Wizara yake iko tayari kushirikiana na kiwanda hicho ili kukiwezesha kuuza bidhaa zake katika masoko hayo kwa kufuata vigezo vilivyopo na kutumia fursa zilizopo ipasavyo katika nchi zote 54 za Afrika.
Vilevile Dkt Kijaji amesema milango iko wazi kwa wawekezaji wengine wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza nchini katika fursa mbalimbali za kuongeza uzalishaji kwenye viwanda na kwamba kama zipo changamoto zibadilishwe kuwa fursa ili kufanya kazi na kuendelea kutengeneza ajira Aidha amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira bora ya biashara kwa kuondoa vipingamizi vya biashara kwa kiwango kikubwa na vilivyobakia vinaendelea kufanyiwa kazi .
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Elsewedy kwa EAC,Ibrahim Qamar alisema kiwanda hicho kilichoajiri vijana wa kitanzania zaidi ya 200 kilianzishwa ili kuifanya Tanznaia kuwa kitovu cha uzalishaji wa bidhaa hizo kwa afrika mashariki na Afrika kwa ujuml alakini pia hata kupenya katika masoko mbalimbali duniani.
Naye Mtaalamu wa Logistiki kiwandani hapo Ishaka Ridhwan amesema amefanikiwa kufikisha bidhaa katika nchi za Kenya, Rwanda Burundi na tayari kwa Kenya wamepeleka zaidi bidhaa za gharama ya dola za Kimarekani 10,000 kwa mwaka 2023.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme pamoja na transfoma cha Elsewedy alipofanya ziara katika Kiwanda hicho kilichoko eneo la Kisarawe 11, Kigamboni Dar es Salaam kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kusikiliza changamoto zao