Friday, 12 January 2024
Thursday, 11 January 2024
WATU WATATU WAFARIKI KWA KUSOMBWA NA MAJI MOROGORO
Watu watatu wa Familia moja Mtaa wa Lukuyu Kata ya Bigwa Manispaa ya Morogoro wamefariki kwa kusombwa na maji wakati wakijaribu kujiokoa baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi pembezoni mwa Mto Mgolole kuzingirwa maji usiku wa kuamkia Januari 10 kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo.
Jeshi la Zimamoto na Ukoaji Mkoa wa Morogoro limeongoza wananchi katika zoezi la uopoaji wa miili ya watu watatu waliofariki kwa kusombwa na maji ambapo miili miwili tayari imekwisha opolewa akiwemo Asnati Thomas (6) na Theresia Adolfu (73) ambao miili yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro Shababi Marugujo amethibitisha taarifa ya vifo hivyo, amesema wamefanikiwa kuopoa miili miwili na jitihada bado zinafanyika kuopoa mwili wa Mwanahamisi Issa (35) ambaye ni Mama wa Familia ambao haujapatikana.
Katika tukio hilo, Sengo Hamis (47) ambaye ni Baba wa Familia hiyo amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake wakati akijaribu kujiokoa na sasa anaendela na matibabu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
SERIKALI YAKUTANA NA TAASISI ZA KIFEDHA KWA NIA YA KUWASAIDIA WAFANYABIASHARA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO HANANG’
NA; MWANDISHI WETU – HANANG’
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), kupitia Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu pamoja na Uongozi wa Mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ imekutana wa wakilishi wa Taasisi za Kifedha pamoja na Mabenki Wilayani humo kupitia kikao kazi chenye lengo la kuwasaidia wafanyabiashara walioathirika na Mafuriko ya Maporomoko ya tope, miti na mawe yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana .
Akiongea katika kikao hicho kilichofanyika leo 10 Januari 2024, Bw. Condrad Millinga, Mkurugenzi wa Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu alisema , Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alitoa wito kwa sekta ya Umma na Serikali kushirikiana na kuona namna gani wafanyabiashara walioathirika na mafuriko yale wanaweza kukwamuliwa kiuchumi na kuendesha Maisha yao kama walivyokuw a wakiendesha hapo awali.
“Pamoja na kwamba Serikali katika ngazi ya Wilaya ilisha kaa na kulifanyia kazi suala hili, Tumekutana hapa na wadau wa Mabenki na Taasisi za kifedha kuona namna tunavyoweza kuishirikisha sekta binafsi kwa mapana yake katika kazi ya kitaifa ikiwa ni utekelezaji wa Agizo la Mhe. Rais, na Tunaamini kabisa kwamba mwananchi mfanyabiashara kwa hatua aliyokuwa amefika anaweza kuwa ameyumba kwa namna moja ama nyingine maana asilimia kubwa wamekuwa na mikopo,sasa ni wakati wa kuona namna gani tunaweza kumtoa mwananchi pale alipo na kumsaidia kusonga mbele.” Alisema Bw. Millinga.
Akiongea katika kikao kazi hicho, Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi. Beng’i Issa Alisema Lengo la kukutana na Watoa huduma za kifedha ambao wamekuwa wakifanya Biashara na wananchi wa Hanang’ ni kuwa na lengo la kusaidia wafanyabiashara walioathirika baada ya kufanya tathmini ya awali na kuwasikia watoa huduma hao kwa upande wao wanaweza kushirkiana vip na Serikali katia suala hilo.
Awali akifungua kikao kazi hicho Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi Maryam Ahmed Muhaji alisema, Baada ya Maafa yale kutokea wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa Hanang’ walipata madhara makubwa, Serikali ilifanya jitihada za kukaa na wafanyabiashara wa taasisi za kifedha ambazo wengi wao wamewapatia mikopo kwa lengo la kufanya biashara na kufanya marejesho.
Hivyo kwa kuwa wafanyabiashara hao wameathirika na maafa hayo “Tumeona tukae sasa kwa pamoja tuone namna gani swala hilo linaweza kufanyiwa kazi bila kuumiza pande zote mbili.” Alisisitiza.
Sambamba na Hilo, Serikali Tasisi za Kifedha na wafanyabiashara wa Hanang’ Watakaa pamoja Tarehe 11 Januari kuona namna ambavyo Suala hili linavyoweza kufanyiwa kazi.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji Kichumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Condrad Millinga akizungumza katika kikao kazi cha Serikali na Wadau kutoka Taasisi za Kifedha kilichofanyika 10 Januari 2024 Wilayani Hanang’.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bi Maryam Ahmed Muhaji akizungumza wakati wa kikao kazi cha Serikali na Wadau kutoka Taasisi za Kifedha kilichofanyika 10 Januari 2024 Wilayani Hanang’, kushoto ni Bi Beng’I Issa Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi.
Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) katika kikao kazi cha Serikali na Wadau kutoka Taasisi za Kifedha kilichofanyika 10 Januari 2024 Wilayani Hanang’.
Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) katika kikao kazi cha Serikali na Wadau kutoka Taasisi za Kifedha kilichofanyika 10 Januari 2024 Wilayani Hanang’.
Baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi za kifedha katika katika kikao kazi cha Serikali na Wadau kutoka Taasisi za Kifedha kilichofanyika 10 Januari 2024 Wilayani Hanang’.
Wednesday, 10 January 2024
CMSA YATINGA ZANZIBAR KUTOA ELIMU YA UWEKEZAJI
CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI CHATEMBELEA KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED