Tuesday, 15 August 2023

HAWA NDIYO WASHINDI PROMOSHENI YA VUNA ZAIDI NA MERIDIANBET


Hatimaye ile promosheni kubwa Zaidi ya Vuna zaidi na Meridianbet iliyozinduliwa Agosti 2 mwaka 2023 imeanza kutoa washindi, wiki hii simu zimetoka sana pale Meridianbet.

 

Kwa ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya simu hapa nchini Airtel inayotoa huduma ya miamala ya simu maarufu kama Airtel Money, Meridianbet inatoa zawadi ya simu janja na Bodaboda kwa wateja watakaoongeza salio kwenye akaunti zao kupitia Airtel Money.

 

Zaidi ya washindi 5 wamefanikiwa kujipatia smartphone mpya aina ya Samsung A32, kwa kuongeza salio tu kwenye akaunti zao ili wabashiri soka kwa odds kubwa, au kucheza sloti na michezo ya kasino ya mtandaoni.

 

Mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao, moja ya washindi kutoka Tegeta Jijini Dar Es Salaam alifunguka kuhusu Meridianbet.

 

“Niliongeza salio kwenyeakaunti yangu ya Meridianbet nikiwa na wazo la kubeti kwa sababu ligi zimeanza, mara baada ya hapo Nilipokea ujumbe wa maandishi kuwa nimejishindia simu, nilifurahi sana na niliamini kweli Meridianbet hawana janja janja”-Mshindi kutoka Tegeta

 

Kwa upande wa mshindi wa pili yeye alibainisha kwamba ni kawaida uake kubeti Meridianbet kwakuwa wanatoa odds kubwa na machaguo mengi, ,moja kati ya chaguo lake bora Zaidi ni Turbo/Cash out kwa sababu humpata nafasi ya kuokoa dau lake pindi anapoona mkeka wake unakaribia kuchanika.

 

Ukiachana na zawadi hizi za simu janja kuna zawadi kubwa itatoka Agosti 25, 2023 zawadi ya Bodaboda mpyaa!! Nafasi ni yako kuibuka mshindi wa chombo hii. Ongeza salio kwenye akaunti yako ya Meridianbet mara kwa mara kupitia Airtel Money kujiweka kwenye nafasi kubwa ya kushinda Pikipiki.

 

BETI

 

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.



Share:

RAIS SAMIA AZINDUA JENGO LA SAFINA DODOMA





Na Dotto Kwilasa, DODOMA 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dk.Samia Suluhu Hassan amezindua jengo la kitega uchumi la Kanisa la Angikana Central Dodoma (DCT) lililopewa jina la Safina House huku akiweka msimamo wake Katika kuimarisha amani na utulivu nchini.

Amesema Kutokana na utulivu uliopo,kamwe Taifa halitayumbishwa dhidi ya watu wasio itakia mema Tanzania na kutumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri amani, umoja na mshikamano.


Akizindua jengo hilo la kitegauchumi Leo Agosti 15,2023 jijini hapa, DK.Samia amesema,"Niwasihi viongozi wote wa dini nchini kuendelea kuliweka Taifa letu  katika mikono salama ya mwenyezi mungu ili lidumu katika umoja, amani na mshikamano. Kamwe tusikubali kuyumbishwa na mtu yoyote yule asiyelitakia Taifa mema,”anasisitiza


Amesema serikali  inatambua mchango wa taasisi za kidini nchini ambapo zimekuwa zikisaidia katika kutoa huduma za kijamii  kwa wananchi ikiwemo elimu, kilimo na Afya.


Amefafanua kuwa Kabisa Angrikani ni kanisa kongwe zaidi duniani,na kwamba tangu kuingia kwake nchini limekuwa likitoa huduma kwa wananchi kwani shule nyingi zilijengwa ikiwemo shule ya msingi Mvumi,Mazengo na shule ya sekondari ya Msalato.


“Nimefurahi kusikia kuwa mnajihusisha na na kutoa mafunzo ya kilimo hasa Dodoma ambapo kuna ukame lengo ni kuhakikisha watu wanakuwa na chakula cha kutosha na salama kama ilvyonukuliwa katika kitabu cha zaburi ya 15;16,”


Aliongeza kuwa :“Suala la kilimo ni jukumu mlilobeba na ndio nguzo kuu ya serikali ndio maana tunatekeleza mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) lengo ni kuhamasisha vijana kuingia katika kilimo, uvuvi na ufugaji.”


Katika hatua nyingine Dk.Samia alieleza kuwa  serikali itaendelea kuenzi mchango wa kanisa la Anglikana pamoja na kudumisha umoja na mshikamano na kuifikisha Tanzania pale inapotakiwa.


“Muendelee kuwaimiza watanzania  kufanya kazi kwa bidii na kuchangamkia fursa zilizopo Dodoma kwa ninyi ni mashaidi mtaona jiji hili linavyobadilika siku hadi siku  na mwakani tutaitana wana pamoja  kuelezana yote yaliyofanyika,”alifafanua


Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT) Dk.Dickson Chilongani  alimpogeza Rais Dk.Samia kwa  kushiriki tukio hilo kwani  ujio wake unaonyesha kuwa yeye ni kiongozi wa Dini zote.


Alisema hiyo  sio mara ya kwanza kushiriki Rais Dk.Samia kushiriki katika matukio kama hayo.


“Sisi tunaendelea kukupongeza Rais Dk.Samia  kwa uongozi wako  mahili wako na kazi unazoendelea kuzifanya kwa maendeleo ya wananchi.Tangu umepokea kijiti hujayumba wala kuteteleka kwani miradi yote ya kimkakati iaendelea ikiwemo ujenzi wa bwawa la mwalimu nyeerere.


Ameongeza kuwa :”Miradi mingine ambayo inaendelea kutekelezwa ni ujenzi wa reli ya kisasa, barabara ya mzunguko, kukamilika kwa mji wa serikali, ujezi wa ikulu chamwio a ujenzi wa vituo vya afya a shule katika kila koa ya Tanzania hivyo uchumi kuendelea kukua.Tuamuomba mungu akujalie ili utuvushe hapa tulipo  utupeleka katika Tanzania mpya.


Dk.Chilongani amesema  DCT inaundwa na wilaya tatu za Dodoma ikiwemo Chamwino, Bahi na Mpwapwa ambapo kwa sasa  ina jumla ya waumini 700,000 na wachungaji 300  ambapo kati ya wachungaji hao 65 ni wanawake ambao wamehitimu ngazi mbalimbali za elimu.


 “Naishukuru serikali yako kwa kuendelea kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo vitabu, walimu na chakula ambapo Hadi sasa DCT imefanikiwa kusomesha vijaa 7,000  wa shule za msigi a sekodari amapo wapo katika hatua mbalimbali za maendeleo.


Akizungumzia kuhusu jengo hilo Dk.Chilonga amesema  ujenzi wake ulianza  mwaka 2017 ambapo hadi kukamilika kwa jengo hilo wametumia sh.bilioni nane  ambapo kati ya hizo sh.bilioni mbili ni msaada kutoka kwa rafiki kutoka Newyork.


Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Angrikana Tanzania Dk.Maimbo Mndolwa alisema kanisa hilo limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na serikali.


“Leo umechukua nafasi ya kipekee kuungana nasi.kanisa linafanya kazi za kimaendeleo na kijamii  na tunafanya kazi na makundi mbalimbali ya watu wenye changamoto.”


Ameongeza kuwa :”Kanisa linaendelea  kuiombea serikali kwasababu hata Rais Dk.Samia anapigwa maneno mengi lakini watu hao ndio wa kwanza kula matunda ambayo yanatokana na uongozi wa serikali yake.

Share:

TGNP WAFANYA ZIARA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO NDANI NA NJE YA KISHAPU


Vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyangan vikiwa kwenye picha ya pamoja na kibao cha SIDO,Agosti 13,2023 wakiwa kwenye ziara na TGNP.

Na Halima Khoya,Kishapu

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umefanya ziara ya kutembelea miradi iliyo hai Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga mara baada ya kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vituo vya taarifa na maarifa Wilayani humo ili kujifunza mbinu na kuelewa namna ya kuendesha miradi mbali mbali.

Zoezi hilo limefanyika Agosti 13,2023 ambapo walitembelea miradi mbali mbali nje na ndani ya Wilaya hiyo na kubaini fursa na maendeleo makubwa ya kiuchumi yatokanayo na udhubutu wa baadhi ya wajasiriamali.

Akizungumza baada ya kutamatisha ziara hiyo,Frida Saidi amesema wanaishukuru (TGNP) kwa kuwapa mwangaza kwenye ujasiriamali wao kwa kuwakutanisha na wataalamu kutoka Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) na wajasiriamali wenye miradi.

“Tumeanza kujifunza kwa nadharia,vile vile tumepata nafasi ya kutembezwa kwenye miradi mbalimbali,tumepata ujuzi wa kuendesha miradi na biashara shughuli zetu,ytunaamini mwanamke akiwezeshwa anaweza,tunaishukuru sana TGNP kwa kutuwezesha kiujuzi wanawake”amesema Frida.

Nae mmiliki wa mradi wa kufuga kuku Wilaya ya Kishapu,Edina Kaluta amesema ameweza kuuendeleza mradi wake kwa kuthubutu baada ya kupatiwa mafunzi kutoka kwenye shirika la Grown women linaloshirikiana na TGNP 2021 lililokuwa likitoa elimu ya jinsia,haki na usawa na mwanamke na uongozi sambamba na kufanya kongamano la siku tano.

“Mwanamke anayetaka kujikita na ufugaji wa kuku,ninawakaribisha sana na nitatoa elimu niliyonayo kwa wenye uhitaji na uthubutu,TGNP imenisidia sana hadi kufikia hapa ninafuga kuku Zaidi ya 700 wa kisasa na wakienyeji” amesema Kaluta.
Vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyangan wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi,wakiwa kwenye Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Mkoani humo (SIDO) agosti 13,2023.
Vituo vya taarifa na maarifa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyangan wakiendelea na ziara ya kutembelea miradi,wakiwa kwenye mradi wa kuku agosti 13,2023.
Share:

PINATA LOCA SAKA UBINGWA MERIDIANBET!!

 

Unapoizungumzia nchi ya Mexico kwa haraka haraka kichwani mwako inakuja taswira ya aina gani kuhusu nchi hii, bila shaka watu wengi wanafikiria historia ya Pablo Escobar mwanaume aliyetikisa sana ulimwengu kwa shughuli yake ya biashara ya madawa ya kulevya. Meridianbet inakuletea sura mpya ya nchi ya Mexico kupitia kasino ya mtandaoni.

 

Hii ni nchi inayosifika kwa kuwa na aina ya watu wenye juhudi kubwa ya kufanya kazi na kujituma bila kukata tamaa, ukichukua sifa ya watu hawa ukaihamishia Meridianbet unakuwa kwenye nafasi kubwa ya kuwa tajiri.

 

Meridianbet kama kawaida imekuja na mchezo mpya wa kasino ya mtandaoni, huu sasa unaaambiwa unatema hela kama mashine za ATM.

 

Kutoka kwa watengenezaji wa michezo ya kasino ya mtandaoni, Expanse wamekuja na game hii ya casino inaitwa Pinata Loca.

 

Studios za Expance zina mchezo mpya ambao utaupenda! Sloti ya pinata loca inakuongoza kwenda Mexico!

Kusanya alama za Ushindi kama pinatata, sombrero, tequila, cactus na jaribu kukusanya haraka baada ya alama zilizotawanyika kuonekana zikiwa na machaguo yatakayokuvutia zaidi!

 

Mchezo huu wa kasino ya mtandaoni unaruhusu kuanza na dau dogo kabisa huku ukipata mizunguko na bonasi kibao, lakini pia malipo ya mchezo huu yanafanyika kulia na kushoto.

 

Safari yako ya Mexico! Spawn, Sombrero yenye utajiri inakusubiri hapa Meridianbet!

CHEZA HAPA

 

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.

 

 


Share:

PEPFAR YAJIVUNIA MIAKA 20 KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU KWA WATOTO, WANAUME WENGI KUFANYIWA TOHARA



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wakati Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) ukitimiza miaka 20 tangu uanzishwe mnamo mwaka 2003, mafanikio makubwa yameelezwa kufikiwa nchini Tanzania ikiwemo watoto wengi kuzaliwa bila Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI lakini pia maambukizi kupungua kufuatia wanaume kupata huduma ya tohara kinga.


Akizungumza Jumatatu Agosti 14,2023 na Waandishi wa Habari wanaofanya ziara Mkoani Mara kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 20 ya PEPFAR, Mratibu wa PEPFAR nchini Tanzania Bi. Jessica Greene amesema mapambano dhidi ya UKIMWI yamekuwa na matokeo chanya kwa kupunguza maambukizi hususani kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.


“Tunapotimiza miaka 20 ya PEPFAR nchini Tanzania tunajivunia kuwa na matokeo chanya kwa watoto. Wakati tunaanza mpango wa PEPFAR ,kwa watoto wengi walikuwa wanaambukizwa Virusi vya UKIMWI kupitia mama zao wenye maambukizi ya VVU, na sasa hii ni dunia tofauti maana kuna watoto wengi wanaozaliwa bila kuwa na maambukizi kutokana na huduma ambazo mama zao wanazipata kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua”,amesema Greene.
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene

“Sasa hivi watoto wengi wanaishi maisha wakiwa wenye afya njema na tunaelekea kwenye kizazi kisichokuwa na maambukizi ya UKIMWI ,haya ni mafanikio makubwa sana tuliyofikia tangu Serikali ya Marekani na Serikali ya Tanzania ilianzisha Mpango wa PEPFAR mnamo mwaka 2003 baada ya Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kutangaza Mpango wa Dharura wa Kukabiliana na UKIMWI”,ameeleza Bi. Greene.

Amefafanua kuwa PEPFAR kupitia Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na wadau mbalimbali wakiwemo Amref Health Africa Tanzania wamekuwa wakitekeleza afua mbalimbali za afya kama vile kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lakini pia kutoa bure huduma ya tohara ya kitabibu kwa wanaume.

“Serikali ya Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa misaada ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania, ikiwa imewekeza zaidi ya dola bilioni 6.6 kumaliza janga la VVU. Tuna ubia na makampuni ya madawa na wabia wenye wigo mkubwa wa usambazaji ili kukuza upatikanaji wa ARV. PEPFAR inafadhiliwa moja kwa moja kutoka serikali ya Marekani kisha ufadhili huo unapelekwa kwa mashirika watendaji manne nchini Tanzania ambavyo ni USAID, Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa CDC, Walter Reed, Idara ya Ulinzi na Peace Corp.Tumejitahidi kutanua kazi zetu kwenye vituo vya afya”,ameongeza Bi. Greene.


“PEPFAR ilipoanza kazi nchini Tanzania, kulikuwa na watu wasiozidi 1,000 waliokuwa kwenye matibabu. Leo PEPFAR inasaidia zaidi ya watu milioni 1.5 kwenye matibabu ya ARV ya kuokoa maisha. Mwisho wa VVU/UKIMWI kama tishio la afya ya umma ifikapo 2030 ni lengo kubwa linaloweza kufikiwa”,amesema Bi. Greene.


Amesema Serikali ya Marekani inajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania kufikia malengo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Kupambana na Ukimwi Duniani (UNAIDS) 95/95/95 (95% ya watu wanaoishi na VVU wanajua hali zao, 95% ya waliogundulika wako kwenye matibabu, 95% ya wanaopata matibabu virusi vitakuwa vimefubazwa ifikapo 2025.
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (The U.S. Center for Disease Control -CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination amesema huduma za tohara kinga wanazozitoa bure kwa wavulana na wanaume Mkoani Mara ili kuzuia maambukizi ya VVU kwa asilimia 60 zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi ya VVU kwenye migodi na makambi ya Wavuvi.


“Tumekuwa tukitoa huduma za tohara kinga bure kwa wanaume kwenye vituo vya afya lakini kwa kuwafuata wananchi kwenye maeneo yao kupitia huduma ya Mkoba ambapo huwa tunapeleka huduma ya tohara katika jamii mfano kwenye migodi na makambi ya wavuvi. Huduma ya tohara inafanya vizuri Mara licha ya changamoto ya mila”,ameeleza bw. Swamination.


Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Murangi kilichopo katika halmashauri ya Musoma, Dkt. Anceth Elias amesema kituo hicho kimekuwa kikitoa huduma za tohara kwa wanaume ikiwemo kupeleka huduma za tohara kwa wavuvi na wachimbaji wa madini ambapo mwitikio ni mzuri kwani tangu walipoanzisha huduma ya tohara kinga bure mwaka 2018 wanaume 35,539 wamepatiwa huduma ya tohara na wameendelea kujitokeza kupata huduma
Muuguzi na Mtoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi halmashauri ya Musoma, Bi. Fasines Mwashitete.

“Mafanikio haya makubwa yanatokana na msaada mkubwa kutoka PEPFAR, tumekuwa tukitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa tohara na mwitikio ni mzuri, wanaume watu wazima ambao hawakupata tohara wanajitokeza kwa wingi, tunawapa huduma ya tohara salama kabis tofauti na ile ya kimila ambayo ina madhara mengi ikiwemo kuvuja damu nyingi, maumivu makali na hatari ya kupata maambukizi ya VVU kwa sababu vifaa vinavyotumika kwenye tohara ya kimila siyo salama”,ameongeza Bi. Fasines Mwashitete na Musa Makele ambao ni wauguzi na watoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi.


Naye Stephano Maphuru ambaye ni mnufaika wa huduma ya tohara anayetoa elimu ya umuhimu wa tohara amewaomba wanaume ambao hawajafanyiwa tohara kujitokeza kupata huduma hiyo ili kujikinga na maambukizi ya VVU kwa asilimia 60.
Gari maalumu lenye huduma zote za Tohara Kinga kwa wanaume.

Mkuu wa Afua za UKIMWI kutoka CDC Tanzania, Dkt. Edward Machage na Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Musoma Lameck Andrea Magori wamesema Maambukizi ya VVU kwa mjamzito na mama anayenyonyesha yanaweza kutokea wakati wowote (mtoto anapokuwa tumboni, wakati wa kujifungua au unyonyeshaji) hivyo ni muhimu kufanya vipimo vya marudio ili kujua hali yake na kumkinga mtoto asipate maambukizi.


Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Chitare iliyopo kata ya Makojo Halmashauri ya Musoma, Neema Mshama na Muuguzi Mkunga wa zahanati hiyo, Hamis Zuberi wameishukuru PEPFAR kwa kuwapatia mafunzo kuhusu vipimo vya marudio kwa kwa akina mama ambapo kwa kipindi cha mwaka 2005- 2023 wamefanikiwa kuokoa watoto wawili wasipate maambukizi ya VVU baada ya kufanya vipimo vya marudio na kubaini mama zao wamepata maambukizi.


Mmoja wa akina mama walionufaika na huduma za PEPFAR Mariam Wambura (jina siyo halisi) mkazi wa kata ya Makojo Halmashauri ya wilaya ya Musoma ameishukuru PEPFAR kwa huduma inazotoa hali iliyochangia aendelee kuwa na afya njema licha ya kuwa na maambukizi ya VVU lakini pia kujifungua mtoto ambaye hana maambukizi ya VVU.
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI - The U.S. President’s Emergency Plan for AIDS Relief (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR Agosti 14,2023 katika kituo cha Afya Murangi Halmashauri ya Wilaya ya Musoma Mkoani Mara. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR 
Mratibu wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) nchini Tanzania Bi. Jessica Greene akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR 
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR 
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR 
Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani (CDC) nchini Tanzania Bw. Mahesh Swamination akielezea mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha miaka 20 tangu kuanzishwa kwa PEPFAR 
Mkuu wa Afua za UKIMWI kutoka CDC Tanzania, Dkt. Edward Machage akielezea umuhimu wa vipimo vya marudio kwa akina mama katika Hudhurio la kwanza la kliniki (atakapogundua tu ni mjamzito), Ujauzito ukiwa na wiki 32 hadi 36 (miezi 8 hadi 9 ya ujauzito), Miezi 3 baada ya kujifungua, wakati wa kunyonyesha na Miezi 6 baada ya kujifungua, wakati wa kunyonyesha.
Waandishi wa habari wakiwa katika kituo cha afya Murangi Halmashauri ya Wilaya ya Musoma
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya Murangi kilichopo katika halmashauri ya Musoma, Dkt. Anceth Elias akielezea huduma wanazotoa ili kukabiliana na maambukizi ya VVU
Muuguzi na Mtoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi halmashauri ya Musoma, Musa Makele  akielezea huduma za tohara kinga kwa wanaume
Muuguzi na Mtoa huduma za tohara katika kituo cha afya Murangi halmashauri ya Musoma, Bi. Fasines Mwashitete akielezea huduma za tohara kinga kwa wanaume
Mnufaika wa huduma ya tohara Stephano Maphuru akihamashisha wanaume kupata huduma ya tohara kinga
Gari maalumu lenye huduma zote za Tohara Kinga kwa wanaume likiwa katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma ambapo huduma za tohara zinatolewa bure kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaokelezwa na Shirika la Amref Health Africa kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR
Gari maalumu lenye huduma zote za Tohara Kinga kwa wanaume likiwa katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma ambapo huduma za tohara zinatolewa bure kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaokelezwa na Shirika la Amref Health Africa kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR
Huduma za Upimaji VVU na tohara zikiendelea katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma 
Vijana wa kiume wakipata elimu ya Tohara kinga katika uwanja wa shule ya Msingi Kigera kata ya Kigera Manispaa ya Musoma ambapo huduma za tohara zinatolewa bure kupitia Mradi wa Afya Kamilifu unaokelezwa na Shirika la Amref Health Africa kupitia CDC kwa ufadhili wa PEPFAR
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Musoma Lameck Andrea Magori akielezea juhudi mbalimbali zinazofanyika kukabiliana na maambukizi ya VVU ndani ya miaka 20 ya PEPFAR 
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Halmashauri ya wilaya ya Musoma Lameck Andrea Magori akielezea juhudi mbalimbali zinazofanyika kukabiliana na maambukizi ya VVU ndani ya miaka 20 ya PEPFAR 
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Chitare iliyopo kata ya Makojo Halmashauri ya Musoma, Neema Mshama akielezea huduma zinazotolewa na PEPFAR ikiwemo vipimo vya marudio kwa mjamzito na mama anayenyonyesha
Mmoja wa akina mama walionufaika na huduma za PEPFAR Mariam Wambura (jina siyo halisi) mkazi wa kata ya Makojo Halmashauri ya wilaya ya Musoma akielezea jinsi alimwepusha mtoto wake kupata maambukizi ya VVU kupitia huduma za PEPFAR
Muuguzi Msaidizi wa Zahanati ya Chitare iliyopo kata ya Makojo Halmashauri ya Musoma, Hamis Zuberi akielezea huduma zinazotolewa na PEPFAR.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog




Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 15,2023






Share:

Monday, 14 August 2023

KASINO YA DICE DICE DICE MZUKA WAKE USIPIME

Dice Dice Dice ni mchezo wa kisasa wa kasino ya mtandaoni Meridianbet uliotengenezwa na Red Tiger. Katika mchezo huu unapata bonasi kibao. Alama za jokeri zinakupa ushindi mara mbili zaidi, na wakati wa Bonasi ya Kuzungusha Upya/Respin, nyaraka za kuzidisha kubwa zaidi zinakusubiri.

 

Sifa za Kasino ya Mtandaoni Hii.

 

Dice Dice Dice ni kasino ya mtandaoni yenye gridi ya safu tatu na nguzo tano na ina mistari 10 ya malipo iliyowekwa. Ili kupata ushindi, lazima uunganishe alama tatu au zaidi zinazolingana kwenye mstari wa malipo.

 

Katika kasino ya mtandaoni hii malipo hufanyika kwenye nguzo ya kwanza kutoka kushoto na kulia.

 

Kwenye mstari wa malipo mmoja, unaweza kupata ushindi mmoja tu. Ikiwa una mchanganyiko wa ushindi zaidi ya mmoja kwenye mstari wa malipo mmoja, utalipwa mchanganyiko wenye thamani kubwa zaidi.

 

Inawezekana kuongeza ushindi kwenye kasino ya mtandaoni kwa kuunganisha kwenye mistari ya malipo zaidi.

 

Ndani ya sehemu ya "Salio," kuna mishale vya kuongeza na kupunguza ambavyo vinakusaidia kuweka thamani ya dau kwa kila kuzungusha.

 

Pia kuna chaguo la kucheza Automatic unaloweza kuchagua wakati wowote. Kupitia chaguo hili, unaweza kuweka hadi mizunguko 100 itakayochezwa moja kwa moja. Kabla ya kuanza kuwezesha chaguo la Automatic, unapaswa kuweka kikomo cha hasara unachoweza kuvumilia.

 

Ikiwa unapenda mchezo wa kasino ya mtandaoni wenye kasi kubwa, unaweza kuchagua "Kuzungusha Haraka" kwa kubofya eneo la "Turbo." Unaweza pia kurekebisha mpangilio wa sauti katika kona ya juu upande wa kulia.

 

Linapokuja suala la alama kwenye mchezo huu, alama zinazolipa kidogo ni pamoja na alama za matunda: cherry, ndimu, na plamu.

Alama yenye thamani kubwa kati ya alama za matunda ni tikiti maji. Alama tano za tikiti maji kwenye mchanganyiko wa ushindi zitakuletea mara nne ya dau lako.

 

Kisha kuna alama ya kengele ya dhahabu ambayo pia ni ya kawaida kwenye inafaa za kawaida. Ukishikiza alama tano za kengele hizi kwenye mchanganyiko wa ushindi, utashinda mara saba ya dau lako.

 

Moja ya alama zenye thamani kubwa zaidi kwenye mchezo ni alama ya almasi. Ukishikiza alama tano za almasi kwenye mchanganyiko wa ushindi, utashinda mara kumi ya dau lako.

 

CHEZA DICE

 

Alama inayolipa ushindi mkubwa zaidi katika mchezo huu wa kasino ya mtandaoni ya Meridianbet, ni alama nyekundu ya 7. Ukipata alama tano za 7 katika mchanganyiko wa ushindi, utashinda mara kumi na tano ya dau lako. Tumia nafasi hii na upate ushindi mkubwa. Bonasi za Mchezo

 

Alama ya jokeri inawakilishwa na kete. Inachukua nafasi ya alama zote za mchezo na inasaidia kuunda mchanganyiko wa ushindi.

 

Jokeri hutokea tu kwenye nguzo ya tatu, na mara nyingi inaweza kujaza nguzo nzima.

 

Unapopata jokeri kwenye mchanganyiko wa ushindi, kete itaanza kuzunguka. Namba ambayo kete itasimama itatumika kuzidisha ushindi wako.

Bonasi ya "Kuzungusha Upya" unaipata katika mchezo huu.

 

Baada ya hapo, mchezo utapata kete ya kuzidisha ambayo inaanza na x1. Kila jokeri inayopatikana kwenye nguzo pia itapata kete ya kuzidisha. Kwa kila mzunguko wakati wa Bonasi ya kuzungusha upya ya jokeri huongezwa pamoja.

 

Usikose burudani nzuri, cheza kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ya Dice Dice Dice!

 

 

NB: Ukijisajili Meridianbet unapewa bonasi ya mizunguko ya bure kucheza michezo ya kasino ya mtandaoni. Jisajili na Cheza.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger