Thursday, 10 August 2023

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAPONGEZWA KWA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YA MIGONGANO BAINA YA BINADAMU NA WANYAMAPORI

Na  John I. Bera  
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Taasisi zake za Uhifadhi zilizopo ndani ya mikoa ya kusini pamoja na halmashauri za wilaya kwa jitihada zake kubwa za kupambana na changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori.


Ametoa pongezi hizo Agosti 10, 2023 wakati akifungua warsha ya utambulisho wa mradi wa kutatua changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori katika Ukanda wa Ruvuma Mkoa wa Lindi katika Wilaya ya Liwale na Ruvuma Wilaya za Namtumbo na Tunduru.


"Migongano hii inahatarisha maisha ya wananchi na mali zao na usalama wa chakula kwa mfano kwa mwaka mmoja pekee 2022/ 2023 wanyamapori wakali na waharibifu wamesababisha uharibifu wa takriban jumla ya ekari 1,0724.05 za mazao mbalimbali." amesema.


Aidha, amesema Serikali ina matarajio makubwa na mradi huo ambao mara utakapoanza kutekelezwa utasaidia kupunguza au kumaliza changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori katika mikoa na wilaya husika.


"Hivyo, ni matumaini yetu kuwa mradi huu utawezesha mambo ya msingi ambayo yatatatua changamoto hii ikiwemo vitendea kazi na matumizi ya teknolojia katika kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu", ameongeza.


Wakati huo huo, Kanali Laban ametumia fursa hiyo kutoa shukrani zake kwa Shirika la Ujerumani (GIZ) kwa kukubali kuleta mradi huu katika ukanda wa Ruvuma.

"Mradi huu umekuja wakati muafaka kutokana na ongezeko la matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo hayo. Nafahamu kuwa mradi huu utatekelezwa katika wilaya za Namtumbo, Tunduru na Liwale lakini niwaombe tuweke mpango mahsusi wa baadaye ili kupeleka mafanikio yatakayopatikana kutokana na Mradi huu kwenye mikoa na wilaya nyingine zenye changamoto hii", amesema.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Bi. Antonia Raphael amesema ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ujerumani katika kutekeleza Mradi huo ni muendelezo wa jitihada za Serikali katika utatuzi wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori katika maeo mbalimbali nchini.


Vilevile, amesema Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii itahakikisha kuwa Mradi huo unatekelezwa kikamilifu ili kuepusha madhara kwa wananchi na mali zao kutokana na migongano baina ya binadamu na wanyamapori hususan katika Mikoa ya Ruvuma na Lindi.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Programu hiyo kutoka Shirika la GIZ, Bw. Jens Bruggemann amesema, wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutatua changamoto hiyo ili kuhakikisha wananchi wa mikoa hiyo wanakuwa na mtazamo chanya juu ya wanyamapori na sio kero katika maisha yao.


Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano na Shirika la GIZ kutoka Ujerumani imekuja na mradi huo utakao saidia kutatua changamoto ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori utakao tekelezwa katika mikoa ya Lindi na Ruvuma.

Mradi huo ni matunda ya ushirikiano kati ya Serikali ya Ujerumani na Serikali ya Tanzania ambao utatekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Shirika la GIZ la Ujerumani kwa kuhusisha Taasisi za TAWA, TFS TANAPA, TAWIRI, mikoa na wilaya husika pamoja na wadau wengine wa Uhifadhi.
Share:

MCHUNGAJI MTATA ATANGAZA MAJI YA UPAKO WA UTAJIRI.. "UNAKUNYWA AU KUOGA UNAPATA GARI"


Mhubiri maarufu nchini Kenya Victor Kanyari sasa anasema amepata dawa ya kukabiliana na umaskini.

Mchungaji huyo wa kanisa la Salvation Healing Ministry alinaswa kwenye video akizungumzia kuhusu maji maalum ambayo alidai yakitumiwa humfanya mtu kuwa tajiri, akiunga mkono hadithi yake na andiko la Biblia.

Alisema alipata gari la KSh 15 milioni na mengine mengi kutokana na maji. Mhubiri huyo alidai zaidi kwamba alimsaidia mjakazi ambaye alitii shauri lake la kuoga kwa maji mahsusi na kupata utajiri mara moja.

"Unapooga na hii na huna pesa mara moja inaanza kuja. Ninakuambia kuwa nimebarikiwa. Gari hili ni KSh 15 milioni, na ninazo nyingi. Kuna mwanamke mmoja ambaye alifanya kazi ya ujakazi. Nilimpa maji haya akaoga nayo akaacha kazi na kununulia gari atatupa ushuhuda,” alisema.

Kanyari wa umaarufu wa "mbegu ya 310 " anayehusishwa na sarakasi za kimiujiza alijenga bwawa kanisani mwake kuwaponya waumini.

Hivi majuzi aliweka bomba na bwawa la maji ndani ya kanisa lake. Katika video nyingine isiyo na tarehe iliyowaacha watu mitandoani wakiwa wameduwaa, kasisi huyo alifichua kuwa kisima hicho kitaitwa Bethsaida. 

Kanyari anayejulikana kwa tabia zake zisizo za kawaida, alionekana akimshauri mmoja wa wafuasi wake kunywa na kuoga kwa maji hayo. Kulingana naye, maji hayo yana uponyaji na miujiza yenye uwezo wa kutatua shida za watu zote.

"Nawa mikono, unaweza hata kuoga kisimani ukipenda. Kunywa kidogo pia. Sasa matatizo yako yamekwisha," alimwambia msichana mmoja.
Share:

TEA KUTUMIA BILIONI 8 MIRADI YA ELIMU MWAKA WA FEDHA 2023/24


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Bi Bahati Geuzye akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma

******************

Mamlaka ya Elimu Tanzania imepanga kutumia kiasi cha Sh. Bilioni 8 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini ili kusaidia upatikanaji wa elimu bora kwa usawa nchini..

Akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari, Agosti 10, 2022 katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO jijini Dodoma, Mkurugenzi MKuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye amesema kiasi hicho cha fedha kitatumika kufadhili miradi 82 katika shule 81 zikiwemo shule 48 za msingi na 33 za sekondari katika maeneo mbali mbali ya Tanzania Bara.

Ametaja miradi itakayofadhiliwa kuwa ni ujenzi wa madarasa 82, matundu ya vyoo 336, mabweni 10, ujenzi wa maabara 18 za masomo ya sayansi na nyumba za walimu 32 na hivyo kuwanufaisha wanafunzi 39,484 na walimu 169 katika shule za msingi na sekondari.

Aidha katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 Mfuko wa Elimu wa Taifa utatoa ufadhili kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia katika taasisi moja ya elimu ya juu Tanzania – Zanzibar ambapo kiasi cha Sh. Milioni 300 zitatumika katika utekelezaji wake.

Mkurugenzi Mkuu wa TEA ametumia fursa hiyo kushukuru wadau wanaochangia Mfuko wa Elimu wa Taifa ambapo katika mwaka wa fedha wa 2022/23 miradi yenye thamani ya Sh. Milioni 404 ilifadhiliwa na wadau mbali mbali wa elimu

Wadau waliochangia ni pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), BRAC Maendeleo Tanzania, Taasisi ya Asilia Giving, Taasisi ya Flaviana Matata, Taasisi ya SAMAKIBA, CAMARA Education Tanzania na Kampuni za Sayari Safi na Dash Industries Ltd.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ni Taasisi ya Umma inayofanya kazi chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. TEA inaratibu Mfuko wa Elimu wa Taifa ambao unasaidia jitihada za Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa. Pia TEA inaratibu Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (SDF) unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Bi Bahati Geuzye akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma

Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi Bahati Geuzye katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO

Share:

NEC: AJIRA ZA WATENDAJI WA UCHAGUZI ZIZINGATIE SIFA NA UWEZO


Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mstaafu) Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakati akifunga mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi mkoani Morogoro leo tarehe 10 Agosti, 2023.
Sehemu ya wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wakimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati akifunga mafunzo hayo Mkoani Morogoro leo.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha Wasimamzi wa Uchaguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba ajira za watendaji wa uchaguzi zinazingatia sifa na uwezo.


Ukumbusho huo umefanywa na Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mstaafu) Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk mkoani Morogoro leo tarehe 10 Agosti, 2023 wakati akifunga mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi.


Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku tatu na kuhudhuriwa na washiriki 88 ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara.


“Tunayo imani kuwa mtateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hii muhimu, jambo hili limekuwa likisisitizwa tokea siku ya kwanza ya mafunzo kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni. Kazi ambayo inahitaji umahiri, umakini na weledi katika kuitekeleza,” amesema Jaji Mbarouk.


Amesisitiza juu ya kuhakikisha kwamba mafunzo kwa watendaji wa vituo vya kupigia kura yanafanywa kwa ufanisi ili wawe na uelewa na kuweza kufanya kazi zao kwa usahihi na kujiamini.


“Ni imani yetu kuwa mafunzo ya watendaji wa vituo yatafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo ili waweze kufahamu majukumu yao na kuyatekeleza ipasavyo wakati wa uchaguzi,” amesema Jaji Mbarouk.


Aidha, amewahimiza watendaji wa uchaguzi kutenga muda kujisomea ili kupata ufahamu wa sheria, kanuni na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


“Natumia nafasi hii kuendelea kuwasisitiza kuhusu umuhimu wa kutenga sehemu ya muda wenu kusoma Katiba, Sheria na Maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ili yawaongoze katika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki,” amesema.


Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara utafanyika tarehe 19 Septemba, 2023, wagombea watachukua fomu kuanzia tarehe 13 hadi 19 Agosti, 2023, siku ya uteuzi itakuwa tarehe 19 Agosti, 2023 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 20 Agosti, 2023 hadi tarehe 18 Septemba, 2023.


Kata zitakazofanya uchaguzi mdogo ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
Share:

HAKUNA MRADI UTAKA SIMAMA CHINI YA UONGOZI WA RAIS SAMIA - BITEKO

Na Mathias Canal, Geita

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Waziri wa Madini Mhe Dkt Doto Mashaka Biteko amewahakikishia Wananchi wa Mkoa Geita kuwa Miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano inaendelea kutekelezwa na hakuna mradi utakaosimama ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Biteko ameyasema hayo katika wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Geita na kufanyika katika Mtaa wa Kalangalala jimbo la Geita mjini uliowakutanisha wabunge wote wa mkoa huo kuelezea utekelezaji wa ilani ya CCM.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kauli mbiu ya Kazi iendelee amehakikisha Miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa katika kipindi cha Serikali ya awamu ya tano inaenndelea kutekelezwa na hakuna mradi uliosimama wala mradi utakaosimama” amesema Biteko

MNEC Biteko amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa ya kupeleka fedha nyingi za maendeleo kote nchini kuanzia ngazi ya kijiji mpaka miradi ya kitaifa kama Ujenzi wa reli ya SGR na bwawa la kuzalisha umeme la Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambayo yote inaendelea kutekelezwa.

“Nawaomba wananchi wote na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi tuendelee kumuunga mkono Rais na Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kumwaga fedha za maendeleo kote nchini na ana maono makubwa ya kufikisha nchi yetu mahala pazuri” Amesisitiza

Aidha, Biteko amewakumbusha Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuendelea kuisimamia serikali katika ngazi zote na kupaza sauti pale wanapoona watu wachache wanakwamisha utekelezaji wa Ilani ya CCM kupita miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.




Share:

HII DAWA IMEFANYA KILA MWANAMKE ANATAKA KUWA NAMI KIMAPENZI

Jina langu ni Kev, ni kijana wa miaka 24 kutokea Mathare, nimekuwa nikifanya kazi ya ujenzi maeneo mbalimbali hapa nchini Kenya na kweli nashukuru nimekuwa nikipata fedha nzuri.

Kwa sasa naendesha maisha yangu vizuri tu, nimefanikiwa kujenga na kuwekeza mradi mdogo wa kuuza mbao kwa ajili ya ujenzi maeneo ya mjini.

Licha ya umri wangu kuonekana kwenda, bado sijafanikiwa kuoa wala kuwa na mtoto katika maisha yangu, lakini ni kitu ambacho nilikitamani sana tangu nikiwa na umri wa miaka 22.

Tatizo langu kubwa lilikuwa ni kila mwanamke ninayemtongoza alikuwa akinikatalia licha ya kutoa ahadi ya maisha mazuri na fedha lakini bado hakuna aliyekuwa tayari kuwa na mimi.

Nilijaribu mbinu mbalimbali ili kuweza kufanikiwa katika hilo lakini sikuweza, niliwaomba hadi rafiki zangu waweze kunitongozea mwanamke wa kuwa naye lakini walikuwa wanakubali kwa hao rafiki zangu ila wakiniona wanakataa.

Siku moja niliona tangazo katika mtandao kuwa African Doctors anatoa tiba ya kuongeza mvuto wa mapenzi, nilichukua namba yake katika tangazo lile ambayo ni +254 769404965 na kuwasiliana naye.

African Doctors alinipatia dawa ya kuongeza mvuto ambayo nimeona inafanya kazi kweli kweli, wanawake zaidi ya wanne ambao nilikuwa nawasumbua kila mara kwenye simu kuwaomba wawe na mimi, wamenipigia simu na kuniomba niwe nao.

Hapa nilipo sasa nimepata kiwewe, nashindwa nimchukue mwanamke yupi na nimuache yupi maana wote ni wazuri sana na wote wananing'ang'ania sana. Je, nifanyaje?.

Kumbuka African Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.

Wasiliana na  African Doctors  kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com




au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.

 


Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI AUGOSTI 10,2023





































































Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger