Wednesday, 9 August 2023

JAMII NAMBA KUCHOCHEA UCHUMI WA KIDIJITALI ZANZIBAR


Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Mifumo na Huduma za TEHAMA (DISDS) Bw, Mohammed Mashaka wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, akizungumza wakati wa kikao kazi cha kutoa uelewa kwa wadau wa Zanzibar kuhusu Mradi wa Huduma Pamoja na uanzishwaji wa Mfumo wa Utambuzi wa Kidijitali kwa kutumia Jamii Namba leo Zanzibar tarehe 08/8/2023.
Mratibu wa Mradi Bw. Bakari Mwamgugu akizungumza wakati wa kikao kazi cha kutoa uelewa kwa wadau wa Zanzibar kuhusu Mradi wa Huduma Pamoja na uanzishwaji wa Mfumo wa Utambuzi wa Kidijitali kwa kutumia Jamii Namba leo Zanzibar tarehe 08/8/2023.


Na Mwandishi wetu -Zanzibar


Kwa kuzingatia umuhimu wa TEHAMA na lengo la serikali la kuwa na serikali mtandao, Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Mifumo na Huduma za TEHAMA (DISDS) Bw.Mohammed Mashaka amesema kuna hitajio kubwa la kuwatambua wale wote ambao wanapewa huduma ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na Teknolojia.


Kauli hiyo imetoleo leo August 8.2023 na Mkurugenzi huyo katika kikao kazi cha kutoa uelewa kwa wadau wa Zanzibar kuhusu Mradi wa Huduma Pamoja na uanzishwaji wa Mfumo wa Utambuzi wa Kidijitali kwa kutumia Jamii Namba ambapo amesema kuna haja ya kuwa na namba moja ya kumtambua anayepokea huduma za serikali.


Aidha,Bw. Mohammed amesema kwenye utoaji wa huduma kwa wananchi hakuna mipaka,hivyo serikali inatoa huduma na sekta binafsi zinatoa HUDUMA lengo ni kuhakikisha tunawatambua wale wote ambao wanapokea huduma na italeta urahisi katika kuwatambua.


"Mwananchi anayetokea Magu Bara kule anakuja Chakechake Pemba anataka huduma za serikali, lazima aweze kutambulika maana sisi tupo ndani ya mpaka wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". amesema Bw. Mohammed.

Kwa upande wake Mratibu wa Mradi wa Tanzania ya Kidijitali, Bw.Bakari Mwamgugu ametaja faida za Mfumo wa Utambuzi wa Kidijitali kwa kutumia Jamii Namba ni pamoja na kuhifadhi taarifa mbalimbali za kijamii ikiwemo Ardhi,Afya pamoja shuleni.

"Mfano mtoto anapozaliwa lazma awe na hiyo Namba jamii ambayo itamsaidia akiwa anafanya taratibu za Afya atatumia namba hiyo,na anapo sajiliwa shule mpaka chuo huko atatumia namba hiyo mpaka kifo chake". Amesema Bw. Bakari.


Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Unguja, pamoja na Taasisi zake Zanzibar wanaendelea na kikao kazi cha kutoa uelewa kwa wadau wa Zanzibar kuhusu Mradi wa Huduma Pamoja na uanzishwaji wa Mfumo wa Utambuzi wa Kidijitali kwa kutumia Jamii Namba.
Matukio ya picha ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Unguja, pamoja na Taasisi zake Zanzibar kwenye kikao kazi cha kutoa uelewa kwa wadau wa Zanzibar kuhusu Mradi wa Huduma Pamoja na uanzishwaji wa Mfumo wa Utambuzi wa Kidijitali kwa kutumia Jamii Namba leo tarehe, 08/8/2023.
Share:

WAKULIMA WAIMWAGIA SIFA BENKI YA CRDB MBELE YA RAIS SAMIA


Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo mafupi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa Benki ya CRDB, Ndugu Maregesi Shaaban alipotembelea Banda la Benki ya CRDB katika kilele cha maadhimisho ya Nanenane yaliyofanyika kitaifa Jijini Mbeya. Wakishuhudia ni Spika wa Mbunge Mh. Dkt. Tulia Ackson na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Ndungu Fredrick Nshekanabo.
BAADHI ya wakukima mkoani Mbeya wameishukuru Benki ya CRDB mbele ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa imewasaidia kupata mikopo ya fedha na nyenzo ikiwemo trekta aina ya Power Tiller, kuwa vitawasaidia kuinua kilimo na kupata kipato.


Mmoja wa wakulima hao kutoka Wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya Halima Ally, ametoa ushuhuda huo leo mbele ya Rais Dkt. Samia alipotembelea Banda la Benki ya CRDB kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nane Nane) yaliyofanyika kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.


"Sisi wakulima wa Mbarali tunaishukuru Benki ya CRDB kwa kutuwezesha kupata mikopo ya fedha na zana za kufanyia kazi kama ilivyotukopesha Power Tiller. Kwa kupata Power Tiller hii itaniwezesha kuendeleza kilimo changu cha mpunga na mahindi" alisema Ally.
Wakulima zaidi ya 600 kutoka Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wanatarajiwa kukopeshwa na Benki ya CRDB trekta, power tiller, zana za kuvunia, fEdha za mikopo ya kulimia na pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu, mbolea na madawa, na mikopo ya Stakabadhi Ghalani.


Rais Dkt. Samia, aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuweza kukopesha wakulima kwa riba ya asilimia tisa, huku akiitaka benki hiyo kuendelea kufuatilia l zana za kilimo wanazowakopeaha wakulima ili ziendelee kufanya kazi, na ikibidi kuwasaidia kutengeneza pindi zinapoharibika, kwani baadhi yao zana hizo zikiharibika, wanazitelekeza.


"Nawapongeza CRDB kwa kuweza kutoa mikopo ya riba ya asilimia tisa. Itawasaidia wakulima kuweza kukopa kwa wingi na kulima kwa tija.


"Na mikopo ya Power Tiller mnayotoa kwa wakulima muweze kuifuatlia na muwasaidie au kuweza kuwasaidiia waweze kutengeneza. Wakati mwingine power tiller linaharibika na kulitelekeza hivyo kushindwa kuleta tija" alisema Rais Dkt. Samia.


Awali, Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa Benki ya CRDB Maregesi Shaaban alisema Benki ya CRDB imeendelea kutoa mikopo inayofikia sh. trilioni 3.9 kwa misimu mitano iliyopita hadi kufikia Julai, 2023, sawa na asilimia 43 ya mikopo yote itolewayo na mabenki kwenye Sekta ya Kilimo na Mifugo hapa nchini.


"Tunatoa mafunzo kwenye vituo atamizi chini ya mpango maalum wa BBT kupitia Wizara ya Kilimo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Tunaendelea kutoa elimu ya fedha na usimamizi wa miradi kwenye vituo vilivyoko kote nchini. Uwezeshaji vijana na wanawake kwenye kilimo, uvuvi, mifugo, viwanda na biashara Bara na Visiwani.


"Benki ya CRDB kupitia kampuni yetu tanzu ya CRDB Bank Foundation, inawekeza kwa vijana na wanawake ili waweze kutimiza ndoto zao ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo na kuwapatia mitaji kwa ajili ya uanzishaji wa miradi mipya (startup capital).


Mitaji hii hutolewa kwa vijana na wanawake wenye mawazo bunifu kibiashara, na Benki ya CRDB inatoa mitaji ya awali ikiwa ni mbegu itakayoleta matunda na kuwafungulia kesho yao yenye tija zaidi kiuchumi, chini ya program ya kipekee ijulikanayo kama IMBEJU".alisema Shaaban.


Shaaban alisema Benki ya CRDB imefanikiwa kufufua matumaini ya wana ushirika kwa kuongezea mtaji inayofikia sh. bilioni 10.2, ambapo sh. bilioni 3.2 kwa TACOBA na sh. bilioni 7.0 kwa KCBL. Taasisi hizo zilikuwa zikijiendesha kwa hasara na baada ya kupata mtaji na usimamizi madhubuti kutoka Benki ya CRDB, zimeanza kujiendesha kwa faida kubwa na kutokana na mikakati madhubuti ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia, wanaendelea kutekeleza ndoto nzuri ya kiuchumi ya uanzishwaji wa Benki ya Ushirika ya Taifa.


Shaaban alisema, Benki ya CRDB ikishirikiana na wauzaji wa vifaa madhubuti vya kilimo (Agricom), imeweza kuwakabidhi baadhi ya wanufaika waliopata mikopo ya kununua Power Tillers kwa ajili ya kilimo cha mpunga mkoani Mbeya.


"Benki ya CRDB itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuendeleza fursa za uwekezaji zilizopo Bara na Visiwani.


Tunawakaribisha wadau wote walipo ndani na nje ya nchi yetu ya Tanzania wafike kwenye matawi yetu yaliyoko kote nchini na kwenye nchi jirani za Burundi na Congo DRC ili tuweze kuwahudumia.


"Tunatoa Shukran za dhati kwa Business Units zote za CRDB na uongozi wa Benki yetu pendwa ya CRDB (kipekee tunatoa Shukran kwa our MD&Group CEO, CCO, COO, CFO, DCA, DCB, DRB, DC, DCA, MD-CRDB BANK FOUNDATION & the entire CRDB MARKETING TEAM) kwa kutuwezesha vilivyo hadi kufikia kilele cha maadhimisho haya ya Maonesho ya Nane Nane kitaifa mkoani Mbeya kwa mafanikio makubwa" alisema Shaaban.

--
Share:

Tuesday, 8 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO AUGOST 9,2023























Share:

BASI LA AL -SAEDY LAPINDUKA TABORA


Basi la Al-Saedy limepinduka alfajiri leo Jumatatu Agosti 7, 2023 katika Wilaya ya Uyui mkoani Tabora huku abiria wakipata majeraha akiwemo mmoja aliyevunjika mkono.

Basi hilo lilikuwa likielekea Dar es salaam kutoka Tabora ambalo liliondoka saa kumi na mbili asubuhi leo.

Share:

MWAROBAINI WA KUTOKOMEZA AJALI ZA BODABODA WILAYA YA CHAMWINO WAPATIKANA


Na Okuly Julius-Dodoma

KATIKA kukabilia na ongezeko la ajali za barabarani nchini Chuo cha Udereva cha WIDE kwa kushirikiana na Serikali ya wilaya ya Chamwino wameanzisha programu ya mafunzo maalum kwa madereva pikipiki zaidi ya 600.


Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Chuo hicho Faustine Matina, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapatia elimu bodaboda ambao wamekuwa wakisababisha ajali kutokana na kukosa uelewa wa sheria za usalama barabarani.


“Lengo la mafunzo haya ni kutokana na ongezeko la ajali barabarani na bodaboda ni moja kati ya vyombo ambavyo vimekuwa vikisababisha ajali kwa wingi hali ambayo inasababisha wengi wao kupata ulemavu na wakati mwingine ajali hizo kusababisha vifo”amesisitiza Matina


Aidha amesema kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabau za Serikali (CAG) ya hivi karibuni inaonyesha kuwa kumekuwa matukio mengi ya ajali nchini ambayo yanasababishwa na waendesha pikikipi maarufu kama bodaboda.


“Matukio hayo mengi yamekuwa yakisababisha vifo na ulemavu kwa baadhi yao hivyo sisi kama chuo kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Chamwino tumeamua kuunga jitihada zinazofanywa na serikali yetu ya awamu sita kwa kutoa mafunzo haya ambapo yanalenga kuwafikia bodaboda zaidi ya 600 katika kata mbili za Buigiri na Chamwino Ikulu”amesema


Kadhalika, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafikia waendesha pikipiki wote zaidi ya 1,800 wa wilaya ya Chamwino ili kupunguza ajali za barabarani na kuufanya usafiri huo kuwa salama kwa watumiaji.


Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri Kenneth Yindi ambaye ndio mhanasishaji Mkuu wa Mafunzo hayo amesema kuwa wanatekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Chamwino la kuwataka Madereva wote wa Bodaboda kupata Mafunzo na leseni ili wawe kamili barabarani na kuepusha ajali.


"Tupo hapa kutekeleza agizo la Mkuu wetu wa Wilaya ambalo ni kuwataka Bodaboda wote kupata Mafunzo haya baada ya hapa hutaruhusiwa kuendesha pikipiki kama huna cheti na leseni ni bora ukafanye kazi nyingine tofauti na Bodaboda,"


Na kuongeza kuwa "hakuna Afisa usafirishaji ambaye Hana cheti Wala leseni ya Udereva Kwa hivyo ili kukidhi vigezo vya kuwa Afisa usafirishaji ni muhimu sana kupata Mafunzo na ukizingatia Chamwino ni Sebule ya Ikulu hatutaweza kuvumilia yeyote ambaye hatakuwa amekamilisha vigezo vya kuwa barabarani,"amesisitiza Yindi


Naye Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Chamwino, ASP Bwire Machunde amewataka waendesha pikipiki wote wa wilaya hiyo kujitokeza kupata mafunzo hayo ili kujengewa uwezo wa kutambua sheria za usalama barabarani na kutambua haki zao.


“Bodaboda wote mnatakiwa kuja kupata mafunzo haya ili kusaidia kupunguza tatizo la ajali nchini mara baada ya mafunzo hayo kutakuwa na msako kwa watu ambao wanaendesha vyombo vyao bila kuwa na mafunzo ya usalama barabarani”amesema ASP Bwire


Baadhi ya bodaboda walioshiriki mafunzo hayo waliishukuru serikali kwa kuwapatia fursa hiyo ambayo inakwenda kuwasadia kuondokana na ajali za barabarini.


Nyemo Chedego, amesema moja ya sababu ambazo zimekuwa zikichangia ongezeko la ajali nchini ni pamoja na bodaboda wengi kuendesha vyombo vya moto bila ya kuwa na mafunzo rasmi kutoka vyuo vinayotambulika.


“Mafunzo haya kwetu yamekuja wakati mwafaka kwani watu wengi wamekuwa wakipata ajali na wengine kufa kutokana na kutokujua sheria za usalama barabarani hivyo mafunzo haya yatakwenda kuwa msaada kwetu kuondokana na hali hiyo”amesema Chedego


Share:

NSSF INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA NANENANE

 


Share:

Monday, 7 August 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE AGOSTI 8,2023





















Share:

MFUMO WA REEFER CONTAINERS KUNUFAISHA WAKULIMA



Kukamilika kwa Mfumo wa Makasha yanayotumia Umeme kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa ambazo zinaweza kuharibika kutokana na Joto kutawezesha wakulima mbalimbali wanaotaka kusafirisha bidhaa hizo kwenda nje ya nchi kupitia Bandari ya Tanga Kusafirisha bidhaa hizo bila kuharibika.

Hayo yamesemwa na Afisa Masoko na Huduma kwa Wateja wa bandari ya Tanga Habiba Godigodi wakati wa Maonyesho ya Wakulima Nanenane kanda ya Mashariki Mjini Morogoro ambapo Bandari ya Tanga wanashiriki ili kuweza kutangaza fursa zilizopo.

Habiba alisema kuwa kulikuwa na changamoto kwa Wakulima wanaosafirisha bidhaa kama Matunda mbalimbali pamoja na Maua kushindwa kusafirisha bidhaa hizo kutokana na kutokuwepo kwa njia sahihi ya kuhifadhi bidhaa hizo hivyo bandari ya Tanga imetengeneza  eneo maalum la  kuhifadhia makasha yenye mfumo wa umeme ili waweze kuhifadhi wakati wanapotaka kusafirisha bidhaa hizo.

"Hivyo ni fursa kwenu wafanyabiashara kuitumia Bandari ya Tanga kusafirisha bidhaa hususani wakulima wa matunda mbalimbali pamoja na maua kutokana na uwepo wa sehemu sahihi ya kuhifadhi bidhaa hizo  kupitia makasha yenye mfumo wa umeme "Alisema 


Share:

WAFUGAJI WA KUKU WATAKIWA KUJIFUNZA MBINU MPYA ZA UFUGAJI

 

Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi na Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM- Taifa Donard Megitii amewataka Wafugaji wa kuku nchini kuongeza uzalishaji wenye tija Kwa kujifunza mbinu mpya kupitia Maonesho ya wakulima yanayoendelea .

Megitii ameeleza hayo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Nanenane na kueleza kuwa Sekta ya kuku ina nafasi kubwa katika kukuza uchumi wa Taifa na kuongeza kipato na fursa za ajira.

Amesema, Sekta hiyo husaidia Kwa kiasi kikubwa huhifadhi rasilimali za asili na kwamba vizazi vijavyo vitaendelea kufurahia urithi huo.

Sambamba na hayo ameeleza tathmini ya Sekta ya kuku Kwa ukanda wa kati kuwa,kwa mwaka 2022 Sekta hiyo ilikua kwa asilimia 5 ikilinganishwa na asilimia 4.2 kwa mwaka 2020 na kueleza kuwa lengo ni kufikia asilimia 9 kila mwaka.

"Ufugaji wa kuku Kwa ukanda wa kati upo Katika mfumo wa asili na kibiashara,mfumo wa asili huchangia zaidi ya asilimia 70 ya kuku wote wanaofugwa na hutoa nyama na mayai,ni jambo la jujivunia zaidi iwapo tutaongeza kasi zaidi,"amesisitiza

Pia ametumia nafasi hiyo kuwataka Maafisa ugani  kwenda vijijini kutoa elimu juu ya ufugaji bora wenye tija kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja mmoja hata Taifa kwa ujumla.

Megitii amesema wafugaji wa vijijini bado wana shida ya wataalam na hivyo baadhi Yao kushindwa kufuga kwa tija na kuendelea kufuga kwa mazoea na kueleza kuwa huu ndo wakati mzuri wa kuwaelimisha wafugaji.


Share:

DAWA ITAKAYOKUSAIDIA KUSHINDA MIGOGORO YA ARDHI!

Hakuna jambo ambalo limekuwa likiwapa watu wakati mgumu kama migogoro ya ardhi, kuna jamii hasa za wafugaji na wakulima zimekuwa zikifikia hatua ya kupigana kutokana na ardhi.

Jina langu ni Gabriel kutokea Meru, kuna ndugu yetu aliwahi kuleta ugomvi na familia yetu kisa ardhi ambayo alikuwa anadai ni yake lakini kiuhalisia haikuwa yake maana katika ukoo kila moja alishapewa eneo lake.

Alichokuwa anafanya ni kutaka kutupora eneo letu, hata wazee wa kimila walimuendea na kumuambia hakuna kitu kama hicho maana wakati eno hilo lilipogawanywa na Babu yetu wao walikuwepo kama mashahidi.

Hata hivyo, hakuweza kusikia, kila mara alikuwa anakuja nyumba na kuanza kupiga kelele wakati wa jioni hasa akiwa amelewa na kusema eneo ambalo ipo nyumba yetu ni la kwake.

Kitu ambacho kamwe siwezi kuja kusahau ni pale siku moja tulipoamka asubuhi kukuta amefungulia ng'ombe na mbuzi wake katika mazao yetu ya mahidi ambayo tulikuwa tunategemea kwa ajili ya chakula.

Tulishindwa hata kitu gani cha kufanya maana hayo mazao hatuwezi kuyapata tena hata tukisema tukamshtaki atulipe itakuwa ni kazi bure tu maana hana uwezo wa kulipa na maisha yake yote tunaweza kusema kwa ajili 100 anayepambana ni mke wake.

Hili liliniumiza kichwa sana, basi siku moja nikiwa kwenye mitandao ya kijamii niliona mjadala kuhusu migogoro ya ardhi katka jamii, katika kusoma maoni ya wachangiaji mada (comments) niliweza kuona ujumbe wa jamaa mmoja aliyesema kuwa  African Doctors ana uwezo wa kushughulia hilo.

Nilimfuata inbox yake katika mtandao huo na ndipo aliponipatia namba ya  African Doctors ambayo ni +254 769404965, nilichukua uamuzi wa kuwasiliana naye na kumuomba anisaidie kuondoa mgogoro huo wa ardhi katika familia yangu.

Kiukweli nashukuru baada ya tiba yake tangu wakati huo ule mgogoro uliisha kwani yule ndugu yetu alikuja kuumwa sana hadi kuwaita wazee wa kimila na kuwatuma waje nyumbani kwetu kuomba msamaha. Walikuja tukawasikiliza na sisi tulikubali kumsamehe maana ni ndugu kabisa.

Tangu wakati huo hajarudia tena kuleta mgogoro wa ardhi ndani ya familia na amekuwa mtu mpole sana, anajua akirudia tena hilo anaweza kukumbana na kuumwa kwa ajabu!. Asante sana African Doctors.

Kumbuka African Doctors ana uwezo kumfanya mtu kuwa na bahati maishani mwake, kushinda michezo ya bahati nasibu, kukukinga na maadui zako, kukufanya ushinde migogoro kama ya ardhi, kuwa na mvuto wa kimapenzi, kuongeza mauzo katika biashara.

Pia anatibu magonjwa kama kaswende, kisonono, kifua kikuu, presha, kifafa, upungufu wa nguvu za kiume, kuvimba miguu, kaswende, vile vile anawezesha wanawake kubaba ujautizo, wanaume kutungisha mimba n.k.

Wasiliana na  African Doctors  kwa namba; +254 769 404965, tembelea tovuti yao; www.african-doctors.com




au watumie email; africandoctorheals@gmail.com.

Mwisho.


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger