Friday, 24 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 25,2023



















Share:

TMDA YATOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA NA VIFAA TIBA KWA SHULE ZA SEKONDARI WILAYANI UBUNGO

Baadhi ya picha kutoka Manispaa ya Ubungo wakati TMDA ikiwa kwenye utaratibu wake wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba, madhara yanayoweza kutokea na namna ya kutoa taarifa juu ya madhara hayo.
Share:

WAZIRI MABULA ATAJA MAGEUZI MAKUBWA YA TEHAMA KUONGEZA UKUSANYAJI KODI YA PANGO LA ARDHI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akiwasilisha Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa makini kuhusu uwasilishaji wa Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakifuatilia kwa makini kuhusu uwasilishaji wa Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24 kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii.
Baadhi ya Wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakimfuatilia kwa makini Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula wakati akiwasilisha kwao Makadirio ya Matumizi na Mapato ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2023/24.

***
Na Anthony Ishengoma

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.Angeline Mabula ameimbia kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii kuwa Wizara yake inakuja na mageuzi makubwa ya tehama kwa lengo la kuboresha mifumo ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi ili serikali iweze kuongeza mapato yake kupitia kodi hiyo.

" Tunaenda kuwa na mageuzi makubwa kwa upande wa tehama kwa kuwa Wizara sasa inapitia mifumo upya ili wananchi waweze kupata ujumbe kwa njia Simu kama njia rafiki ya ukusanyaji mapato."Alisema Dkt.Angeline Mabula Waziri Wizara ya Ardhi.

Waziri Mabula amesema hayo leo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii inayokutana leo kujadiliana kuhusu utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Waziri Mabula ameiambia kamati hiyo kuwa hata kabla ya bunge la bajeti kuanza baadhi ya wananchi wataanza kupokea ujumbe mfupi kupitia mitandao ya simu kuhusu makadirio ya kodi ya pango la Ardhi.

Waziri Mabula aliongeza kuwa zoezi hili liko mbioni kukamilika kwani timu ya wataalamu wa tehama iko kazini na wananchi wataanza kulipia kama zilivyo bili za maji zinazotolewa na mamulaka za maji hapa Nchini.

Akiwasilisha taarifa yake kwa Wabunge hao Waziri Mabula amesema azima ya serikali ni kuimarisha usalama wa milki kwa kuhakikisha kila kipande cha Ardhi nchini kinatambuliwa,kupimwa na kumilikishwa na hivyo kudhibiti Migogoro ya matumizi ya Ardhi.

Waziri Mabula aliongeza kuwa hatua hiyo itawezesha kukua kwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.

Aidha Waziri Mabula ameiambia kamati hiyo kuwa Wizara yake imeendelea kufanyia kazi mapendekezo na ushauri vilivyotolewa wakati kamati yake ilipofanya ziara ya kikazi jijini Arusha na kuwapongeza kamati kwa jinsi ushauri wao unavyo unavyowezesha kufikia malengo ya Serikali.

Waziri Mabula amewasilisha mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi fungu 48 na Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi fungu 3 kwa mwaka wa fedha 2023/24 ambayo yanajumuhisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2022/23 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2023.
Share:

WATUMISHI WAKUMBUSHWA KUHUSU HAKI NA WAJIBU


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla akizungumza wakati akifungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Machi 24, 2023 jijini Dodoma. Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi la Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bi. Laurencia Masigo akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika leo Machi 24, 2023 jijini Dodoma. Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma, Bw. Samwel Nyungwa akizungumza wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari uliofanyika leo Machi 24, 2023 jijini

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, mawasiliano na Teknolojia ya Habari uliofanyika leo Machi 24, 2023 jijini Dodoma.

***********************

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Mohammed Khamis Abdulla amelitaka Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kutumika kuwakumbusha watumishi kuwajibika katika maeneo yao ya kitaaluma.

Akifungua kikao cha Baraza hilo kilichofanyika leo Machi 24, 2023 jijini Dodoma, Bw. Abdulla amesema pamoja na jukumu la Baraza kutetea haki za wafanyakazi bado wanatakiwa kuwajibika katika maeneo yao kwani hakuna haki bila wajibu.

“Baraza ni kiungo muhimu kati ya Menejimenti ya Wizara na wafanyakazi, ni wajibu wetu kufahamu na kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo inayohusu haki, wajibu,stahiki za wafanyakazi na utawala bora”, Amesisitiza Bw. Abdulla

Aidha, Bw. Abdulla amesisitiza wafanyakazi kuwa na upendo, uwajibikaji, uadilifu, ubunifu na mshikamano ili kutekeleza malengo ya Wizara kwa ufanisi na ofisi yake ipo wazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo amewapongeza watumishi wa Wizara hiyo kwa kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara na miradi ya maendeleo ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano; Mfumo wa Anwani za Makazi; na Mradi wa Tanzania ya Kidijitali.

Naye, Mwenyekiti wa TUGHE wa Tawi la Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bi. Laurencia Masigo amewataka wafanyakazi kufanya kazi kwa kushirikiana na kuombeana mem ana pale patakapokuwa na changamoto yeyote itawasilishwa kwa viongozi ili zitatuliwe.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa BW. Samwel Nyungwa ameipongeza Wizara kwa kufanya vikao vya Baraza kwa wakati na kusisitiza ushirikishwaji wa wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na matukio ya Kitaifa.

Kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilikuwa mahususi kwa ajili ya kupitia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka wa fedha 2022/23 na Makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Share:

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI YAAGIZWA KUCHUNGUZWA BAADHI YA VIONGOZI WANAOJIHUSISHA NA VITENDO VYA MGONGANO WA MASLAHI


WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,akizungumza wakati akifungua Baraza la wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililofanyika leo Machi 24,2023 jijini Dodoma.


KAMISHNA wa Maadili Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi ,akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililofanyika leo Machi 24,2023 jijini Dodoma.



WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Baraza la wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma lililofanyika leo Machi 24,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA



WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama,ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwachunguza baadhi ya viongozi wanaojihusisha na vitendo vya rushwa na mgongano wa maslahi nchini.

Agizo hilo amelitoa leo Machi 24,2023 jijini Dodoma wakati akifungua Baraza la wafanyakazi wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Waziri Mhagama amesema kuwa wapo baadhi ya viongozi wa umma wanaojihusisha na vitendo vya mgongano wa maslahi wanapotimiza majukumu yao na wengine kukinza hasa katika halmashauri ambako serikali imeelekeza fedha nyingi za miradi.

“Kwa kutumia mbinu za uchunguzi mlizonazo, fuatilieni kwa ukaribu viongozi wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo rushwa na mgongano wa maslahi ili haki iweze kutendeka ikiwemno kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika.

”kiongozi wa umma anapotoa kauli inayokinzana na kiongozi mwenzake au na mamlaka iliyomteua ni ukiukwaji wa maadili na tabia hiyo sio nzuri katika kuwaletea wananchi maendeleo.''amesema Mhagama

Hata hivyo amewataka kutumia baraza hilo kukumbushana kuwa wanapotoa elimu kwa viongozi wa umma wakumbushe matumizi sahihi ya madaraka kwa kutunza siri.

“Zingatieni viapo vyenu vya usiri wa taarifa mnazozipata ili na nyie mthaminiwe na muaminike na wadau wenu wa nje na ndani. Kumbukeni kuwa kila taarifa ya kiongozi inayokujia ni siri, isipotunzwa vizuri inaweza kuharibu taswira nzuri ya kiongozi na Serikali kwa ujumla,”amesisitiza

Kwa upande wake Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi amesema watajadili mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 na pia kujadili mipango na mikakati kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa 2023/24.

“Tunaahidi tutaendelea kutekeleza majukumu yetu tuliyokabidhiwa kisheria bila kupoteza uelekeo ili kufikia dira ya kuwa taasisi yenye ufanisi na kuaminika katika kukuza na kusimamia misingi ya maadili ya viongozi wa umm.'amesema Jaji Mstaafu Mwangesi

Share:

ACHOMWA MKUKI AKIFUKUZA MIFUGO SHAMBANI



Mohamed Salumu (44) mkazi wa Kijiji cha Olpopong kata ya Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara amenusurika kifo kwa kuchomwa mkuki kifuani wakati akizuia mifugo isiharibu mazao yake shambani.


Watuhumiwa hao waliamuru mifugo hiyo iharibu mazao hayo shambani ambapo jumla ya ekari 6 zimeteketezwa na mifugo hiyo.

Awali vijana hao walifika kwa mkulima huyo na kufungua uzio uliokuwa umewekwa hapo shambani na baada ya kuzuiwa mkulima huyo walimrushia mkuki ambao umemjeruhi kifuani na kwa sasa majeruhi huyo amelazwa hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa matibabu zaidi.

Via EATV
Share:

MAANDALIZI TAMASHA LA PASAKA YANOGA, WAIMBAJI MAARUFU WAENDELEA KUTAMBULISHWA


Na Mwandishi Wetu Michuzi TV

MAANDALIZI ya Tamasha la Pasaka yanazidi kunoga baada ya mwimbaji mwingine mahiri wa nyimbo za Injli nchini, Christopher Mwahangila kuthibitisha kushiriki tamasha hilo linalotarajia kufanyika Aprili 9 mwaka huu kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki na wapenzi wa muziki wa Injili nchini hasa wa Jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani.

Akizungumza leo mbele ya Waandishi wa Habari katika Ofisi za Msama Promotion ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Mwahangila ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na nyimbo zake za Injili zikiwemo Mungu ni Mungu,Fungua Milango,Moyo Furahi,Yesu yuko hapa na nyinginezo amesema tamasha la pasaka limekuja wakati muafaka kwani wamelikosa kwa miaka mingi.

Amefafanua miaka saba imepita sasa bila kufanyika tamasha hili, hivyo wanawashukuru waandaaji wa tamasha hilo ambao ni Msama Promotion kwa kulirudisha tena mwaka huu,hakika ni jambo la kumshukuru Mungu huku akisisitiza yuko tayari na amejipanga vema kwa ajili ya tamasha la Pasaka.

“Tamasha la Pasaka litakonga nyoyo za waumini mbalimbali wa nyimbo za Injili na nitaimba 'live' usipange kukosa, lakini pia tujitokeze katika kumpongeza Rais Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya ndani ya miaka miwili, njooni tusifu kwa pamoja,” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha mbalimbali ya Injili nchini, Alex Msama amesema tamasha la mwaka huu litakuwa la kihistoria na kufanyika bure.

Ameongeza maandalizi ya tamasha la Pasaka yanaendelea vizuri na kwamba awali tamasha hilo lilitakiwa lifanyike uwanja wa Taifa, lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao tamasha hilo litafanyika Leaders club.

"Kwa hiyo tamasha lipo kama kawaida Aprili 9, 2023 na mpaka sasa waimbaji wengi wamethibitsha kushiriki" amesema Msama na kuongeza tamasha hilo pia litakuwa la kumshukuru Mungu katika kusherehekea miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.Tutatumia nafasi hiyo kumuombea ili aendelee kuiongoza nchi ya Tanzania kwa amani."

Pia tamasha hilo litakuwa la kumshuru Mungu kwaajili ya uongozi wa mama yetu , Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani kwa mafanikio makubwa, miradi mingi imeendelea, kila kitu kinaenda vizuri, tunaishi kwa amani na utulivu hivyo ni lazima tumshukru Mungu kwa uongozi wa Rais wetu" ameongeza Msama.

Kuhusu waimbaji ambao watashiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na mwimbaji mahiri wa nyimbo za kusifu na kuabudu Upendo Nkone, kundi la Zabron Singers Emmanuel na wengine wengi ambao wanaendelea kutangazwa.

Wakati huo huo Mratibu wa Tamasha la Pasaka Emmanuel Mabisa amesema waimbaji wote walioalikwa kushiriki kwenye tamasha hilo wamethibitisha ushiriki wao na kwamba maandalizi yote yanaenda vizuri."Tamasha hili lilikuwa likisubiriwa kwa muda mrefu.

"Lakini kwa sasa limewadia, hivyo niwaombe wananchi wasisite kutoka na familia zao kuhudhuria kwenye tamamsha hilo vyakula na vinywaji vitakuwepo kwa bei nafuu", amesema Mabisa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Pasaka kila mwaka Alex Msama (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika bure bila kiingilio April 9, 2023 katika Viwanja vya Leders Club Jijini Dar es salaam.

Mratibu wa tamasha la Pasaka Bw. Emmanuel Mabisa (kulia) akifafanua jambo kuhusu maandalizi ya Tamasha hilo.


Mwimbaji mahiri wa Nyimbo za Injili Christopher Mwahangila (pichani kushoto) akiimba moja ya wimbo wake mbele ya waandishi wa habari kuonesha namna alivyojiandaa kutumbuiza kwenye Tamasha la pasaka linalotarajiwa kufanyika bure katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni,Jijini Dar,kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha hilo kila mwaka Alex Msama, akifurahi jambo.
Share:

Thursday, 23 March 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 24,2023

























Share:

DREAM CATCHER INAIFANYA NDOTO YAKO KUWA HALISI!

Kila binadamu jambo la kuota ndoto ni kitu cha kawaida, wengi wetu tunaota ndoto za mapenzi, kumiliki mali au zingine za kutisha, hata mie gwiji wa kasino ya mtandaoni huwa naota ndoto ya kupiga mpunga mrefu kutoka michezo mingi ya kasino.

 

Inakuaje pale ambapo ndoto unayoota inageuka na kuwa kweli! Hapo ndio utajua hujui au mjanja utakua wewe, pale Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet unaweza kugeuza ndoto yako na kuwa kweli kupitia mchezo wa Dream Catcher ikiwa na maana ya kamata ndoto yako.

 

Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, usikose pia Kasino ya mtandaoni ya Meridianbet yenye michezo rahisi ya sloti kama Poker, Aviator, Roulette.

 

 

Dream Catcher ndani ya Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet!

 

Dream Catcher ni jina la mchezo mmoja bora, wa moja kwa moja unahusisha gurudumu la pesa, maarufu kama Money Wheel. Gurudumu hili linahusisha ndoto yako ya kunasa ushindi mkubwa. Mchezo huu unalenga zaidi kufurahisha wachezaji na kuwapa fursa ya kuondoka na ushindi.

 

 Mchezo huu wa kuvutia sana unaoonekana umeundwa kwa kutumia gurudumu la bespoke likiwekwa vyema kwa usahihi kabisa na kuchezeshwa kwa umakini kukupa nafasi ya kufukuzia mchongo wako wa ushindi na Kasino ya Mtandaoni Meridianbet.

 

Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kucheza michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni.

 

Muhudumu wa moja kwa moja, unayemuona LIVE akichezesha mchezo wako pendwa, atakuvutia kwa utanashati, na namna anavyokurahisishia mchezo wako. Utafurahia sauti nzuri zikisindikiza safari yako ya kufukuzia ndoto ya ushindi. Hili huwawezesha wachezaji kufurahia mchezo wakiwa wanaona kila kitu kwenye skrini. Inafaa kujaribu.

 

Muhudumu huzungusha gurudumu na kuwashirikisha na wachezaji.  Wachezaji huweka dau kwenye nambari wanayofikiri gurudumu itasimama ikiwa ni: 1, 2, 5, 10, 20 au 40. Mchezaji akiweka bashiri kwenye nambari sahihi atashinda malipo yanayolingana (k.m. 1 hadi 1, 2 hadi 1, 5).  hadi 1, na kadhalika).

 

 Sehemu za vizidishi 2x au 7x za bonasi hutoa uwezekano wa malipo ya ukubwa wa juu. Bila kusahau unaweza kucheza michezo mwingine mingi kwenye casino ya Meridianbet na kufukuzia Casino Jackpots na bonasi kibao kwenye ubashiri wa kawaida. Ingia windoni kuifukuzia ndoto ya ushindi sasa! Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet Kasino ya mtandaoni, sloti, Poker, Aviator na Roulette- Chagua Tukupe.



 
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger