Tuesday, 14 March 2023

Picha : PAP YAENDESHA WARSHA YA MAFUNZO KWA WABUNGE JUU YA USIMAMIZI WA UHAMIAJI BARANI AFRIKA

Bunge la Afrika (Pan - African Parliament - PAP) limeendesha Warsha ya mafunzo ya kuwajengea uwezo Wabunge wa  Bunge la Afrika juu ya Masuala ya Usimamizi wa Uhamiaji (Migration Governance) katika Bara la Afrika.

Warsha hiyo (Capacity building training workshop on labour migration governance and administration for members of Pan – African Parliament)  imefanyika leo Jumanne Machi 14,2023 katika Ukumbi wa Bunge la Afrika, Midrand Afrika Kusini. Miongoni mwa sababu zilizotajwa kusababisha ongezeko la watu kuhama nchi zao ni pamoja na ukosefu wa Kazi na Ajira kwa vijana  baada ya kuhitimu masomo ya Chuo katika nchi za Afrika hali inayochangia kuhamia maeneo ili kutafuta ajira.

Tazama matukio katika picha wakati wa warsha..... Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog





Share:

DITOPILE AMLIPUA LEMA, AMTAKA AJITOKEZE KUOMBA RADHI


Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ajitokeze aombe radhi kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu Vicoba ambayo ni ya kuwadhihaki wanawake.

Katiba hotuba yake Lema alikaririwa  akisema Vicoba ni umasiki na ndio maana alimwondoa mkewe kwenye benki hizo.


Ditopile ametoa wito huo alipo kuwa mgeni rasmi katika kongamano la Vicoba na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa  kutimiza miaka miwili madarakani  liloandaliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria (JUST).

“Kama kweli tunataka kurekebisha pale ambapo serikali imekosea basi tuwe na lugha nzuri,kama kuna mtu anaona vikoba havifai basi aje na hoja zake  sio kudharau kwasababu wapo wanawake wengi wanaendesha shughuli zao kupitia fedha hizo kidogo",alisema.


Amesema “Ndugu yangu huyu Godbless Lema kiukweli ametumia lugha ambayo   imetudhihaki sisi wanawake na inawezekana hata mama yake alikuwa ni miongoni na kama anahoja aishauri serikali"


"Mimi namuomba ashuke chini akafuatilie vikoba hivi ni kwa namna gani vimeinua maisha ya watanzania ajifunze na kama anaona kuna sehemu ya kujirekebisha aseme, ikiwezekana atoke na afute kauli yake kwasababu ametukosea sana, asitumie uhuru vibaya aliopewa na Rais Dkt. Samia",ameongeza.


Ditopile amesisitiza kuwa uanzishwaji wa huduma ndogo za fedha  upo kwa mujibu wa sheria ambayo ilitungwa wakati Godbless Lema akiwa Mbunge. 

Alisema wizara ya fedha ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha mwaka 2017 lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inaleta tija kwa wananchi.

Share:

RAIS SAMIA AWAKUMBUKA WANAWAKE WA VICOBA KONDOA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa Sh.milioni 10 kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake wa Vikundi mbalimbali vya vicoba wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati akikabidhi fedha hizo Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariamu Ditopile amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua jitihada za wanawake nchini katika kazi wanazozifanya kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.


“Rais Dkt. Samia anawapenda sana wana Kondoa na wakati nakuja hapa niliwasiliana nae akanikabidhi Sh.Milioni 10 na amesema fedha hizo zikabidhiwe kwa vikundi vya vicoba zikawasaidie wanawake kujiimarisha kiuchumi",amesema.


Katika hatua nyingine Ditopile ameahidi kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kumkomboa mwanamke kiuchumi kwa kuwachangia Sh.Milioni Tano.
Share:

RC KINDAMBA AANZA KAZI RASMI TANGA...AZITAKA HALMASHAURI KUONGEZA JUHUDI UKUSANYAJI WA MAPATO

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akipokelewa rasmi na viongozi mbalimbali mkoani Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akipokelewa rasmi na viongozi mbalimbali mkoani Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza na viongozi mbalimbali Mkoani Tanga


Na SALMA AMOUR, TANGA

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewataka watumishi wa sekretarieti ya mkoa wa Tanga na Taasisi mbalimbali kufanya kazi kwa weledi na juhudi katika kukuza uchumi wa Tanga ili kuleta maendeleo kupitia ukusanyaji wa mapato kwenye halmashauri zote 11 ili kuufanya mkoa huo kukua katika ngazi za Taifa kwa ujumla .


Akizungumza mara baada ya kupokelewa na watumishi wa umma, wakurugenzi wa wilaya na Makatibu tawala ikiwa ndiyo mara ya kwanza kuwasili Mkoani Tanga tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutumikia wananchi wa Tanga mkuu wa mkoa huyo amebainisha kuwa ili maendeleo yaweze kuonekana ni lazima kuwe na viongozi bora watakaoshikilia usukani wa kuleta mabadiliko ikiwemo ukusanyaji wa mapato ambayo ndio lango kuu la kukuza uchumi wa nchi, kusimamia shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo ipasavyo ikiwemo miradi ya elimu, afya, maji na mengineyo.


"Niwaombe tu viongozi na watumishi kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato katika kuimarisha mkoa wetu kuwa ni mkoa wa maendeleo, na imani ili suala mutaweza kulipokea na kulifanyia kazi kuanzia sasa, wananchi wana hamu ya kuona matokeo mazuri ya Mabadiliko kwenye ngazi tofauti tofauti za kiutendaji na sio vinginevyo", alisema Waziri Kindamba.


Aliongeza kuwa Ili kuleta mabadiliko kwa kufikia lengo ni lazima viongozi washirikiane bega kwa bega katika mambo muhimu ya kuiboresha mkoa huo kuwa na maendeleo.


"Mpaka kufikia Sasa mkoa wa Tanga umekusanya asilimia 56 za mapato ili kuweze kufikia lengo ni lazima kufanye kazi kwa bidii ili tufikishe asilimia 100 ambapo tutakuwa kumeshafikisha lengo kwenye Jiji letu ya Tanga", alisisitiza Waziri Kindamba.


Kwa upande Wake Katibu Tawala Tanga Pili Mnyema ameahidi kutoa ushirikiano na viongozi wengine katika kuleta Mabadiliko ya kimaendeleo kwa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii kama alivyoagiza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ya maendeleo kwa Taifa.


" Ninaahidi Mimi pamoja na watumishi wenzangu na viongozi wa taasisi mbalimbali ambao wako kwenye jiji letu la Tanga kuwa tunaendelea kushirikiana na kupambana kwa pamoja kwenye mambo mbalimbali ya kutuletea mabadiliko,kama ambacho serikali yetu ilivyotuamini basi hatuna budi kuidumusha imani hivyo kwa kutenga yake wenye msingi lakini pia nikutue hofu mkuu wa mkuu kuwa Tanga ndio Mama wa ukusanyaji wa mapato tutapambana vyema katika kuhakikisha kuwa halmashauri zote zilizopo zinafsnya vizuri.


Aidha Waziri Kindamba amewataka wanaohusika katika usimamizi wa miradi mbalimbali kuenda na muda husika ili kuepusha ukwamishaji wa kuleta maendeleo na mabadiliko kwa muda husika uliopangwa.

"Tusisubiri mpaka viongozi wa kitaifa kuja kutukosoa, tunatakiwa sisi wenyewe kukaguana katika kutekeleza shughuli za kuleta maendeleo kwenye jamii yetu ili tuwe mfano mzuri katika mikoa mingine waweze kuiga namna ya uendeshaji wa shughuli zetu.


Katika hatua nyingine amelitaka Jeshi la polisi kutoa kipaumbele katika kupambana na watu wanaokiuka sheria za nchi kwa kwa kujihusisha na vitendo vya uuzaji wa dawa za kulevya ambazo zinaathiki vijana wengi mkoani hapo ikiwa ndio nguvu kazi ya Taifa.


"Niwaombe Jeshi la polisi kuwa macho wakati wote na kufuatilia kwa umakini walee wote wanaouza,wanaotumia dawa za kulevya kuchukuliwa hatua za kisheria ili kuwanusuru vijana wetu katika mambo yasiyofaa na pia kuendelea kupambana na watu wakaidi ambao wanafanya vitendo kwa ukatili wa kijinsia kwenye jamii yetu suala la ulawiti, ubakaji na ushoga limekuwa gumzo hatarishi katika jiji hili ikawa niwapongeze jeshi la Polisi kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali ambapo Hali ni nzuri  kwa sasa lakini pia matukio kama haya bado yapo", alisema.

*********

MWISHO
Share:

MWANAUME AUAWA AKIJARIBU KUMUOKOA JAMAA ALIYEKUWA ANAPIGWA NA MKE


Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 24 ameaga dunia baada ya kujeruhiwa katika vita vya wanandoa wawili eneo la Rachuonyo Kasikazini katika kaunti ya Homa Bay nchini Kenya.

Dan Ouma anaripotiwa kujaribu kuwatenganisha wanandoa wawili waliokuwa wakipigana lakini badala yake akapigwa na kifaa kichwani butu katika vita hivyo. 

Akithibitisha kisa hicho, Chifu wa kata ya Kanyaluo Magharibi Elius Ombim amesema kuwa mwanaume mmoja kutoka kijiji ca Seme Kaloo alikuwa akipigwa na mke wake na watoto kufuatia mzozo wa nyumbani.

Hili lilisababisha majirani - akiwemo Ouma - kuingilia kati lakini akawa ndiye aliyebeba msalaba wa vita hivyo.

Alipigwa kwa kifaa butu kichwani na kukimbizwa hadi Hospitali ya Kadienge kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Homa Bay akiwa hali mahututi.

 Kwa bahati mbaya, aliaga dunia katika hospitali hiuo akipokea matibabu na mwili wake kuhamishiwa katika makafani ya Homa Bay.

Chanzo - Tuko News
Share:

KAMATI YA SIASA CCM IMESELA YATISHWA HALI MBAYA YA VYOO SHULE YA NYIKA...YATOA MAAGIZO

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Kata ya Imesela ikitembelea ujenzi wa mradi wa choo shule ya msingi Nyika.
Kajala Jeremia Katibu Mwenezi na itikadi kata ya Imesela akizungumza kwenye ziara ya kamati ya Chama Cha mapinduzi.
OFisi ya serikali ya kijiji chaMwamanyuda kata ya Imesela iliyojengwa na sungusungu,nguvu za wananchi na mfuko wa serikali.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyika akitoa taarifa mbele ya kamati ya chama.
Diwani wa kata ya Imesela Seth Msangwa akizungumza katika mwendelezo wa ziara ya siasa ya kamati ya chama cha Mapinduzi.


Na Halima Khoya,Shinyanga.


Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Imesela halmashauri ya Shinyanga imeutaka uongozi wa shule ya Msingi Nyika kufanya kikao na uongozi wa serikali ya kijiji ili kuitisha mkutano wa hadhara na wananchi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa choo cha walimu pamoja na wanafunzi.


Maagizo hayo yametolewa Machi 10,2023 kwenye mwendelezo wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Imesela baada ya kutembelea mradi unaoendelea katika shule hiyo na kukuta ujenzi wa umesimama.


Diwani wa Kata ya Imesela Seth Msangwa amesema ujenzi wa choo cha walimu umetumia muda mrefu kukamilika kutokana na changamoto tofauti ikiwa ni pamoja na ushirikiano mdogo wa wananchi na uongozi wa kijiji ambapo amewataka kuitisha kikao kwa ajili ya kuchangia ujenzi huo ili kuweka mazingira salama kwa walimu na wanafunzi.


Msangwa amesema katika ujenzi wa choo cha walimu atachangia saruji, kuleta mtu wa kufyatua matofali na mchanga na kwamba miongoni mwa changamoto walizozikuta watazichukua na kuzipeleka kwenye uongozi wa juu huku changamoto zingine amewataka wananchi na uongozi wa kijiji kukaa kikao kujadili uwiano uliopo kati ya vyoo vya wanafunzi na idadi ya wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo ambavyo havina kiwango.


"Kipindi naomba nafasi katika eneo hili niliahidi kutoa ushirikiano kwa wananchi wote lakini kama nyie msipokuwa na ushirikiano tutafikiaje malengo, Kaeni chini muijenge Nyika yenu, hali ya vyoo vya wanafunzi ni mbaya na wala sitaki kupaona,kaeni na wananchi mchangie ili hata serikali iwe na wepesi kutia mkono wake baada ya nyie kuanza",amesema Msangwa.


Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Imesela,Richald Nyanda amesema katika shule hiyo kuna uhaba wa matundu ya vyoo kutokana naa idadi ya wanafunzi iliyopo na kwamba hali iliyopo kwenye matundu hayo ni mbaya hali inayohatarisha afya kwa waafunzi.


"Taarifa uliyotupa na uhalisia uliopo Nyika hatuna vyoo hata wewe ukienda saivi unaweza ukaogopa kuingia, watoto wetu wana hali mbaya, kufikia tarehe 25 kuwe na kamati mpya ya kijiji, matundu yanayohitajika ni 21 na yaliyopo ni 6 alafu tumekaaa tu hakuna utaratibu wa kujenga mengine,bada ya kikao hicho itisha serikali ya kijiji ili kushughulika na hili",amesema Nyanda.


Awali akitoa taarifa ya shule Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyika,Marco Sylivester amesema kuwa Shule hiyo ina matundu ya vyoo 6 na uhitaji wa matundu ya vyoo 21 pia ina uhaba wa matundu ya vyoo vya walimu mawili na kwamba inafanya taratibu za kujenga vyoo hivyo ambavyo vimefikia kwenye msingi.


"Shule ya Msingi Nyika ina wanafunzi 512 na walimu 8, shule ina madarasa 8 mahitaji 21,mahitaji ya matundu ya vyoo vya walimu ni 02 yaliyopo ni 0, shule ina jumla ya wanafunzi 83 kwa miaka miwili waliofanya mtihani ni 82 waliofaulu 46,waliofeli 37 ambayo ni sawa na asilimia 57%,Tutafanyia kazi maagizo yote tuliyopewa",amesema Sylivester.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger