Thursday, 2 March 2023

Picha : RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA FARAGHA WA MAWAZIRI, MAKATIBU WAKUU..... APIGA 'STOP' KUAJIRI MAAFISA HABARI BINAFSI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali kabla ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.

Rais Samia amezitaka wizara kujibu kauli za upotoshaji zinazotolewa na wanasiasa kuhusu utendaji wa Serikali ambapo  katika kulitekeleza hilo, amewataka mawaziri kuacha kuajiri maafisa habari binafsi, badala yake wavitumie vitengo vya habari kutoa taarifa za Serikali.

“Najua kila Wizara ina kitengo cha habari, vitengo hivi vinatumikaje, vipo tu vimekaa havifanyi kazi lakini bado mawaziri mmeajiri maafisa wenu habari binafsi wa kutoa taarifa zenu na si taarifa za Serikali, sasa hili tukarekebishe”, amesema Rais Samia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali kabla ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali kabla ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali kabla ya kufungua Mkutano wa Faragha wa viongozi hao uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 02 Machi, 2023.
Share:

TBS YAKAA KIKAO WADAU WA MIFUKO MBADALA NA VIFUNGASHIO VYA PLASTIKI

Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Dkt.Athuman Ngenya akiongoza Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Viwango (TBS), Bw. David Ndibalema, Mkurugenzi wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi Redempta Samwel na kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt.Candida Shirima pamoja na Kaimu Meneja wa Ukaguzi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Bw.Moses Mbambe. Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Dkt.Athuman Ngenya akifungua Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Dkt.Athuman Ngenya akizungumza Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt.Candida Shirima akizungumza katika Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi na Uzingatiaji wa Sheria TBS, Dkt.Candida Shirima akitoa neno la utambulisho katika Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki wakiwa katika kikao ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kikao hicho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki wakiwa katika kikao ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kikao hicho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki wakiwa katika kikao ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kikao hicho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam. Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki wakiwa katika kikao ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Kikao hicho kimefanyika leo Machi 2,2023 katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki hutumika kwa namna mbalimbali, hivyo endapo hazitadhibitiwa kikamilifu huweza kusababisha athari katika mazingira na vilevile, endapo mtumiaji atanunua bidhaa zisizokidhi vigezo vya ubora kuendana na matarajio yake husababisha malalamiko.

Kwa mantiki hiyo, kila mmoja anao wajibu wa kuzingatia matwaka yote ya ubora ili kukuza pato la taifa, kupunguza gharama za udhibiti, kuleta ushindani wa haki katika biashara, kulinda mazingira, kuwezesha wanunuzi kupata bidhaa zinazoendana na thamani ya fedha wanazolipa na kuepusha malalamiko.

Ameyasema hayo leo Machi 2,2023 Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya wakati akifungua Kikao cha Waagizaji, Wazalishaji na Wasambazaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki , Kikao ambacho kimefanyika katika Ofisi za TBS Makao Mkuu Jijini Dar es Salaam.

Amesema Shirika limeandaa mkutano huo mahususi kwa lengo la kukuza uelewa wa wadau wa mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki vilivyoruhusiwa ili waweze kukidhi matakwa ya Sheria ya Viwango Sura 130 pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Aidha Dkt.Ngenya amesema TBS inawajibika kikamilitu kuhakikisha kuwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na zile zinazoingizwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mifuko mbadala na vifungashio vya plastiki vilivyoruhusiwa zinakidhi matakwa ya viwango ili kukuza uchumi wa nchi yetu.

"Kwa mantiki hii, TBS itaendelea kutilia mkazo suala la usimamizi wa viwango na kudhibiti bora wa bidhaa hizo ili kuhakikisha zinakidhi vigezo vya ubora unaotakiwa". Amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzingatiaji wa Sheria na Utunzaji wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mhandisi Redempta Samwel ametoa wito kwa wazalishaji na waagizaji kuzingatia viwango vilivyowekwa na TBS kuhakiisha ile dhana nzima ya ya serikali ya kuruhusu vifungashio viendelee kuwepo ili kuhifadhi ubora, haitumiki vinginevyo ili kuweza kulinda mazingira.

Pamoja na hayo amesema katika kufanya ufuatiliaji, utekelezaji na uzingatiaji wa sheria wamegundua kwamba kuna changamoto nyingi hivyo kupitia kikao ambacho TBS wamekiandaa wataenda kujadiliana kuona ni namna gani wanaweza kupunguza changamoto katika suala la mifuko mbadala pamoja na vifungashio vya plastiki.

Nae Meneja wa Masoko ya Nje wa Kampuni ya A to Z Textile Millers ambao ni Wazalishaji wa Mifuko Mbadala na Vifungashio vya Plastiki Bw.Sylvester Kazi amesema kupitia kikao hicho wanakwenda kupata fursa kutoka soko dogo la Afrika Mashariki na kwenda kwenye soko kubwa zaidi ambalo ni soko huru la Afrika kwa kutambua viwango vya bidhaa na kuzalisha kwa kufuata viwango husika.
Share:

MFUKO WA SELF MF UNAVYOTIMIZA NDOTO ZA WATANZANIA WA HALI YA CHINI

Na Dotto Kwilasa,DODOMA

ILI kukuza Mitaji itakayowezesha kuzifikia fursa zitakazoboresha maisha ya wananchi hususani wa pembezoni, Serikali kupitia Mfuko wa SELF Microfinance Fund (SELF MF)umetumia jumla ya shilingi bilioni 313 kuwezesha watanzania laki mbili na ishirini na tano elfu hali inayosaidia kuongeza kipato na kuondokana na umaskini.


Meneja Masoko na uhamasishaji wa SELF MF Linda Mshana amesema hayo Jijini hapa wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko huo na kuongeza kuwa ili kuboresha upatikanaji wa fedha mfuko huo unatoa huduma ya mikopo ya jumla na ya Mteja mmoja mmoja.


Amesema, Taasisi hiyo ikiwa imejikita kutoa huduma ya kubadili maisha ya watu na kutoa fursa ya kufanya kazi kwa kutoa mikopo kwa masharti nafuu inaendelea na utoaji wa elimu na mafunzo ya fedha ikiwa ni pamoja na kusaidia Taasisi kutengeneza na kuanzisha mifumo ya fedha.

"Kwa kuwa Mfuko wa SELF ni wa Serikali na uko chini ya Wizara ya fedha na mipango una jukumu la kutoa huduma za kifedha kwa wananchi wenye kipato cha chini ili kuwapa fursa ya kushiriki shughuli za uzalishaji mali ikiwa ni pamoja na kukuza mtaji na kuongeza wigo wa utoaji wa huduma za mikopo kwa wananchi,"amesema.


Kwa upande wake Meneja wa SELF MF Tawi la Dodoma Aristid Tesha aliitaja aina ya mikopo inayotolewa kuwa ni pamoja na mikopo ya kilimo, biashara,imarika,mtaji, mkulima, mikopo ya mishahara ,mkopo wa pamoja na mkopo wa makazi.


Alisema masharti ya mikopo ya Mfuko wa SELF MF ni pamoja na kuwa mjasiriamali mtanzania,uwe na dhamana au wadhamini ,uwe na nyaraka muhimu kuthibitisha uhalali Kutokana na aina ya mkopo pamoja na mkopaji kutakiwa kuwa na Ofisi ya kudumu.


"Sifa za mikopo ya Mfuko huu ni riba nafuu, kupokea mkopo ndani ya muda mfupi,marejesho rafiki na kiwango cha mkopo ni Kutokana na uhitaji wa mkopaji Kwa kuambatanisha viambatanisho vya awali ikiwemo Nida,leseni ya udereva,barua ya utambulisho wa Serikali za mitaa na leseni ya biashara.


Kutokana na hayo mmoja wa wanufaika wa mikopo ya Mfuko huo Aziza Nasib amesema ili kufikia uchumi wa kati na kitimiza malengo, wafanyabiasha ndogo ndogo wanapaswa kuchukua hatua ya kukopa kwenye Taasisi zinazoaminika.


Amesema biashara zenye malengo zinahitaji mtaji mkubwa hivyo kuwashauri wafanyabiashara kukuza biashara zao kupitia mikopo yenye riba nafuu.


"Nawashauri wafanyabiasha kutumia Mfuko wa SELF kukuza kipato kwa kuwa upo chini ya uangalizi wa Serikali na hauna ubabaishaji,"alisema mnufaika huyo ambaye kwa Sasa anamiliki kiwanda cha kusaga chupa.
Share:

GGML YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA USALAMA KWA MWAKA WA 4 MFULULIZO


Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dkt Kiva Mvungi (wa pili kulia) pamoja na watendaji wa idara ya afya na usalama kutoka Geita Gold Mining Limited wakifurahia ushindi wa nne mfululizo katika tuzo ya kimataifa ya usalama mahala pa kazi. Kampuni hiyo imeiongoza Tanzania imezipiku nchi za Australia, Ghana na Afrika Kusini.

Na Mwandishi wetu 
MISINGI imara ya udhibiti wa hali ya usalama katika utendaji kazi ndani na nje ya Mgodi wa Geita Gold Mining Limited. (GGML), imeendelea kuifanya kampuni hiyo kuandika historia duniani baada ya kushinda kwa mara ya nne mfululizo tuzo ya kimataifa ya usalama mahala pa kazi (Global Safety Award).


Katika tuzo hiyo inayotolewa na kundi la makampuni ya AngloGold Ashanti (AGA), GGML imeshinda mwaka 2019, 2020, 2021 na wiki hii imeshinda tuzo hiyo kwa mwaka 2022.


Akizungumzia ushindi huo katika mahojiano maalumu na Mwandishi wetu mkoani Geita, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dkt Kiva Mvungi alisema tuzo hiyo inamaanisha kuwa AGA imeitambua GGML kama kampuni kinara inayofanya vizuri katika masuala ya usalama duniani.

AGA ambayo imeorodheshwa katika masoko ya hisa ya Johannesburg, New York, Australia na Ghana inamiliki migodi katika nchi za Australia, Columbia, Argentina, Brazil, Ghana na Tanzania. Katika nchi zote hizo,GGML au Watanzania kwa ujumla ndio vinara wa kuzingatia masuala ya usalama mahala pa kazi.


Dkt Kiva Mvungi alisema mafanikio hayo hayakuja kirahisi kwani GGML imefanikiwa kuimarisha ushirikiano wa wafanyakazi ambao wamekuwa wakiuonesha katika kujali afya zao pamoja na kujali usalama kazini.


Alisema kitu ambacho wamefanya tofauti na wenzao ni kwamba walibadilisha mfumo wa mawasiliano ya kiusalama, badala ya kutoka kwa viongozi kwenda kwa wafanyakazi, waliweka utaratibu kwamba mfumo huo wa mawasiliano utoke kwa wafanyakazi kuja kwa viongozi.


“Kwa hiyo tunapofanyakazi, wafanyakazi hutuambia hii ni salama au sio salama au angetaka ifanyike vipi, kwa hiyo sisi huongeza tu masuala mengine ya kiuongozi kuhakikisha suala linafanikiwa,” alisema.


Alisema tangu wameanza kutumia mfumo huo wa kuwasikiliza zaidi wafanyakazi, mafanikio yamekuwa makubwa katika utendaji kazi. Anatolea mfano kuwa zaidi ya miaka 10 hawajapoteza maisha ya mfanyakazi yeyote kazini, lakini zaidi ya miaka mitano hakuna mfanyakazi aliyeumia kiasi cha kushindwa kuingia kazini. Pia wamekaa zaidi ya miaka minne bila ya kuwa na mtu aliyeumia kazini.


Aidha, alimpongeza kila mtu aliyeshiriki kuhakikisha mfanyakazi au mkandarasi anapokuja kazini anafanya kazi kwa usalama na anaondoka nyumbani kwa usalama.


Aidha, akizungumza ushindi huo wa tuzo nne mfululizo, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong aliipongeza timu nzima ya idara ya afya, usalama na mazingira pamoja na wafanyakazi wote wa GGML kwa kudumisha usalama wao ndani na nje ya kampuni.


Mbali na tuzo hiyo ya kimataifa ya usalama, anasema GGML pia ilipata tuzo ya utendaji bora wa jumla.


“Hakika tuzo hii inaonesha namna tunavyofanya vizuri na kuthaminiwa. Juhudi zenu zinatambuliwa vyema na kampuni nzima. Kama tunavyojua sote bado tuna changamoto nyingi za kufanyia kazi kama timu lakini nina uhakika tunaweza kufanya kazi pamoja na kutimiza yote tuliyojiwekea Kongole kwenu wote.,” alisema Mkurugenzi huyo.

Mmoja wa wafanyakazi wa idara hiyo ya usalama, afya na mazingira ndani ya GGML, Dkt. Subira Joseph ambaye amefanya kazi ndani ya kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 10 kama daktari kwenye kituo cha afya cha GGML pamoja na Josephine Kimambo ambaye ni mhandisi wa mazingira, walisema ushindi mfululizo wa tuzo hiyo, umewafanya waone wanafanya kazi kwenye mazingira salama.

“Mazingira ya kazi yasingekuwa salama hata tuzo hii tusingeipata. Lakini pia imenifanya nione idara yetu ya usalama, afya na mazingira kazini inafanya kazi vizuri na watu,” alisema Josephine.

Share:

MBUNGE KIRUMBA AKUTANA NA WANACHAMA WA UWT SEGESE KAHAMA


Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amekutana na kuongea na wanawake wanachama wa UWT kata ya Segese halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga ili kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu Chama Cha Mapunduzi (CCM) ambapo pia amelipia kadi za UWTA kaa wanachama 37 sa kata hiyo.

Share:

Wednesday, 1 March 2023

HII DAWA NDIO ILIYONITOA JELA BAADA YA KUFUNGWA KWA KOSA LA UONGO

Ukweli ni kwamba sio kila aliye jela ametenda kosa, wapo wengi wamefungwa vifungo virefu jela kwa mambo ya kusingiziwa na kufungwa kutokana pengine waliofanya hivyo walitoa rushwa ambayo ni adui ya haki.

Nasema jambo hilo nikiwa na ushahidi wa kutosha na uzoefu kwa sababu niliwahi kupitia hilo, nilifungwa kwa kosa la kusingiziwa kuwa nimevunja duka la mtu na kuiba kitu kitu ambacho hakikuwa kweli.

Asubuhi moja nikiwa katika eneo langu la kazi nilishangaa Polisi wakija na kunikamata, nilishtuka na nilipouliza tatizo ni nini hasa?, waliniambia kuwa nitaenda kujieleza huko mbele ya safari, basi nilifikishwa kituo cha Polisi na baada ya siku mbili, nilifikishwa Mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya wizi.

Nilikana mashtaka yote yaliyonikabili, niliambiwa kuwa nimeiba fedha na mali katika duka lile ambalo kiukweli nilikuwa na muda mrefu tangu niende hapo kupata huduma, siwezi kusahau jinsi ambavyo nilipitia maumivu makali kihisia.

Kwangu maisha yalikuwa ni magumu sana maana sikuweza kupata dhamana, hivyo kila kesi yangu ilipotajwa nilitolewa mahabusu na kuletwa Mahakamani, asikuambie mtu maisha ya mahabusu ni magumu sana, siwezi hata kusimulia jinsi yalivyo.

Kumbe huo ulikuwa ni mwanzo tu, picha kamili lilianza pale ambapo nilisomewa hukumu na kuhukumiwa jela miaka sita, ilikuwa ni siku mbaya sana kuwahi kutokea maisha mwangu, nilichukulia na kupelekwa Jela kuanza kutumilkia kifungo changu.

Nikiwa Jela na nimeshapoteza matumaini ya maisha, alikuja rafiki yangu kunitembelea na kuniambia kuwa Dr. Kiwanga anaweza kunisaidia kushinda kesi hiyo, hivyo nachotakiwa ni kumwambia wakili wangu akate rufaa ya kesi hiyo.

Siku iliyofuata Wakili wangu alikuja Jela kunitembelea na kuniambia ameshapata nakala ya hukumu, nilimwambia kuwa akate rufaa kwani rafiki yangu ananifuatilia dawa kwa Dr. Kiwanga, hivyo nitaweza kushinda kesi hiyo.

Basi alikata rufaa na hukumu ilipokuja kupitiwa upya, ilikuja kubainika kuwa sikuwa na hatia yoyote, hivyo nikaachiwa huru, binafsi namshukuru sana Dr. Kiwanga kwa tiba yake ya ajabu.

Kumbuka Dr. Kiwanga ana uwezo wa kukuwezesha kuwa mtu wa bahati maishani, ana uwezo wa kukukinga kutokana na adui zako wanaokutakia mabaya kwa wakati wowote ule kwa muda wa siku tatu utaona matokeo yake.

Kwa mengi zaidi wasiliana naye kupitia barua pepe kiwangadoctors@gmail.com ama kwenye wavuti www.kiwangadoctors.com au waweza kuwasiliana naye kupitia nambari ya simu +254 769404965.

Mwisho.

Share:

DKT MABULA ATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA ZOEZI LA URASIMISHAJI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi Hatimiliki za Ardhi kwa wananchi waliorasimishiwa makazi yao katika kata za Muriet na Olasiti mkoani Arusha tarehe 1 Machi 2023. Sehemu ya wananchi wa kata za Muriet na Olasiti mkoani Arusha wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa kukabidhi hati miliki za ardhi kwa wananchi waliorasimishiwa makazi tarehe 1 Machi 2023.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Gasper akizungumza katika zoezi la kukabidhi Hatimiliki za Ardhi kwa wananchi waliorasimishiwa makazi yao katika kata za Muriet na Olasiti mkoani Arusha tarehe 1 Machi 2023. Diwani wa kata ya Ilerai mkoani Arusha Bw. Losoiki Laizer akizungumza wakati wa zoezi la kukabidhi hatimiliki kwa wananchi waliorasimishiwa makazi holela tarehe 1 Machi 2023. Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Arusha Idrisa Kayera akizungumza katika zoezi la kukabidhi hatimiliki kwa wananchi waliorasimishiwa makazi holela tarehe 1 Machi 2023.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikabidhi hatimiliki za ardhi kwa mume na mke wakati wa zoezi la kukabidhi Hatimiliki za Ardhi kwa wananchi waliorasimishiwa makazi yao kwenye kata za Muriet na Olasiti mkoani Arusha tarehe 1 Machi 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

*********************

Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Amgeline Mabula amewataka wananchi kuchangamkia zoezi la urasimishaji linaloendelea nchini ili kuondokana makazi holela.

Dkt Mabula alitoa kauli hiyo leo tarehe 1 Machi 2023 mkoani Arusha wakati wa zoezi la kukabidhi Hatimiliki za Ardhi kwa wananchi waliorasimishiwa makazi yao katika kata za Muriet na Olasiti mkoani humo.

Zoezi la urasimishaji makazi holela ni zoezi la miaka kumi na lilianza mwaka 2013 na linatarajiwa kukamilika mwaka huu wa 2023.

"Serikali inaendelea na program ya kupanga na kupima ardhi ikiwa na lengo la kuondoa makazi holela, program hii inafanyika katika meneo mbalimbali ilianza mwaka 2013 na inategemea kuisha mwaka huu" alisema Dkt Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mkoa wa Arusha una jumla ya mitaa 112 inayofanyiwa urasimishaji ambapo michoro ya mipango miji 391 imeandaliwa na kuidhinishwa yenye viwanja 104,097 na tayari viwanja 55,023 vimewekewa beacon huku upimaji wa viwanja 46,197 ukiwa umeidhinishwa.

Hata hivyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesikitishwa na muitikio mdogo wa wananchi waliojitoleza kuchangamkia zoezi hilo la urasimishaji makazi holela nchini.

Amesema, takwimu katika zoezi hilo kwa kata ya Olasiti inaonesha kuwa hadi sasa ankara 4,009 zimetolewa kwa wananchi lakini ni wananchi 934 tu ndiyo waliowasilisha maombi ya hati na kati ya hao ni 517 waliochukua hati zao.

Aliwasihi wananchi waliorasimishiwa makazi yao kuhakikisha wanalipa kwa wakati gharama za kurasimishiwa maeneo yao ili zoezi la urasimishaji katika mitaa yao liishe kwa wakati.

Amesema, wizara ya ardhi kwa kuhirikiana na wadau wote wanaoguswa na shughuli za urasimishaji itaendelea kushirikiana ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua mbalimbali za kutatua kero za wananchi zilizobainika katika halmashauri zinazotekeleza kazi za urasikishaji.

Aliwakumbusha wananchi kuhusu msamaha wa riba ya kodi ya ardhi uliotolewa na mhe rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutaka wadaiwa wakubwa kutumia fursa hiyo kabla haijaizha tarehe 30 April 2023 kwa kuwa kumekuwa na kawaida kwa wananchi kulalamika kwamba wanaomba kuongezewa muda ikifika mwisho wa siku za msamaha.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Felician Gasper alisema, pamoja na serikali kuamua kuwarasimishia makazi wananchi lakini tatizo linaonekana lipo kwa wananchi kutokana na kwa kushindwa kulipia gaharama za kurasimishiwa na wengine kushindwa kuchukua hati ambapo aliwaomba wananchi wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa ya zoezi la urasimishaji kabla halijafungwa.

"Sitegemei kuona wananchi wanakuja ofisini kuomba kuongezewa muda na kuwataka kuutumia muda wa sasa vizuri kwa kurasimishiwa makazi yao kutaka uhamasishaji zaidi kwa wananchi katika zoezi hilo" alisema Gasper

Kamishna wa ardhi Msaidizi mkoa wa Arusha Idrisa Kayera aliweka wazi kuwa, kwa sasa muitikio wa kuchukua hati kutoka kwa wananchi waliorasimishiwa maeneo yao ni mdogo na kutoa rai kwa wananchi kulipia ankara kwa wakati ili waweze kupatiwa hati.

Diwani wa kata ya Ilerai Losoiki Laizer ametaka wananchi kuhakikisha wanalipia gharama za urasimishaji ili waweze kupatiwa hati kwa lengo la kupunguza migogoro ya ardhi na kutaka uhamasishaji zaidi kutoka kwa viongozi mbalimbali.
Share:

JESHI LA POLISI LAMSHUKURU RAIS  SAMIAKUBORESHA MAZINGIRA YA UTOAJI MAFUNZO YA KITAALUMA


********************

Na mwandishi wetu Jeshi la Jeshi la Polisi

Jeshi la Polisi Nchini linamshukuru mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha utaratibu katika mafunzo ya Jeshi hilo kwa kuwawezesha vitendea kazi ikiwa nipamoja na kuondoa makato ya fedha ya chakula kwa askari walioko mafunzoni katika vyuo mbalimbali vya Jeshi hilo.

Hayo ya mesemwa leo march 01 2023 na Kamishina wa opereshi na mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini CP AWADHI JUMA HAJI alipokuwa akiongea na wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam ambapo amebainisha kuwa hapo awali kulikuwa na utaratibu wa askari kukatwa fedha anapokuwa mafunzoni.

Aidha Kamishina Awadhi amewataka askari hao kujitoa kikamilifu katika mafunzo hayo kwa kupokea mafunzo yanayotolewa na walimu ndani ya darasa na katika medani za kivita ili kutimiza adhima ya amiri Jeshi ya kujenga mazingira rafiki katika kozi za Jeshi hilo.

Sambamba na hilo ujio wake pia ni katika kuungana na kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Jamal Rwambow ambae ni mstaafu wa Jeshi la Polisi ambapo amebainisha kuwa kamishina uyo amejikita katika uandishi wa vitabu lengo likiwa ni kuikomboa jamii kupitia uandishi wake na kushauri Jeshi la Polisi katika utoaji huduma kwa wananchi.

Pia katika hafla hiyo amepata wasaa wa kuzindua kitabu kilichoandikwa Salam za marehemu nakuwaomba askari kusoma vitabu hivyo ambavyo vina toa dira na mweleko sahihi katika kutoa huduma kwa jamii.

Kwa upande wake kamishina msadizi mwandamizi mstaafu Jamal Rwambow amesema kuna baadhi ya watu wanasimamia kazi za upelelezi ambapo amebainisha kuwa kuna watu hao hawana uwezo mkubwa wa maswala ya upelelezi na kusema kuwa Jeshi hilo linaouwezo mkubwa wa upelelezi hivyo ameiomba serikali kuliwezesha kifedha hasa kitengo cha upelelezi ili kuwa naufanisi mkubwa.

Nae mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Daktari LAZARO MAMBOSASA amesema kuwa anamshukuru mkuu wa Jeshi la Polisi kwa namna anavyopigania maslahi ya askari na kuahidi kuwa wao kama wakufunzi watahakikisha wanasimamia mafunzo hao kwa weledi mkubwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger