Tuesday, 7 February 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 7,2023













Share:

Monday, 6 February 2023

CHARLES HILARY ATEULIWA KUWA MSEMAJI WA SERIKALI YA ZANZIBAR



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Charles Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali. Charles Hilary ni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano - Ikulu, Zanzibar.

Charles Hilary

Ikumbukwe Charles Hilary ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari wa siku nyingi nchini Tanzania.


Cheo hicho hakikuwahi kuwepo ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tangu utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk Salmin Amour
Share:

MAWAKALA UTALII WAMIMINIKA NCHINI


MAWAKALA wa Utalii wameanza kumiminika nchini ili kuangalia vivutio vya Utalii hapa nchini na kwenda kuvitangaza nchini mwao.

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Eliamani Sedoyeka jana aliongoza mapokezi ya Mawakala hao kutoka katika masoko ya kimkakati katika nchi tofauti.

Nchi walizotoka Mawakala hao ni Marekani, Canada, Mexico, Ubelgiji na Brazil.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea Mawakala hao, Prof. Sedoyeka amesema "Leo tumeanzisha Mega Trip ambayo kwa kawaida Wizara kupitia Bodi ya Utalii ( TTB) uandaa safari kama hizi ambazo uwaleta waongoza Utalii, Waandishi wa Habari na wadau wakuu wa utalii wa kimkakati ili waje Tanzania kuangalia maeneo yetu mbali mbali ya vivutio".

Sedoyeka amesema watalii wanavyokuja nchini uletwa na makampuni ambayo tayari kama nchi imeshawajengea uwezo Mawakala wa nchi hizo juu ya vivutio vilivyopo nchini.

"Ziara hii inakuja baada ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuwa na mashirikino mazuri na kampuni ya Ndege ya Qatar na pia ni muendelezo wa matunda ya Royal Tour iliyoongozwa Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. " Amesema Sedoyeka

Amesema, Tanzania imeingia makubaliano ya kimkakati kuanzisha mahusiano ya kibiashara ili kuwatangazia duniani kuwa Tanzania kuna vivutio vya aina gani, mahusiano ya kimkakati ili kumtengenezea mtiririko wa wageni.

Amesema, kufunguka kwa masoko ya kimataifa yanasaidia kukua kwa uchumi wa nchi na kuongezeka kwa pato la taifa. Wafanyabiashara wanapata fedha.
Share:

SBT NA TEMDO WABUNI MITAMBO YA KISASA YA SUKARI ITAKAYO MSAIDIA MKULIMA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA MIWA










Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Antony Mavunde akitoa maelekezo Kwa Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO muhandisi Prof. Frederick Kahimba alipo tembelea Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO)lililopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha








Mkurugenzi Mkuu wa TEMDO muhandosi Prof. Frederick Kahimba akitoa maelezo ya Mtambo wa Kuzalisha Sukari ulio Buniwa na Kutengenezwa na TEMDO kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Antony Mavunde alipo tembelea Shirika la Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO)Waziri aliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof. Kenneth Bengus


Na Woinde Shizza , ARUSHA

Bodi ya sukari (SBT)inashirikiana na wadau wa maendeleo wakiwemo taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo (TEMDO) ilikuboresha kuboresha na kubuni mitambo ya kisasa ya kuzalisha sukari kwa wingi itakayowezesha wakulima na wafanyabiashara kuanzisha viwanda vya kuzalisha sukari hapa nchini.


Sekta ya viwanda nchini ni kiungo muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa taifa hali ambayo iliyopelekea Naibu Waziri wa Kilimo Antony Mavunde kufanya ziara katika taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO)na kuona ubunifu wa mitambo ya kilimo itakayokuza biashara ya sukari hapa nchini.


Akiongea katika ziara hiyo Naibu waziri huyo alisema kuwa ni lazima tutengeneze mashine au viwanda ambavyovitasaidia wakulima kuongeza thamani katika mazao yao.


"Lazima tufikie katika kuongeza thamani na nyinyi mliopo chini ya wizara ya viwanda , biashara na uwekezaji mhakikishe mnafanya kazi ya kutengeneza mitambo ya kuongeza thamani na hasa katika mazao ya kilimo ,uvuvi pamoja na mifugo mmepewa jukumu kubwa kama temdo na mimi ningependa kila siku muendelee kuja na bunifu mbalimbali", alisema.


Alisema kuwa wanaamini mitambo hii ikikamilika kwa muda muaafaka kama walivyomuaidi hadi kufika mwezi Junu itasaidia kumtoa mkulima katika ukulima wa miwa na kwenda kuwa mzalishaji wa sukari.


"Niwaombe muendelee kuboresha huduma mnayo nafasi kubwa ya kuwasaidia wananchi ,pia nimpongeze mkurugenzi wa bodi ya sukari kwa bunifu walioufanya na kuamua kushirkiana na TEMDO mlikaa na kutafuta jinsi ya kumsaidia mkulima kuondoka na tatizo la miwa kubaki shambani na kuharibuka ,kuna kipindi uwezo wa uchakataji wa miwa katika viwanda vikubwa uliwaliwazidi nakuanza kutokuchukuwa miwa ya wakulima ,bodi iliamua kuchukua hatua kwamba huyu mkulima aliyekwenda shambani akaweka muda wake akatumia gharama leo miwa yake inaozea shambani hali ambayo ilikuwa inawavunja moyo wakulima ,lakini pia kama nchi tulikuwa tunajipunguzia mapato lakini pia tulikuwa tunawafanya watu wachukie kilimo hivyo Mtambo wa Kuzalisha Sukari utamuokoa mkulima .


Alibainisha kuwa mtambo huu utasaidia kuongeza dhamani ya mazao ya kilimo kwa yule mkulima ambaye analima miwa na yupo sehemu ambayo awezi kupeleka miwa yake katika kiwanda kikubwa na utasaidia kukuza uchumi wetu wa nchi yetu ,na alisisitiza kuwa lazima taasisi hizo zijikite katika kutengeneza mitambo itakayosaidia kuongeza thamani katika mazao ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa bodi ya sukari Prof. Keneth Bengesi alisema kuwa lengo la kutengeneza mashine hii ni kuhakikisha wanamsaidia mkulima pamoja na kuhakikisha kwamba hawauzi mazao ya miwa ambayo hayajaongezewa dhamani maana mkulima anapoongeza thamani mazao yake anapata pesa nyingi zaidi.



Mkurugenzi wa taasisi ya ubunifu na usanifu mitambo (TEMDO) Mhandisi Prof. Frederick Kahimba alisema wameshaanza kutengeneza mitambo mbalimbali itakayomsaidia mwananchi na kuhakikisha yale matatizo ambayo yapo katika wizara ya kilimo wao kama Taasisi ya usanifu wanayatatua na kufanyia kazi.
Share:

AUAWA BAADA YA KUMUUA HOUSE GIRL NA KUMCHOMA KISU MAMAAKE

Watu wawili wameuawa huku mmoja akijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu maeneo ya Magomeni Kagera, Mtaa wa Ludewa


Inadaiwa kijana Erick aliyekuwa akiishi nyumbani kwa mzazi wake amemuua dada wa kazi (Anna) baada kukataliwa kimapenzi na baada ya mauaji Erick akautupa mwili chooni; muda mfupi baadaye akamchoma kisu tumboni mama yake mzazi ambaye alihoji alipo dada wa kazi baada ya kukuta damu zimetapakaa kila sehemu.


Kelele za mama mtu kuchomwa kisu ziliwashtua majirani ambao walifika eneo la tukio na kuanza kumshambulia mtuhumiwa hadi kusababisha kifo chake
Share:

TANZANIA GIRL GUIDES ASSOCIATION WAENDESHA KAMPENI YA UPANDAJI MITI SHULE YA MSINGI NDEMBEZI

 

Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association

Kampeni ya upandaji miti ikiendelea katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

CHAMA kisicho cha kiserikali Tanzania Girl Guides Association kimeendesha Kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari za mazingira.

Kampeni hiyo imefanyika leo Februari 3, 2023 ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya kuhamasisha wananchi kupanda miti kwenye Kaya zao, pamoja na Taasisi za Serikali zikiwamo shule za Msingi na Sekondari, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo.

Akizungumza kwenye Kampeni hiyo ya upandaji Miti Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga, amesema kampeni hiyo ya upandaji miti ilianza Rasmi mwaka 2021, na wameshapanda miti mingi katika shule za Msingi Manispaa ya Shinyanga.

Amesema upandaji miti katika shule hiyo ya Msingi Ndembezi ni mwendelezo wa Kampeni ambayo wamekuwa wakiiendesha mashuleni kupanda miti, ambapo wameshapanda pia miti 300 katika shule ya Msingi Ujamaa, Miti 200 shule ya Msingi Jomu.

“Leo katika Shule hii ya Msingi Ndembezi tumepanda Miti zaidi ya 1,000, na kampeni hii ni endelevu ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na athari za mazingira,”amesema Maganga.

“Nawaomba viongozi na watoa maamuzi katika vikao vyenu ajenda ya kuhamasisha wananchi kupanda miti hasa katika msimu wa mvua iwe ya kudumu, ili ipandwe miti mingi ya kutosha na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,”ameongeza.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, amepongeza kampeni hiyo ya upandaji miti ambayo itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kupata mvua za kutosha na kuondokana na hali ya ukame.

Mgeni Rasmi Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akimwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa huo, amewataka wanafunzi kuitunza miti hiyo ili ikue na kuwapatia faida mbalimbali ikiwamo kivuli na kuzuia mmomonyoko wa udongo.

Ametaja faida nyingine ya miti ni kuondoa hewa ya ukaa na kupata hewa nzuri, huku akiwaagiza viongozi kuwachukulia hatua kali wafugaji ambao wamekuwa wakipitisha mifugo kwenye maeneo yaliyopandwa miti.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya msingi Ndembezi.

Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga, akizungumzia namna wanavyoendesha kampeni ya upandaji miti.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Mohamed Makana, akizungumza kwenye Kampeni ya upandaji Miti

Kamishina wa Skauti Bi. Suzani Kidima akizungumza kwenye Kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ndembezi Rubeni Dotto akizungumza kwenye Kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.

Mwanafunzi Noelina Busisi akitoa elimu ya umuhimu wa upandajimiti kwa wananafunzi wenzake ili wawe Mabalozi wazuri wa kupinga uharibifu wa mazingira.

Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga, akizungumzia namna wanavyoendesha kampeni ya upandaji miti.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akipanda mti katika shule ya Msingi Ndembezi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakipanda mti.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza kwenye kampeni ya upandaji miti katika shule ya Msingi Ndembezi, akiwa na Wakala wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia Nchi Joyce Maganga, wakipiga picha na wanafunzi.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Ndembezi Manispaa ya Shinyanga wakitoa burudani kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Walimu wakiwa kwenye Kampeni ya upandaji miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Kampeni ya Upandaji Miti.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association Joyce Maganga.

Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura (kushoto) akipiga picha ya pamoja na Wakala Mtetezi wa Mradi wa Msichana na Mabadiliko ya Tabia nchi kutoka Tanzania Girl Guides Association, Joyce Maganga.

Picha na pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha na pamoja zikiendelea kupigwa.

Picha na pamoja zikiendelea kupigwa.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger