Wednesday, 25 January 2023

WATAALAMU WATUMIKE KUKIBIDHAISHA KISWAHILI-MAJALIWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo pamoja na hundi ya Dola 5,000, mshindi wa kwanza wa Ushairi, Salum Makamba, kwenye hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu – ALAF Tanzania Ashish Mistry, Mkurugenzi Mkuu SAFAL Group Anders Lindgren, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo pamoja na hundi ya Dola 5,000, mshindi wa kwanza wa Riwaya, Dotto Daudi, kwenye hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu – ALAF Tanzania Ashish Mistry, Mkurugenzi Mkuu SAFAL Group Anders Lindgren, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa zawadi maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu SAFAL Group Anders Lindgren katika hafla ya utoaji tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, kwenye Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukabidhi Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, kwenye Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kukabidhi Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, kwenye Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, katika Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, katika Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.

Mkurugenzi Mkuu SAFAL Group Anders Lindgren akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022, katika Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa Tuzo ya Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022 katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.


Wadau mbalimbali wakifuatilia hafla ya utoaji tuzo Kiswahili ya Safal – Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022 katika Ukumbi wa Mlimani, jijini Dar es salaam Januari 19, 2023.



(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezielekeza Wizara na Taasisi zote zinazohusika na maendeleo ya lugha ya kiswahili wawatumie vema wataalamu wa lugha hiyo waliopo nchini wakiwemo kutoka Vyuo Vikuu, Mabaraza ya Kiswahili na Vyama vya Kiswahili katika kukitangaza na kukibidhaisha kiswahili ili kitumike kama lugha ya ukombozi na kusaidia kuleta umajumui wa Afrika.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa balozi za Tanzania kuhakikisha zinaendeleza jitihada za kukuza na kufundisha Kiswahili katika ofisi za ubalozi na kuwashirikisha wadau wengine kama Diaspora na asasi nyingine zenye nia ya kukuza na kuendeleza Kiswahili.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Januari 25, 2023) wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo ya Kiswahili ya Safal-Cornell ya Fasihi ya Afrika mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Tuzo hizo zinadhaminiwa na Kampuni ya Mabati ya ALAF Limited - Tanzania ikishirikiana na kampuni ya Mabati Rolling Mills ya Kenya, chini ya uratibu wa Chuo Kikuu cha Cornell cha nchini Marekani.

“Muda mrefu imekuwa ikizoeleka kwamba lugha ya kiswahili inatumika katika masuala ya kitaaluma. Lugha hii kwa sasa imeshavuka mawanda ya kitaaluma na inatumika katika nyanja za uchumi na biashara. Kwa kuzingatia ukweli huo leo tunashuhudia kwa macho yetu Kampuni ya ALAF ikitoa tuzo na ufadhili wa wanafunzi wanaosomea shahada ya umahiri katika Kiswahili.”

Waziri Mkuu amewasisitiza waalamu wa kiswahili wakikishe kwamba wanaweka mikakati thabiti ya kupenyeza lugha ya kiswahili nje ya nchi kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandika kamusi na vitabu vitakavyowasaidia watu kujifunza lugha hiyo adhimu. “Vilevile, sambazeni vijitabu vyenye misamiati muhimu kwa wasomaji wa awali wa lugha ya Kiswahili, viwekeni kwenye mitandao ili viweze kusomwa na watu wengi zaidi duniani.”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo yenye dhamana ya lugha ya Kiswahili, ieendelee kuratibu vema na kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha lugha ya Kiswahili inakua na kuenea. “Tunataka Tanzania iendelee kuwa kinara wa maendeleo ya lugha ya Kiswahili, waunganisheni wadau wa Kiswahili ili waone kwa namna gani watashiriki katika utekelezaji wa Mkakati wa Kubidhaisha Kiswahili Kitaifa na Kimataifa.”

“Ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo yoyote hayawezi kufikiwa bila kuwekeza vya kutosha katika lugha. Nchi zilizoendelea zimepiga hatua kubwa ya maendeleo kwa kutumia lugha zao. Hivyo, ninaendelea kutoa wito kwa washiriki wote kila mmoja aweke dhamira ya kuwekeza katika lugha ya Kiswahili kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.”

Amewahakikishia kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu itaendelea kuwaunga mkono watu wote wenye nia ya dhati ya kuleta maendeleo ya Taifa pamoja na kuendelea kuunga mkono juhudi zote zenye lengo la kuendeleza nchi yetu na wananchi wake.

Akizungumzia kuhusu utoaji wa tuzo hizo amesema tangu kuanzishwa kwake tayari waandishi 15 wameshinda na jumla ya waandishi 847 walijitokeza katika kuwania tuzo hiyo ambapo katika shindano la mwaka 2022 pekee walijitokeza waandishi 264 ikilinganishwa na waandishi 65 waliojitokeza mwaka 2015. “Hivyo basi, ni matumaini yangu kwamba shindano la mwaka 2023 litakuwa na idadi kubwa zaidi ya waandishi watakaothubutu.” Walioshika nafasi ya pili wamepata Dola za Marekani 2,500 na Dola za Marekani 5,000 kwa nafasi ya kwanza.

Amesema mbali na kampuni ya ALAF kudhamini tuzo hizo pia imeendelea kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa Shahada ya Umahiri ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kwamba hadi sasa wanafunzi 12 wamenufaika na ufadhili huo.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuanza kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili kutoka nchi za nje za Bara la Afrika na ufadhili wao unahusisha vipengele vyote ikiwa ni pamoja na ada na fedha za kujikimu. “Hii ni hatua muhimu sana kwa maendeleo ya Lugha Kiswahili ndani na nje ya nchi.”

Amesema kitendo hicho kinaonesha ni kwa namna gani Serikali inatekeleza dhamira yake ya kuendeleza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania. “Kitendo hicho kimefuta ile dhana ya Watanzania kuwa wapokeaji wa ufadhili kutoka nchi mbalimbali. Tulizoea kuona Watanzania wanaomba ufadhili katika vyuo na nchi mbalimbali lakini sasa umefika wakati Tanzania inatoa ufadhili kwa nchi nyingine kuja kujifunza Kiswahili.”

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amesema katika kuendeleza ukuzaji wa lugha ya kiswahili, wizara inaendelea kufuatilia mchakato wa kujengwa kwa Chuo Kikuu cha Kiswahili na Stadi za Kiafrika, ambapo ujenzi wa chuo hicho utakuwa ni matunda ya jitihada za serikali ya awamu ya sita ambayo imekuwa ikisimamia kwa karibu maendeleo ya lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa wizara yao tayari imekwisha zindua Mfuko wa Utamaduni na Sanaa na umeanza kuwanufaisha wasanii na wanautamaduni wote wenye sifa na waliokidhi vigezo ikiwemo watunzi na wataalamu wa Lugha ya kiswahili nao ni moja ya wanufaika na mfuko huo ambao wameanza kupatiwa mikopo nafuu ili waweze kuiendeleza na kuikuza lugha hiyo.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ALAF-Tanzania, Ashish Mistry alisema kila mwaka kampuni yao inatoa Dola za Kimarekani 50,000 kila mwaka kwa ajili ya kufanikisha utoaji tuzo hizo. Pia kampuni hiyo imeweza kutoa udhamini wa wanafunzi 12 wa Shahada ya Umahiri (M.A) ya Kiswahili tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo na wataendelea kufanya hivyo hadi mwaka 2025. Lengo la ALAF ni kuimarisha matumizi sambamba na kukitangaza Kiswahili barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Share:

CHUO CHA OLMOTONYI CHATAKIWA KUWA BUNIFU KATIKA KUTAFUTA VYANZO VYA MAPATO


************** 

Menejimenti ya Chuo cha Misitu Olmotonyi imetakiwa kubuni mikakati mipya ya kujiongezea mapato ili kuongeza udahili wa wanafunzi, motisha kwa wafanyakazi pamoja na kuzalisha mazao yatokanayo na misitu zikiwemo fenicha zenye ubora wa hali wa juu.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ameyasema hayo leo katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo hicho Jijini Arusha ambapo amesema kuna haja ya kukiboresha chuo hicho ili kiweze kuleta tija kwa Taifa. 

“Moja ya kazi ya kufanya ni kuendelea kubuni vyanzo vya mapato lakini pia ni lazima muwe na maandiko mahususi yanayojenga hoja kuwafanya wanaotoa ukomo wa bajeti waweze kuliona kwa macho ya kipekee” amesisitiza Mhe. Masanja. 

Amesema kuna haja ya kufanya mabadiliko hasa katika mfumo wa uendeshaji wa chuo hicho kwa kuwafundisha vijana vitendo zaidi kuliko nadharia ili kuwawezesha kuchakata mazao ya misitu yenye ubora wa hali ya juu yatakayoweza kushindanishwa na bidhaa zinazotoka nje ya nchi. 

Aidha, Ameilekeza Menejimenti hiyo kuzalisha vijana wakomavu na wenye taaluma ili wasaidie katika uhifadhi wa misitu kutokana na nchi kukumbwa na changamoto ya uvamizi wa misitu na ukataji wa miti hovyo. 

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii ina matumaini makubwa na vijana wanaopatiwa ujuzi katika chuo hicho na kwamba wanakwemda kuwa Mabalozi wa kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza misitu sambamba na kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu 

Katika hatua nyingine, Mhe. Masanja amesema Wizara itaendelea kutatua changamoto zinazokikaboli chuo hicho ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya watumishi na kuboresha muundo wa watumishi. 

Awali, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji Makamu Mkuu wa Chuo hicho , Stephen Kingwele amesema chuo kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi unaopelekea kuajiri watumishi wa mkataba ili kusaidia nguvukazi.Pia ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo imekuwa ikisaidia fedha za utekelezaji wa majukumu kupitia Mfuko wa Misitu. 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru , Mhe. Mhandisi Richard Ruyango amemshukuru Naibu Waziri kwa kufanya ziara katika chuo hicho kwa kuwa ndio mwanzo wa kutatuliwa kwa changamoto mbalimbali zinazokikabili. 

Chuo cha Misitu Olmotonyi kilianzishwa mwaka 1937 kwa lengo la kuzalisha wafanyakazi katika sekta ya misitu ili kuwepo na uhifadhi endelevu.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATANO JANUARI 25,2023










Share:

Tuesday, 24 January 2023

Breaking : RAIS SAMIA ATUMBUA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI, DC MBARALI, YUMO MWAGENI WA USHETU



Share:

THEATRE ARTS FEMINISTS, PERFOMANCE WOMAN WATOA ELIMU YA UKATILI WA KIJINSIA SHULE YA MSINGI MUGABE DAR


Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman kwa kushirikiana na Shirika la Theatre Arts Feminists wamefanya uraghibishi katika shule ya msingi Mugabe iliyopo kata ya Sinza wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam na kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi 720 kati yao wavulana ni 359 na wasichana ni 36.

Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasabila  wameelezea mazingira yanayopelekea ukatili na mbinu za kuepuka ukatili. 

 "Pia tumebaini changamoto zilizopo shuleni hapo za ukatili ikiwa ni pamoja na ubakaji na kupata visa mkasa vya ubakaji viwili na visa viwili vya ulawiti ambapo kesi zimeshughulikiwa kwa ushirikiano wa ofisi ya Mtendaji Kata.

Perfomance Woman na Theatre Arts Feminists tumefurahishwa na ushirikiano uliopo kati ya shule na uongozi wa ofisi ya kata hali inayopelekea matukio ya ukatili kupatiwa ufumbuzi kwa haraka",wamesema.

"Perfomance Woman na Theatre Arts Feminists (Taf group) tunaahidi kushikiana katika ujenzi wa nguvu za pamoja (TAPO) ili kuweza kufikia watu wengi zaidi na kuhakikisha tunapambana na ukatili wa kijinsia ndani ya jamii", wameeleza.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasabila  akitoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasabila  akitoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Perfomance Woman, Rose Mwasabila  akitoa elimu ya masuala ya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Shirika la Theatre Arts Feminists, Aluwa Mkilindi akitoa elimu ya kukomesha ukatili wa kijinsia
Share:

JAJI MGEYEKWA AWAITA WANANCHI KUJIFUNZA USULUHISHI MIGOGORO YA ARDHI


**************************

Katika kuadhimisha wiki ya sheria, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeandaa siku moja ya kutoa elimu na kukutana na wadaawa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam siku ya Alhamisi Januari, 26, 2023.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi Mhe. Agnes Mgeyekwa amesema siku hiyo Majaji wa Mahakama yake watakuwepo katika viwanja hivyo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika masuala mazima ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kwa mujibu wa Mgeyekwa, Majaji wa Mahakama hiyo watakuwemo katika Banda hilo la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi kuanzia saa 3 asubuhi hadi 9 alasiri ambapo watatoa elimu na kukutana na wadaawa.

"Ninawaomba wananchi wajitokeze kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika utatuzi wa migogoro ya ardhi". Alisema Jaji Mgeyekwa.
Share:

PROFESA AFIKISHWA MAHAKAMANI KISA KAOA MKE WA PILI KWA SIRI



Profesa Christopher Kasanga, akiwa na mke wake aliyemuoa kwa siri

Mahakama ya wilaya ya Morogoro imempandisha kizimbani Profesa Christopher Kasanga wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa shtaka la ugoni baada ya kufunga ndoa ya pili kwa siri na mwanamke mwingine Oktoba 29 mwaka 2022.

Imeelezwa kuwa kesi hiyo ya madai namba 57/2022 imefunguliwa Desemba 16, 2022 na Matlida Sigareti dhidi ya mumewe Profesa Christopher Kasanga ambaye wamefunga ndoa miaka 25 iliyopita.

Bi. Matlida amelazimika kufungua keshi hiyo baada ya kubaini mume wake Profesa Kasanga kufunga ndoa nyingine kwa siri na mwanamke mwingine anayefahamika kwa jina la Linael Makundi ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya CRDB.Mjini Morogoro.

Kesi hiyo inasikilizwa chini ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Morogoro Emmael Lukumai, ambapo katika upande wa mashtaka kesi hiyo inasimamiwa na wakili Emmanuel Chengula na Gervas Semgabo wakati upande wa utetezi ikisimamiwa na wakili Asifiwe Alinanuswe.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo Wakili wa mlalamikaji Emmanuel Chengula amesema kesi hiyo imesikilizwa kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo ambapo mteja wake ambaye ni Matlida Sigareti anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 za Kitanzania kutokana na madhara ambayo ameyapata.

Kwa upande wake Wakili wa utetezi Asifiwe Alinanuswe alipotakiwa kuzungumzia shtaka hilo alisema hajapewa maelekezo ya kuzungumzia kesi hiyo kutoka kwa mteja wake.

Hata hivyo, Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha ambapo imepangwa kusikilizwa tena Februari 21 mwaka huu.

Chanzo -  EATV
Share:

MTOTO WANGU ALIKUWA MWISHO DARASANI ILA KAFIKA CHUO KIKUU


Kila mtu ninayemwambia kuwa mtoto wangu ambaye sasa yupo Chuo Kukuu mwaka wa pili aliwahi kuwa mtoto wa mwisho darasani, haamini, wanaona kama ninadanganya.

Jina langu ni Mama Wini kutokea Kericho nchini Kenya, wakati mtoto wangu yupo shule ya msingi alikuwa mtu wa kupata maksi za chini sana katika masomo yake.

Kwa hakika kama mzazi jambo hilo lilinihuzunisha sana, mawazo yalikuwa ni mengi kiasi kwamba sikujua ni kitu gani hasa cha kufanya maana nilipenda mtoto wangu aje kufanikiwa kimaisha na elimu ndio msingi wa mafanikio hayo.

Nilijaribu kumtafutia masomo ya jioni pamoja na kipindi ambacho anakuwa likizo ili aweze kujifunza vizuri yale ambayo hakuelewa darasani, ila hivyo bado jitihada zangu hizi hazikuweza kuzaa matunda.

Hali hiyo ilizidi kunitia wasiwasi kuhusu hatma ya mtoto wangu, kama hatofanya vizuri katika elimu atakuja kuwa mgeni wa nani, atakuja kufanya nini katika hii dunia. Hayo ndio yalikuwa mashaka yangu.

Nashukuru rafiki yangu wa miaka mingi tangu utotoni, alipokuja kuniambia kuwa AfricanDoctors wanaweza kumaliza tatizo hilo kwani hata watoto wake walikuwa hawafanyi vizuri shuleni ila sasa wanapasi kila mtihani wanaofanya.

Ndipo mara moja tuliweza kuwasiliana nao na waliweza kunihakikishia kuwa tiba zao ni uhakika kabisa kwani wamesaidia maelefu ya watu ukanda wa Afrika Mashariki.

Ingawa moyoni nilikuwa na wasiwasi kuhusu jambo hilo maana ndio maana yangu ya kwanza kusikia tiba ya aina hiyo, niliamua kujaribu nione kama kweli inafanya kazi.

Kwa hakika naweza kusema tiba zao ni uhakika kwa asilimia 100, tangu wakati huo mtoto wangu akiwa darasa la sita, alianza kufaulu mfululizo hadi sasa ambapo yupo Chuo Kukuu. Asante sana AfricanDoctors.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Mwisho.
Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JANUARI 24,2023

















Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger