Friday, 20 January 2023

SERIKALI YAVITAKA VYUO VYA MAFUNZO KWA WALEZI WA WATOTO KUWA NA MPANGO WA PAMOJA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Dkt. Nandera Mhando,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia huduma za Jamii Ofisi ya Raisi-TAMISEMI Bi Amina Mfaki,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Kaimu Mkurugenzi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Asha Shami,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 

Mkurungenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Majid Mjengwa,akielezea taasisi hiyo ilivyoanza mpango huo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 


Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananachi Karumo Bi.Osmunda Kilasi,akizungumzia umuhimu wa mpango huo wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo ya Malezi wa Watoto nchini kilichofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dodoma. 

....................................... 

Na Alex Sonna-DODOMA 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amewataka watoa Mafunzo ya Walezi wa Watoto nchini kuwa na Mpango kazi wa pamoja utakaotumika kuwafundishia walezi wa Watoto. 

Hayo ameyasema leo Januari 19,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Vyuo vinavyotoa mafunzo hayo ya Malezi. 


“Kuna haja ya kuja na Mtaala wa pamoja ili kutatua changamoto ya Malezi na Makuzi ya Awali kwa watoto. Iwepo pia bodi ya usimamazi na Mwongozo utakaosaidia kuratibu eneo hili ili wahitimu wawe na Ujuzi utakaosaidia Watoto wetu”Alisema Wakili Mpanju. 

Wakili Mpanju amewasisitiza Wadau hao juu ya umuhimu wa kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya awali ya Watoto Nchini Ili kujenga watu wenye maadili na nidhamu kwa Taifa. 

Mpango wa ufundishaji wa mtaala mmoja uliasisiwa na Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) ambao walianza mafunzo kwa chuo kimoja Kisha wakapeleka kwa vyuo 10 kati ya 54 vya Maendeleo ya Jamii. 

“Tusipowekeza vya kutosha tutapata majanga ,Mnyonyoko wa Maadili utaendelea na hatimaye Taifa litapotea.”Ameongeza Mpanju. 

Kwa upande wake Kamishna wa Ustawi wa Jamii,Dkt. Nandera Mhando amesema lengo ni kuweza kufikia yale yaliyokusudiwa kupatikana kwenye Vyuo hivyo vinavyotoa Mafunzo kwa walezi Wa Watoto. 

“Kwa pamoja tuweke igezo vya pamoja ikiwemo Mitaala na mitihani ili tuweze kupata Wahitimu wanaokidhi na hatimaye kufanikisha nia ya Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii”amesema Dk.Mhando 

Aidha Dk.Mhando amesema kuwa msingi uliopandwa na KTO unapaswa kuendelezwa ili kuzaa matunda yatakayosambaa nchi nzima badala ya kuwa walalamikaji kuhusu kuharibiwa kwa maadili ya watoto. 

Naye Mkurungenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Karibu Tanzania Organization (KTO) Bw.Majid Mjengwa amesema kuwa taasisi hiyo ilianza mpango huo mapema kwa kushirikiana na baadhi ya vyuo ndipo wakabaini kwamba kuna ulazima wa kupeleka elimu hiyo Kwa vyuo vyote. 


Mjengwa amesema mwelekeo wa sasa ni kuona mtoto wa Kitanzania analelewa na kufundishwa misingi impasayo mwanadamu kuliko ilivyo sasa ambapo vituo ni vingi lakini kila mmoja anatoa mafunzo ya mwelekeo wake. 

Hata hivyo Bw. Mjengwa amesema kuwa mitaala inayotazamwa ni ya vituo vya watoto wadogo (Day care) ambako ndiko uliko msingi wa Mkuu wa ujifunzaji kwa mwanafunzi. 

"Tunashukuru Serikali imekubali mpango huu na kuahidi kupeleka vyuo vyote 54, hili ni jambo jema sana kwamba tunakwenda kuzalisha wataalamu wazuri wa malezi ya watoto Wetu," amesema Bw. Mjengwa. 


Mkurugenzi Msaidizi anayesimamia huduma za Jamii Ofisi ya Raisi-TAMISEMI Bi Amina Mfaki amesema Serikali inatoa kipaumbele kwa malezi na Makuzi ya Awali kwa watoto Nchini ili kujenga Taifa la Wananchi Wazalendo. 

“Mnaowandaa Walezi wa Watoto mna jukumu kubwa la kuhakikisha Mafunzo yanayotolewa Vyuoni yanaweza kuwakuza watoto na Vipaji vyao na Mwisho wa siku tutapata vijana wabunifu watakaoleta Maendeleo katika Taifa letu”amesema Bi.Mfaki 

Awali Kaimu Mkurugenzi Idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Bi Asha Shami amesisitiza juu ya Maudhui ya kuzingatia katika utoaji wa Elimu ya Awali kwa Watoto. 

“Tunategemea mtawalinda watoto kwa kuzingatia maudhui sahihi katika ufundishaji maana kumekua na changamoto nyingi za kimaadili zitokanazo na vitu ambavyo watoto wanajifunza mashuleni na Majumbani,Hivyo Maudhui yenye kuzingatia Mila na Tamaduni zetu ni muhimu.”Alisema Bi Asha . 


Nao Wakuu wa Vyuo na Wadau wanaotoa Mafunzo Kwa Walezi wa Watoto Nchini wameiomba Serikali kuhakikisha Mchakato wa kupata Mtaala wa Pamoja Nchini unakamilika Haraka ili waweze kuuanza kuutumia Katika Mafunzo yao .
Share:

Thursday, 19 January 2023

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 20,2023










Share:

MAMA MWENYE NYUMBA ANALILIA PENZI LANGU!

Hapa duniani kuna mambo yanaweza kukutokea hadi wewe mwenyewe ukawa unashangaa maana yake ni ipi hasa, ndicho nilichonikuta mimi pale ambapo mama mwenye nyumba aliponiita nyumbani na kuniambia kuwa ananitaka kimapenzi.

Jina langu ni Moses kutokea Lamu nchini Kenya, jioni moja nikiwa nimetoka kazini, nilimkuta mama mwenye nyumbani ameketi nje, aliniambia siku hiyo nisipike kwani kwake amepika chakula kingi sana, hivyo nitaenda kula kwake baada ya kuoga.

Basi nilipomaliza kuoga nilienda kugonga mlango wake, alipokea na kuniambia siku nyingine nikitaka kuja wala nisigonge bali niingie tu.

Nilikaa kwenye sofa na akaniletea chakula, cha ajabu alikuja akaa pembeni yangu, wakati nikila akawa ananipapasa mgongoni, mara akaniomba anivue shati kwa madai joto limezidi ndani na anaona mwili wangu umechemka sana ila nilimwambia haina shida kwani namalizia kula nitatoka nje kwenye upepo.

Kumaliza kula sikutaka kuendelea kukaa pale ndani, nilitoka nje huku yeye akinisistizia niendelee kuwa naye maana hana hata mtu wa kuzungumza naye. Sikujali hilo nilitoka na kwenda kwenye chumba changu na kuchukua maji nikaenda kuoga tena ili niweze kulala.

Nilipotoka kuoga nilikuta SMS yake kwenye simu akiniambia kuwa ananipenda na angependa kama nitamkubalia niwe mpenzi wake, aliomba sana nisije kumkatalia kwani yeye hajiwezi tena kwangu. Niishiwa nguvu na kujiuliza maswali mengi, nilishindwa kusema hapa maana kweli huyu mama kaumbika!.

Aliniambia yeye atakuwa ananipa fedha za matumizi na chochote nitakacho, kikubwa zaidi nitakuwa naishi katika nyumba yake bila kulipa kodi, hilo ndilo limenichanganya sana maana nahitaji fedha hizo.

Lakini ukweli ni kwamba hali hii ilinitokea baada ya mimi kutumia dawa za mvuto wa mapenzi kutoka kwa AfricanDoctors, ila mimi nilikuwa nahitaji binti ila huyu mama ni mzuri ajabu na ana fedha sana, kwa kweli moyo wangu umezidiwa sana, mwenyewe namtamani sana sijui hata nifanyaje!.

Wasiliana na AfricanDoctors kwa namba +254719153099.

Mwisho.
Share:

Video & Picha : SHOW YA MAMA USHAURI, WAKATI MAKAMU WA RAIS AKIWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI TINDE

 
Malunde 1 blog imekusogezea VIDEO na Picha Msanii wa Nyimbo za Asili Maarufu MAMA USHAURI kutoka Tinde Shinyanga akitoa Burudani wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiweka Jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwenye Mji wa utakaonufaisha wananchi 60,000 katika vijiji 22 vya Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Dkt. Mpango ameweka jiwe la Msingi la Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria kwa Mji wa Tinde leo Alhamis Januari 19, 2023 katika Tangi la Maji la Buchama – Tinde wilaya ya Shinyanga. 

Tazama Video na Picha Hapa chini Mama Ushauri Akitoa Burudani
 
Mama Ushauri akiimba


Mama Ushauri na Vijana wake wakitoa burudani

PICHA ZOTE Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog




Share:

PPRA YAFANYA UTAFITI WA AWALI KUHUSU MATUMIZI YA KIKOSI KAZI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO NCHINI.


Moja ya shule ya sekondari Halmashauri ya Kahama inayojengwa kwa kutumia nguvu kazi “Force account” . Ujenzi huo unatekelezwa kwa kupitia mradi wa SEQUIP 

************** 

Na. Zawadi Msalla 

Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma nchni (PPRA) imeeleza kuwa utumiaji wa utaratibu wa kikosi kazi “ Force Account “katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni njia inayofaa ikiwa itasimamiwa vyema. 

Hayo yalibainishwa katika utafiti mdogo uliofanywa na Mamlaka, ili kuangalia ufanisi wa utumiaji wa kikosi kazi katika miradi ya maendeleo ya ujenzi inayoendelea hapa nchini. Utafiti huo ulihusisha miradi 175 iliyofanywa kwa njia ya kikosi kazi . 



Meneja Utafiti na Nyaraka wa Mamlaka Mhandisi Nashon Masunya alieleza kwamba, hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la matumizi ya njia ya kikosi kazi katika miradi ya umma hasa katika ujenzi wa shule, vituo vya afya, majengo ya Serikali na ujenzi wa nyumba zinazomilikiwa na Serikali. 

Alisema, ongezeko hilo limepelekea baadhi ya maeneo hoja nyingi kuibuliwa juu ya ukiukwaji wa maadili ya ununuzi na usimamizi wa mikataba na hivyo kupelekea matumizi makubwa ya fedha wakati wa utekelezaji wake. 

Mhandisi Masunya alieleza utafiti huo ulilenga kuangalia thamani ya fedha (Value for Money) na kuona endapo njia hiyo ni njia sahihi kwa matumizi ya kutekeleza miradi ya maendeleoili kuiwezesha Mamlaka kutoa ushauri sahihi kwa Serikali na wadau wengine wa maendeleo juu ya matumizi ya kikosi kazi. 

“Tuliamua kufanya utafiti ili tuone kama njia hiyo ya Force Account ni salama kutumiwa na Serikali kutokana na hoja nyingi zinazoibuliwa sio tu na viongozi bali hata wananchi” Alisema. 

Mhandisi Masunya alisema yapo maeneo ambayo yamefanikiwa katika utekelezaji wa miradi kwa kutumia njia hii licha ya baadhi ya maeneo mengine kushindwa kufanya vizuri. 

Mhandisi Masunya alieleza kuwa PPRA ndiyo Mamlaka yenye wajibu wa kusimamia ununuzi wa Umma nchini, hivyo ina wajibu wa kuhakikisha thamani ya fedha na uwazi katika ununuzi unaonekana. Akieleza zaidi kuhusu njia hiyo alisema Sheria imeweka wazi kuwa yapo mazingira yanayo weza kulazimu taasisi kutumia njia hiyo. Mazingira hayo ni kama taasisi inayotaka kutekeleza mradi inaona kazi hiyo sio kubwa na maeneo ya mradi huo ni mbali kufikika. 

Mhandisi Masunya alizikumbusha taasisi kuwa kigezo cha muhimu ni lazima zihakikisha kuwa wapo wataalamu ndani ya taasisi wanaoweza kusimamia na kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi. 

Utafiti huo ulijumuisha miradi iliyofanywa katika sekta ya afya, maji na elimu kwa kutumia fedha za UVIKO – 19. Utafiti huo uliangalia pia pia kaguzi maalum zilizofanywa na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa fedha za Serikali (CAG) katika miradi yasekta ya Elimu kwa mwaka 2020 na Kaguzi maalum zilizofanywa na PPRA katika sekta ya afya mwaka 2020.
Share:

DUCE WAZINDUA KITUO CHA UTAFITI MASUALA YA KIJINSIA



Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam. 


Naibu Rasi ,Taaluma,Utafiti na Ushauri elekezi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Dkt.Christina Raphael,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam. 


Wadau mbalimbali wa Tafiti kwenye masuala ya Jinsia wakifatilia hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam. 


Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka akiwa pamoja na Mwakilishi wa Ubalozi Irish Bi.Mags Gaynar akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam. 


Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka,akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa utafiti masuala ya kijinsia mara baada ya kuzindua Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam. 



Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) Prof.Stephen Maluka,akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa utafiti masuala ya kijinsia mara baada ya kuzindua Kituo cha Utafiti Masula ya Kijinsia hafla iliyofanyika leo Januari 19,2023 jijini Dar Es Salaam. 

PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO 

........................ 

Na Emmanuel Mbatilo-DAR ES SALAAM 

CHUO Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE) kimezindua Kituo cha Utafiti Masuala ya Kijinsia kwa Ufadhiri wa Ubalozi wa Irish kitakuwa na kazi ya kufundisha masuala ya kijinsiana na masuala ya tafiti za kijinsia pamoja na kufanya ushauri kwa mambo mbalimbali yanayohusu masuala ya kijinsia. 

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo Januari 19,2023 DUCE Jijini Dar es Salaam, Rasi wa Chuo Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Prof.Stephen Maluka amesema Kituo hicho kinaenda kuwa sehemu ya tafiti mbalimbali za kijinsia zinakwenda kuratibiwa na na kinaenda kujenga uwezo wa watafiti mbalimbali nchini. 

"Kituo hiki kinaenda kutoa uwezo wa namna ambavyo hata Serikali na mashirika mengine yanaweza kwenda kuangalia namna wanvyoweza kuyaingiza masuala ya usawa wa kijinsia kwenye mipango yao, sera zao na hata kwenye mambo mbalimbali ili kuweza kuhakikisha kwamba kila tunachokifanya tunaweka usawa wa kijinsia mbele". Amesema 

Amesema wanafunzi watakuwa ni sehemu ya kituo hiki kwani wataanza kujengewa uwezo kuhusiana na namna ambavyo wanaweza kufanya utafiti kuhusiana na masuala ya kijinsia lakini pia Vyuo Vikuu huwa wanawashirikisha wanafunzi katika kufanya tafiti hivyo watawahimiza wanafunzi kufanya tafiti zinazohusiana na masualaya kijinsia. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Bw.Yohana Sekimweli ameshauri vyuo vingine kuona Chuo cha DUCE kama mfano kuanzisha vituo vya utafiti kwenye masuala ya kijinsia ili kuweza kulikomboa taifa linafikia kwenye usawa wa kijinsia wa hamsini kwa hamsini. 

Amesema mpaka kumekuwa na uwanzilishwaji wa madawati ya kijinsia kwenye maeneo mbalimbali hivyo basi kuanzishwa kwa vituo kama hivi vitasaidia kupunguza mauala ya unyanyasaji wa kijinsia kwenye taifa letu na baadae kuweza kuondokana na masuala kama haya. 

Nae Mratibu wa Kituo cha Utafiti Masuala ya Kijinsia DUCE Dkt.Cresencia Massawe amesema kundi la walimu ni muhimu katika kufikisha uelewa wa masuala ya kijinsia na kueleta mabadiliko makubwa endapo wakiivishwa kwenye masuala ya kijinsia .
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger