Monday, 28 November 2022
WADAU WA NISHATI NCHINI WAKUTANA KUJADILI MPANGO WA MATUMIZI BORA YA NISHATI KWENYE MAJENGO
Shirika la Umoja la Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati imeandaa warsha ya siku mbili ya wadau wa nishati kutoka Wizara ya Nishati, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, EWURA, TANESCO, Baraza la Taifa la Ujenzi, na TAMISEMI yamefanyika Bagamoyo kuanzia 25-26 Novemba 2022 kujadili namna bora ya matumizi bora ya nishati nchini.
Mradi huu wa Mpango wa Matumizi Bora ya Nishati Tanzania unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) na kutekelezwa na Wizara ya Nishati kwa kushirikiana na Shirika la Umoja aa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP).
‘Mratibu wa mradi wa Mpango wa Matumizi Bora ya Nishati Tanzania, Bwana Aaron Cunningham alisema “warsha hii imekusudia kujadili majukumu ya washikadau katika kutekeleza na kuendeleza matumizi bora ya nishati katika majengo, kwa kushirikiana na Baraza la Ujenzi la Taifa tumekusudia kushirikiana na wizara ya ujenzi kuandaa mfumo wa matumizi bora ya nishati katika majengo makubwa.
Aliongeza kwa kusema ‘mpango huu wa uundaji na uendelezaji wa majengo yenye kuzingatia matumizi bora ya nishati yatasaidia kupunguza matumizi yasiyosahihi ya nishati na kuokoa fedha pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya Tabianchi.” – Aaron Cunningham, UNDP.
Ripoti ya nishati Tanzania ya mwaka 2018 inaonyesha nishati kwa kiasi kikubwa inatumika kwenye majengo ya biashara, makazi ya watu na viwandani. Mpango kazi wa taifa wa nishati umetambua sekta ya majengo kama sekta muhimu kwenye kupunguza matumizi yasiyo sahihi ya nishati.
Nae mkurugenzi wa huduma za kiufundi kutoka baraza la Taifa la Ujenzi, Mhandisi Moses Lawrence alisema ‘Wizara ya ujenzi na uchukuzi ipo kwenye mchakato wa kuandaa sheria ya ujenzi wa majengo (building act and building codes) ambapo itazingatia nishati bora na endelevu na hivyo kuwataka wadau kutoa michango ya mawazo ili kufanikisha mchakato huu.
Mradi wa Mpango wa Matumizi Bora ya Nishati Tanzania unaotekelezwa na UNDP kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati utangalia na kuzingatia namna bora ya kushirikiana na Baraza la Taifa la Ujenzi kufanikisha malengo haya.
Mhandisi Moses aliongeza kwa kusema uzingatiaji wa matumizi bora ya nishati kwenye majengo katika hatua za mwanzo za ujenzi ni wa gharama nafuu zaidi kuliko uboreshaji baada ya ujenzi. Kwa hiyo, maamuzi yaliyofanywa hatua za mwanzo za ujenzi wa jengo yataamua matumizi ya baada ya jengo kukamilika. – Eng. Moses Lawrence.
Ujenzi wa kuzingatia matumizi bora ya nishati utasaidia kubadilisha sekta ya ujenzi kuwa mazingira rafiki, gharama nafuu, na matumizi bora ya nishati. Kama matokeo ya muda mrefu, kanuni za ujenzi wenye kuzingatia matumizi bora ya nishati zitachangia lengo la 7 la Maendeleo Endelevu (SDGs) ambalo linahusu nishati safi na himilivu (Affordable and Clean Energy) kwa wote, na lengo la 13 linalohusu hatua za kuchukuwa kupambana na mabadiliko ya tabianchi (Climate Action) ambalo linalingana na vipaumbele vya maendeleo vya kitaifa.
Mpango wa matumizi bora ya nishati katika sekta ya ujenzi utasaidia juhudi za serikali za kutoa nishati ya kutosha na ya uhakika, hususani umeme, ili kukidhi ongezeko la mahitaji. Pia itaongeza ufahamu wa watumiaji kuhusu manufaa ya majengo yenye kufuata kanuni za ujenzi na matumizi bora ya nishati.
STAKEHOLDERS MEET TO DISCUSS ENERGY EFFICIENCY AND BUILDING CODES IN TANZANIA
Bagamoyo, 26 November 2022. The United Nations Development Programme (UNDP) in collaboration with the Ministry of Energy has organized a two-day workshop for Tanzania energy stakeholders from the Ministry of Lands, Housing and Human Settlement, EWURA, TANESCO, National Construction Council (NCC) and the President's Office - Regional Administration and Local Government (PO-RALG), held in Bagamoyo from 25-26 November 2022 to discuss the stakeholder’s roles to effectively implement Project Action 3 "Development and implementation of a framework for energy performance certification in large buildings in the country.
The Tanzania Energy Efficiency Action Plan project is funded by the European Union (EU) and implemented by the Ministry of Energy in collaboration with UNDP.
The Energy Efficiency Project Coordinator, Mr Aaron Cunningham, argues that the workshop intends to discuss stakeholders’ roles in effectively implementing Project Action 3 "Development and implementation of a framework for energy performance certification in large buildings.
He added, "This plan for the development and promotion of energy-efficient building codes and building energy performance certification will help reduce greenhouse gas emissions and pollution produced by the combustion fuel fossils, also the potential to save money."
The 2018 Energy Report in Tanzania estimates that 67% of energy consumption is in residential, commercial, and public buildings. As a result, the national action plan on energy efficiency has identified the building sector as an important sector for energy consumption reduction.
Eng. Moses Lawrence, the director of technical services for the Tanzania National Construction Council, said that the Ministry of Works and Transportation is in the process of developing the Building Act, which has considered the importance of energy efficiency in buildings. Through the NCC, the government will work with UNDP and other stakeholders to ensure the energy efficiency segment is part of the new Building Act and aligned with the National Energy Policy of 2015 and Goal 7 (Affordable and Clean Energy) of the Sustainable Development Goals (SDGs).
He added, "improvement of buildings’ efficiency at the planning stage is more cost-effective compared to improvements after their initial construction. Therefore, decisions made during a building’s project phase will hence determine consumption over a building’s lifetime".
Energy efficiency building codes can help transform the sector to be more environmentally friendly, cost-effective, and energy efficient. As a long-term impact, the energy efficiency building codes will contribute to SDG 7 on energy and promote progress towards Goal 13 on climate action, which aligns with the national development priorities. Energy efficiency in the building sector will support the effort of the government to provide sufficient and reliable energy, particularly electricity, to meet increased demand. It will also raise awareness among users of the benefits of more energy-sustainable buildings.
Written by Jolson Masaki, Communications Analyst - UNDP
Sunday, 27 November 2022
RAIS WA BURUNDI AIPONGEZA BENKI YA CRDB
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye akiwa kwenye mazungumzo na ujumbe wa Benki ya CRDB, ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Dkt. Ally Laay na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati walipomtembelea kwenye makazi rasmi yaliyopo eneo la Kiriri, Bujumbura, Novemba 25, 2022. Mkutano huo ilikuwa ni sehemu ya muendelezo wa maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi, ambayo kilele chake kilifanyika mwishoni mwa wiki. Picha zote na Othman Michuzi.
========= ======== ========
Bujumbura, Burundi. Ikitarajia kufungua tawi la tano mapema mwakani itakapofikisha miaka 11 ya kutoa huduma za fedha nchini Burundi, Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye ameipongeza Benki ya CRDB kwa huduma bora ilizozitoa kwa muongo mmoja sasa.
Benki hiyo iliyoingia nchini Burundi mwaka 2012 ina matawi manne kwa sasa yanayotoa huduma pamoja na mawakala zaidi ya 600 wanaohakikisha wananchi na wafanyabiashara wanahudumiwa kwa wakati na mapato ya Serikali kukusanywa kwa utaratibu rahisi nchini humo.
Rais Ndayishimiye ametoa pongeza hizo alipozungumza na menejimenti ya Benki ya CRDB iliyoongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wake, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi kusherehekea miaka 10 ya kutoa huduma nchini humo.
“Burundi tumeipokea Benki ya CRDB kwa mikono miwili na tunajivunia uwepo wake. Tanzania na Burundi ni ndugu wa karibu, hata mipaka iliyopo ni matokeo ya ukoloni lakini haiwezi kuwa kikwazo cha mahusiano mazuri yenye historia kubwa ya ushirikiano. Tunashukuru kuwa Tanzania ilishiriki kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa amani Burundi na sasa mnakuja tufanye maendeleo kwa pamoja kwa manufaa ya nchi zetu,” alisema Rais Ndayishimiye.
Katika kipindi hicho cha kutoa huduma nchini Burundi, Benki ya CRDB imefanya vyema sokoni hadi kushika nafasi ya tatu kwa kupata faida kubwa kati ya benki 13 zilizopo. Mpaka Septemba mwaka huu, benki hiyo ilikuwa imetoa mikopo kiasi cha faranga 300 bilioni (Sh338 bilioni).
Mwaka 2019 Serikali ya Burundi iliyahamisha makao makuu yake kutoka Bujumbura kwenda jiji la Gitega hivyo Benki ya CRDB inatarajia kufungua tawi jipya huko ili kuihudumia pamoja na wafanyakazi wake, wafanyabiashara na wananchi wa kawaida. Tawi hilo litafunguliwa mapema mwakani.
“Tunawashuru sana kwa jitihada zenu ya kutoa elimu ya fedha kwa Warundi ili wajifunze namna nzuri ya usimamizi wa fedha na kuwekeza. Tungependa kushirikiana nanyi zaidi katika programu za vijana na wanawake ambao ni kipaumbele chetu kikubwa kwa sasa,” alisema Rais Ndayishimiye.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa CRDB, Nsekela alisema Serikali ya Burundi inawapa ushirikiano mkubwa unaowasaidia kupata mafanikio ndani ya miaka 10. Serikali imeipa benki9 hiyo eneo la kujenga ofisi katika Jiji la Gitega.
“Benki ya CRDB itaendelea kuunga mkono jitihada za kukuza uchumi wa Burundi kwa manufaa ya Warundi, Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla. Tunatarajia kuingia DRC (Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) hivi karibuni na tutafungua matawi katika mikoa iliyo karibu na mpaka wa Burundi na DRC ili kuchochea biashara kati ya nchi hizo mbili,” alisema Nsekela.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa CRDB, Dk Ally Laay alisema haikuwa rahisi kuridhia uamuzi wa kufungua biashara nchini Burundi kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kutoa huduma nje ya nchi.
“Maswali yalikuwa mengi juu ya kuichagua Burundi lakini leo hii sote tunajivunia na kuona nchi zote mbili zinanufaika. Hapa Burundi tunalipa kodi na kutoa ajira huku faida inayopatikana ikiwanufaisha wanahisa wetu hadi Tanzania,” alisema Dk Laay.
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Evariste Ndayishimiye (katikati) akimpongeza Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kulia) wakati walipomtembelea kwenye makazi rasmi yaliyopo eneo la Kiriri, Bujumbura, Novemba 25, 2022. Kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Kahumbya Bashige
Rais wa Jamhuri ya Burundi, Évariste Ndayishimiye akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, baada ya kumaliza mazungumzo yao walipomtembelea kwenye makazi yake rasmi yaliyopo eneo la Kiriri, Bujumbura, Novemba 25, 2022. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fredrick Siwale (wapili kushoto), Afisa Mkuu wa Uwendeshaji wa Benki ya CRDB, Bruce Mwille (kulia), Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, Mjumbe wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Kahumbya Bashige pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Menard Bucumi. Mkutano huo ilikuwa ni sehemu ya muendelezo wa maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi, ambayo kilele chake kilifanyika mwishoni mwa wiki.
SIMBA SC YAIFANYIA UMAFIA POLISI TANZANIA, YAICHAPA 3-1
****************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Simba imefanikiwa kuonoka na alama tatu mbele ya timu ya Polisi Tanzania baada ya kuichapa mabao 3-1 kwenye mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la Ushirika mjini Moshi.
Kwenye mechi hiyo tumeshuhudia mshambuliaji wao Moses Phiri akiweka kambani mabao mawili na kumfanya awe na mabao nane kwenye ligi kuu NBC na kuwa nafasi ya pili kwenye ufungaji mabao huku akiongza Fiston Kalala Mayele ambaye anamabao kumi.
Simba Sc ilianza kupata bao la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao John Bocco ambaye kwasasa amekuwa kwenye kiwango kizuri katika mechi tatu za hivi karibunu alivyoanza kupata nafasi kwenye kikosi.
Bao pekee la Polisi Tanzania limefungwa na Zuberi Khamisi dakika za lala salama
SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA TAASISI ZA DINI KWA TAIFA-DKT MABULA
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akiwasili katika Kanisa la AICT Kizota tayari kuzindua Dayosisi mpya ya Kanda ya Kati ya Kanisa hilo pia kushiriki kusimikwa na kuwekwa wakfu Askofu Mteule Amos Katoto Ngeze kuwa Askofu wa kwanza wa kanisa la African Inland Church Dayosisi ya kati Dodoma. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akiweka tayari kukata utepe kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kanisa Kuu la Africa Inland Church Tanzania Dayosisi ya kati Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akikata utepe kuzindua Ujenzi wa Kanisa Kuu la Africa Inland Church Tanzania Dayosisi mpya ya kanda ya kati Dodoma. 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabura akikata utepe kuzindua Ujenzi wa Kanisa Kuu la Africa Inland Church Tanzania Dayosisi mpya ya kanda ya kati Dodoma. 
Askofu Mteule Amos Katoto Ngeze mara baada ya kuwekwa Wakfu na kusimikwa kuwa Askofu wa kwanza wa kanisa la African Inland Church wa kanda ya Dayosisi ya kati Dodoma.
*********************
Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa taasisi za dini katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo miradi mingi ya kijamii inayosimamiwa na mashirika ya kidini hususani sekta ya afya, elimu na maji .
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabura alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwenye uzinduzi wa Dayosisi mpya ya Kati ya Kanisa la Tanzania Inland Church Jijini Dodoma.
Pamoja na uzinduzi wa Dayosisi ya Kati Kanisa hilo pia limeshuhudia uwekaji wa jiwe la Msingi la Kanisa Kuu na Kusimikwa kwa Askofu mpya wa Dayosisi hiyo Askofu Mteule Amosi Katoto Ngeze kuwa kiongozi mpya wa kanisa hilo Dayosisi ya Kati.
Dkt. Mabula Katika hotuba yake hiyo amebainisha kuwa Watanzania wengi wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma za kijamii zinazotolewa na taasisi na mashirika ya dini na madhehebu mbalimbali na kutoa shukrani zake kwa mchango mkubwa wa kanisa akiliomba kuendelea kuwahudumia Watanzania.
‘’Kutuunga mkono kwa namna hiyo ndiko kunachangia sana nchi yetu kupiga hatua kubwa kwenye maendeleo hususan kufikisha huduma kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu’’.Aliongeza Dkt. Angeline Mabula Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Dkt Mabula pia aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na madhebu ya dini kuboresha maisha ya Watanzania na kupokea ushauri kama ambayo serikali imekuwa ikipokea na kufanyia kazi ushauri huo na kuwashirikisha katika mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Aidha Dkt. Mabula aliongeza kuwa serikali inatambua mchango wa kanisa katika kulinda na kudumisha amani katika nchi akilitaja suala la amani kuwa ni suala muhimu sana kwani bila ya amani hakuna maendeleo.
Dkt. Mabula alibainisha kuwa Taifa bila amani, hata haki na uhuru wa kumwabudu na kumtukuza Mungu wetu utakuwa mashakani hivyo, hatuna budi kusimamia haki sambamba na kuenzi na kuitunza amani yetu kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.
Kwa sababu hiyo, Dkt. Mabula aliwasihi sana viongozi wa dini kuwakumbusha mara kwa mara waumini, na watu wote, kuhusu umuhimu wa kusimamia haki na kudumisha amani aliyotuachia Bwana wetu Yesu Kristu na kuiombea nchi na viongozi wake. ‘
Kuhusu Suhala la maadili Dkt.Mabula aliwaomba viongozi wadini wasichoke kufundisha na kulea vijana katika maadili mema na kuthamini kufanya kazi halali.
‘’Katika nyakati hizi, ni ukweli ulio wazi kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili katika jamii yetu. Vitendo viovu na mambo yasiyompendeza Mwenyezi Mungu yanazidi kuongezeka, Mambo ambayo siku za nyuma yalikuwa nadra sana kutokea au kusikika sasa yanakuwa habari za kila siku na wakati mwingine huonekana ati ni kawaida’’. Aliongeza Dkt Mabula.
Waziri Mabula anaamini kwa dhati kuwa watu, wakiwa pamoja na sisi viongozi wa Serikali na wa vyama vya siasa wakishika mafundisho ya dini, wakawa na hofu ya Mungu, maovu mengi yatapungua sana na nchi yetu itaongozwa vizuri.
Naye Baba Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Mussa Masanja Magwesela amesema kuwa Kanisa la AICT linayo maono ambayo ni kuona “Watu wote wanamwabudu Mungu katika roho na kweli na wanaishi maisha ya utoshelevu”.
‘’Hii maana yake ni kwamba tunatambua kuna watu bado hawajamjua Mungu wa kweli hivyo wanahitaji kufikiwa. Katika Petro 3:9 Neno la Mungu linasema “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba”. Aliongeza Baba Askofu Magwesela.
Aidha,Askofu Magwesela aliongeza kuwa kanisa linao wajibu wa kuwafikia watu kwa mahitaji yao mbalimbali, maana tunaishi katika nafsi tatu, mwili, roho na nafsi. Vyote vinahitaji kuhudumiwa, na nijukumu la Kanisa la Mungu kuwafikia watu wote kwa kuwaangazia mambo yote haya.
NZUNDA AIPA KONGOLE TVLA.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (katikati) akifanya tukio la ufunguzi wa jengo jipya la la Maabara na Ofisi, Kituo cha Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kinachohudumia wafugaji wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa TVLA Dkt. Stella Bitanyi na kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi wa muonekano mpya wa Tovuti ya Wakala (www.tvla.go.tz) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kuhusiana na maabara mpya ya Kituo cha Iringa itakavyofanya kazi mara baada ya kufunguliwa Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (Katikati waliokaa), Watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) na viongozi wa Mkoa wa Iringa walipokuja kwenye halfa fupi ya kuhitimishwa kwa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi wa muonekano mpya wa Tovuti ya Wakala (www.tvla.go.tz) Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) Dkt. Stella Bitanyi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda kuhusiana na maabara mpya ya Kituo cha Iringa itakavyofanya kazi mara baada ya kufunguliwa Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa kwenye hafla ya kuhitimisha wa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda (Katikati waliokaa), Watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) na viongozi wa Mkoa wa Iringa walipokuja kwenye halfa fupi ya kuhitimishwa kwa Wiki ya TVLA iliyoanza Novemba 21 hadi 25, 2022 ambavyo ilikwenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 10 ya TVLA, ufunguzi wa jengo jipya la Maabara na Ofisi, Kituo cha Iringa, uzinduzi wa Tovuti mpya ya Wakala na Mfumo wa Kidigitali kwa ajili ya Usajili wa viuatilifu vya mifugo na ufuatiliaji wa uzalishaji na usambazaji wa Chanjo, Novemba 25, 2022 eneo la Isoka Machinjioni kata ya Kwakilosa Mkoani Iringa. 
**********************
◼️ Yahamasisha uanzishwaji wa Wiki ya Mifugo
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Bw. Tixon Nzunda ameipongeza Waakala ya Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) kwa ubunifu wa kuadhimisha wiki maalum ya wakala hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya kuanzishwa kwake ambapo kufuatia kufana kwa Maadhimisho hayo Nzunda amemuagiza Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo nchini Prof. Hezron Nonga kuweka utaratibu wa kuanzisha wiki ya Mifugo kuanzia mwaka ujao wa fedha ambayo itazishirikisha Taasisi zote za Serikali zilizopo chini ya Wizara ya Mifugo pamoja na zile zilizopo Sekretariati za Mikoa, mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau kutoka Sekta binafsi.
Nzunda ametoa pongezi hizo kwenye kilele cha Maadhimisho hayo kilichofanyika Novemba 25,2022 mkoani Iringa ambapo hafla hiyo pia iliambatana na Ufunguzi wa jengo jipya la kituo cha Wakala hiyo kilichopo eneo la Isoka Machinjioni mkoani humo kinachotarajiwa kuhudumia wafugaji wote waliopo kanda ya nyanda za juu kusini.
“Ubunifu huu ndio mtazamo wa Wizara kwa sasa na kwa kufanya hivi sio tu tumeweza kutangaza shughuli za Taasisi bali tumefanikiwa kuelimisha umma na kufanya mawasiliano ya karibu na jamii tunayoihudumia kupitia vyombo vya habari, vikundi mbalimbali na mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na Tovuti ya Wakala na ninaamini Taasisi nyingine zilizopo chini ya Wizara zitaiga jambo hili” Ameongeza Nzunda.
Akizungumzia jengo jipya la Wakala hiyo alilolizindua Nzunda amewataka viongozi wa Mkoa wa Iringa kuwahamasisha wananchi na wafugaji wote mkoani humo kutumia huduma zinazotolewa kituoni hapo ili waweze kuboresha mifugo yao na kukuza uchumi wa mfugaji mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
“Huu ni wakati wa kufuga kisayansi na ndio maana tumewaletea kituo hiki ili kiwasaidie kutekeleza shughuli zenu za ufugaji kisasa zaidi na kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia yaliyopo ulimwenguni kote hasa kupitia mfumo mpya wa kidijitali wa kusajili viuatilifu vya mifugo, ufuatiliaji, uzalishaji na usambazaji wa chanjo unaotumiwa na TVLA kwa sasa na kwa hili niwapongeze sana kwani mtapunguza upotevu wa mapato na kurahisisha sana utendaji wenu” Amesema Nzunda.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo Dkt. Stella Bitanyi amesema kuwa katika kipindi cha Wiki moja ya Maadhimisho hayo, Wakala hiyo imefanikiwa kutoa bure dozi 150,000 za chanjo ya magonjwa ya Kimeta, Mdondo, Homa ya mapafu ya Mbuzi/Ng’ombe, Chambavu na Kutupa mimba zenye thamani ya zaidi ya Tshs.Mil.5 Kutembelea viwanda 50 vinavyozalisha vyakula vya Mifugo ili kutoa elimu ya uhakiki wa ubora wa vyakula vinavyozalishwa, kuhamasisha wananchi juu ya matumizi ya huduma na bidhaa zinazotolewa na Wakala hiyo kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutembelea na kutoa misaada kwa wasiojiweza na kwenye vituo 7 vya Watoto yatima vilivyopo maeneo mbalimbali hapa nchini, kufanya uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya mifugo bure kwenye sampuli 400 za wanyama mbalimbali katika maabara za Wakala, kutoa huduma za uogeshaji bure kwa Mbwa 200 na kuwahamasisha wananchi kutumia huduma ya usajili na uchambuzi wa ubora wa viuatilifu vya Mifugo ambayo sasa inatolewa na Wakala hiyo kupitia vituo vyake vyote nchini.
“Sambamba na hayo Wakala katika kutekeleza majukumu yake kwa kipindi cha miaka 10 tunajivunia mafanikio tuliyopata katika kutoa huduma na bidhaa za kiveterinari hapa nchini na miongoni mwake ni pamoja na Kuongezeka vituo 2 vya maabara kutoka vituo 11 mwaka 2012 hadi 13 mwaka 2022, Kupatikana kwa Ithibati (accreditation) katika uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya mifugo kulingana na kanuni za kimataifa, kuongeza mapato ya ndani kutoka milioni 220 hadi bilioni 3.1 kwa mwaka 2022, na kujengea uwezo maabara ya kupima ubora wa vyakula vya mifugo, kuangamiza Mbung’o wanaoeneza ugonjwa wa Nagana kwa Ng’ombe na Malale kwa binadamu pamoja na Kupewa jukumu jipya la kusajili na kuthibitisha ubora wa viuatilifu vya mifugo kuanzia mwezi Julai 2022” Ameongeza Dkt. Bitanyi.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Elias Luvanda mbali na kuishukuru Wizara kwa kuamua kujenga Kituo cha Wakala hiyo mkoani kwake, amesema kuwa kituo hicho kimejengwa mahali sahihi kwani mkoa huo ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya Mifugo ambapo mpaka sasa una takribani mifugo Mil. 8.7 ambayo inajumuisha Ngombe Mbuzi, Kondoo, Nguruwe, Punda, Kuku, Mbwa na Paka.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa ambako ndipo kilipojengwa kituo hicho Mhe. Ibrahim Ngwada alisema kuwa Halmashauri yake itaendelea kuweka mazingira Wezeshi kwa Serikali kutekeleza miradi yake ambapo ameahidi kufikisha kwenye vikao vyao vya kisheria suala la lililokuwa eneo la Wakala ya Maabara ya Veterinari nchini lililochukuliwa na Halmashauri hiyo ili lirejeshwe kwa wakala hiyo jambo ambalo litaiwezesha kupanua wigo wa huduma zake.
Akiongea kwa niaba ya wafugaji, mwakilishi wa Mkurugenzi wa ASAS LTD Dkt. Isaya Keto amesema kuwa wao kama sekta binafsi wanajivunia uwepo wa Wakala hiyo nchini ambapo ameishukuru kwa ushirikiano wanaotoa kwa wafugaji huku akisisitiza wafugaji wenzake wote nchini kutumia chanjo zinazozalishwa na wakala hiyo kutokana na ubora wa chanjo zake..
Maadhimisho ya Wiki ya Wakala ya Maabara ya Veterinari nchini (TVLA) yalikuwa na kauli mbiu isemayo “Tambua, Tibu na Dhibiti Magonjwa ya Mifugo” na yalianza rasmi Novemba 21-25 mwaka huu.
Saturday, 26 November 2022
DIT YAANDAA KOZI MPYA ZITAKAZOWEZESHA JAMII KUENDANA NA MAPINDUZI YA NNE YA VIWANDA

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) inaandaa kozi mpya zitakazowezesha jamii kuendana na Mapinduzi ya nne ya viwanda ambazo zitasaidia kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Mkuu wa Taasisi Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam Prof. Ezekiel Amri katika ufunguzi wa warsha kwa wadau iliyofanyika kampasi Kuu ya Dar es salaam yenye lengo la kukusanya maoni kwa ajili ya kuboresha mitaala ya kufundishia kozi hizo katika ngazi ya Uzamili na Stashahada.
Prof. Amiri amezitaja kozi hizo kuwa ni Uzamili katika Uhandisi Komputa, Uzamili katika Uhandisi Mawasiliano Angani, Uzamili katika Usalama wa Kimtandao pamoja na Stashaha ya Mitambo Viwandani.
Prof Amir ameeleza kuwa, DIT imeaanda warsha hiyo ili kupata maoni ya Wadau kulingana na mahitaji ya soko la ajira ambapo amesema kuwa maoni yao yatatumika katika kuandaa mitalaa itakayoendana na mapinduzi ya nne ya viwanda pia kusaidia kutatua changamoto katika jamii.
“Mapinduzi ya nne ya viwanda yanaenda kasi sana na yamejikita katika Tehama, ni muhimu kujiandaa kwa kuwa na mitaala yetu inayoendana na mapinduzi haya ili tusibaki nyuma ". Amesema Prof Amir
Ameeleza kuwa, mapinduzi hayo yana fursa na changamoto za kufanyia kazi hivyo kwa kuboresha mitaala hiyo itawawezesha vijana watakaosoma kozi hizo kuendana na mapinduzi hayo kwa kuwa wataenda kukidhi mahitaji yaliyopo viwandani na kwenye jamii.
Prof Amir ameendelea kusisitiza kuwa, taasisi imeona umuhimu na mahitaji ya kozi hizo na namna ambavyo itawawezesha vijana katika soko la ajira na hiyo ndiyo sababu iliyopelekea kuandaa mitaala itakayoendana na mabadiliko hayo.
Aidha, amewataka wadau kutoa maoni yao kutokana na wanachokiona kwenye jamii kwa sasa na mbeleni kwa kuwa maoni yakiwa mazuri ndiyo yatakayozalisha mitaala bora. Amesema “Uwepo wenu katika warsha hii ni muhimu sana, maoni yenu ni ya muhimu kwani mawazo mtakayoyatoa yatasaidia uboreshaji wa mitaala hii”.
Naye Mratibu wa program hiyo ya kuandaa mitaala, Daktari Paul Mbaga amesema kuwa kikao hicho ni muhimu kwani nia kubwa ni kuiwezesha DIT kuja na mitaala itakayotatua changamoto zilizoko katika jamii.
“Ninyi mtatusaidia kuona tunachokiandaa kama kitafaa katika jamii katika kutatua changamoto za jamii na ndio sababu kubwa iliyopelekea kuwaomba mshiriki kwenye zoezi hilo.
Warsha hiyo iliyofanyika kwa siku moja imeshirikisha wadau kutoka katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.


YANGA HAIKAMATIKI, YASHINDA TENA 2-0 MBELE YA MBEYA CITY
***********************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imeendelea kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara mara baada ya kufanikiwa kuichapa Mbeya City mabao 2-0 na kuwafanya kufika pointi 32 akiwa ameshuka dimbani mara 12.
Fiston Kalala Mayele ameendelea kutikisa nyavu baada ya leo tena kupachika mabao mawili na kumfanya aendelea kushikilia usukani kwa wapachikaji wa mabao ndani ya ligi kuu akifikisha mabao 10.
Bao la kwanza Mayele alifunga dakika 24 ya mchezo kipindi cha kwanza na bao la pili akifunga dakika 79 kipindi cha pili.
DKT. TULIA ATAKA UVCCM KUACHA VIOJA,WAJIBU HOJA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akizungumza kwenye ufunguzi wa mbio za Marathon kuelekea uchaguzi Mkuu ngazi ya UVCCM unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2022 Jijini Dodoma.
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson amewataka vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) kutumia nafasi zao kubishana kwa hoja na kuendelea kudumisha amani ,umoja na mshikamano hali itakayosaidia kuwalinda Viongozi wa taifa .
Dkt.Tulia ameyasema hayo Jijini Dodoma leo Novemba 26,2022 wakati akifungua mbio za Marathon za vijana wa UVCCM katika viwanja vya Jamhuri katika kuelekea uchaguzi Mkuu wa UVCCM ngazi ya Taifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2022 Jijini Dodoma .
Amesema ni jukumu la vijana hao kuacha malumbano na kubishana kwa hoja zinazojenga na kuongeza kuwa ikiwa vijana hao wataenzi amani na mshikamano itawasaidia kuondokana na matumizi ya dawa za kulevya na kuwa na ari ya kufanya kazi kwa bidii .
Spika Tulia amesema,"Hakikisheni katika chaguzi zenu mnaenzi amani kama ilivyo itikadi ya Chama chetu ,msianzishe vioja vinavyolenga kubomoa bali hoja zitakazoeleza maendeleo yanayofanywa na Serikali na si vinginevyo".
Pamoja na hayo ameeleza kuwa vijana hao wana jukumu kubwa la kuwalinda viongozi wao kwa hoja zinazoeleweka ikiwa ni pamoja na kuelekeza mambo mengi yanayofanywa na Serikali.
"Msikae kimya,tangazeni miradi tuliyonayo achaneni kabisa na masuala yanayowapotezea muda ambayo hayajengi,kuna wakati mnasubiri mtu atoe hoja ili muanzishe kuleta vioja vyenu naomba muache hiyo tabia kwani sio utamaduni wa Chama chetu ,"amesema
Pamoja na hayo ametumia nafasi hiyo kuwapongeza vijana wa hamasa wa Chama hicho kwa juhudi zao
katika kuamsha ari kwenye matukio ya Viongozi wakuu na kueleza kuwa huo ndio uzalendo unaotakiwa kwa Kila kijana.
Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM )Kenani Kihongosi amemshukuru spika Tulia kwa kukubali kuungana nao katika mbio hizo zilizoambatana na matembezi ya amani na kueleza kuwa hiyo ni fursa ya vijana kujenga Afya na kuepuka magonjwa.

































.jpeg)





.jpeg)


