Thursday, 3 November 2022

WATEJA BENKI YA CRDB WAJISHINDIA SAFARI YA QATAR KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA


Benki ya CRDB leo imehitimisha awamu ya kwanza ya kampeni yake ya “Tisha na TemboCard” kwa kuwakabidhi tiketi za kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia wateja wake wanne walioibuka washindi wa jumla wa kampeni hiyo.


Akizungumza katika hafla ya kubadhi tiketi hizo iliyofayika kwenye makao makuu ya Benki hiyo yaliyopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Manunuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon aliwapongeza washindi hao ambao walipatikana kutokana na kufanya miamala mingi zaidi kupitia kadi zao za TemboCard wakati kampeni hiyo ikiendelea.

“Kwa niaba ya benki niwapongeze kwa kuibuka washindi katika kampeni hii ambayo lengo na madhumuni yake ilikuwa ni kuwajengea watanzania utamaduni wa kutumia kadi zao kufanya malipo mbalimbali” alisema Pendason.


Pendason alisema Benki hiyo inafahamu namna ambavyo Watanzania wanapenda michezo na katika msimu huu wa kuelekea mashindano makubwa ya Kombe la Dunia, imeona ni vyema ikawa sehemu ya kutimiza shauku yao ya kushiriki katika mashindano hayo.

Akielezea kuhusiana na zawadi hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Bonaventure Paul alisema pamoja na tiketi hizo za kushuhudia mechi za Kombe la Dunia, safari nzima ya washindi hao itagharamiwa kuanzia tiketi za ndege kuelekea Doha Qatar, malazi, pamoja na fedha za matumizi wakifika huko.


Washindi walioibuka kidedea kwenye safari ya kushuhudia Kombe la Dunia mwaka huu wa 2022 ni:, Haji Athumani Msangi, Erick Boniface Kashangaki, Kelvin Jackson Twissa na Rajabu Dossa Mfinanga wote ni wakazi wa jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo Benki ya CRDB pia ilikabidhi zawadi za fedha taslimu kwa washindi wengine watatu wa kampeni hiyo ambao ni, Janeth Nyingi amejishindia shilingi Milioni Moja, Benedict Tilisho na Marsh Bakari wamejishindia shilingi laki tano kila mmoja.

Akitoa shukrani kwa wateja na wadau wote walioshirki katika kampeni hiyo, Meneja Masoko wa Bidhaa na Huduma Benki ya CRDB, Julius Ritte alisema kampeni hiyo ya “Tisha na Tembocard” sasa inakwenda kuingia katika awamu ya pili huku akiwataka wateja kuendelea kutumia kadi zao za TemboCard.
Mkurugenzi wa Manunuzi wa Benki ya CRDB, Pendason Philemon (wa pili kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya safari iliyolipiwa kwenda Doha – Qatar kushuhudia mashindano ya kombe la Dunia mmmoja wa washidi Haji A. Msangi (katikati) katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa jumla katika hitimisho la awamu ya kwanza ya kampeni “Tisha na TemboCard”, iliyofanyika Makuu ya Benki, Palm Beach, jijini Dar es salaam leo Novemba 03, 2022. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati Bonaventure Paul, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Joseline Kamhanda, na Mkuu wa Biashara ya Kadi Benki ya CRDB, Farid Seif.
Share:

MISA-TAN YATOA MAFUNZO UHURU WA KUJIELEZA KWA WANAHABARI

Marko Gideon akitoa mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa wana habari yaliyo ratibiwa na Misa-Tan.

Na Marco Maduhu, SINGIDA

WANAHABARI wapatao 40 kutoka Mikoa ya Tabora, Dodoma, Shinyanga, Simiyu na Singida, wamepewa mafunzo ya kuandika habari za kukuza uhuru wa kujieleza.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Novemba 3, 2022 mkoani Singida ambayo yatachukua muda wa siku tatu ,yakiratibiwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania( Misa-Tan) kwa ufadhili wa ubalozi wa Kanada nchini Tanzania.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Marko Gideon, amesema mafunzo hayo yametolewa mara baada ya kufanyika utafiti na kubainika kuwa habari za uhuru wa kujieleza hapa nchini zimekosekana.

"Unapokosekana uhuru wa kujieleza, utawala wa Sheria hautakuwepo, uwajibikaji wa viongozi, hakutakuwa na usawa wa kisheria, hakuna uwazi, uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki, na kudhibiti matumizi mabaya ya viongozi," amesema Gideon.

Naye Andrew Marawiti kutoka Misa-Tan amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kuona wanahabari wakiandika habari nyingi zinazohusu uhuru wa kujieleza.

Nao baadhi ya wanahabari walioshiriki mafunzo hayo, wamesema wanatarajia mafunzo hayo kuwaongezea maarifa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya uandishi wa habari.

Marko Gideon akitoa mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa wana habari yaliyo ratibiwa na Misa-Tan.

Andrew Marawiti kutoka Misa- Tan akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Andrew Marawiti kutoka Misa- Tan akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.
Share:

TANZANIA NA KOREA KUSINI ZAINGIA MAKUBALIANO KUIMARISHA SEKTA YA ARDHI


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Tanzania Dkt Angeline Mabula (Kulia) na Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini Bw. Won Hee-ryong wakisaini hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia jijini Seoul Korea Kusini jana.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Tanzania Dkt Angeline Mabula (Kulia) na Waziri wa Ardhi, Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini Bw. Won Hee-ryong wakionesha hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia mara baada ya kusaini jijini Seoul Korea Kusini jana.

………………………………….

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeingia makubaliano na Wizara ya Ardhi Miundombinu na Usafirishaji ya Korea Kusini kwa ajili ya kuimarisha sekta ya ardhi.

Makubaliano hayo yametiwa saini jana na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wa Tanzania Dkt Angeline Mabula na yule wa Ardhi, Miundombinu na Usafirishaji wa Korea Kusini Bw. Won Hee-ryong katika mji wa Seoul Korea Kusini kipitia hati ya makubaliano (MOU) ya ushirikiano kwenye sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia.

Makubaliano ya nchi hizo mbili yanalenga kuweka mazingira rafiki kwa watanzania kupata utaalam na uzoefu kwenye nyanja za upimaji na ramani kupitia mipango/miradi ya mafunzo ya kuendeleza rasilimali watu kwa maendeleo endelevu ya sekta ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa fursa zaidi kwa watanzania kupata mafunzo ya muda mrefu nchini Korea.

Pia kuimarisha ushikiano uliopo kati ya Wizara ya Ardhi ya Tanzania na ile ya Korea Kusini katika kukuza matumizi ya teknolojia za kisasa kwenye sekta ya ardhi ili kuboresha utoaji huduma katika fani zote za utawala wa ardhi na kutimiza azma ya Serikali ya kusajili ardhi yote nchini.

“Wizara inaona upo umuhimu wa kuwa na makubaliano rasmi ya kukuza na kuimashira ushirikiano wa nchi hizi mbili kupitia Wizara ya Ardhi na wenzetu wa Korea kupitia Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ardhi na menejimenti ya taarifa za kijiografia” alisema Dkt Angeline Mabula.

Mbali na utiaji saini makubaliano hayo Dkt Mabula akiwa nchini Korea Kusini atashiriki mijadala kwenye maonesho ya maendeleo ya teknolojia ya taarifa za kijiografia – Smart Geospatial Expo 2022.

Maonesho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka sambamba na mikutano ya majadiliano ya kuanzisha na kukuza ushirikiano kwenye sekta ya ardhi inayowakutanisha viongozi wa juu wa serikali na makampuni ya kimataifa yanayojihusisha na taarifa za kijiografia kwa ajili ya maendeleo na usimamizi wa sekta ya ardhi.
Share:

MWENDESHA BODABODA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI GEITA

Kijana Amin Salum Mkazi wa Mtaa wa Nyamarembo Wilaya ya Geita Mkoani Geita Ambaye ni Dereva wa Pikipiki Maarufu Kama Bodaboda amefariki dunia kwa kupigwa risasi na watu wanaozaniwa kuwa majambazi nyakati za usiku.


Salum Alipigwa risasi wakati akiendelea na Majukumu yake ya kutoa huduma ya usafiri wakati wa usiku ndipo tukio hilo la kupigwa risasi eneo la Nyamarembo lilitokea kwa kupigwa Risasi hadi kufariki dunia.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo amesema Amin Salum dereva Bodaboda alipigwa risasi na majambazi ambao walitaka kufanya uporaji kwa Mfanya Biashara ambaye jina lake limehifadhiwa nyakati za usiku na ndipo majambazi hao walipokimbia na kumfyatulia risasi Dereva huyo.


Kamanda Safia Amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi litaendesha msako wa kuwasaka majambazi hao ambao wametekeleza tukio la mauaji la kijana Amin Salum na watakapo kamatwa watafikishwa katika mamlaka husika na kushugulikiwa kwa mjibu wa sheria.

https://ift.tt/JR6NhAf
Share:

DIWANI AAHIDI HUDUMA YA MAJI NA UMEME KWA WANANCHI NA TAASISI ZA ELIMU

Diwani wa kata Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani Mh. Nassar Karama
Diwani wa kata Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze mkoa wa Pwani Mh. Nassar Karama

NA ELISANTE KINDULU, CHALINZE

DIWANI wa kata ya Bwilingu katika Halmashauri ya Chalinze, Mh. Nassar Karama ameahidi huduma ya maji na umeme kwa wananchi na shule za msingi na Sekondari katika kata ya Bwilingu mkoa wa Pwani.


Mh. Nassar ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wakazi wa Kitongoji Cha Mdaula katika sherehe za mahafali ya darasa la saba yaliyofanyika tarehe Novemba 1,2022 katika viwanja vya shule ya msingi Mdaula.


Mh. Nassar alitanabaisha kuwa shule tatu katika kata yake tayari zinapata huduma ya maji ambapo pamoja na msaada wa wadau wengine wa maendeleo lakini pia zikiwemo jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Mh. Ridhiwani Kikwete.


Aidha Mh. Diwani aliendea kusisitiza kuwa, Kata ya Bwilingu hakutakuwa na chaguo la pili na hivyo kufanya wanafunzi wote kuingia kidato cha Kwanza mwakani kutokana serikali kutoa shilingi milioni 600 katika shule mpya ya Sekondari Msolwa, shilingi milioni 60 za madarasa 3 katika Sekondari ya Mdaula, shilingi milioni 100 za madarasa 5 shule ya msingi Chahua na shilingi milioni 500 katika shule ya Sekondari ya Chalinze.


Wakati huo huo Mh. Nassar katika ziara yake katika Kitongoji cha Maluwi aliwaahidi wananchi wa Kitongoji hicho na maeneo mengine yatafikiwa na huduma ya umeme katika bajeti ya 2023/2024.
Share:

Wednesday, 2 November 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI NOVEMBA 3,2022











Share:

MAWAKALA WATANO WAKAMATWA WAKISAJILI LAINI ZA SIMU KWA KUTUMIA NAMBA ZA NIDA ZA WATU WENGINE KAGERA


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa ofisi za Takukuru leo Novemba 02,2022


***

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mawakala watano wa kusajili laini za simu wamekutana na mkono wa Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Kagera kwa kusajilia watu laini za simu kwa kutumia namba za NIDA za watu wengine kinyume cha taratibu na sheria.


Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph leo Novemba 02,2022 katika ukumbi wa ofisi za Takukuru akizungumza na vyombo vya habari wakati akitoa taarifa ya miezi mitatu ya miradi ya maendeleo mbalimbali katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Kagera.


Amesema kuwa pamoja na kufanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo pia wamefuatilia usajili wa laini za simu na kubaini baadhi ya mawakala wa usajili wa laini za simu kutokuwa waadilifu na waaminifu.


Ameongeza kuwa mawakala hao wamekuwa wakisajili laini za simu kwa namba za NIDA za watu wengine na baadhi ya laini hizo kutumika katika uhalifu ambapo vijana watano tayari wamekamatwa na uchunguzi wa kina unaendelea.

Aidha amewataka wananchi wote wa Kagera wanapokwenda kusajili laini zao za simu kuwa makini sana kutokana na namba za simu nyingi zimekuwa na majina tofauti.



Aidha amewataka wananchi kwenda kwa mawakala wa simu ili kuangalia namba zao za NIDA zimesajili namba ngapi na Kama itaonekana namba ambazo huzifahamu uweze kuwasiliana na makampuni ya laini husika ili zifungiwe mara moja ili kuepusha usumbufu.


Share:

TAKUKURU YABAINI MAPUNGUFU BAADHI YA MIRADI YA MAENDELEO KAGERA


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Kagera Bw. John Joseph akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa ofisi za Takukuru.


Na Mbuke Shilagi Kagera.


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imebaini mapungufu katika baadhi ya miradi ya maendeleo wakati wa zoezi la ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi hiyo katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa.


Akizungumza na vyombo vya habari leo Novemba 02,2022 katika ukumbi wa ofisi za Takukuru, Mkuu wa Takukuru Bwa. John Joseph amesema kuwa wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo 48 yenye thamani ya zaidi ya Bilion 16 ambayo ni ujenzi wa mradi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa mradi wa maegesho ya magari makubwa, mradi wa miundo mbinu ya maji, ujenzi wa vituo vya Afya na Zahanati pamoja na ujenzi wa vyoo na kubaini mapungufu kwa baadhi ya miradi hiyo.


Na kwamba mapungufu hayo yamekuwa ya kutumia vifaa vyenye ubora tofauti na ilivyo elekezwa katika BOQ, utoaji wa LPO kwa baadhi ya wazabuni bila kuonesha idadi halisi ya vifaa vinavyotakiwa kununuliwa pamoja na vifaa kutolewa stoo bila kurekodiwa.


Pia wamebaini uwepo wa urushwaji wa bei kwa baadhi ya vifaa kuliko bei ya soko pamoja na kubaini baadhi ya wazabuni wa miradi kupewa malipo ya awali hawakuwa wameanza kazi na kutokuwepo katika maeneo ya miradi.


Aidha ameongeza kuwa miradi hiyo 48 iliyofanyiwa ufuatiliaji imeonekana miradi 31 haikuwa na kasoro na hivyo inaendelea kukamilishwa na baadhi imekamilika huku miradi saba yenye thamani ya zaidi ya Bilion nne imeanzishiwa uchunguzi wa kina.

Share:

HALI YA MAJI MTO RUAHA MKUU NI MBAYA, ZIMETIMIA SIKU 80 BILA KUTIRIRISHA HATA TONE LA MAJI




-Hifadhi ya Taifa Ruaha yasema wanyama wanahangaika, samaki wameanza kufa


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV-Ruaha


IMEELEZWA kwamba Mto Mkuu Ruaha ambao ni kwa uhai wa hifadhi ya taifa ya Ruaha upo kwenye hali mbaya kutokana na maji yanayopita kwenye mto huo kukauka kabisa na hivyo kusababisha hata wanyama kukosa maji.

Akizungumza na waandishi Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki ameeleza hatua kwa hatua kuhusu hali ya mto huo ambapo amefafanua ni mto ambao unafanya hifadhi iweze kuwa na vivutio vingi kwa maana wakati wa kiangazi kama hiki wanyama wengi wakubwa na wadogo wanafika kwa ajili ya kupata maji.

“Lakini kwa wanyama wanaishi kwenye maji hasa mamba, viboko na samaki wanaishi katika mto huu,kwa sasa hali ya mto huu Ruaha ni ngumu sana kwasababu hali ya maji ni mbaya, takribani sasa siku 80 huu mto hautiririshi maji yake , mto umeacha kutiririsha maji yake na maeneo machache yaliyobaki ni maeneo yenye madimbwi ambako kuna maji ambayo yanatumiwa na wanyama wote wanaofika katika maeneo haya

“Ni maeneo ambayo machache sana yamebaki katika mto huu na ukitizama kwa karibu maeneo haya maji yaliyoko kwenye haya madimbwi hata rangi yake imebadilika sio maji ya kawaida kwa maana ni maji machafu kwasababu wanyama wengi wanatumia na wanatumia katika maeneo haya wanaishi humo humo, wengine wanafia humo humo, wanajisaidia humo humo , wengine wanakuja wanakanyaga kwa hiyo maji ni machafu kwa ujumla.

“Maji haya sio mazuri kwa uhai wa wanyama lakini hawana namna , haya maeneo ndio machache yaliyobaki kwa hiyo wanyama wanakusanyika katika maeneo haya kwa ajili ya kupata maji. Uhai wa hifadhi hii kama nilivyosema unategemea uwepo wa mto Ruaha na hasa maji yake yanayotiririka kutoka kwenye bonde kubwa la Usangu ambalo liko ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha.

“Tunatakribani kilometa 164 za mto huu ambao unapita ndani ya hifadhi ya mto huu wa Ruaha , baada ya kupita ndani ya hifadhi basi mto huu hutiririsha maji yake katika bwawa la Mtera , Kidato na Bwawa la Mwalimu Nyerere.Ni mto muhimu sana lakini sasa tunapozungumzia umuhimu wake na hali halisi sasa ilivyo ambapo maji hakuna kabisa hata tone, utabaini changamoto kubwa ya kimazingira kwa maana ya wanyama wanapata shida ya maji safi ya kunywa,”amesema.

Ameongeza lakini pia mazingira ya hifadhi yanaharibika kwa maana ya wanyama wanapokusanyika eneo dogo wanatumia kile kilichopo kwa kufuata maji kwenye madimbwi hayo, hivyo kuleta uharibifu mkubwa wa mazingira ndani ya hifadhi tofauti na kama maji yangekuwa mengi wanyama wangekunywa na kuendelea na shughuli zao.

“Kwa hiyo ukitizama au ukitembelea kando kando ya Mto Ruaha kwa sasa uoto wa asili sasa umeanza kuharibika kutokana na wanyama kuja kwa idadi kubwa katika eneo hili.Tumeona madhara mengine kwamba baadhi ya wanyama wakati mwingine hasa jamii ya samaki wamekuwa wanakufa kutokana na maji yaliyopo yanakuwa ni machafu na hali ya hewa pia hapa ni ya joto kipindi hiki.

“Hivyo maji yanapata joto lakini kutokana na ule uchafu na ukweli kwamba wanyama jamii ya samaki wanahitaji hewa nzuri ya kuvuta kwa maana ya Oxgen inapungua maji yanapokuwa machafu na kunakuwa na joto kwa hiyo wakati mwingine samaki wengi wanakufa katika kipindi hiki.

“Tulipofanya uchunguzi kwenye madimbwi haya tulichobani samaki wanakufa kwasababu ya kukosa hewa ya Oxgen ambayo inafanya waishi kwenye maji lakini pia tumeona katika kipindi hiki wanyama wanatafuta maeneo mengine ya kupata maji ya kutumia na wanatoka nje ya hifadhi na tunajua huko nao wanasababisha migogoro kati ya binadamu katika maeneo hasa kwa kuharibu mazao na mali nyingine,”amesema.

Ole Meing’ataki amesema kuwa madhara mengine yanayotokea ni wananchi kudhuru wanyama , miaka ya nyuma walikuwa wanaona magonjwa.Wanyama wakinywa maji kwenye madimbwi hayo basi vile vimelea vya magonjwa husambaa kwa urahisi, jambo lingine ambalo walikuwa wakiliona huko nyuma ni majangiri ambao walikuwa wanaingia katika baadhi ya maeneo ya hifadhi wanaweza kufika kwenye maeneo yenye maji na madimbwi kama haya na kuweka mitego yao na kuwanasa wanyama lakini pia wakati mwingine wanaweza kutumia sumu inayoweza kuua wanyama mbalimbali.

“Wanyama ambao wanakula mizoga na wanyama wengine ambao wanawakamata, tumeona wakati mwingine wakifanikiwa kufanya hivyo wanaondoka na nyama na hizo nyama zinakwenda kuuzwa kwa wananchi kitu ambacho ni cha hatari sana kwa usalama wa afya zao.

“Kwa hiyo huu Mto Mkuu Ruaha naweza kusema ni muhimu ni muhimu kwa mtazamo huo kwamba kweli ni kivutio kwasababu maliasili ambazo tunazo wanyamapori wakubwa na wadogo wanapatikana katika maeneo haya na ukiangalia utalii unaofanyika katika hifadhi kwa kiasi kikubwa kuna njia nyingi za utalii ambazo zinakwenda kando kando ya huu mto Ruaha kwasababu wageni wanaweza kuona wanyama kwa karibu.

“Kinachotokea katika huu mto ambao unaanzia katika bonde la Usangu tunaona kuna shughuli nyingi za kibinadamu ambazo tunazungumzia shughuli ambazo ni haribifu, ukataji miti ambao unafanyika , uchomaji moto ambao tunauona lakini uingizaji wa mifugo mingi katika eneo lile vyanzo vya maji kama tulivyoona limekuwa tatizo kubwa ambalo linasababisha maji kuisha , kilimo holela kinachofanyika ambacho maji yanapatikana hata kama yamepungua lakini yanatumika kwenye kilimo lakini siku ya mwisho maji haya hayarudi kwenye mkondo asili kwa maana kwenye mto.”

Aidha amesema wanaona kuna uchepushaji mkubwa wa maji katika maeneo mbalimbali ambapo unakuta baadhi ya wananchi wameanzisha mashamba na hawajali kwamba haya maji yanahitajika kwenye matumizi ya maliasili kama hizi za wanyama pori lakini pia kwa ajili ya uzalishaji umeme na matumizi mengine ya kiuchumi hasa kupitia eneo hilo.

“Tunafahamu maji yanapojaa kwenye bonde la Usangu hutiririka kupitia Mto Ruaha mkuu na ukipita basi hifadhi tunanufaika kupitia nafasi hii mazingira yatakuwa mazuri na tutapata idadi kubwa ya wageni wanaotembelea hifadhi kwasababu tunarasilimali hii ambayo imehifadhiwa na inategemea huu mto.

“Lakini huu mto unapotoka nje ya hifadhi ndio sasa huko maji yanakwenda maeneo mengine ambako kuna jamii ambazo zinatumia maji kwa ajili ya shughuli za kiuchumi tunazungumzia kilimo, tunazungumzia uvuvi , mathalani kama maeneo ya Mtera tunaona uvuvi unafanyika na maeneo mengine lakini maji haya baada ya kuzalisha umeme pale Mtera huelekea Kidatu mpaka Bwawa la Nyerere na huko njiani maeneo ambayo mto unapita kuna matumizi mengi mengi kwa hiyo tunapotumia maji vibaya kwenye bonde la Usangu tunafanya huu mto ruaha uendelee kuwa katika hali mbaya na ile nafasi ya mchango wake katika maeneo ya kiuchumi,

“Uhifadhi wa baianoai na matumizi mengine ya binadamu na uzalishaji umeme tunakosa hiyo nafasi kubwa sana , kwa hiyo madhara ya kuupoteza huu mto au kukauka ni makubwa sana sio tu kwa hifadhi kama tunavyoona utalii unaweza kuathirika lakini na huko maeneo mengine ambayo maji haya yanatumika,”amesema Ole Meing’ataki.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki akionesha hali halisi ya Mto Ruaha Mkuu ulivyokauka.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUAHA.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki akionesha hali halisi ya Mto Ruaha Mkuu ulivyokauka .
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki akisalimiana na baadhi ya Watalii waliokuwa wakipita katika daraja la mto Ruaha ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha,mkoani Iringa
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki akiwa amesimama kwenye daraja la Mto Ruaha Mkuu ndani ya hifadi akionesha sehemu ndogo ya maji yaliyobaki,ambayo nao ni machafu hayafai kwa matumizi ya baadhi ya Wanyama.
Baadhi ya Tembo ndani ya Hifadhi ya Ruaha wakihangaika kutafuta maji ya kunywa.
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha Godwell Ole Meing’ataki akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akionesha namna Hifadhi ya Ruaha ilivyo kubwa sambamba na maeneo mbalimbali yaliyomo. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUAHA.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger