Monday, 3 October 2022
BENKI YA CRDB YAWASHUKURU WATEJA MAFANIKIO YA HUDUMA BORA KWA JAMII
MZEE AMUUA BINTI YAKE KWA KUMKATA KATA KWA SHOKA NA VISU KISA KACHELEWA KULETA MAJI
WATU WATATU WAUAWA KOLANDOTO SHINYANGA, ALIYEANZA KUUA ACHOMWA MOTO
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la mauaji Kolandoto Shinyanga.
Na Halima Khoya, SHINYANGA
Watu wawili ambao ni Nicholaus Leonard na Badmalta Melikiad, wameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wao na wengine watatu kujeruhiwa, na mtu ambaye hajafahamika akidaiwa kurukwa na akili ambaye naye ameuawa kwa kupigwa kisha kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali.
Akisimulia tukio hilo leo mmoja wa majeruhi Daniel Emmanuel, amesema mtu huyo alivamia katika nyumba ya bwana Nicholaus Leonard, na kuwakuta mke wa Nicholaus ambaye ni Lucia Luhende akisukana na Rafiki yake Badmalta ndipo akaanza kuwashambulia.
Anasema wakati akiwashambulia akajitokeza kuwasaidia ndipo na yeye akapigwa kichwani na kitu kizito kichwani akapasuka na kuanza kuomba msaada, huku mmoja wa wanawake hao Badmalta akipigwa vibaya na kusabisha kifo chake papo hapo.
“Nilienda kuwasaidia baada ya kusikia kelele katika nyumba hiyo ya bwana Nicholaus, ambapo mtu huyo alikuwa amefunga mlango na mimi nilivyofika nikafungua mlango lakini bahati mbaya jamaa alikuwa amejibanza katika kona nilivyoingia tu akanipiga kichwani nikaanguka chini,”Amesema Daniel.
“Wakati vurugu hizo zikiendelea na mimi kuelemewa kushindwa kutoa msaada kutokana na kuvuja damu nyingi, mume wa Lucia Luhende bwana Nicholaus Leonard aliingia ndani kutoa msaada, lakini na yeye akapigwa kichwani akaanguka chini na kupoteza maisha papo hapo,”anaongeza.
Kwa upande wake Mke wa Marehemu Lucia Luhende, amesema yeye alifanikiwa kutoka nje wakati mtu huyo akiendelea kumshambulia Rafiki yake, ndipo mume wake akaingia ndani ili kumuokoa lakini hakufanikiwa kutokana na kupigwa vibaya kichwani kisha akapoteza maisha.
Naye Diwani wa Kolandoto Mussa Andrew, amesema baada ya kupokea taarifa alifika eneo la tukio na kumkuta jamaa akiwa bado ndani ya nyumba hiyo, akapiga simu kuomba msaada Polisi, lakini wananchi wenye hasira kali walifanikiwa kumtoa nje na kisha kuanza kumkimbiza.
Anasema wananchi hao walifanikiwa kumkamata na kisha kuanza kumpiga kwa mawe na baadae kumchoma moto.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kolandoto Dk. Joseph Wallace, amethibitisha kupokea miili ya marehemu watatu akiwamo na kijana huyo ambaye aliuawa na wananchi, pamoja na majeruhi watatu huku mmoja akipewa rufaa ya kwenda Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la mauaji, na kutoa wito kwa wananchi wakimuona mtu analeta taharuki watoe taarifa ili kuzuia maafa yasitokee.
MASHIRIKA YANAYO LEA USHOGA YAONYWA
MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza, ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yatajihusisha na kutetea ndoa za jinsia moja kuacha mara moja kwani ni kinyume na mila na desturi za kitanzania.
Mahiza, amezungumza hayo jijini Dodoma, wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wakurugenzi wa mashirikika yasiyokuwa ya kiserikali na kueleza kuwa yapo mashirika nchini yanaishi kwa kivuli Cha kutetea ushoga kwa madai ya kulinda haki za binadamu.
Amesema, katika kipindi chake akiwa mwenyekiti wa Bodi hiyo hatopenda kuona jambo hilo linatokea kwa kuwa ni kinyume na mila na desturi za Watanzania na ni aibu .
“Kama kuna shirika lolote ambalo katika utekelezaji wa majukumu yake limepanga kufanya vitu kama hivyo naomba lifute mpango huo mara moja hatuwezi kuviruhusu vitu kama hivi katika taifa ambalo serikali ipo na dini zipo”amesema Mwantumu na kuongeza;
Si jambo la busara kwa taifa kuruhusu vitendo vya ndoa za jinsia moja kwa mwanamke kuolewa na mwanamke mwezake au mwaume kuoa mwanaume mwenzake , tusipofanya juhudi tutashindwa kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke,"anasisitiza
Pamoja na hayo ametilia mkazo suala hilo kuwa Serikali haiwezi kuruhu haki za binadamu zinazopingana na mila na kueleza kuwa takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanawake ni kubwa ukilinganisha na wanaume hivyo ndoa za jinsia moja ni jambo ambalo halipaswi kupewa nafasi.
“Hata ukienda leo hospitali kati ya watoto kumi wanaozaliwa kwa siku wanawake ni saba wanaume ni watatu hivyo kama tusipokuwa makini hii nchi itakuwa ya wanawake tupu wanaume watakwisha kwasababu wanaoana wao kwa wao”amesisitiza
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema lengo la mkutano huo ni pamoja kupata fursa ya kukumbushana mambo mbalimbali.
Mkurugenzi huyo pia ametumia nafasi hiyo kuiomba serikali kufanyia marekebisho ya sera inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwa ni pamoja na kuyaondolea kodi katika vitu mbalimbali ambavyo wamekuwa wakiingiza kutoka nje ya nchi.