Friday, 23 September 2022

DKT. KIJO BISIMBA: ASASI ZA KIRAIA ZINA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUHARAKISHA MAENDELEO NA HUDUMA MUHIMU KWA WANANCHI

 

Jamii imeaswa kulipa umuhimu na kipaumbele suala la elimu kama nyenzo muhimu katika kuleta mabadiliko mbalimbali katika jamii sambamba na kuwa na fikra mbadala za kuwezesha jamii kubadilika

Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam Septemba 23, 2022 na aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Hellen Kijo Bisimba alipokuwa akiongea katika mdahalo ulioandaliwa na Jukwaa la vijana la Reach out Tanzania ulioangazia mchango wa Asasi za kiraia katika maendeleo nchini uliofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dkt. Kijo Bisimba amesema, asasi za kiraia zina mchango mkubwa katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja na hata kuisaidia serikali katika kuharakisha maendeleo kwa wananchi kwa kutekeleza majukumu ambayo pia yangeweza kufanywa na serikali.

Ameongeza kuwa kuna wakati Serikali haifikii malengo yake kutokana na sababu mbalimbali hivyo Asasi za kiraia huisadia Serikali kutimiza jukumu hilo.

"Kuna wakati serikali haifikii malengo yake kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uchache wa rasilimali, kufuatia hilo asasi za kiraia inakuja hapo kwa ajili ya kuziba hilo gap (uwazi) kati ya mahitaji ya raia na serikali inavyopaswa kukidhi mahitaji hayo" alisema Dkt. Hellen,  na kuongeza

"Ingekuwa kwamba Serikali inafanya kila kitu, hata Asasi za kiraia zisingekuwepo, lakini jambo hilo haliwezekani ndio maana asasi za kiraia zipo dunia nzima"

Ameendelea kwa kusema kuwa, kuna Asasi ambazo zinafanya kazi ya kutoa huduma ambazo zinaweza kufanywa na Serikali, ambazo zinajenga hospitali, vituo vya kulelea yatima, shule na vituo vya kutolea msaada wa kisheria na kwamba zote hizo ni huduma za msingi na muhimu kwa wananchi.

Sambamba na hayo Dkt. Kijo Bisimba amewakumbusha wananchi kufahamu umuhimu wa Serikali na malengo yake pindi inapowekwa madarakani kwa kusema kuwa, baadhi ya malengo mahususi ni pamoja na kutatua changamoto za wananchi ikiwemo changamoto ya umasikini, kuwaletea maendeleo na kuhakikisha wananchi wake wanaishi kwa uhuru na furaha.

 
Share:

DOGO AMUAIBISHA MAMA YAKE 'Live' KANISANI...'MAMA AMEIBA MME WA MTU, ANAISHI NAYE NYUMBANI"


Wanamitandao wamechekeshwa na video iliyozagaa mitandaoni iliyomwonesha mvulana mdogo, akimtaka mhubiri kumuombea mama yake aliyemuiba mume wa mtu.

Video hiyo iliyovuma, inamwonyesha mama wa mvulana huyo akijifunika uso wake kwa aibu, huku mwanawe akifichua siri ya aibu


Mvulana mwenye umri wa miaka tisa, aliamua kutoboa siri mbele ya umati wakati wa ibada ya kanisa, na kuwashangaza wengi aliposema kwamba mamaake mzazi anaishi na mume wa mtu hivyo kumtaka pasta amkemee ili aondoke

Mpango wa kando Mvulana huyo mwenye ujasiri alichukua kipaza sauti bila ya kuogopa, na kumuita pasta amuombee mpenzi wa mama yake ili ahame nyumbani kwao, wanakoishi naye.

Video ya hiyo ya kusisimua ilipakiwa kwenye Facebook na Alberto Nyakundi Amenya BananaPeddler aliyesema kuwa:

"9-year old. Kwa mara ya kwanza pastor amechanganyikiwa. Sasa haka kakijana ni ka-genius ama ka-saitaan?" Tazama video ifuatayo ya jinsi mtoto huyo wa kiume alivyomuaibisha mama yake.

Video hiyo iliibua hisia mseto mitadaoni na zifuatazo ni baadhi ya maoni yaliyotolewa:

Francis Kiarie aliandika: "Haya mambo hutokea. Mambo ambayo hufanyika gizani, hujitokeza hadharani kwa nguvu ghafla bin vuu. Inawezekana."

Moses Nyabuto aliandika: "Jiepusheni na haya makanisa ya mitaa. Ni heri ubaki nyumbani kwako ujiomboe na kusali ikiwa inawezekana."

Oindo Douglas Mokaya aliandika: "Na wanasema wako 'I'm single but comfortable'. Yesu ndiye Bwana yangu kumbe ni Baba Jemo mume ya Njeri."
Share:

WAKULIMA CHEMBA WAPEWA ELIMU NA BALOZI WA PAMBA TANZANIA

Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa 17 inayozalisha pamba hapa nchini, ukiwa katika msimu wake wan ne (4) tangu zao hili litambulishwe rasmi msimu wa 2017-18.

Pamoja na kuwa miongoni mwa mikoa mipya kiuzalishaji kwa jitihada za uongozi wa mkoa Dodoma na kushirikiana na Bodi ya Pamba imefanikiwa kufikisha zao hili katika wilaya zake tatu hadi sasa huku wilaya ya Chemba ikiwa miongoni mwa hizo wilaya nyingine ni Bahi na Chamwino.

Katika kuendelea kuhakikisha kuwa kilimo cha pamba kinasambaa kwa wakulima wengi na kufanyika kwa tija Bodi ya Pamba inahakikisha kuwa haiwaachi nyuma wakulima kwa kuwapa elimu ya Mara kwa Mara juu ya Kanuni Kumi za kilimo Bora cha Pamba. Katika muendelezo wa kampeni ya uongezaji tija kwa kumtumia balozi wa pamba maeneo mbalimbali yamefikiwa hadi sasa.

Wakulima wa zao la pamba wilayani Chemba wametakiwa kulima zao Hilo kwa kutumia Vipimo vipya vya sentimeta 60 kutoka mstari hadi mstari na sentimeta 30 kutoka shimo Hadi shimo na kuachana na mtindo wa zamani wa kurusha mbegu.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Bodi ya Pamba Tanzania Aggrey Mwanri kwa nyakati tofauti tofauti alipokuwa akitoa semina elekezi namna ya kuongeza tija kwa kutumia Vipimo vipya katika zao hilo kwa wakulima wa vijiji vya Kidoka, Ombili, Paranga na Kelema.

Mwanri amesema kuwa Mabadiliko hayo ya vipimo yataweza kumuongezea mkulima idadi ya miche kutoka 22, 222 ya awali alipokuwa anatumia vipimo vya sentimeta 90 kwa sentimeta 40 hadi kufikia miche 44,444 kwa kutumia vipimo vipya.

Amesema kuwa endapo wakulima watatumia Vipimo vipya wakati wa kupanda zao la Pamba ifikapo mwaka 2025 wanatarajia kuzalisha tani zipatazo Mil 1 ambapo watakuwa wa kwanza Afrika katika uzalishaji wa Pamba.

" Kama wakulima wakifata maelekezo na kanuni Bora za kilimo Cha zao la Pamba kwa kupanda shamba zima kwa kutumia Vipimo na kuachana na mtindo wa kupanda mstari wa mbele kwa kufata vipimo alafu wanaendelea kumwaga mbegu Kama zamani hatutafikia malengo tuliyojiwekea", alisema Mwanri.

Amesema kuwa Pamba ni zao muhimu la kimkakati, kibiashara hapa Nchini na linachangia takribani Asilimia 10 hadi 20 ya Pato la Taifa na fedha za kigeni pamoja na kutoa Ajira kwa Asilimia 40 ya watanzania hivyo wakulima hawana budi kulima zao Hilo kwa kufata kanuni bora za kilimo ikiwemo kupambana na wadudu waalibifu kwa kutumia dawa.

Aidha amesema kuwa kutokana na wakulima kuwa na uelewa mdogo juu ya ulimaji wa zao Hilo na elimu ndogo ya matumizi ya dawa za kuuwa viwatilifu wameendelea kuchanganya mazao shambani huku kanununi ikimtaka kutochanganya mazao kitu ambacho kinadhoofisha zao hilo la pamba.

"Tunapoendelea kutoa elimu,tutaendelea kuwaelimisha juu ya matumizi sahihi ya dawa pamoja muda mwafaka wa kupulizia dawa na vifaa maalumu vinavyotumika wakati wa kunyunyuzia dawa hiyo",alisema Mwanri.

Sambamba na hayo amefafanua kuwa bodi ya Pamba tayari imeishachukua hatua mbalimbali namna ya kuwasaidia wakulima kupata dawa itakayowasaidia kupambana na wadudu waalibifu shambani.

"Bahati nzuri taarifa tulizonazo ni kwamba sasa wameishaanza kupata dawa ambayo itadili na funza na chawajani na wadudu wengine",alisema Mwanri.

Kamili Makiya ni Afisa kilimo Wilaya ya Chemba amesema kuwa kutokana na programu ya kuhamasisha kilimo cha zao la Pamba wilaya hiyo imeanza kuwa na matarajio ya kunufaika tofauti na kipindi cha nyuma ambapo zao hilo lilianza kuzorota.

"Kwa mfano ukiangalia takwimu za nyuma jinsi tulivyokuwa tuneendesha kilimo mwaka 2018 -2019 tulifanikiwa kuzalisha tani 111 lakini baada ya miaka hiyo tukaachana na programu ya kuhamasisha Mara kwa Mara uzalishaji ulishuka chini 2019_2020 tulizalisha tani 73 mpaka kufikia 2020_2021 tulipata tani 500 kwa mwaka",alisema Kamili.

Aidha alisema kuwa mbali na uzalishaji wa zao hilo kushuka ujio wa Balozi wa Pamba kuanza kuhamasisha wanategemea ongezeko la uzalishaji kuwa tofauti na kipindi cha nyuma, sambamba na elimu ya kilimo Bora waliyoipata hivyo kila Kaya wataweza kuzalisha angalau hekali 1 ya Pamba ambapo awali walizalisha kilo 150_250 lakini kutokana na elimu waliyoipata wataweza kufikia kilo 800 .

Jumanne Ally ni mmoja wa wenyeviti amefafanua kuwa semina waliyoipata itawasaidia kuhakikisha pamba itakayo kuwa na tija na itakayowaletea mafanikio kuondoka umasikini katika vijiji vyao.

"Tutaendelea kuhamasisha wananchi kulima zao hilo kwa kufata Sheria na kanuni ya Vipimo vipya na kuachana na vya zamani yatupa mbegu",alisema Ally.

John Joseph na Shabani Hassani ni baadhi ya wakulima waliopata elimu elekezi namna ya kuongeza tija kwenye zao la Pamba wamesema kuwa elimu hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa kufanya mabadiliko katika zao hilo, na kuiomba bodi ya Pamba kuendelea kutoa elimu namna ya kuendelea kutumia Vipimo vipya ili waweze kuacha na ulimaji usio kuwa na tija.
Share:

KOFIH YAIPIGA JEKI MLOGANZILA VIFAA TIBA VYA MIL 382,650,980


***********************

Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya TZS 382,650,980 Mil kutoka serikali ya Korea Kusini kupitia Taasisi ya Korea Foundation for Health Care (KOFIH) vitakavyotumika kuboresha utoaji wa huduma katika wodi ya watoto wachanga mahututi.

Akikabidhi msaada huo kwa uongozi wa hospitali, Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Kim Sun Pyo amesema serikali ya Korea Kusini itaendelea kuisaidia Tanzania katika eneo la mafunzo na kuboresha huduma za afya kupitia taasisi zake hususani KOFIH.

Mhe. Kim amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru kwa ushirikiano aliouonesha kwa taasisi za Korea Kusini katika kuboresha huduma za afya hospitalini hapa.

“Namtakia Prof. Museru maisha mema, tumekuwa na ushirikiano ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia sana kuboresha huduma za afya katika hospitali hii. Tutaendelea kuhitaji ushauri na maoni yake kuendelea kuboresha huduma za afya nchini” amesema Mhe. Kim.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji MNH-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akipokea msaada huo kwa niaba ya Wizara ya Afya, amesema utasaidia kuendelea kuboresha huduma za watoto wachanga mahututi kufuatia ukarabati wa wodi hiyo uliofanywa na KOFIH miezi michache iliyopita.

“ Vifaa hivi vilivyokabidhiwa leo vitasaidia kuongeza tija katika huduma za watoto wachanga mahututi kwa kuwa ni vingi na muhimu kwenye utoaji wa huduma, kwa niaba ya watumishi wenzangu tutahakikisha tunavitunza , kuvikarabati mara kwa mara na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa” amesema Dkt. Magandi Msaada huo wa vifaa tiba ni pamoja na mashine ya kumsaidia mtoto kupumua, mashine ya kumsaidia mtoto kuondoa manjano (jaundice), mashine inayomsaidia mtoto kutunza joto la mwili kwa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (premature babies).

Mashine nyingine ni ya kufuatilia mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni mwa mama yake, mashine inayomsaidia mtoto ambaye hawezi kupumua mwenyewe na mashine ya kufuatilia ishara za mwili wa binadamu.

Kukabidhiwa kwa msaada huu kunafuatia kuzinduliwa kwa mtambo wa kuzalisha hewa tiba (Oxygen generating plant) wenye uwezo wa kuzalisha mitungi 200 ya ujazo wa 6.3 M³ kwa siku ambao umegharimu dola za Marekani 300,000, pamoja na mradi wa kuboresha huduma ya mama na mtoto uliohusisha uboreshaji wa wodi ya watoto wachanga mahututi (NICU) na kuanzisha Wodi ya Uangalizi Maalumu ya Wazazi (Maternal ICU) kwa gharama TZS 240,808,060 Mil.
Share:

MGEJA ANG'AKA - " CHADEMA MUACHE SIASA ZA VITISHO, CCM NA SERIKALI VISIBEBESHWE LAWAMA"


Mwanasiasa Mkongwe Khamis Mgeja

Na Mwandishi wetu -Kahama

 

MWENYEKITI wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation ya mjini Kahama mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja amekitahadharisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiache kujiona ni chama bora kuliko vyama vingine vya siasa.

 

Mwenyekiti huyo ameelezea kushitushwa kwake na tamko  la vitisho ambalo limetolewa na CHADEMA hivi karibuni lenye viashiria vya vitisho kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake juzi, Mgeja yeye binafsi ameshitushwa na kusikitishwa na tamko la chama hicho ambalo linaashiria kuleta uchochezi na uvunjifu wa amani na halikuzingatia misingi ya utawala bora unaoheshimu sheria.

 

Mgeja ambaye ni miongoni mwa makada wenye misimamo ndani ya Chama Cha Mapinduzi alisema Taasisi anayoiongoza yeye haitakubali kukivumilia Chama chochote cha kisiasa, kikundi au mtu ye yote anayejihusisha na utoaji wa matamko yenye viashiria vya vurugu, uchochezi yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

 

Alisema matamko ambayo yametolewa na Kamati Kuu ya CHADEMA yakiipa CCM na Serikali yake masharti manane yanaonesha ni aina ya vitisho na yamekosa subira na hayazingatii suala la utawala bora wa kisheria.

 

“Mimi naomba ndugu niwaeleze wazi, ni vyema CHADEMA itambue hii Tanzania ni ya watanzania wote na kama ni uzalendo pia unamgusa kila mtanzania, kwa hiyo wao kuonekana ndiyo chama pekee kinachopigania haki ya watanzania siyo kweli,”

 

“Ni vizuri wakatambua kuwa hata  vyama vingine vya kisiasa hapa nchini pia ikiwemo chama tawala CCM vyote vinapigania haki na maendeleo ya watanzania tena kwa kuzingatia  misingi ya utawala bora unaozingatia sheria,” alieleza Mgeja.

 

Mwenyekiti huyo ambaye miongoni mwa kazi zinazofanywa na taasisi yake ni suala la utawala bora, haki na demokrasia alisema suala la mikutano ya hadhara na Katiba mpya siyo takwa la CHADEMA peke yake bali hata vyama vingine ikiwemo CCM yenyewe vinamahitaji hay ohayo.

 

Alisema tofauti na CHADEMA vyama vingine vyote vya siasa hapa nchini vinahitaji michakato ya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na katiba mpya utekelezwe kwa utaratibu mzuri na yawepo maridhiano ya watanzania wote tena kwa kuheshimu misingi ya sheria.

 

“Nichukue fursa hii kukipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya mwenyekiti wake Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kukaa meza moja ya mazungumzo na CHADEMA ambayo yatapelekea kupatikana kwa maridhiano, na nimpongeze vilevile kwa kuunda Kikosi Kazi cha kupitia maoni mbalimbali kuhusu suala la katiba,” alieleza Mgeja.

 

Katika hatua nyingine Mgeja alikiomba na kukipa ushauri wa bure chama hicho cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba kiitumie fursa iliyotolewa na Rais Samia ya maridhiano ya pamoja kwa manufaa mapata ya Taifa la Tanzania kuliko kuonesha dalili za kutaka kuweka mpira kwapani.

Pia amevipongeza vyama vyote vya siasa nchini ikiwemo CCM kwa kuendelea kuwa na subira kukipa nafasi kikosi kazi kilichoundwa na Rais ili kifanye kazi yake vizuri na mwisho ni wazi kwamba watanzania wote watatangaziwa matokeo ya kazi inayoendelea kufanyika hivi sasa.

 

“Niwaombe watanzania tuendelee kuwa na subira na kujiepusha na upotoshwaji, uchochezi na mashinikizo yoyote yanayotolewa na CHADEMA, tuendelee kuheshimu suala la utawala wa kisheria na utii wa sheria pasipo shurti,”

 

“Hata hili suala la wabunge kumi na tisa wa viti maalumu wa CHADEMA ni wazi lipo nje ya uwezo wa CCM na Serikali yake, tusiwabebeshe lawama, tuwe na subira na tuuachie mhimili husika (mahakama) itekeleze wajibu wake wa kisheria, tusishinikize uvunjifu wa sheria za nchi,” alieleza Mgeja.

Share:

MHUNI ANAYEDAIWA 'POPOBAWA' AZUA GUMZO KUWAINGILIA KINGONO WAKE ZA WATU KICHAWI MOROGORO


Wakazi wa Kijiji cha Igawa, Malinyi mkoani Morogoro, wameiomba serikali wilayani hapo kuwasaidia kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa popo bawa anayewaingilia watoto wa kike na wake za watu nyakati za usiku, na kwamba wanahofu ya kupata magonjwa ikiwemo VVU.

Wananchi hao wamedai popobawa huyo alikuwa anatumia imani za kishirikina ndipo aingie ndani ya nyumba na kutekeleza matukio hayo.

Hali hiyo imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mathayo Masele, kufika kwenye Kitongoji hicho na kukutana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo, na kusema kwamba Popobaya huyo amepelekea wanaume wasiheshimike ndani ya ndoa zao kwani imefikia hatua wakiamka wanakuta wake zao wameshaingiliwa.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Sungu Sungu kitongoji cha Igoloka Pius Mbala amesema sungusungu kwenye kitongoji hicho wamefanikiwa kumkamata popobawa huyo ambaye anatuhumiwa kufanya matukio hayo pia ni binadamu mwanumume na jina lake limehifadhiwa.

Kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa wilaya ya Malinyi akizungumza na wakazi wa kitongoji hicho baada ya kufika mara moja katika eneo hilo, amewaomba wakazi hao kuwa watulivu na kwamba Jeshi la Polisi linafuatilia ukweli wa taarifa hizo.

Chanzo - EATV
Share:

WATOTO WALIOGONGWA NA BASI WAKIENDA SHULE WAZIKWA


Watoto wawili wa familia moja waliogongwa na basi la Machame Investment Septemba 21 majira ya saa 12.30 asubuhi wakati wakienda shule mkoani Kilimanjaro wamezikwa jana huku Polisi wakitoa tahadhari.


Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limesema halitasita kufunga leseni kwa baadhi ya madereva watakaothibitika kutotii sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali vikiwamo vyombo vya moto.

Aidha Polisi imeomba ofisi ya katibu tawala wa wilaya ya Moshi kwa kushirikiana na halmashauri ya manispaa ya Moshi, kupanga vyema vituo vya waendesha pikipiki za kubeba abiria maarufu kama bodaboda, Bajaji na daladala katika maeneo ambayo havitaleta usumbufu kwa abiria wakiwamo wanafunzi.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema hayo wakati wa salamu za rambirambi za jeshi hilo kwenye mazishi ya watoto wawili wa familia moja waliogongwa na basi la Machame Investment Septemba 21 majira ya saa 12.30 asubuhi wakati wakienda shule.

Katika ajali hiyo basi la Machame lenye namba za usajili T 525 DZP liliendeshwa na Kombo Hassan liliwagonga na kuwaua papo hapo watu watatu, waliotajwa kuwa ni Calistes Agust (57) aliyekuwa ambaye alikuwa bibi pamoja na wajukuu zake wawili Jesca Erick (9) mwanafunzi darasa la nne shule ya msingi Mawenzi Na Witness Audax (7) mwanafunzi wa darasa la pili shule ya msingi Muungano katika manispaa ya Moshi.

Akizungumzia ajali hiyo kamanda Maigwa amesema polisi inamshikilia dereva wa basi hilo….. na kwamba atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapomalika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa chekereni wa bonite bw. ayubu juma aliomba jeshi la polisi kutoa mafunzo mbalimbali ya usalama barabarani kwa madereva pamoja na wanafunzi wawapo barabarani.

Nao baadhi ya washiriki latina misma hubo uliowaliza wazazi patoja na wote walioshiriki wamesema tukio hilo hawana budi kulipokea ila cha kikubwa ni sherry ifuatwe katika kupata haki za wahusika.

Chanzo - EATV

Share:

MBINU ILIYOWASAIDIA WENGI KUONGEZA MAUZO KATIKA BIASHARA ZAO NI HII HAPA!

Share:

Thursday, 22 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 23,2022



















Share:

MTOTO WA DARASA LA AWALI ADAIWA KUBAKWA CHOONI SHULENI... POLISI SHINYANGA KUCHUNGUZA


Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, limeombwa kufanya uchunguzi wa kina ili kumbaini mtu aliyehusika katika tukio la kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita, anayesoma darasa la awali katika shule ya Msingi Bugimbagu, iliyopo kijiji cha Bugimbagu, kata ya Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga.



Ombi hilo limetolewa na Babu pamoja na Baba mdogo wa mtoto huyo, ambao kwa pamoja wameiomba Serikali kupitia vyombo vyake kuchunguza kwa kina tukio hilo, ili kumbaini mtu aliyehusika na kumchukulia hatua kali za kisheria.

 Akielezea tukio hilo ambalo limetokea Septemba 15, 2022, katika eneo la shule ya msingi Bugimbagu, Babu wa mtoto huyo  amebainisha kuwa, alishangaa kuletewa taarifa kutoka shuleni juu ya mjukuu wake kukutwa katika eneo la choo cha shule hiyo akiwa ameumizwa vibaya sehemu zake za siri, kutokana na kile kinachoelezwa kuwa amebakwa na mtu asiyejulikana. 


Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo, Baba mdogo wa mtoto huyo , amesema baada ya kufika shuleni alikuta mtoto wao akiwa hawezi kutembea huku akitoka damu sehemu zake za siri, na alipouliza kwa Walimu alielezwa kuwa, wamemkuta akiwa amelala katika eneo la choo cha shule baada ya kupewa taarifa na wanafunzi wenzake, ambapo baada ya kumchunguza walibaini kuwa anatoka damu sehemu zake za siri. 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugimbagu Bi.Mwajuma Kashinje, amesema alipewa taarifa za tukio hilo na walimu wa shule hiyo, ambapo baada ya kufika shuleni hapo, alimkuta mtoto huyo akiwa ameumizwa vibaya sehemu za siri, lakini hakuna aliyefahamu chanzo cha tukio hilo. 

Naye Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Bugimbagu Bi.Neema Ngongi, amekiri kutokea kwa tukio hilo shuleni kwake na kubainisha kuwa, walimkuta mtoto huyo akiwa hawezi kutembea katika eneo la choo cha shule, baada ya kupewa taarifa na Wanafunzi wenzake, ambapo alitoa taarifa kwa mamlaka za juu za shule ikiwemo kamati ya shule na uongozi wa Kijiji, kwa ajili ya hatua zaidi. 


Baada ya Redio Faraja kufika katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga alipokuwa amelazwa mtoto huyo kwa matibabu, imekutana na Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt.Luzila John ambaye amebainisha kuwa, walimpokea mtoto huyo hospitalini hapo mnamo Septemba 15, 2022 na kumwanzishia matibabu na kwamba, vipimo vinaonesha aliingiliwa katika sehemu zake za siri na kupata majeraha, ingawa hakutaja moja kwa moja kama amebakwa.

Dkt.Luzila amebainisha kuwa, kwa sasa mtoto huyo ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali yake kuendelea vizuri, lakini wanaendelea kusubiri vipimo vingine ambavyo wamevipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali kwa uchunguzi zaidi.

 SOMA ZAIDI HAPA 


CHANZO RADIO FARAJA

Share:

ELIMU YA URAIA ITOLEWAYO SHULENI INA MCHANGO MDOGO KUSAIDIA VIJANA WA KITANZANIA

Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari akizindua ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchin, hafla hiyo imefanyika leo Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari wakionesha ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchin, hafla hiyo imefanyika leo Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam.Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi Mkuu HakiElimu Bw.Godfrey Bonventure akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mwasilishaji wa Matokeo ya Utafiti, Dkt.Perpetua Kalimasi akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wadau wa elimu nchini wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wanafunzi wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

*******************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UTAFITI uliofanywa na asasi ya HakiElimu mwaka 2022 kwa lengo la kuangalia mchango wa Elimu ya Uraia shule za sekondari katika kumwandaa kijana kujifunza na kushiriki vema michakato ya kidemokrasia nchini umeonesha kuwa Elimu ya Uraia itolewayo shuleni ina mchango kidogo katika kumsaidia kijana wa Kitanzania kujifunza na kushiriki shughuli za kisiasa na demokrasia.

Ameyasema hayo leo Septemba 22,2022 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu HakiElimu Bw.Godfrey Bonventure katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Mchango wa ‘Elimu ya Uraia’ Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Michakato ya Kidemokrasia Nchini.

"Kwa mujibu wa utafiti huu, uliofanyika katika Wilaya za Mkuranga, Tabora, Ukerewe, Kilwa, Sumbawanga and Arusha; unaonesha ushiriki hafifu wa vijana katika mifumo ya kidemokrasia ndani na nje ya shule; unachangiwa na mapungufu yaliyopo katika mtaala wa elimu ya uraia itolewayo shule za sekondari, namna ya ufundishaji pamoja na mifumo ya ukuzaji demokrasia kama vile utawala na uongozi shuleni, namna ya uendeshaji vyumba vya madarasa na mtazamo hasi wa jamii juu ya shughuli za kisiasa na kidemokrasia kwa ujumla". Amesema

Amesem utafiti umebaini kuwepo kwa changamoto kubwa katika mtaala wa somo la uraia shule za sekondari ambao kwa kiwango kikubwa haumpi mafunzo stahiki mwanafunzi yatakayomfanya aelewe vyema na kushiriki shughuli za kidemokrasia katika ngazi mbalimbali kwa nafasi yake.

Aidha amesema kwa upande wa walimu, utafiti umeonesha kuwa sehemu kubwa ya walimu ambao wanafundisha somo la uraia hawana maarifa stahiki yanayowawezesha kuwafundisha na kuwaaandaa vijana kuelewa maana ya siasa safi na umuhimu wa ushiriki wao katika mifumo ya kidemokrasia katika ngazi ya shule, familia na jamii.

Ameeleza kuwa kwa mujibu wa utafiti huo vijana wanatarajia kuwa shule ndio chanzo kikuu cha kujifunza na kujengewa uzoefu katika michakato ya kidemokrasia ukilinganisha na radio, televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na kujisomea vitabuni.

Hata hivyo amesema pamoja na matarajio makubwa ya kujifunza siasa na demokrasia kupitia elimu ya uraia itolewayo shuleni; matokeo ya utafiti huu yanaonesha bado kuna mapungufu katika utoaji wa Elimu ya Uraia shuleni na ushiriki wa vijana katika michakato ya kidemokrasia.

Amesema katika ngazi ya shule, utafiti unaonesha asilimia 44.4 ya wanafunzi hawaelewi maana ya demokrasia, asilimia 85.5 hawajawahi kushiriki au kushirikishwa katika vikao rasmi vya shule vinavyofanya maamuzi kuhusu mapato na mgawanyo wa rasilimali za shule.

Huku asilimia 68.9 hawajawahi kugombea au kuonesha nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ngazi ya shule, asilimia 44 hawashiriki katika chaguzi za uongozi wa wanafunzi, asilimia 26 hawajawahi kushiriki kabisa midahalo na mijadala ya hoja kama sehemu ya kuwajengea uwezo wa ushawishi na demokrasia.

Amesema Utafiti pia umeonesha kuwa asilimia 47 ya viongozi wa wanafunzi shule za sekondari hawapatikani kwa njia ya chaguzi za kidemokrasia bali kwa kuteuliwa na uongozi wa shule 11% kwa kujitolea na asilimia 42 pekee ndio ambao hupatikana kwa kufanyika uchaguzi ambao wanafunzi wenzao hupata fursa ya kupiga kura na kuchagua.

"Hali hii inaelezwa kuchangia kwa kiasi kukubwa kudumaza ushiriki wa vijana katika shughuli za kidemokrasia katika maisha yao". Amesema

Amesema katika ngazi ya jamii, zaidi ya asilimia 80 ya vijana waliko shuleni hawajawahi na hawahamasishwi kushiriki mikutano ya kampeni na siasa; asilimia 67.8 hawajawahi kuhudhuria mikutano ya Kijiji au mtaa na asilimia 67.5 hawajawahi na hawaoni umuhimu wa wao kushiriki shughuli za kijamii husasani zinazohusu maendeleo ya vijiji au mtaa kwa kujitolea.

"Sehemu kubwa ya jamii bado inashidwa kuoanisha elimu ya uraia na maandalizi ya viongozi na siasa safi za baadae; hali hii imechangia jamii kutoa hamasa kidogo kwa vijana kushiriki katika shughuli za siasa na demokrasia wakiwa bado shuleni". Amesema

Ameeleza kuwa kwa ujumla matokeo ya utafiti huo yanaonesha kutoridhika kwa vijana na namna mfumo wa elimu na jamii unavyowaandaa kuelewa na kushiriki katika mfumo wa siasa na demokrasia.

Amesema kuwepo kwa sheria kama za uchaguzi zinazolazimisha vijana kuanza kupiga kura katika umri wa miaka 18, zinatajwa kuchangia katika kuchelewesha vijana kuanza kushiriki katika masuala ya demokrasia.

Hata hivyo amesema Utafiti unapendekeza mapitio ya mtaala wa elimu ya uraia ili kutilia mkazo maudhui na mbinu za ufundishaji vinavyomwandaa kijana katika mawanda mapana ya ufahamu juu ya maana na umuhimu wa ushiriki wao katika medani za siasa na uga wa demokrasia angali mapema.

Pamoja na hayo amesema Katika ngazi ya familia, wazazi na walezi wanashauriwa kuachana na mfumo wa malezi usiowashirikisha au unao watenga Watoto,katika maamuzi ya kifamilia na maslahi yao.

Kwa upande wake Kamishna wa Elimu Tanzania Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema ili kuhakikisha vijana wanashiriki kikamilifu shughuli za demokrasia ni vyema Elimu ya uraia ikaanza kutolewa katika ngazi ya awali ili kuwaandaa mapema zaidi.
Share:

TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA PLAN INTERNATIONAL WAANDAA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO KWA WATOTO WA KIKE KUJIAMNINI


                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

22nd September 2022

 

“TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA PLAN INTERNATIONAL WAANDAA MAFUNZO YA KUJENGA UWEZO KWA WATOTO WA KIKE KUJIAMNINI”

 

 

KAULI MBIU: ‘’Wakati wetu ni sasa—haki zetu, mustakabali wetu”

 

DAR ES SALAAM SEPTEMBER 21, 2022: Taasisi za Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) na Plan International Tanzania zimeandaa mafunzo ya kuongeza uwezo wa kujiamini kwa  watoto wa kike 40 juu ya kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao hususan katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike pamoja na ufahamu wa sheria za nchi juu ya maswala hayo.


Mafunzo hayo, ni sehemu ya shughuli za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike duniani, yatafanyika mnamo Septemba 24, 2022 katika hoteli ya Regency jijini Dar es salaam. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni imelenga ile ile ya kimataifa ya: “Wakati wetu ni sasa—haki zetu, mustakabali wetu”

 

“Mafunzo hayo yataenda kwa jina la “Wasichana Washika Hatamu” na ni jukwaa lakuwapa mafunzo Watoto wa kike ya kuongeza uwezo wa kujiamini ,kutambua afya ya akili, kukuza ustawi wao hususan katika masuala ya lishe na ukakamavu, haki za mtoto wa kike pamoja na ufahamu wa sheria za nchi katika nafasi za kufanya maamuzi”, anasema Mtendaji Mkuu wa JMKF, Bi. Vanessa Anyoti.

 

Bi Anyoti anaeleza kwamba Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike imekuwa jukwaa muhimi katika kutambua haki za msichana pamoja na changamoto kubwa anazopambana nazo duniani, na kwamba sasa kuna wito wa kuchukuliwa kwa hatua za makusudi za kuleta mageuzi  kijamii na kisiasa ili kuondoa vizuizi mbalimbali vya ubaguzi na chuki vinavyoendelea kurudisha nyuma maendeleo ya wasichana.

 

“Tanzania inaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kukuza ufahamu wa jamii juu ya masuala yanayowakabili wasichana na kuwapatia fursa ya kupaza sauti zao.

 

“Duniani, wasichana wanaendelea kukabiliana na changamoto za uongozi, elimu, masuala ya afya ya akili na ukatili wa kijinsia, wakati wao ndio mawakala wakuu wa mabadiliko katika jamii zao”, anaongezea Bi. Anyoti.

 

Kwa Habari zaidi wasiliana na Beatrice Mnzava via 0764065164 na  beatrice.mnzava@jmkfoundation.org

 


Muhidin Issa Michuzi

AFISA MAWASILIANO

JAKAYA MRISHO KIKWETE FOUNDATION


Share:

WAVUNAJI MKAA WATAKIWA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akiwataka wavunaji wa mkaa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu swali Bungeni jijini Dodoma leo.

**************************

Serikali imewataka wananchi wanaofanya biashara ya mkaa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu kwa kuwa kumekuwepo na wimbi la uvunaji wa mazao ya misitu, ukataji na uchomaji wa mkaa bila kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia biashara hiyo.

Hayo yamesemwa leo Septemba 22,2022 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Nicodemus Maganga (Mbogwe).

“Inapotokea mwananchi anasafirisha mazao ya misitu (mkaa) bila kufuata utaratibu, mazao hayo hutaifishwa na Serikali” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amesema uvunaji holela wa mkaa umesababisha kutoweka kwa kasi kwa maeneo ya misitu na hatimaye kujitokeza kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Kuhusu kauli ya Serikali juu ya askari wa Misitu wanaopiga na kuwanyang’anya mkaa wananchi wa Mbogwe, Mhe. Masanja amesema Wizara haitosita kuwachukulia hatua watumishi wake wanaohusika na uvunjaji huo wa sheria, kanuni na taratibu.

Pia, amewataka Wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama wanapotendewa vibaya na watumishi hão ili hatua stahiki zichukuliwe.

Akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka kuhusu lini Serikali itatoa vibali vya Uwindaji, amesema Vibali vya uwindaji wa kitalii vinaendelea kutolewa kwa mujibu wa Kanuni husika ambapo hadi sasa jumla ya minada saba (7) imefanyika na wadau wamepewa vibali vyao.
Share:

NZUNDA AWATAKA WASIMAMIZI WA VITUO ATAMIZI KUWA WABUNIFU


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda akifunga mafunzo ya wasimamizi wa Vituo Atamizi vya Ufugaji Mifugo Kibiashara kwa Vijana yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Morogoro ambapo amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanakwenda kusimamia utekelezaji wa mwongozo na kuwa wabunifu katika kuhakikisha malengo ya serikali ya kuwa na vijana wenye uwezo wa kufuga mifugo kisasa na kwa tija yanatimia. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Dkt. Pius Mwambene na kushoto ni Dkt. Moses Olenesele, Mtumishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO). 


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Dkt. Pius Mwambene (kulia) akichangia mada wakati wa mafunzo ya wasimamizi wa Vituo Atamizi vya Ufugaji Mifugo Kibiashara kwa Vijana yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Morogoro. Dkt. Mwambene amesema kuwa LITA kupitia kampasi zake imejipanga kuhakikisha malengo ya serikali yanatimizwa. 


Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya wasimamizi wa Vituo Atamizi vya Ufugaji Mifugo Kibiashara kwa Vijana yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Morogoro wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa mafunzo hayo. 


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Chama cha Ushirika cha Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO), Joseph Massimba (wa pili kutoka kulia) wakati alipokuwa akikagua shughuli wanazozifanya katika kituo chao ambapo amewasihi kuanza kujikita kwenye ufugaji kwa kuwa zipo fursa nyingi kupitia Sekta ya Mifugo. 


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Shamba katika Chama cha Ushirika cha Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUGECO), Marcelina Lubuva (kushoto) wakati alipokuwa akikagua shamba la alizeti kwenye kituo chao. 

.................................................. 

Katibu Mkuu anayesimamia Sekta ya Mifugo, Bw. Tixon Nzunda amewataka wasimamizi wa Vituo Atamizi vya Ufugaji Mifugo Kibiashara kwa Vijana kuwa wabunifu na kuhakikisha wanasimami utekelezaji wa mwongozo uliotolewa kuhusu vituo hivyo. 

Nzunda ameyasema hayo leo Septemba 21.09.2022 wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya wasimamizi wa vituo atamizi vya ufugaji mifugo kibiashara kwa vijana yaliyofanyika kwenye Chuo cha Mafunzo ya Mifugo Kampasi ya Morogoro. 

Wasimamizi hao wa vituo wametakiwa kuwa wabunifu hasa katika kukabiliana na changamoto watakazo kutana nazo, huku wakitakiwa kuwajenga vijana hao uwezo wa kuweza kufuga kisasa kwa vitendo, kuwa na mahusiano na mawasiliano mazuri ambayo yatawasaidia katika masoko ya mifugo pamoja na mazao ya mifugo watakayokuwa wanazalisha. 

Lakini pia amewataka wasimamizi hao kuwapatia vijana elimu ya utunzaji wa malisho na upandaji wa malisho mapya ili hata watakapotoka katika vituo hivyo waweze kwenda kuanzisha mashamba ya malisho kwa ajili ya mifugo yao. 

Nzunda amesema serikali kwa sasa imeamua kufungua milango kwa vijana kupitia Sekta ya Mifugo ambapo vituo hivyo vitasaidia kuwabadilisha vijana kifikra kuhusu ufugaji, kupunguza tatizo la ajira, na kuongeza uzalishaji wa mifugo na mazao yake kwa kuzingatia viwango na kuongeza kipato cha vijana na taifa kwa ujumla. 

Serikali katika kuhakikisha vituo hivi vinaanza kazi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imatenga kiasi cha shilingi bilioni 4 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kuanza kupata mafunzo ya ufugaji wa kisasa kwenye vituo 8 vilivyopo LITA na TALIRI ambapo usahili wa vijana hao tayari ulishakamilika. 

“Vijana hawa wanakwenda kupatiwa ujuzi kuhusu maisha, ujuzi kuhusu uzalishaji wa kazi, ujuzi wa uzalishaji fedha, ujuzi wa kupata mitaji, na ujuzi wa kwenda kujenga uchumi wa nchi kupitia Sekta ya Mifugo,” alisema Katibu Mkuu Nzunda 

Vijana waliochaguliwa kujiunga na vituo atamizi wametakiwa kuwa na moyo wa kujituma na kujitambua kwamba wao ni wawekezaji ambao wameingia kuwekeza kwenye Sekta ya Mifugo. 

Nzunda ameitaka LITA na TALIRI kuhakikisha kazi hii inaanza kutekelezwa Septemba 26, 2022 na kwamba fedha zilizotolewa kwa kazi hii zisitumike kwa ajili ya kuendeshea ofisi wala kazi nyingine yoyote nje ya kazi iliyokusudiwa na serikali. 

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA), Dkt. Pius Mwambene amesema kuwa LITA inakwenda kuanzisha vituo 6 katika kampasi za Kikulula (Kagera), Mabuki (Mwanza) na Buhuri (Tanga) ambapo kila kituo kitachukua vijana 30 ambao watafundishwa namna ya kufuga kibiashara kwa muda wa miezi 12. 

Dkt. Moses Olenesele, Mtumishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) amewasihi vijana waliopata nafasi ya kujiunga na mafunzo hayo kuhakikisha wanaitumia fursa hiyo vizuri kwa kuwa serikali imeweka matumaini kwa vijana hao kuja kuwa wafanyabiashara wakubwa wa mifugo iliyo bora.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger