Saturday, 17 September 2022
TBS YASHIRIKI VIWANGO SPORTS BONANZA
MAMIA WAMZIKA MAREHEMU ASANTINA SEBASTIAN JIJINI DAR ES SALAAM
SEPESHA RUSHWA MARATHON KUTIKISA DODOMA
Mwenyekiti wa Sauti ya wapinga Rushwa Mkoa wa Dodoma Haruna Kitenge akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu Sepesha rushwa marathon inayo tarajiwa kufanyika Desemb 11,2022 Dodoma. |
Na Dotto Kwilasa,DODOMA
JUMLA ya washiriki 2000 wanatarajia kushiriki mashindano ya Sepesha Rushwa Marathon yanayotarajia kufanyika Desemba 11 mwaka huu Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Sauti ya wapinga Rushwa Mkoa wa Dodoma,ambaye ndio mratibu wa mbio hizo,Haruna Kitenge alisema washiriki hao ni wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo,watumishi wa serikali na taasisi mbalimbali pamoja na wakimbiaji mbalimbali.
Kitenge alisema mbio watakazokimbia ni Km 21,10,5 na 3 lengo la mashindano hayo ni kuwaelewesha vijana kuhusu madhara ya rushwa pamoja na kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza kampeni ya Sepesha Rushwa katika Jiji la Arusha.
Hata hivyo Kitenge aziomba kampuni,taasisi binafsi na mashirika kujitokeza kudhamini mbio hizo.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dodoma,Robert Mabonye aliwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki mbio hizo.
Alisema hiyo ni fursa kwao kwani matukio kama hayo yamekuwa ni nadra kufanyika mkoani humo.
TBS YAENDELEA NA ELIMU KWA UMMA ILEMELA
SINDI MZAMO: RAIS SAMIA NI CHAMPION WA UTALI AFRIKA, AUNGWE MKONO
ZAIDI YA WATU 1000 KUHUDHURIA KONGAMANO LA UWEZESHAJI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.,
Na Dotto KwilasaDODOMA.WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la sita la uwezeshaji Wananchi kiuchumi ambalo litafanyika Septemba 19 Mwaka huu Jijini Dodoma.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule ameyaeleza hayo jana Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Kongamano hilo ambalo litahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wadau wa maendeleo.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma ametoa Wito kwa wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa kupitia Kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuandaa miundombinu mbali mbali ya kiuchumi ikiwemo biashara ya chakula na malazi.Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Beng' Issa akaeleza lengo la Kongamano hilo kuwa ni fursakatika kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.Amesema jukwaa hilo litahudhuriwa na zaidi ya watu1000 kwa kuhusisha jopo la majadiliano la wakuu wa Mikoa pamoja na Wataalam kuhusiana na masuala yakuwawezesha wananchi kiuchumi.Naye Meneja wa Benki ya Stanbic Tawi la Dodoma Opi Ligolola ametumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali kutokana na jitihada zake katika kuwawezesha wanachi kiuchumi na kueleza Mkataba walioingia na Baraza la uwezeshaji Wananchi kiuchumi,
Friday, 16 September 2022
HII NDIYO MIJI YENYE MATAJIRI WENGI ZAIDI DUNIANI 2022
ATUPWA JELA MIAKA 20 KWA KUJINUFAISHA KINGONO KWA MTOTO WA MIAKA MITATU
Thursday, 15 September 2022
ABBASI :TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA MUSIC IN AFRICA
OJADACT YATOA MAPENDEKEZO KUKOMESHA MATUKIO YA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI NA KULETA HOFU KWA JAMII
TAARIFA KWA UMMA
MATUKIO YA MAUAJI YANAYOENDELEA NCHINI NA KULETA HOFU KWA JAMII
Septemba 15, 2022
Chama Cha Waandishi wa Habari za Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT) kinalaani mwenendo wa matukio ya mauaji yanayoendelea kwenye jamii na kusababisha hofu kwa jamii pamoja na kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
OJADACT inasikitika kuona matukio hayo yakiendelea kutokea na kuchafua taswira ya Taifa kwenye kulinda amani na usalama wa raia wake pamoja na kutumia rasilimali nyingi za Taifa kwenye kupambana na vitendo vya kihalifu.
Baadhi ya matukio yaliyotokea ni tukio la Septemba 14, 2022, la mauaji ya Mwanafunzi wa Chuo Kikuu, Maria Bosco lililotokea eneo la Kawe Mzimuni, Jijini Dar es salaam lililofanywa na vijana zaidi ya thelathini ambao walitekeleza mauaji , kujeruhi na kupora vitu mbalimbali vikiwemo simu na fedha.
Tukio jingine, tukio la mauaji ya watu wanne lililotokea Jijini Mbeya ambapo Mwalimu wa Shule ya Msingi Bwana Saimon Mtambo (44) alimkata mapanga mke wake na watoto wake wawili na kisha yeye kunywa sumu na kupoteza Maisha.
Tukio jingine, tukio lililotekea Mkoa wa Mtwara, ambapo Kijana Kristatus Victory (23) Mkazi wa Lukuledi Wilaya ya Masasi anatuhumiwa kumuua Baba yake Mzazi Victory Milanzi (74)kwa madai ya kushindwa kumtafutia mchumba wa kuoa.
Tukio jingine, tukio la Mkazi wa Kihesa Kilolo Mkoani Iringa Enea Mkimbo (55) aliyefariki Dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge kwa madai ya kuzongwa na madeni ya vikoba.
OJADACT imebainisha matukio haya Machache ikiwa ni sehemu tu ya matukio yanayoendelea kwenye jamii, matukio hayo yamekuwa yakisabishwa na sababu mbalimbali ikiwemo, tamaa za kujipatia fedha, wivu wa kimapenzi, mmomonyoko wa maadili , hali ngumu ya maisha na ushirikina na mani potofu kwenye jamii.
OJADACT inatoa mapendekezo yafuatayo.
1. Kuundwa kwa mkakati wa kitaifa wa kuzuia uhalifu ili kusaidia kupunguza matukio haya ya mauaji na uhalifu mwingine kwa kuwaleta wadau pamoja na kuweka mikakati mahususi.
2. Kuimarisha maadili ndani ya jamii ili kuwa na jamii yenye kuheshimu utu na ubinadamu.
3. Serikali kupitia taasisi zake za kupambana na uhalifu pamoja na ustawi wa jamii kufanya tafiti za kutosha ili kugundua chanzo cha mauaji na uhalifu Nchini.
4. Jeshi la Polisi kuongeza kasi ya kupambana na matukio ya kihalifu hasa vikundi visivyo rasmi vinavyofanya uhalifu.
5. Vyombo vya habari na taasisi za kihabari kutengeneza maudhui yenye kuhamasisha watu kutofanya uhalifu Zaidi kuliko kuripoti matukio ya kihalifu Zaidi.
*Edwin Soko*
*Mwenyekiti*
*OJADACT*
*15.09.2022*
MIFUGO VAMIZI CHANGAMOTO YA UHIFADHI NCHINI
Na. Catherine Mbena/Iringa
Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),tarehe 14 Septemba 2022 imefanya ziara ya kutembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha mkoani Iringa kujionea athari za uvamizi wa mifugo katika eneo la Bonde la Ihefu . Katika ziara hiyo, Bodi ilishuhudia takribani mifugo zaidi ya laki Mbili ikiwa ndani ya hifadhi.
Awali, akiwasilisha taarifa ya Hifadhi kwa Bodi, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Godwell Meing’ataki alibainisha kwamba operesheni iliyofanyika kwa siku mbili ilifanikiwa kukamata mifugo zaidi ya elfu moja na mia tisa katika eneo hilo la Ihefu na itaendelea kwa siku 10 zaidi kuanzia tarehe 13 septemba 2022 hadi tarehe 23 septemba 2022.
Akipokea taarifa hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya TANAPA,
Jenerali (Mstaafu) George Waitara alisema “ leo tumejionea uvamizi mkubwa wa mifugo ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha. Ikumbukwe hifadhi hizi ni mali yetu sote watanzania na ni sehemu ya uchumi wa Tanzania, wakati mifugo ni mali ya mtu mmoja mmoja. Hivyo ni jukumu letu kulinda hifadhi ambayo ni ya Watanzania wote kwa faida ya sasa na ya baadaye”
Aidha, Jenerali Waitara aliongeza kuwa mifugo itakuwa chanzo cha kufa kwa hifadhi zetu, kwani inaua mifumo ya Ikolojia na kuhatarisha kutoweka kwa wanyama na mimea. Hivyo ni muhimu hifadhi hizi zikalindwa kufa na kupona.
Naye Prof. Wineaster Anderson ambae ni mmoja wa wajumbe wa Bodi hiyo, alisema TANAPA ina wajibu mkubwa wa kulinda maliasili zilizomo hifadhini kwa faida ya Watanzania wote.
“Tuna wajibu mkubwa katika Taifa hili wa kulinda maliasili hizi pamoja na miradi ya kimkakati kama Bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere ambalo linategemea maji kutoka vyanzo vilivyomo hifadhini Ruaha. Kiasi kikubwa cha fedha kimekwishatumika kujenga bwawa hilo na wananchi wana mategemeo makubwa ya kunufaika nalo.
Hivyo sisi tukishindwa kulinda hivi vyanzo vya maji tutadaiwa na Watanzania sio tu leo, bali hata baada ya maisha yetu hapa duniani” aliongeza Profesa Wineaster.
Kwa upande wake Mjumbe mwingine wa Bodi, Kamishna wa Polisi Nsato Marijani, alisisitiza kuongeza nguvu katika kufanya doria na kuendeleza operesheni ya kuwaondoa wavamizi wote katika eneo la hifadhi hiyo.
Naye Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, William Mwakilema aliishukuru Bodi ya Wadhamini kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha kujionea changamoto kubwa ya uvamizi wa mifugo ambayo ni tishio kwa uhifadhi nchini.
Alibainisha kuwa endapo hapatakua na juhudi madhubuti na za dhati za kudhibiti mifugo, itapelekea kufa kwa hifadhi zetu ambazo ni tunu kwa Taifa, na zimekuwa zikituletea fedha, sifa na fahari ndani na nje ya nchi yetu.