Thursday, 15 September 2022

MAMA AJIUA KWA MADAI YA KUZIDIWA NA MADENI YA VIKOBA

Mkazi wa Kihesa Kilolo mkoani Iringa, Enea Mkimbo (55) amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kitenge kwa madai ya kuzongwa na madeni ya Vikoba.

Inadaiwa Septemba 13, 2022 wanakikundi wenzake walienda nyumbani kwake kudai madeni na ilipofika jioni akamuaga mumewe, Edward Sanga kuwa anakwenda nyumbani kwa mama yake mzazi na badala yake aliingia jikoni na kujitundika kitanzini hadi kufa.

Via Mwananchi
Share:

NJIA YA KUTHIBITI FEDHA ZAKO ZISIWEZE KUPOTEA KIRAHISI

Share:

Wednesday, 14 September 2022

TUMIENI MAWASILIANO KUJIIMARISHA KIUCHUMI

Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John akizungumza na wananchi kuhusiana na matumizi ya simu kwa maaendeleo ya uchumi wakati wa Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako na viunga vyake mkoani Njombe. Afisa Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano Mabel Masasi akitoa maelezo kuhusiana na matumizi ya simu kwa kujiletea maendeleo na namna ya kutumia kwa usalama wa mtandaoni kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako na Viunga vyake mkoani Njombe . Afisa Mwandamizi wa Uhusiano na Mawasiliano Mabel Masasi akizungumza na mwananchi kuhusiana na matumizi ya simu na namna ya kuwa makini na matumizi ya simu wakati TCRA ikiwa katika utoaji wa elimu kwa wananchi katika mikusanyiko kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako na Viunga vyake mkoani Njombe . Picha za matukio mbalimbali kwenye Gulio la Wiki katika Mji wa Makambako ambapo TCRA ikiwa inatoa elimu juu matumizi salama ya simu na kutumia simu kwa katika maendeleo ya kiuchumi.

**************************

Wananchi wa Makambako wameshauriwa kutumia huduma za mawasiliano kujiimarisha kiuchumi ndani na nje ya nchi.

Akizungumza katika Gulio la wiki lililofanyika katika eneo la Soko Kuu la Makambako Meneja wa Kanda ya Nyanda za juu kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Asajile John amesema mawasiliano yamerahisisha upatikanaji wa fursa mbalimbali zikiwemo za kiuchumi.

Mhandisi Asajile amesema katika Ulimwengu wa sasa taarifa nyingi za uboreshaji wa huduma, biashara, masoko na kilimo zinapatikana mtandaoni na kuwataka wananchi wa makambako kutumia fursa hizo.

Ametoa mfano wa taarifa za uboreshaji wa kilimo, upatikanaji wa masoko ya bidhaa za kilimo na misitu pamoja kutangaza bidhaa katika masoko ya ndani na ya kimataifa kuwa zinaweza kupatikana mtandaoni na kuwasihi wananchi badala ya kutumia mitandao kufanya mambo yasiyo na faida wajielekeze katika maeneo hayo ya msingi

Huu ni muendelezo wa kampeni ya kuelimisha umma juu ya matumizi bora na salama ya huduma za mawasiliano ijulikanayo kama kwea kidijitali inayoendeshwa na TCRA nchi nzima.
Share:

NAIBU WAZIRI KATAMBI AWAOMBA WADAU KUWEZESHA TIMU YA WATU WENYE ULEMAVU TEMBO WORRIORS KUSHINDA KOMBE LA DUNIA


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi
Amewataka wadau mbalimbali kuchangia timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu Tembo Warriors ili ifanikiwe kushinda mashindano Kombe la Dunia na imekuwa fahari ya Tanzania na kuwa mfano wa kuigwa na Nchi zingine kuwa Watu Wenye Ulemavu wanaweza kila kitu.


Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Katambi katika mkutano wa mwisho wa kuhimiza na kuagana kuelekea kambi itakayo wekwa Nchini Uturuki kwa maandalizi ya shindano la kidunia.


Aidha ameeleza kuwa serikali inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ipo pamoja na watu wenye Ulemavu na imetoa zaidi ya Milioni mia moja na hamsini kuhakikisha timu inachukua Kombe la Dunia.


Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu iko bega kwa bega nao, huku akitoa zaidi ya Shilingi Milioni mbili kwa Team kuwa chachu ya kuhimiza wadau mbalimbali kuisaidia timu hii ya watu Wenye Ulemavu kuimarika Kimataifa na kuleta heshima ya Taifa.


“Tunawaomba wadau mbalimbali taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali tuwasaidie wafike mbali maana ukiwasaidia Watu Wenye ulemavu ni umefanya dua, ni sala, ni Ibada na ni sadaka zaidi ya zaka”, alisema mhe.Katambi.

Katambi akaongeza kusema kuwa Mhe. Rais anawapenda sana watu wenye Ulemavu kafanya mengi ikiwemo kufufua vyuo zaidi ya 6 vya Watu wenye ulemavu kwa Tshs bilioni 3, Kuzalisha mafuta maalumu Nchini kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi, kutoa mikopo kwa mtu mmojammoja, kukutana nao Ikulu kuwasikiliza na kuitambua Jumuiya Band ya Watu wenye ulemavu pamoja na kuhakikisha kuwa anasimamia asilimia 3% ya ajira wapewe hawa watu wenye ulemavu, Ujenzi miundombinu rafiki, kupunguza kodi na Ugawaji Vifaa wezeshi, Sasa tunabadilisha Sera na Sheria kwa faida ya Makundi haya maalumu na muhimu.


"Nitahakikisha Watu wenye Ulemavu wanapewa haki zao ni lazima na sio hisani wala hidaya.Mungu atubariki sote!", alisema mhe.Katambi.
Share:

Breaking : MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA IGUNGA AFARIKI KWENYE AJALI



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omary na dereva wake pamoja na mtu mwingine mmoja, wamefariki dunia kufuatia ajali mbaya iliyohusisha magari matatu, iliyotokea mchana wa leo katika mteremko wa Inyala Mkoani Mbeya.


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa gari la mkurugenzi aliyekaidi amri ya jeshi la polisi kusimama ili kupisha msafara wa malori.

Ajali hiyo imehusisha pia magari mengine mawili, likiwemo lori la kubebea mafuta, mali ya kampuni ya Lake Oil na lori lingiine la mizigo.
Share:

DC MKUDE AKAGUA MIRADI YA MAJI BUBIKI, BUPIGI...AIPONGEZA RUWASA, WANANCHI WACHEKELEA ...."MATESO YETU YA MAJI YAMEFIKA KIKOMO"


Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akifungua maji kwenye moja ya vituo vya kuchotea maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.

Na Kadama Malunde  - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Joseph Modest Mkude amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maji katika kata ya Bupigi na Bubiki inayotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi ili kuboresha hali ya maisha.


Mkude amefanya ziara hiyo leo Jumatano Septemba 14,2022 akiwa ameambatana na maafisa wa RUWASA wakiongozwa na Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima.


Miradi aliyotembelea ni pamoja na mradi wa Maji ya Bomba ambacho chanzo chake ni Kisima kirefu wa Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki uliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 967 (Tsh. 967,811,515/=) pamoja na Mradi wa maji ya bomba ambao chanzo chake ni Ziwa Victoria wa Bupigi - Butungwa katika kata ya Bupigi unaojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 499 (Tsh. 499,514,650/=.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mkude amesema lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salamba pamoja na kumtua mama ndoo kichwani na kumpunguzia umbali wa kwenda kutafuta maji na badala yake kumuongezea muda wa kufanya shughuli zingine za maendeleo ili kujiimarisha kiuchumi na kijamii.

Mkude ameipongeza RUWASA Kishapu kwa kusimamia vizuri mradi wa maji wa Mwamishoni - Nyasamba na kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi sambamba na kumtua mama ndoo kichwani.


"Nawapongeza Mkandarasi anayetekeleza mradi huu pamoja na RUWASA kwa usimamizi mzuri, mradi umekuwa na matokeo mazuri. Lengo la Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuleta fedha nyingi ni kutaka kuona fedha zinaleta matokeo makubwa na kuondokana na tatizo la maji...

Licha ya kwamba mradi huu wa maji umeshaanza kuwanufaisha wananchi,wanapata huduma ya maji, Tunachohitaji kuona sasa ni mradi unakamilika mapema, kamilisheni sehemu zilizobaki ikiwemo ujenzi wa fensi ", amesema Mkude.


Mkuu huyo wa wilaya amewataka viongozi wa vijiji pamoja na wananchi kushirikiana kulinda miundombinu ya maji huku akiziagiza Jumuiya za watumiaji maji kukusanya fedha na kutumia fedha kwa ajili ya uendelevu wa mradi wa maji.


"Hongereni kwa kupata maji safi na salama, Jukumu lililobaki sasa ni kutunza miundombinu ya maji. Hiki ni kitu chenu, mmepunguza adha ya kutafuta maji kwa umbali mrefu, tunzeni mradi huu..

Wilaya ya Kishapu bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwani tupo chini ya asilimia 60. Serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ndani ya mita 400", ameongeza Mkude.



Akiwa katika mradi wa maji Bupigi - Butungwa, Mkuu huyo wa wilaya ya Kishapu licha ya kushuhudia huduma ya maji ikitolewa, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi huo, uliofikia 85%, Bent Company Ltd kukamilisha mradi huo haraka kwa kujenga fensi, chemba na kupaka rangi.

"Nafurahi kuona huduma ya maji imeanza kutolewa lakini Mradi huu unasuasua. Mkandarasi hakikisha unakamilisha mradi huu ndani ya wiki mbili kama ulivyoahidi. Wewe ni ndugu yangu tusiharibiane. Meneja RUWASA nakupongeza kwa kazi nzuri wananchi wanapata maji lakini nataka mradi ukamilike kwa wakati", amesema Mkude.

Naye Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu,Mhandisi Dickson Kamazima amesema mradi wa maji Bupigi - Butungwa unaojengwa kwa fedha za UVIKO - 19 unatakiwa kukamilika kabla ya Septemba 30,2022 ujenzi wake umefikia 85% ukitarajiwa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 2000 ukiwa na vituo vinne vya kuchotea maji huku mradi wa maji Mwamishoni - Nyasamba uliokamilika kwa 90% ukinufaisha wananchi zaidi ya 6500 ukiwa na vituo 13 vya kuchotea maji (DP 6 Nyasamba na Mwamishoni 7).

“Mradi wa maji wa Bupigi – Butungwa ulianza kujengwa Januari 2022 unatarajiwa kukamilika Septemba 2022. Fedha hizi ni ufadhili wa Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO - 19 kutoka serikali kuu”,amesema Mhandisi Kamazima.


Aidha ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi wote kushirikiana kulinda miundombinu ya maji ili kuiwezesha huduma ya maji kuwa endelevu kwa manufaa ya kizazi cha leo na kijacho.


Kwa upande wao wananchi akiwemo Magdalena Stephano na Japhet Joseph na Daudi Ndaki wameishukuru serikali kuwapatia huduma ya maji safi na salama wakieleza kuwa ilikuwa changamoto ya muda mrefu walikuwa wanatumia muda mwingi kufuata maji na asilimia kubwa maji machafu kwenye mabwawa, mashimo na mito.

"Changamoto hii ya maji sasa imekwisha..Tumemaliza changamoto ya maji, Mateso yetu ya maji yamefikia kikomo", wamesema.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akiangalia Tanki la maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu leo Jumatano Septemba 14,2022. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akiwa amepanda kwenye ngazi za Tanki la maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima (kulia) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kuhusu ujenzi wa Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude kuhusu mahali panapotishwa bomba la maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza jambo katika eneo la Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Muonekano eneo la Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akiendelea kukagua Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akifungua maji kwenye moja ya vituo vya kuchotea maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi kwenye moja ya vituo vya kuchotea maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa wananchi kwenye moja ya vituo vya kuchotea maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akizungumza kwenye kituo cha kuchotea maji katika Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki unaotekelezwa na Mkandarasi Jonta Investment kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu.
Mkazi wa Bubiki Magdalena Stephano akizungumza wakati Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki.
Mkazi wa Bubiki Daudi Ndaki akizungumza wakati Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki.
Mkazi wa Bubiki Japhet Joseph akizungumza wakati Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude akitembelea Mradi wa maji ya bomba Mwamishoni - Nyasamba katika kata ya Bubiki.
Muonekano eneo la mradi wa maji Bupigi - Butungwa unaotekelezwa na Mkandarasi Bent Company Ltd kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu ambao ujenzi wake umefikia asilimia 85 na wananchi wameanza kupata huduma ya maji safi na salama.
Muonekano sehemu ya tanki la maji la mradi wa maji Bupigi - Butungwa unaotekelezwa na Mkandarasi Bent Company Ltd kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu ambao ujenzi wake umefikia asilimia 85 na wananchi wameanza kupata huduma ya maji safi na salama.


Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima (katikati) akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) kuhusu mradi wa maji Bupigi - Butungwa unaotekelezwa na Mkandarasi Bent Company Ltd kwa usimamizi wa RUWASA Kishapu ambao ujenzi wake umefikia asilimia 85 na wananchi wameanza kupata huduma ya maji safi na salama.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akihoji kwanini mradi wa maji Bupigi - Butungwa unaotekelezwa na Mkandarasi Bent Company Ltd unasua sua huku akimwagiza mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi haraka.
Mwakilishi wa Mkandarasi Bent Company Ltd, Riziki Masoud (kulia) akimuahidi Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) kukamilisha ujenzi mradi wa maji Bupigi - Butungwa ndani ya wiki mbili.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akizungumza katika mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akizungumza katika mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kulia) akikagua chemba katika kituo cha kuchotea maji cha kijiji cha Butungwa kwenye mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akikagua kituo cha kuchotea maji cha kijiji cha Butungwa kwenye mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akifungua maji katika kituo cha kuchotea maji cha kijiji cha Butungwa kwenye mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (katikati) akimtwisha ndoo ya maji mwanachi katika kituo cha kuchotea maji cha kijiji cha Butungwa kwenye mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude (kushoto) akizungumza katika kituo cha kuchotea maji cha kijiji cha Butungwa kwenye mradi wa maji Bupigi - Butungwa kata ya Bupigi.


Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger