Sunday, 11 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI SEPTEMBA 11,2022

















Share:

Saturday, 10 September 2022

WAZIRI MKENDA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA IRAN NA MKUU WA CHUO CHA KIMATAIFA CHA JAMIAT

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Na Mwandishi wetu , DODOMA 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (Mb)hivi karibuni amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania Alvandi Hossein pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Jamiat - Mustafa Al Alamiya cha nchini Iran Dkt Ali Abbasi.


Katika mazungumzo yao Waziri Mkenda na wageni hao kutoka Iran, wamekubaliana kuendeleza ushirikiano kwenye Taasisi za elimu ya Juu katika maswala ya Teknolojia, Sayansi, na Elimu ujuzi.


Aidha Waziri Mkenda amemwomba Balozi huyo kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kubadilishana utaalamu baina ya Vyuo Vikuu vya hapa nchini na Iran ili kuongeza wigo wa ujuzi kwa pande zote mbili.


Kadhalika, Waziri Mkenda amemueleza Balozi huyo wa Iran kuwa Tanzania inafanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na mabadiliko ya mitaala ili kuongeza ubora wa elimu na mafunzo.



Share:

SERIKALI KUTATHMINI UPYA MIPAKA YA MAPORI YA AKIBA YALIYOPANDISHWA HADHI



***********************

Serikali imejipanga kutathmini upya Mapori ya Akiba ya Luganzo-Tongwe, Igombe, Wembere, Inyonga na Ugalla ili kutatua changamoto ya muingiliano wa mipaka yenye hadhi tofauti na kupelekea baadhi ya maeneo ya Mamlaka za Serikali za Mitaa vikiwemo Vijiji na maeneo mengine kuingizwa ndani ya mapori hayo.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) alipokuwa akitoa tamko la Serikali katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.

“Hii ni mojawapo ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwamba tupunguze taharuki na migongano kati ya wananchi na maeneo ya hifadhi” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amesema mipaka mipya ya Pori la Akiba Igombe imepishana na kusababisha malalamiko kwa wananchi kwa kuwa kuna sehemu imemega maeneo ya vijiji ambayo yanatumika kwa ajili ya kilimo na makazi Serikali.

Kuhusu Pori la Akiba Luganzo Tongwe Mhe. Masanja amefafanua kuwa mipaka yake imechukua maeneo mengine ya ziada yakiwemo Hifadhi ya Msitu wa Mpanda line, Hifadhi ya Msitu wa Tongwe West, Sehemu ya Hifadhi ya Msitu wa Masito, Eneo la Makazi ya Wakimbizi la Mishamo, sehemu ya maeneo ya vijiji katika kata ya Mishamo (Kijiji cha Kapemba), na vijiji vya Nguruka, Malagarasi na Itebula.

Ili kutatua changamoto hiyo Serikali imeamua kuanzisha upya mchakato wa uanzishwaji wa Pori la Akiba Luganzo – Tongwe kwa kushirikisha Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi, Mamlaka za Serikali za Mitaa (Tabora, Katavi na Kigoma), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Aidha, katika Pori la Akiba Ugalla Serikali imeamua kuondolewa kwa Hifadhi ya Msitu wa Walla River kwenye mipaka ya Pori la Akiba Ugalla na kwamba utaendelea kusimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya Sikonge.

Pia, amesema Pori la Akiba Wembere Serikali itatuma wataalam kutoka Wizara za Ardhi, Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuandaa ramani ya Pori la Akiba Wembere lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,385.81 litakalotanda kwenye eneo la Bonde la Ardhi Oevu la Wembere kwenye wilaya za Igunga, Uyui, Sikonge na Manyoni kwenye mikoa ya Tabora na Singida kama ilivyokusudiwa tangu awali na kutamkwa kwenye Tangazo la Serikali. Na. 456 la tarehe 25/06/2021.

Mhe. Masanja ametoa rai kwa wananchi kuheshimu maeneo yatakayoainishwa kwa ajili ya uhifadhi na pia amewataka wawe wadau wa uhifadhi kwani wao ni wanufaika wakuu kwa kuwa uhifadhi unasaidia kutunza vyanzo vya maji, mazingira na kuondoa ukataji wa miti .



Share:

WAHITIMU TaSUBa WATAKIWA KUTUMIA ELIMU YAO KUSAIDIA JAMII



Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wasabato Mchungaji Jeremiah Izungu akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato kwenye Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa yaliyofanyika leo Septemba 10,2022 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wasabato Mchungaji Jeremiah Izungu akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato kwenye Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa yaliyofanyika leo Septemba 10,2022 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wasabato Mchungaji Jeremiah Izungu akikabidhi vyeti kwa wahitimu wa Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato kwenye Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa yaliyofanyika leo Septemba 10,2022 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wasabato Mchungaji Jeremiah Izungu akizungumza katika Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato ambayo yamefanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).Mkufunzi Idara ya Muziki TaSUBa, Bw.Heri Kaare akizungumza katika Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato ambayo yamefanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).Mwanafunzi wa Mwaka wa tatu Bi.Aksa Nhyenje akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato leo Septemba 10,2022 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). Kwaya mbalimbali zikitumbuiza Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato leo Septemba 10,2022 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

*************

NA EMMANUEL MBATILO, BAGAMOYO

WAHITIMU wa Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wasabato wametakiwa kuyaishi yale yote ambayo wamefundishwa na kuwafundisha wengine ili iwe baraka kwa watanzania na watu wote.

Wito huo umetolewa leo Septemba 10,2022 na Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kusini mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wasabato Mchungaji Jeremiah Izungu wakati wa Mahafali ya Tisa ya Mafunzo ya Muziki TaSUBa ambayo yanaendeshwa na Jimbo Kuu la Kusini Mashariki mwa Tanzania la Kanisa la Waadventista wa Sabato ambayo yamefanyika katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

Amesema imekuwa ni muhimu kwa vijana kupata mafunzo hayo kwasababu kumtumikia mungu kunatakiwa akili, maarifa na roho ndo maana wameamua kupeleka kozi eneo hilo ambayo inasaidia waimbaji wao kumuimbia mungu kwa maana ya kumtukuza kwasababu ni wajibu kufanya hivyo.

"Nyimbo ni ibada lakini pia namna ya kufanya amani katika mioyo ya watu ni hubiri ni mafundisho ambayo ni muhimu sana kwa watanzania kwa ujumla na hapa ujumbe ambao nimeuleta nikuwataka washiriki wa kanisa na watanzania kupenda nyimbo za ibada". Amesema Mchungaji Izungu.

Aidha amewataka watanzania kuwa na umuhimu wa kupenda maandiko matakatifu na kuyasoma, kuyasikia, kuyaishi na kuyafundisha kama nyenzo ya kufanya amani idumu kuwepo ulimwenguni kote.

Nae Mkufunzi Idara ya Muziki TaSUBa, Bw.Heri Kaare amesema wamekuwa na programu za muda mfupi kwa kanisa la waadventista wasabato ambapo ili mtu aonekane amehitimu haya mafunzo anapaswa kuja awamu tatu, kwahiyo wapo walikuja kwa awamu ya kwanza, ya pili na yatatu.

Amesema tangu waanze mpaka sasa mabadiliko ni makubwa, wengi wanafika wakiwa hawajui chochote kuhusu muziki lakini wanaondoka wanaweza kusoma muziki kwenye karatasi ama kwenye vitabu pamoja na kupiga ara za muziki.

"Watu wote ambao wanatamani kuja kujifunza muziki waje, muziki ni taalumu kwa maana lazima uingie darasani uweze kunolewa". Amesema

Share:

YANGA SC YAANZA VIZURI KLABU BINGWA, YAICHAKAZA ZOLAN FC MABAO 4-0

TIMU ya Yanga SC imeanza vyema katika kampeni za kuwania kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa baada ya kuwachapa mabao 4-0 wenyeji Zalan FC kutoka nchini Sudan Kusini mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walipata mabao ya yote manne kipindi cha pili mara baada ya kipindi cha kwanza timu zote kwenda mapumziko bila kufungana.

Mshambuliaji hatari kwa sasa Fiston Mayele amefunga hat-trick akifunga dakika 45,85 na 88 huku bao moja likifungwa na Fei Toto dakika ya 55

Yanga watarudiana na Zalan FC Septemba 16,2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa wakiwa kama wenyeji
Share:

WALIOWACHAPA VIBOKO WAKULIMA USIMBE WAKAMATWA



_Na.Abel Paul wa Jeshi la Polisi,kibiti Pwani_

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama vimefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa saba wa matukio ya uchochezi wa migogoro baina ya wakulima na wafugaji katika kitongoji cha Usimbe kata ya Maparoni  tarafa ya Mbwera Wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani iliyotokea Agosti 30 mwaka huu.

Akitoa taarifa hiyo leo Septemba 10 2022 alipofika katika Kata ya Maparoni wilaya ya kibiti kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo Nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa saba wa waliohusika katika tukio la kuwapiga wananchi wa Usimbe Kata ya Maparoni wilaya ya Kibiti mkoa wa Pwani.

Pasua amesema watuhumiwa hao bado wanashikiliwa na Jeshi hilo huku akisema kuwa majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi na kubainisha kuwa wamehojiwa na kukiri kufanya matukio hayo kama iliyoonekana katika video iliyosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Kamanda Pasua ameeleza kuwa  watuhumiwa wote watafikishiwa katika vyombo vya sheria pindi upelelezi utakapokamilika kujibu tuhuma zinazowakabili.

Sambamba na hilo ACP Pasua amewaeleza waandishi wahabari kuwa Jeshi la Polisi linawataka wale wote waliohusika katika tukio hilo baya  wajisalimishe katika vituo vyao Polisi kabla wajakumbana na mkono wa dola.

Hata hivyo ameongeza  kuwa kuna taarifa za baadhi ya wafugaji wanaohamisha mifugo kutoka eneo moja kwenda eneo jingine kwa lengo la kutafuta malisho ambapo amesema vitendo hivyo vimekuwa chanzo cha migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mengi hapa nchini ambapo amewataka kufuata matumizi bora ya ardhi.
 
Naye diwani wa kata Maparoni katika wilaya ya Kibiti ameliomba Jeshi la Polisi hususani kikosi kinachoshughulika na migogoro ya wakulima na wafugaji kuongeza kasi ya kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio hilo.

Abel Paul
Afisa habari wa Jeshi la Polisi 
0759783894

Share:

Friday, 9 September 2022

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPTEMBA 10,2022











Share:

RC KAGERA AVITAKA VYOMBO VYA DOLA KUCHUNGUZA KITUO CHA FORODHA MUTUKULA

 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila 

Na Mbuke Shilagi Kagera.


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Albert Chalamila ameagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa watumishi katika kituo cha Forodha cha Mutukula mpaka wa nchi ya Tanzania na Uganda kutokana na kubainika kwa baadhi ya Watumishi wasio waadilifu kushirikiana na raia kughushi nyaraka na kupelekea Serikali kupoteza mapato.


Akizungumza na Watumishi wa Idara zilizopo katika kituo hicho, Mhe. Chalamila ameeleza kuwa iliundwa kamati ya kuchunguza mwenendo wa usafirishaji wa mazao kutoka Tanzania kwenda nchi ya Uganda na kubaini kuwepo kwa baadhi ya watumishi wasio waadilifu, iligundulika baadhi ya watu kuwa na nyaraka feki ambazo zinatumika kugongwa mihuri kwa kushirikiana na maafisa wa kituo hicho cha forodha na wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.


“Kama mmeona taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera siku chache zilizopita kuna baadhi ya watu ambao waligundulika kuwa na nyaraka feki ambazo zinatumika kugongwa mihuri kwa kushirikiana na maafisa wa kituo hiki cha forodha hivyo Serikali kupoteza mapato,” ameeleza Mhe. Chalamila.


Mkuu wa Mkoa amezitaka Mamlaka za watumishi hao kuchukua hatua za haraka za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kuwahamisha katika kituo hicho cha forodha.


Ameeleza kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera alimtaja mtuhumiwa mmoja ambaye si Mtanzania kumiliki mihuri mitatu ya bandia ambapo vyombo vya dola vinaendelea kumfanyia upekuzi na ambaye imebainika kushirikiana na watumishi wa kituo hicho. 


"Mtuhumiwa huyo alikiri kumiliki mihuri bandia ukiwemo mhuri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania aliokuwa anautumia kugonga nyaraka za kuvusha mazao aina ya maharage kutoka Tanzania kwenda Uganda nyaraka ambayo ilikamatwa na Afisa wa Mionzi, afisa huyo baada ya kukamata nyaraka hiyo alimpelekea Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania ili kufahamu kwanini Afisa huyo aligonga mhuri huo ili kuruhusu gari kuingia nchini Uganda bila utaratibu wa mihuri mingineyo kama mhuri wa mazao kutogongwa",ameeleza.


"Baada ya kukagua nyaraka hiyo Afisa wa TRA aligundua mhuri uliotumika ni bandia hivyo kumtaka mtuhumiwa huyo kutoa rushwa ili gari iendelee na safari ya kwenda Uganda. Watumishi hao walifanya kazi nzuri, kubaini nyaraka ya kughushi lakini wakaishia kumuomba rushwa mtuhumiwa",amesema.


Pamoja na hao pia wapo mawakala wa fedha ambao wahusika huwatumia kutuma fedha kwa watumishi wa kituo hicho na baadhi ya mawakala wamekiri kufanya vitendo hivyo.


Kufuatia  hali amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa kuchunguza watumishi wa kituo hicho kwa kushirikiana na mawakala hao ili kuona katika mitandao na kubaini mawasiliano yanayofanyika.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Ndg. Toba Nguvila ameeleza kuwa ziara ya kwanza ya Mkuu wa Mkoa alitembelea mpaka wa Mtukula na kuzungumza na watumishi.


 Katika mazungumzo hayo Mkuu wa Mkoa alitoa maelekezo mengi juu ya uadilifu na nidhamu ya Watumishi katika kusimamia shughuli mbalimbali za kibiashara kati ya nchi na nchi. Na msisitizo mkubwa uliwekwa juu ya kumsaidia Rais Samia kwa vitendo kwa kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali na kusimamia kanuni na taratibu zinazoendesha kituo cha forodha zinazingatiwa.



Share:

MWILI WA MALKIA ELIZABETH II KUAGWA SIKU NNE


Malkia Elizabeth II.

MWILI wa Malkia Elizabeth II utasafirishwa kutoka Kasri la Buckingham kwa msafara utakaokuwa ukiendeshwa polepole wakiambatana na gwaride la kijeshi la familia ya Kifalme.


Baada ya jeneza lake kurudi mjini London, utalazwa katika ukumbi wa Westminister siku nne kabla ya mazishi yake ili kuruhusu raia wa Uingereza kuutazama mwili wake na kuuaga.

Picha za mwili wa mamaake Malkia ukiwa amelazwa.

Ukumbi huo ndio wa zamani zaidi ikilinganishwa na kumbi nyingine Westminister, katikati ya serikali ya Uingereza. Mtu wa mwisho wa familia ya Ufalme huo kuwekwa katika hali hiyo alikuwa mamake Malkia mwaka 2002, wakati zaidi ya watu 200,000 walipopanga foleni kutazama jeneza lake.


Jeneza la Malkia litawekwa katika eneo la juu, linalojulikana kama Catafalque, chini ya dari lililojengwa na mbao. Kila kona ya eneo hilo litalindwa na wanajeshi kutoka vitengo vyake ambao wanahudumia familia ya Kifalme.

Watu wataweza kuutazama msafara huo wakati utakapokuwa ukipita barabarani huku skrini kubwa zikionesha matukio hayo ambazo zinatarajiwa kuwekwa katika bustani za kifalme. Jeneza lake litafunikwa kifalme na litakapowasili Westminister litawekewa taji la Kifalme orb na fimbo.

Picha zinazoonesha kile kitakachokuwa juu ya jeneza la Malkia. Bendera, taji na fimbo ya kifalme

Share:

TBS MWANZA YATEKETEZA TANI TATU YA BIDHAA ZENYE VIAMBATA SUMU NA ZILIZOISHA MUDA WAKE


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limefanikiwa kukamata na kuteketeza shehena ya vipodozi na chakula zaidi ya tani tatu zenye viambata sumu na zilizoisha muda wa matumizi ambazo zilikamatwa kupitia ukaguzi maalumu uliofanyika katika maduka mbalimbali Kanda ya Ziwa.

Akizungumza Ijumaa Septemba 09, 2022 wakati wa zoezi la kuteketeza shehena hiyo lililofanyika katika dampo la Buhongwa jijini Mwanza, Afisa udhibiti ubora TBS Kanda ya Ziwa Arnold Kubingwa amesema hatua hiyo inalenga kuondoa sokoni bidhaa zote zenye zisizofaa kwa matumizi kwani zina madhara kwa watumiaji.

Kubingwa ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wafanyabiashara kuhakikisha bidhaa wanazoziagiza na kuziuza zinakidhi matakwa ya viwango ikiwemo kuangalia tarehe ya uzalishaji na mwisho wa matumizi.

Amesema TBS itaendelea kutoa elimu kwa jamii kutambua bidhaa zilizopigwa marufuku sokoni na kuwa na utamaduni wa kukagua bidhaa kabla ya matumizi na kwamba wafanyabiashara wanapaswa kuwa waaminifu kwa kuteketeza bidhaa zisizofaa.

“Wafanyabiashara wanapaswa kufuata matakwa ya Sheria katika utunzaji wa bidhaa zinazopaswa kuwa sokoni, uhifadhi wake wake katika maghala na uteketezaji wa bidhaa ambazo hazifai kuwa sokoni, wakishindwa kufanya hivyo tutaendelea kuziondoa na kuchukua hatua dhidi yao” amesema Kubingwa.

Naye Afisa usalama wa chakula TBS Kanda ya Ziwa, Elikaneny Minja amesema bidhaa za chakula zilizoisha muda wa matumizi na ambazo zina viambata sumu ni hatari kwa afya ambapo zinaweza kusababisha maradhi ya ngozi ikiwemo kansa kwa watumiaji na kwamba madhara hayo yanaweza kuhamia kwa watoto walio tumboni ikiwa mtumiaji ni mjamzito.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa jamii kuzitambua bidhaa zilizopigwa marufuku na zenye viambata sumu, pia tumeziweka kwenye tovuti ya TBS ili wananchi wazitambue na kujiepusha na matumizi yake” amesema Minja na kuongeza kuwa TBS inashirikiana na maafisa afya na biashara katika ngazi za Halmashauri ili kufanya ukaguzi na kuondoa sokoni bidhaa zisizofaa.

Nao baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza akiwemo Happyness Enock pamoja na Amos Makinga wameipongeza TBS kwa jitihada za kuondoa sokoni bidhaa zilizoisha muda wa matumizi na zenye viambata sumu na kuongeza kuwa ni vyema wafanyabishara wanaokamatwa wakiuza bidhaa hizo wakachukuliwa hatua kali za kisheria.

Share:

MPANGO WA NYP+ WAZINDULIWA KUKABILIANA NA VVU

 
Naibu katibu Mkuu,Ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na Bunge Kasper Mmuya akizungumza kwenye uzinduzi wa NYP+

Na Dotto Kwilasa,DODOMA.

NAIBU katibu Mkuu,Ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu na Bunge Kasper Mmuya ameitaka tume ya kudhibiti ukimwi nchini TACAIDS  kuja na mifumo mizuri ya ugawaji kondomu ili kudhibiti changamoto ya uhaba wa kondomu nchini unaotokana na baadhi ya watu wachache kuzichukua kwa wingi na kuzitumia isivyo sahihi.

Mmuya amesema  hayo  Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa mtandao wa vijana wanaoishi na VVU nchini (NYP+)  ambapo amesema hakuna sababu ya kuwepo uhaba huo kutokana na kuwa kondomu zinazoingia nchini ni nyingi na zinazoweza kukidhi mahitaji yaliyopo.

Amesema katika juhudi za kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi vijana wanatajwa kuwa kundi muhimu kufikiwa , kutokana na kundi hili kuwa kundi  linaloongoza katika kupata maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

"Katika kuendelea mapambano lazima juhudi zifanyike kulifikua kundi hili, kupitia mpango mkakati wa mtandao wa vijana wanaoishi na VVU nchini NYP+, lazima  changamoto ziishe na kuanzisha mafanikio ambayo yameshafikiwa  katika kukabiliana na  maambukizi ya VVU na Ukimwi,"amesema

Katika hatua nyingine amewataka vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi(VVU)nchini kuendeleza mapambano dhidi ya Virusi hivyo  ili kuondokana na maambukizi mapya yatakayoweza kukatisha ndoto zao.

Amesema pamoja na mafanikio yaliyopo ni vyema kuongeza jitihada katika kuhamasisha upimaji wa VVU ili  kufikia malengo ya Kitaifa ya 95 kwa mwaka  2025 na ifikapo mwaka 2030 iwe imefikia sifuri (0 ).

“Nitoe wito kwa wadau wote wanaotekeleza afua za mwitikio wa UKIMWI kufanya tathimini ya mwelekeo wa utekelezaji katika kufikia malengo  ili palipo na changamoto tuweze kurekebisha na kuimarisha na penye mafanikio tuongeze nguvu na Mipango yetu ya kimkakati ionyeshe wazi jinsi tutakavyofikia Tanzania isiyo na UKIMWI ifikapo mwaka 2030,”amesema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Amesisitiza kuwa kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ambao ni waratibu wa shughuli za UKIMWI ndani ya mikoa wawe chachu ya utekelezaji wa maelekezo hayo ndani ya mikoa yao.
 
“Niwasisitize watumishi wa Serikali kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa mkasimamie na kuratibu vyema Halmashauri zote kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) tuweze kutimiza vyema azma yetu,”amesisitiza.

Aidha amesisitiza  Uhamasishaji Kwa wanaume kuhakikisha wanatumia huduma za VVU na upimaji kwa ajili ya kufikia 95 ya kwanza pamoja na kufuatilia vijana wakike watumie  huduma za VVU ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Pudensia Mbwiliza, Mwenyekiti wa NYP+ amesema asilimia arobaini ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi nchini yanatajwa kuwakabili vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 28 huku wasichana wakiwa ni asilimia themanini ya kundi hilo na kusisitiza kuwa wako tayari kuendelea kushirikiana na serikali kulifikia kundi la vijana na kuliwezesha kukabiliana na maambukizi ya vvu.
Share:

AJIUA KISA KANYIMWA TENDO LA NDOA NA MKEWE


Polisi katika kijiji cha Ebungaya, kaunti ya Kakamega wanachunguza kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 50, anadaiwa kukatiza maisha yake baada ya mzozo wa kinyumbani mnamo Jumatatu, Septemba 5,2022.

Mwili wa Ezra Skim ulipatikana ukininginia kwenye mti ukiwa na kamba shingoni mnamo Jumanne, Septemba 6,2022. 

Marehemu anaripotiwa kutoweka nyumbani kwake mnamo Jumatatu, Septemba 5, kabla ya mwili wake kupatikana na wapita njia.

 Akithibitisha kisa hicho, Afisa Mkuu wa Polisi wa Khayega, Elizabeth Kagehi aliomba kutafuta njia bora ya kusuluhisha migogoro yao badala ya kujitoa uhai.

Akizungumza na waandishi wa habari, dada yake marehemu Jetina Tegeno alisema kaka yake amekuwa akilalamikia kudhulumiwa katika ndoa kabla ya kifo chake. 

Alisema mke wake marehemu amekuwa akimtesa kaka yake na kumyima haki zake za ndoa kila mara.

 "Katika siku zake za mwisho, yeye (Skim) alionekana kuwa na msongo wa mawazo. Amekuwa akimtuhumu mke wake kwa kumdhulumu," Tegeno alisema.

 Akisimulia matukio hayo, mke wake mwendazake Maximila Anyika, alisema walikuwa wamelala wakati Skim kutoka nje ya nyumba bila kurejea.

 "Ghafla alitoka kitandani tulipokuwa tumelala, bila maelezo alitoka nje na kugonga mlango nyuma yake. Tulishtuka kukuta mwili wake ukining'inia kwenye mti," Anyika alisimulia. 

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Mukumu ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger