Monday, 29 August 2022
Sunday, 28 August 2022
TAIFA STARS ILIVYOJIANDAA KUIVURUGA UGANDA JIONI HII

KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Uganda utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es salaam.
Mchezo huo wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN), unatarajiwa kuanza saa 10:00 jioni.
Akizungumza na Spoti Xtra, Poulsen alisema wanatambua Uganda ni moja ya timu ngumu inayohitaji umakini kwenye kupambana nao.
“Uganda tunawatambua hasa kwa namna ambavyo wanatumia nguvu kutafuta ushindi, utakuwa ni mchezo ambao unahitaji nguvu na akili kubwa kwenye kutafuta ushindi ila tupo tayari, muunganiko unazidi kuwa imara.
“Kiakili na mbinu tumejipanga ukizingatia wachezaji wametoka kucheza mechi za ligi, hiyo inaongeza uimara, mchezo huu wa Uganda ni wa kwanza na mchezo wa pili ugenini utatupa picha ya sisi kufuzu CHAN ukichanganya na nguvu ya mashabiki basi kutakuwa na kitu cha kipekee,” alisema Poulsen.
Aishi Manula, Nahodha Msaidizi wa Taifa Stars, alisema: “Wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda, ambacho tunahitaji ni kufuzu CHAN, benchi la ufundi limefanya kazi kubwa na tunawatambua Uganda na wao wanatujua pia.”
Video Mpya : NYASANI - SENSA
Msanii Maarufu Nyasani kutoka Shinyanga ameachia video mpya ya wimbo wa Sensa. Audio producer ni Sheddy the Mix, Paradox Empire Records, Video grapher📸 Davy Skerah, CM Production.
JAMAA AUA CHUI KWA MIKONO

Chui
NDUMISO MONA; ni mwanaume mwamba kabisa wa nchini Afrika Kusini ambaye kwa sasa ni gumzo nchini humo baada ya kupambana na chui na kumuua kwa mikono yake mwenyewe.
Ndumiso alipambana na chui anayedaiwa kutoroka kutoka Hifadhi ya Kitaifa ya Kruger (KNP) huko Afrika Kusini.
Akiwa amesimama kwenye mwinuko wa nyumba yake katika Kijiji cha Matsulu Manispaa ya Mbombela huko Mpumalanga, Ndumiso aliyevalia ovaroli, soksi za kijivu na viatu alisimulia masahibu yake yaliyotokea asubuhi ya Julai 21, mwaka huu.
Ndumiso anasema; “Nilikuwa nikibarizi nje ya duka moja na marafiki zangu tuliposikia kuhusu chui anayezurura karibu na nyumba yangu.
“Akili yangu iliniambia nikimbilie nyumbani. Nilikuwa na wasiwasi na wadogo zangu wawili ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi.
“Nilikimbia na kupita nyumbani kwangu nilipomuona chui. Niligeuka na kushangaa akiunguruma nyuma ya mgongo wangu.
“Tulitazamana machoni. Sote tulisimama kwa takriban dakika mbili tukitazamana.
“Moyo wangu ulikuwa ukipiga sana. Nilimuona akifungua kinywa chake, nikaona meno makali. Alikuwa tayari kuruka. Nilikunja ngumi. Hakukuwa na kurudi nyuma.
“Nilijiambia kwamba mmoja kati yetu lazima afe.”
Ndumiso anasema kuwa, dakika 2 baadaye chui huyo alimrukia, wakaanza kupigana hadi chui akafa.”
Cc; @sifaelpaul
MAMA AFUNGIWA CHUMBANI NA MWANAE AKIDAIWA ELFU 7 NA MWENYE NYUMBA SHINYANGA MJINI
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi Adam akizungumza na Mariam Hamis kupitia dirishani akiwa amefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela
Kulia ni Mariam Hamis akizungumza kupitia dirishani akiwa amefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela
Mlango wa chumba cha Mariam Hamis ukiwa umefungwa na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela huku yeye akiwa ndani
Zoezi la kuvunja kufuli kwenye Mlango wa chumba cha Mariam Hamis uliofungwa na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela likiendelea
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi Adam akifungua mlango wa Mariam Hamis aliyefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga Abdi (kushoto) akizungumza na Mariam Hamis aliyefungiwa kwenye chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanamke aitwaye Mariam Hamis mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga amefungiwa ndani ya chumba chake na mwenye nyumba aitwaye Evodia Charles Mahela takribani saa 10 hadi serikali ya mtaa ilipofika kuvunja mlango kutokana na kile kilichoelezwa kuwa anadaiwa shilingi Elfu saba na mia nne (7400) ya bili ya maji.
Mariam Hamis amefanyiwa ukatili wa kufungiwa ndani ya chumba chake tangu jana Jumamosi majira ya saa tano usiku mpaka leo asubuhi saa tatu asubuhi wajumbe wa serikali ya mtaa wa Mabambasi walipopata taarifa kuhusu tukio hilo na kufika nyumbani kwake na kulazimika kuvunja kufuli lililofungwa na mwenye nyumba aliyopanga aliyejulikana kwa jina la Evodia Charles Mahela.
Wajumbe wa Serikali ya Mtaa wa Mabambasi wakiongozwa na Abdi Adam wamesema wamelazimika kuvunja kufuli hilo kutokana na kwamba kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Akielezea kuhusu kisa hicho, Mariam amesema ameshangaa kuona mama mwenye nyumba anafunga chumba hicho kwa madai kwamba hajalipa bili ya maji shilingi 7,400/=.
“Wapangaji tupo wanne,kila mpangaji anadaiwa shilingi 7400, mmoja amelipa bili ya maji, watatu hatujalipa bili ya maji lakini nashangaa mimi nimefungiwa nyumba. Humu ndani naishi na mtoto wangu mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu. Kanifungia mlango kwa kufuli tangu jana saa tano usiku, hiki chumba hakina choo ndani”,ameeleza Mariam.
Malunde 1 blog imemtafuta Evodia Charles Mahela ambaye kwa kujiamini amesema amemfungia mpangaji wake kutokana na kwamba alitaka kutoroka na pesa.
“Alikuwa anataka kutoroka na pesa,nikawaambia wafunge mpaka nitakapokuja,nikampigia simu huo usiku nikamwambia akitaka kuondoka atoe pesa au aache kitu maana wamekuwa na tabia ya kuondoka bila kulipa halafu mimi nabaki na madeni,sasa namwambia anaanza kunijibu vibaya na alikuwa anatoroka anatoroka na deni sasa mimi nitakuwa wa kulipa madeni ya watu..na geti jana usiku alilifunga funguo akakaa nazo yeye kwamba usiku huo atoroke.
“Nimeomba kufuli kwa mmoja wa wapangaji nikafunga nikawaambia asubuhi nichukue kitu chochote atoe hela, wameshahama wawili na hela na kwanini atoroke? Kwani asiage?”,amesema
Saturday, 27 August 2022
WAMILIKI WA MAKAMPUNI MAKUBWA DUNIANI WAJA KUWEKEZA NCHINI

***********************
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Leo Agosti 27,2022 kimekutana na Wafanyabiashara wa Marekani ambao ni jamii ya watu wa China kwenye kongamano kubwa la Kibiashara na Uwekezaji ambalo limefanyika katika hoteli ya Serena, Jijini Dar es Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kongamano hilo Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda ambaye amemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia wafanyabiashara hao kawa Tanzania ni mahali salama pa kuja kuwekeza na wamewaandalia mazingira mazuri.
“Ni watu kutoka Marekeni ambao ni jamii ya watu wenye asili ya China na tumejaribu kuwaonyesha kuwa fursa ziko nyingi” - Mhe. Mizengo Pinda
“Yapo mambo ya msingi kwa mwekezaji yoyote ya kutaka kuja kuwekeza kwenye nchi yeyote ile, moja ni Amani na Utulivu ambapo kwa Tanzania tunamshukuru Mungu jitihads zimefanyika kwa krasi kikubwa na utuliva upo mpaka sasa”- Mhe. Mizengo Pinda
Kwa upande mwingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini ( TIC ) Ndg. John Mathew Mnali amesema kuwa wafanyabiashara hao wenye Makampuni Makubwa wamekuja kuwekeza kwenye sekta ya Utalii kwa kujenga hoteli za kitalii zenye hadhi ya nyota tano pamoja na kumbi kubwa za mikutano ya kimataifa na pia kuwekeza kwenye utengenezaji wa Madawa ya Binadamu.


BABU WA MIAKA 92 AFAULU MTIHANI DARASA LA TANO KWA ALAMA ZA JUU ZAIDI
Mwanamume mkongwe wa miaka 92 anayeaminika kuwa mwanafunzi mzee zaidi nchini Uingereza kufanya mtihani wa GCSE amefaulu mtihani wake wa somo la hesabu darasa la tano – kwa alama ya juu zaidi.
Derek Skipper, kutoka Orwell huko Cambridgeshire, alifanya mtihani baada ya kusoma kupitia Zoom.
Mara ya mwisho alifanya mtihani wa hesabu mwaka wa 1946 alipotumia mfumo wa slaidi, lakini wakati huu alikuwa na kikokotoo na miwani ya kumwezesha kuona vizuri zaidi kwa sababu ya matatizo ya macho.
Alisema alifurahishwa na kupita mtihani huo.
Chanzo - BBC Swahili
FULL POWER NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya tendo la ndoa kikamilifu ,shughuli ya tendo la ndoa huhusisha akili, homoni, neva, misuli, hisia na mirija ya damu. Upungufu wa nguvu za kiume huashiria kutokuwa sawa kiafya hivyo ni tatizo linalohitaji tiba.
Tatizo la nguvu za kiume lina vyanzo vingi ambavyo mara nyingi wengi huvipuuza, hivyo vyanzo huathiri taratibu na vingine huathiri haraka, tunashauri watu kuwa makini sana ili kujiimarisha vizuri. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata tatizo la nguvu za kiume nayo ni pamoja na;
1. Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P) au ugonjwa wa moyo
2. Kuvuta sigala na unywaji wa pombe
3. Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
4. Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
5. Kisukari
6. Kuwa na mawazo na wasiwasi
7. Matumizi ya madawa mbalimbali
8. Umri hasa wazee
9. Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
10. Kuwa na tatizo la kibofu
11. Tabia za kujichua kwa muda mrefu
12. Kutopata usingizi kamili
13. Matumizi makubwa ya dawa zenye kemikali za kutibia magonjwa kama kansa, vidonda vya tumbo, moyo, kisukari, B.P, na magonjwa mengine
DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Dalili za kuonesha kuwa una tatizo la upungufu wa nguvu za kiume karibia zote zinahusiana na hali itakayo onekana katika tendo la ndoa au mda wa kujamiiana, hizo dalili zake ni kama;
1. Kuwahi kufika kileleni
2. Kukosa hamu ya mapenzi
3. Kushindwa kurudia tendo la ndoa
4. Uume kusimama kwa ulegevu au kushindwa kusimamisha
5. Kuchoka sana baada ya tendo la ndoa na hata kukinai kabisa au hata kusikia kichefuchefu; Miguu, uso na tumbo kuvimba na kujaa maji
6. Kuhisi maumivu wakati wa tendo la ndoa au baada ya tendo hilo
7. Kuchelewa sana kufika kileleni (au kushindwa kufika kileleni kabisa)
8. Kukosa pumzi na uchangamfu wa mwili katika utendaji
TIBA SAHIHI YA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME
FULL POWER
⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.
⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa
⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.
ZAT 50
⇨ Inarutubisha maumbile ya uume na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4
⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.
Pia tunatibu Magonjwa mengine kama
Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonda vya tumbo, Kisukari, Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kung’oa
Ndugu mteja Epuka midawa inayouzwa mitaani ambayo sio sahihi kwa matumizi ya binadamu JALI AFYA YAKO OKOA NDOA NA MAISHA YAKO
Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga
Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27 au 0754568767 utatumiwa sehemu yoyote ulipo
AFARIKI KWA MOTO WA SIGARA BAADA YA KUBUGIA POMBE KUPITA KIASI
Mwanamume mmoja ameungua moto hadi kuaga dunia nyumbani kwake katika Kaunti ya Busia nchini Kenya baada ya kurejea akiwa mlevi.
Moto unasemekana kuanza baada ya mwanaume huyo kwa jina George Otieno kuwasha sigara kisha kushikwa na usingizi.
Moto huo ulisambaa katika nyumbani lakini Otieno alikuwa bado mlevi na alishindwa kuutoroka wakati alipogutuka usingizini.
Monicah Oteno, mama wa mwanaume huyo aliyekuwa mfugaji, amebaki na machungu kwa kumpoteza mwanawe aliyekuwa na umri wa miaka 33.
MWALIMU MKUU AFARIKI AKIAMUA UGOMVI WA JIRANI YAKE

Mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni Moi Buruma
**
MWALIMU Mkuu wa Shule Ya Msingi Taisi iliyopo kata ya Burmea mkoani Mara, Ibrahimu Maryoba ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu wakati akienda kuamua ugomvi wa jirani yake.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni, Moi Buruma aliyesema kuwa mwalimu huyo mauti yalimukuta wakati akiwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Nyairoma alipokwenda kuamulia ugomvi wa jirani yake Juma pamoja na mkewe baada ya kusikia kelele za kuomba msaada zilizopigwa na mke wa bwana huyo.
Mwalimu huyo baada ya kutoka nje alianguka na kupoteza fahamu ambapo wasamaria wema walifika na kumpeleka Kituo cha Afya cha Sirari, lakini alifariki dunia akiwa bado anapatiwa huduma.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarikikya amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambacho kilitokana na shinikizo la damu kulingana na maalezo ya daktari wa hospitali alipofia marehemu pia amewataka wananchi kuwa watulivu na kuacha kueneza habari zisizo nauhakika.

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Tarime Rorya ACP Geofrey Sarikikya
“Tunaendelea na uchunguzi zaidi na tunawaomba wananchi kuwa watulivu na kuacha kueneza mambo yasiyo na uhakika na badala yake wafuate mambo ya kitaalamu kama ilvyoelezwa na daktari kwamba marehemu amefariki kutokana na shinikizo la damu” alisema kamanda huyo.
Mwili wa marehemu ulipelekwa hospitali ya wilaya ya Tarime kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na ulirejeshwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Nyairoma kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Imeandikwa na: Oswald Mwesiga wa msaada wa mitandao.
HUYU NDIYE RUBANI MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI ALIYEVUNJA REKODI

Mack Rutherford
MACK Rutherford mwenye umri wa miaka 17 raia wa Uingereza aliyekulia nchini Ubelgiji ameweka rekodi ya kuwa rubani mwenye umri mdogo zaidi kuendesha ndege ndogo pekeyake.
Awali rekodi hii ilikuwa ikishikiliwa na rubani Muingereza Travis Ludlow ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 na siku 150 alipoanza safari yake mwaka 2021.

Mack Rutherford raia wa Uingereza
Katika safari yake ya miezi mitano akizunguka nchi takribani 52 Mack Rutherford alitua katika mji wa Sofia huko nchini Bulgaria.
Mack anaeleza kuwa kipindi cha safari yake alikumbana na dhoruba za mchanga huko Sudan na kulala usiku kucha kwenye kisiwa cha Pasifiki kisichokaliwa na watu.

Mack Rutherford ana umri wa miaka 17
Hata hivyo dada yake mkubwa Zara anashikiria rekodi kuwa mwanamke mdogo zaidi kuendesha ndege peke yake duniani kote.
Imeandaliwa na Simon Molanga kwa msaada wa mtandao.









































