Friday, 8 April 2022

WATU WENYE ULEMAVU NA WAZEE WA MSALALA WAKABIDHIWA KADI ZA BIMA ZA MATIBABU NA VIFAA VYA USAIDIZI KUTOKA BARRICK


Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi baiskeli Salome Samwel. 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu, wamekabidhiwa vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kutoka kampuni ya Barrick, ili kuwaongezea furaha na kuwawezesha kushiriki shughuli za kiuchumi.

Vifaa hivyo vimekabidhiwa Aprili 7,2022 na Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul, wakati wa hafla fupi iliyohudhuriwa na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Msalala wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Mhe. Charles Fussi.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni Baiskeli 30 za kawaida na zile za kusaidia kutembea kwa watu wenye ulemavu, vifaa vya kusikia 5, fimbo nyeupe 6, vyerehani vya kushonea ngozi 2, vyerehani vya kawaida 8 na vya Overlock 2, samani na seti ya Televisheni kwa ajili ya Kituo cha afya Bugarama na pikipiki moja itakayotumika katika ofisi ya Dawati la Jinsia kusaidia kuwezesha kushughulikia masuala ya wasichana na Wanawake.

“Vifaa hivi tulivyokabidhi vina thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 40 zikiwa ni kati ya shilingi Bilioni 2.5 zilizotengwa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa ajili ya miradi ya Uwajibikaji wa Jamii (CSR) kwa mwaka 2021/2022 katika Halmashauri ya Msalala. Dhamira yetu ni kuhakikisha tunatekeleza wajibu wetu katika jamii na kushirikiana nao katika kupanga mipango ya maendeleo hasa inayohusu kukuza uchumi wao na wa jamii kwa ujumla kupitia mpango wetu wa CSR”,amesema Paul.

“Tunajivunia kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunajali watu wenye ulemavu wanaoishi maeneo jirani na mgodi wetu ili kuwaongezea furaha na kuwawezesha kushiriki shughuli za kiuchumi kwa kuwapa vifaa vya kazi. Tutaendelea kujivunia kuwajali makundi maalumu kwa ujumla wake ikiwa ni pamoja na dawati la jinsia linaloshughulika na wasichana na Wanawake nao wananufaika”,ameongeza.

Akizungumza wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya CSR ili kuhakikisha jamii inapiga hatua kimaendeleo.

“Niwapongeze Barrick kwa vifaa hivi mlivyotoa leo kwa kuhakikisha watu wenye mahitaji maalumu wanapata vifaa vitakavyowezesha kufanya kazi. Kwa kweli mmeunga mkono kwa vitendo dhamira na nia ya Mhe. Rais Samia Suluhu, mtetezi namba moja wa watu wenye mahitaji maalumu ambaye mara kwa mara amekuwa akisisitiza makundi maalumu yasiachwe nyuma yapewe kipaumbele katika jamii”,amesema Kiswaga.

Kiswaga amesema Serikali itaendelea kuwajali na kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu katika kupambana na umaskini ili kuhakikisha wanawapa ahueni ya maisha huku akiwashauri watu wenye mahitaji maalumu kuchangamkia fursa ya mikopo inayotolewa katika halmashauri za wilaya.

Kiswaga amesema Barrick wamekuwa wakitoa fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali hivyo kuwaagiza watendaji wote kuhakikisha fedha zinatumika kuwaletea maendeleo wananchi na kwamba hatasita kuwashughulika wale wataothubutu kudokoa fedha hizo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Charles Fussi amewataka watu wenye ulemavu kujitokeza kupata mikopo bila riba inayotolewa katika halmashauri huku akishauri kuwa kabla ya kuchukua mikopo ni vyema wakapata ushauri kuhusu miradi inayotekelezeka ili wainuke kiuchumi na kuweza kurudisha mikopo hiyo.

Nao Watu wenye ulemavu akiwemo Salome Samweli na Mshikila Juma ameushukuru Mgodi wa Barrick Bulyanhulu na Halmashauri ya Msalala kwa kuwapatia vifaa vya usaidizi ambavyo watavitumia kutembea kutoka eneo moja hadi jingine na kujitafutia kipato ili kujiinua kiuchumi.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Watu wenye Ulemavu kata ya Bulyanhulu, Abbas Hassan ameishukuru Serikali na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwathamini na kuwajali watu wenye ulemavu na kwamba kutokana na vifaa hivyo walivyopatiwa sasa wataweza kuwahi kufika kwenye maeneo yao ya kazi.

Naye mwakilishi wa wazee, Ramadhan Salehe amesema Barrick Bulyanhulu wameonesha upendo kwa kuwapatia bima za afya ambazo zitawawezesha kupunguza gharama za matibabu kwao na wategemezi wao.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu. Wa kwanza kushoto ni Mrakibu wa Mahusiano ya Jamii Barrick Bulyanhulu Bi. Zuwena Senkondo akifuatiwa na Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Charles Fussi. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Mhe. Charles Fussi akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mrakibu wa Mahusiano ya Jamii Barrick Bulyanhulu Bi. Zuwena Senkondo akizungumza wakati kampuni ya Barrick ikikabidhi vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa mbalimbali vya usaidizi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa mbalimbali vya usaidizi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya vifaa mbalimbali vya usaidizi vilivyotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu wapatao 210 kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Muonekano wa sehemu ya baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akimkabidhi baiskeli mmoja wa watu wenye ulemavu. Baiskeli hizo zimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Salome Samweli akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa Baiskeli na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga. Baiskeli hizo zimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mshikila Juma akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa Baiskeli na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (aliyeshikilia kipaza sauti kushoto). Baiskeli hizo zimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Cherehani ya Overlock kwa ajili ya kikundi cha wazee. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akikabidhi Cherehani ya Overlock kwa ajili ya kikundi cha wazee. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Cherehani ya Ngozi kwa ajili ya kikundi cha watu wenye ulemavu. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Cherehani ya kawaida kwa ajili ya kikundi cha wazee. Vyerehani hivyo vimetolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (wa pili kulia) akikabidhi Dish la DSTV ambayo ni sehemu seti ya Televisheni kwa ajili ya Kituo cha afya Bugarama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kulia) akikabidhi TV ambayo ni sehemu seti ya Televisheni kwa ajili ya Kituo cha afya Bugarama.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga (wa pili kulia) akiwasha pikipiki iliyotolewa na Barrick Bulyanhulu itakayotumika katika ofisi ya Dawati la Jinsia kusaidia kuwezesha kushughulikia masuala ya wasichana na Wanawake.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akiangalia baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi baiskeli zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Fimbo nyeupe zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi Fimbo nyeupe zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Meneja Mahusiano na Mazingira kutoka Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Bw. Agapiti Paul akikabidhi Vifaa vya kusikia vilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Festo Kiswaga akikabidhi kadi za bima ya afya zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu.
Zoezi la kukabidhi kadi za bima ya afya zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu likiendelea.
Zoezi la kukabidhi kadi za bima ya afya zilizotolewa na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa wazee kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu likiendelea.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Watu wenye Ulemavu kata ya Bulyanhulu, Abbas Hassan akiishukuru Serikali na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuwathamini na kuwajali watu wenye ulemavu.
Mwakilishi wa wazee, Ramadhan Salehe akitoa neno la shukrani.
Wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kutoka kampuni ya Barrick
Wazee na watu wenye Ulemavu kutoka vijiji vinavyozunguka Mgodi wa Bulyanhulu wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya usaidizi na kadi za matibabu kutoka kampuni ya Barrick.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

DAWA HIZI UNAPENDA KUZITUMIA LAKINI ZINAWEZA KUWA HATARI KWA AFYA YAKO


Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, dawa hizo zinapoteza ufanisi wake kwa kasi ya kushangaza

Kula vyakula vya kukaanga ama vilivyo na mafuta mengi kunaweza kusababisha kuumwa na tumbo au kuvimbiwa.

Baadhi ya wanapokabiliwa na tatizo kama hilo hukimbilia duka la dawa na kupata vidonge vya kujitibu bila ushauri wa daktari.


Kununua dawa bila maelekezo ya daktari sio jambo geni muongoni mwa rais wa nchi za Afrika Mashariki.

Ijapokuwa nchi hizo zina utaratibu wa kudhibiti ununuzi bila ushauri wa daktari, maduka mengi ya kuuza dawa hayafuati utaratibu huo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, dawa hizo zinapoteza ufanisi wake kwa kasi ya kushangaza kutokana na matumizi mabaya na yasiyo ya kukusudia ya antibiotiki.


Lakini dawa hizi zinaweza kuwa na madhara gani kwa afya zikitumiwa bila ushauri wa daktari?

Paracetamol

Watu wengi hutumia paracetamol kwa maumivu au homa.

Madaktari mara nyingi huagiza paracetamol kwa homa au maumivu ya mwili. Makampuni tofauti huuza kwa majina tofauti.

"Tunabainisha jinsi na kwa muda gani wa kula. Lakini baadaye wagonjwa hununua na kula tu wakati wana homa au maumivu ya mwili. Matokeo yake, inapoteza ufanisi wake wakati fulani'' anasema mtaalamu mmoja.

Matumizi ya muda mrefu ya paracetamol au acetaminophen yanaweza kusababisha uharibifu wa ini.

Matumizi yasiyodhibitiwa ya dawa za kuzuia maumivu au kushindwa kumaliza dozi kunaweza kusababisha hatari kubwa kwa mwili

Aspirin

Aspirin ni dawa muhimu sana lakini inaweza kuwa hatari ikitumiwa kiholela kwa sababu sio salama kwa kila mtu.

Dawa hii inajulika kwa ubora wake wa hali ya juu ya kutuliza maumivu na wakati mwingine hutumiwa kutuliza homa.

Wazee, ambao wana magonjwa ya moyo- madaktari huwapa dawa hii kwa kipimo fulani. Ikiwa kuna madhara pia hufuatiliwa.


Madhara

Inaweza kusababisha chakula kisisagike vizuri hali ambayo inaweza kumsababishia mtu kupatwa na vidonda vya tumbo.


Usimpatie mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 16 asprin bila ushauri wa daktari.


Inaweza kuwafanya watoto kupatikana na ugonjwa hatari unaojulikana kama Reye syndrome ambayo inaweza kuathiri (ini au ubongo).


Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu na uvimbe huchangia ongezeko la hatari ya kupata maradhi ya moyo, utafiti umebaini.

Diclofenac na dawa zingine

Madaktari wanasema kuwa kununua dawa bila agizo la daktari imekuwa jambo la kawaida


Watu wengi hutumia dawa mbalimbali za kutuliza maumivu ya mwili, maumivu ya mguu au maumivu ya kichwa. Hasa ikiwa unapata maumivu kwa sababu yoyote, kununua ibuprofen au diclofenac kutoka kwa maduka ya dawa na kuanza kuitumia.


''Inaweza kusababisha matatizo ya tumbo, kuharibu tumbo, na kusababisha kutokwa na damu. Mikono na miguu ya watu wengi hutoka maji, huvimba,'' anasema Dk Maula.


Matumizi ya muda mrefu ya madawa haya yanaweza kusababisha kutokwa na damu ya utumbo. Baaadhi ya watu wanakabiliwa na mmeng'enyo mbaya wa chakula, wana vidonda, na wanaweza kuwa waraibu wa dawa za kulevya.


Dawa kama vile Ibruprofen, Naproxen na Diclofenac ndizo dawa hutumiwa sana kupunguza maumivu na kuvimbiwa.

Metronidazole

Dawa nyingine ambayo inatumiwa vibaya inafahamika kama metronidazole. Baadhi ya watu huzinunua bila maelekezo ya dakatari wakiwa na maumivu ya makali ya tumbo kwani pia ni aina ya dawa ya kutuliza maumivu.

Madhara ni pamoja na upele na kuvimbiwa. Kisha yanafuatiwa na shida nyingine kama kutokwa na damu katka sehemu za siri Mgonjwa anapata choo kigumu,ambacho kinasababisha maumivu wakati wa kwenda haja kubwa.

Shirika la Afya Ulimwenguni linasema unyanyasaji wa viua vijasumu unaweza kuua watu milioni 300 ulimwenguni ifikapo 2050

Dawa zingine hatari zaidi


Baadhi ya watu hununua dawa za tezi au steroid kutoka kwa maduka ya dawa kwa matatizo ya koo. Lakini matatizo ya dawa hizo kiholela yanaweza kuwa na madhara makubwa kwa afya.


Madaktari wa kitaalam wametoa ushauri juu ya matamizi ya dawa hizi.

Ikiwa una tatizo la dharura sana kama vile maumivu, hata ukinunua dawa moja au mbili za dharura kutoka kwa duka, unahitaji kushauriana na daktari haraka iwezekanavyo.
Hakuna antibiotics inapaswa kumezwa kwa ushauri wa wafanyakazi wa maduka ya dawa.
Ukiwa na homa, maumivu ya tumbo au tatizo lolote la kimwili, ushauri wa daktari unapaswa kuzingatiwa kabla ya kumeza dawa yoyote kiholela.
Angalia madhara na muda wa dawa yoyote kabla ya kutumia.
Wakati wa kununua dawa, nunua dawa kwa kuzingatia maagizo ya daktari.

Chanzo - BBC SWAHILI
Share:

Thursday, 7 April 2022

UTAFITI WAONESHA BINADAMU ANAPOTEZA 26 KILA MWAKA BILA KUFANYA KITU CHOCHOTE


Matumizi ya mitandao ya kijamii
Kusubirishwa kwenye simu kunapoteza muda
Foleni ya barabarani nayo inapoteza muda mwingi

***
JE umeshawahi kujiuliza kwa mwaka ni muda kiasi gani unaoupoteza kutokana na kutofanya chochote? Mathalani, mtu anakusubirisha tu sehemu halafu mwisho wa siku hatokei. kimsingi unakuwa umepoteza muda wako bure.

Matukio ya aina hiyo ya kupotezewa muda wako bure ukiyajumlisha kwa mwaka mzima kadri yanavyokutokea unadhani mwisho wa mwaka utakuwa umepotezewa muda kiasi gani?

Majibu ya swali hili yanahitaji utafiti.
Kwa mujibu wa Utafiti uliodhaminiwa na Duolingo na kufanywa na Onepoll umebaini kuwa binadamu wa kawaida anapoteza muda wa mwezi mzima kila mwaka kwa kutofanya chochote.


Utafiti uliofanywa kwa watu 2000 raia wa Uingereza umebaini kuwa binadamu wa kawaida anapoteza muda wa zaidi ya siku 26 kwa mwaka kwa kutofanya chochote, masaa 12 kwa wiki au zaidi ya masaa 624 kwa mwaka.

Kwa zaidi ya nusu ya waliohojiwa wamekiri kwamba kusubirishwa kwenye simu ndiyo jambo linalopoteza muda kwa asilimia kubwa, maana yake ni kwamba mtu anakupigia simu halafu anakuambia nisubiri kidogo! (Anakusubirisha) unapoteza dakika kadhaa kusubiri mtu huyo muda wote huo unakuwa haufanyi chochote kwahiyo muda unakuwa unapotea bure.

Asilimia 45 ya kupoteza muda ni pale unapokuwa umepanga foleni ya kupata huduma kwa mfano Benki, sehemu ya huduma ya maji, hospitali n.k

Sababu nyingine zinazopelekea kupotea bure kwa muda ni kama kukaa kwenye foleni za barabarani ambayo utafiti umeonesha ni kwa asilimia 44, matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo utafiti umeonesha yanapoteza muda kwa asilimia 21 na kusubiri kitu kichemke mathalani maji au chai muda hapo hupotea kwa asilimia 15.

Kusubiri nguo zifuliwe na mashine, kusubiri huduma mgahawani au hotelini na kusubiri bidhaa uliyoagiza ifike (Delivery) vyote hivi vinakula muda.

Katika utafiti huo asilimia 47 ya wazee wamesema wanajikuta wanakaa bila kitu cha kufanya takribani mara tatu kwa siku na hiyo inatokana na kukosa hamasa ya kufanya kazi, na kwa nyongeza tu ni kwamba asimilia 56 ya watu waliohojiwa katika utafiti huo wamekiri kuwa wanatakiwa kulifanyia kazi suala zima la matumizi sahihi ya muda.

Katika kupambana na suala la kutunza muda imebainika kuwa asilimia 38 ya binadamu wanapoteza muda wao mwingi katika kuangalia televisheni pamoja na matumizi ya mtandao wa intaneti.

Majibu ya watu waliohojiwa kuhusu nini kifanyike ili kuwa na matumizi sahihi ya muda kwa asilimia 70 wamesema watautumia mwaka huu wa 2022 kujifunza njia na ujuzi mbalimbali ili kuokoa muda unaopotea bure.
Share:

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AHUDHURIA MAZISHI YA SPIKA WA BUNGE LA UGANDA


Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson akiaga mwili wa Spika wa Bunge la Uganda Jacob Oulanyah
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki ibada ya kitaifa ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Jacob Oulanyah katika Viwanja vya Kololo, Jijini Kampala nchini Uganda.

Marehemu Jacob alifariki dunia Machi 20, 2022 nchini Marekani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kabla ya kufariki Spika huyo wa Bunge la Uganda alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa na japo kifo chake kimeacha sintofahamu kutokana na taarifa kuwa alipewa sumu, taarifa ambayo imethibitishwa na baba yake Nathan Okori.

“Najua wote mliokuja hapa kwenye kuomboleza taarifa za kifo chake siyo nyepesi kuzipokea kwasababu najua hakufa kwa kifo cha kawaida aliwekewa sumu",alisema Okori
Share:

PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG UWE UNAPOKEA HABARI KWA URAHISI ZAIDI


Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>
Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>

Habari Njema Wasomaji wa Malunde 1 blog !! Ili kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio  ya ukweli na uhakika kwa wakati yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla tunakushauri kupakua/ kudownload Aplikesheni ya Malunde 1 blog

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotokea… Pakua leo App ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani mwako kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. 


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Toleo Jipya Kabisa la App ya Malunde 1 blog, Kama unayo kwenye simu Pakua Upya mtu wangu...  Bofya mara Moja <<Hapa>>



Share:

Wednesday, 6 April 2022

AANGUKA NA KUFARIKI KANISANI AKIHUBIRI KUHUSU WACHAWI



Tukio la kusikitisha limetokea katika Kanisa la Evangelical Winning All (ECWA) nchini Nigeria baada ya shemasi kuanguka ghafla na kufariki papo hapo akihubiri dhidi ya mauaji ya kiibada na dhabihu za kibinadamu.

Imeibuka kuwa kisa hicho kilitokea Jumapili, Aprili 3,2022 wakati shemasi huyo aliyetambulika kwa jina moja la Ogunnusi, alipokuwa akihubiri wakati wa ibada. 

Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Ogunnusi anaonyeshwa akihubiri kwa lugha ya Kiyoruba na ananukuliwa akisema: “Fedha unazopata kwa njia zisizo halali, kuua watu, kunyonya damu ya binadamu; kifo kikija, kitakuwa cha mtu mwingine.” Mkalimani katika ibada hiyo alikuwa bado anajaribu kutafsiri maneno yake kwa Kiingereza wakati Ogunnusi alipoanguka ghafla.

Kulingana na ripoti ya Daily Trust, shemasi huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Shirikisho, Idi-Aba, Abeokuta, ambapo alithibitishwa kufariki.

 Mmoja wa mashahidi aliyezungumza na chapisho hilo alisema: “Mtu huyo hakuwa mchungaji wa kanisa hilo, alikuwa tu mzee wa kanisa. Alikuwa Baale wa Onikoko. Lakini yeye ndiye aliyetoa mahubiri siku ya Jumapili." “Alikuwa anazungumzia kifo na watu wanaopata pesa kwa kuua watu wengine. Ghafla, alianguka.

Alikimbizwa FMC, lakini alikufa. Hatujui kilichotokea. Niliogopa sana. Kila kitu kilivurugika. Tulishiriki tu ombi la neema na tukarudi nyumbani."

Mauaji ya kiibada yamekuwa yakiongezeka nchini Nigeria katika siku za hivi karibuni.

 Katika azma ya kukabiliana na maovu hayo, Serikali ya Shirikisho ilikuwa imefichua mipango ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji dhidi ya mila ya pesa ambayo imegharimu maisha ya wengi, haswa wanawake na wasichana. 

Waziri wa Habari na Utamaduni nchini humo Alhaji Lai Mohammed alisema serikali inasikitishwa na kuongezeka kwa visa hivyo kidesturi yanayofanywa na watu wasio waaminifu, wengi wao wakiwa ni vijana wanaotaka kutajirika haraka.

Serikali ya shirikisho pia ilielekeza watengenezaji filamu wa Nigeria kuacha maudhui ya tambiko ya pesa kutoka kwa sinema zao.

 Mohammed alisema baadhi ya watu wanaoshukiwa kuwa wauaji wa kitamaduni ambao wamekamatwa walikiri kwamba walijifunza vitendo vya mauaji ya kiibada kwenye mitandao ya kijamii na hii imetaka Serikali ya Shirikisho ibadilishwe ili kusafisha mitandao ya kijamii.
Share:

KIJANA WA MIAKA 25 ATANGAZA KUFUNGA NDOA NA BIBI WA MIAKA 85


Kijana akiwa kwenye mahaba mazito na Bibi mpenzi wake
Mwanaume mchanga mwenye umri wa miaka 25, amewashangaza wengi baada ya kufichua mipango yake ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka 85.

Wapenzi hao wanalandana sana wazimu na kuzama katika bahari ya mapenzi na sasa wanapanga kufanya harusi hivi karibuni ili kuweka rasmi uhusiano wao.

 Wote wawili wanaazimia kuishi pamoja maisha yao yote licha ya kwamba mpangilio huo haujawafurahisha wengi.

"Hili ni chaguo langu. Hii ni furaha yangu, kama mtu mwingine yeyote ana yake. Kabla ya kuwafurahisha wengine, kwanza, jifurahie mwenyewe na uamue kutozingatia maoni ya mtu mwingine yeyote," Muima aliiambia Afrimax English.

Muima na wenzake walikuwa wakiwinda nyumba walipotua nyumbani kwa Thereza, ambapo walilipa kodi na kuanza maisha mapya.

 "Jinsi alivyotenda na kunijali (mimi) kulinichochea kumpenda na ingawa yeye ni mwanamke mzee na kwa kweli, anaweza kuwa nyanya yangu lakini ninampenda," Muima alisema. 

Alisimulia siku ambayo mwenzake hakuwepo, na alikuwa anakeketwa na njaa na hakuwa na chakula katika nyumba yake ya kupanga. Mwanamke huyo alimletea chakula na kumpa kwa uangalifu sana kabla ya kuomba busu, ambayo alikubali kumpa.

Uhusiano huo ulipozidi kuimarika, wapenzi hao walitumia muda wao kucheza, kuinuana na kusafiri licha ya umri wa Thereza. 

Ananipenda na pia mimi nampenda Watu wengi ambao hawafahamu uhusiano wao hufikiria ni bibi anafurahia wakati wake na mjukuu wake au mwanawe. Thereza ana wajukuu wakubwa kuliko mpenzi wake, lakini haoni aibu kuwa kwenye uhusiano na Muima. "Nina watoto wanane na wajukuu 20. Kulingana na umri wa mpenzi wangu, anaweza kuwa mjukuu wangu wa tano. Ananipenda na mimi nampenda. Niko tayari kuvaa nguo ya harusi na pete," alisema.

Muima yuko tayari kulipa mahari ya ng'ombe 12 ambao watoto wa mpenzi wake wameitisha.

 Mwanaume huyo amepata mapenzi na nyanya huyo baada ya kuwa katika mahusiano mengi ambayo yalikuwa yakivunjika.

 "Sitawahi kuchagua msichana yeyote zaidi ya huyu. Naomba asife kabla yangu," Muima aliongeza. Thereza hakupuzilia uwezekano wa kuanzisha familia na mpenzi wake mchanga, akisema kuna mifano katika Biblia inayompa tumaini.
Share:

BENKI YA CRDB KUCHOCHEA BIASHARA KATI YA TANZANIA, BURUNDI NA DRC


Waziri Mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk Jilly Maleko (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Dk Ally Laay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (watatu kushoto), Mjumbe wa Bodi Benki ya CRDB Burundi, Kahumbaya Bashige (wapili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fred Siwale (wa kwanza kushoto), na Menard Bucumi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi.

Benki ya CRDB inaonekana kuwa daraja muhimu la kukuza biashara na mahusiano ukanda wa katika Afrika Mashariki, hasa miongoni mwa nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na Burundi.

Benki hiyo kwa sasa inatoa huduma katika nchi ya Burundi na inaelezwa kuwa katika robo ya tatu yam itazindua huduma zake kupitia kampuni tanzu huko Lubumbashi, jiji la pili kwa ukubwa baada ya Kinshasa, nchini DRC.
Kuanzishwa kwa kampuni tanzu hiyo kunaendana vyema na hatua za hivi karibuni ambapo nchi ya DRC imekubaliwa ombi lake la kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kufanya jumla ya nchi saba wanachama katika ukanda huu.

Waziri Mkuu wa Burundi, Alain Guillaume Bunyoni, alisema amefurahishwa kusikia kwamba Benki ya CRDB inafungua kampuni yake tanzu nchini DRC itakayokuwa na makao yake makuu mjini Lubumbashi na kutaka huduma hizo kusogezwa karibu na mpaka wa Burundi na DRC pia.


"Ninaiomba benki kufungua matawi karibu na mipaka ya Burundi na DRC, katika miji ya Uvira na Bukavu ili kuimarisha biashara," Bunyoni alisema hayo wakati alipotembelewa na ujumbe wa Benki ya CRDB ofisini kwake mwishoni mwa juma lililopita kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inayoipa benki hiyo.


Ujumbe huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Ally Lay na Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, ambao waliambata Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt Jilly Mareko.
Madhumuni yalikuwa kwa wajumbe wa Kikundi cha Benki ya CRDB kufahamu msaada ambao benki hiyo inapata kutoka kwa serikali ya Burundi tangu wakati mkopeshaji alipofungua kampuni yake tanzu nchini Burundi mwaka 2012.

Katika mazungumzo yaliyofanyika, Benki hiyo ilimhakikishia Bunyoni kuendelea kushirikiana na serikali zote mbili za Burundi na Tanzania kufadhili miradi ya pamoja inayofanywa na nchi hizo mbili hususan mradi wa reli ya kisasa (SGR) na miradi mingineyo.

Waziri Mkuu huyo aliishukuru Benki ya CRDB kwa kusaidia kukuza uchumi wa Burundi kupitia uwezeshaji mkubwa inaoufanya nchini humo kwa kutoa mikopo inayogusa makundi mbalimbali ya wateja kuanzia kupitia watu binafsi, makampuni na hata serikali.

"Niwahakikishie kuwa serikali yetu inaunga mkono jitihada mnazozifanya katika kuinua uchumi wa Taifa letu la Burundi, na tupo tayari kushirikiana nanyi katika utekelezaji miradi mikubwa kwani baadhi yao inahusisha hata nchi zetu mbili za Tanzania na DRC," Bunyoni alisema.
Aliukumbusha ujumbe wa benki hiyo kuwa ndiyo ilikuwa ya kwanza kuanzisha huduma za kibenki kupitia simu za mkononi nchini humo “SimBanking”, nakubainisha kuwa huduma hiyo imeleta mapinduzi makubwa nchini humo na kuwa kichocheo kikubwa katika kuongeza ujumuishi wa kifedha.

Pia aliishukuru Benki ya CRDB kwa uwezo wake wa kukusanya fedha kwenye masoko ya kimataifa bila masharti magumu kama ambavyo imekuwa ikifanywa na baadhi ya wakopeshaji kutoka nje ya Afrika.

"Pia ni muhimu kutambua kwamba benki hii kupitia programu yake ya mageuzi ya kidijitali imekuwa ikisaidia kurahisha miamala ya kibiashara ya kati ya Burundi na Tanzania kwa kuweka mifumo na miundo mbinu inayowezesha miamala ya kifedha kufanyika kwa urahisi ikiwamo malipo ya bandari na kodi mbalimbali zinazotozwa na serikali,” alioongezea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Benki ya CRDB, Dkt Laay, alimweleza Waziri Mkuu huyo kuwa benki hiyo imewekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali ili kuwawezesha wateja kuokoa muda na hata kupanua huduma za benki katika maeneo ambayo hayajafikiwa.

"Hii itasaidia Burundi katika utekelezaji wa ajenda yake ya kuongeza ujumuishi wa kifedha," Dkt Laay alisema na kuongeza:


"Ni katika muktadha huo benki sasa inasambaza huduma za CRDB Wakala wajulikanao kama ‘Turihose’ nchini humo, pamoja na kuhamasisha matumizi ya huduma za SimBanking, na huduma ya kibenki kupitia mtandao ‘Internet banking’ kwa wateja wake.”

Sambamba na miaka 10 ya Programu ya Maendeleo ya Taifa la Burundi, Mwenyekiti huyo alisema, benki hiyo inatarajia kuelekeza nguvu zake katika maendeleo ya sekta za kiuchumi kama vile kilimo, viwanda, miundombinu na makazi, na utalii ambazo ni muhimu katika kukuza ajira kwa vijana na kutengeza fedha za kigeni nchini humo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB alimweleza Waziri Mkuu Bunyoni kuwa kwa sasa benki hiyo inashika nafasi ya tatu kwa utoaji wa mikopo nchini Burundi baada ya miaka 10 ya kufanya kazi na asilimia 20 ya mikopo yake imetolewa katika sekta ya ili kusaidia Warundi wengi.

"Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, benki imeendelea kusaidia uchumi wa Burundi kwa kutoa bidhaa na huduma bunifu kwa makampuni, watu binafsi na taasisi wateja kupitia bidhaa za kuweka kuweka amana na mikopo," Nsekela alisema.

Hivi Karibuni ujumbe wajumbe wa viongozi wa Chemba za Biashara za nchi za Burundi, Misri, Zambia, Botswana, Rwanda, Ethiopia na Uganda ukiongozwa na Rais wa Baraza la Biashara Barani Afrika Dr. Amany ASFOUR walitembelea makao makuu ya Benki ya CRDB na kupongeza mkakati wa benki hiyo wa kupanua biashara yake katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Benki hiyo - ambayo imekuwa nchini Burundi tangu 2011 ina jumla ya matawi manne, matatu Bujumbura na moja katika mji wa Ngozi, mwaka huu Benki ya CRDB inatarajia kufungua tawi la tano katika Wilaya ya Gitega.

Akielezea matokeo ya kifedha ya kampuni tanzu ya Burundi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Fred Siwale amesema mwaka jana walipata faida ya Shilingi bilioni 12.8 ikiwa niongezeko la asilimia 14 kulinganisha na faida ya Shilingi bilioni 11.1 iliyopatikana mwaka 2020.

Benki hiyo pia ilipata matokeo mazuri katika viashiria vingine vya utendaji; Jumla ya Risilimali imeongezeka hadi kufikia Shilingi bilioni 551.1 kutoka Shilingi bilioni 350 iliyorekodiwa mwaka 2020, wakati amana za wateja ziliongeka kwa asilimia 66 kufikia Shilingi bilioni 329.4 kulinganisha na Shilingi bilioni 198.6 iliyorekodiwa mwaka 2020.

Mikopo iliongezeka kwa asilimia 62 kutoka Shilingi bilioni 225 mwaka 2020 hadi Shilingi bilioni 598. Siwale alisema Benki hiyo imekuwa mlipakodi mkubwa kwa serikali ya Burundi pamoja na kutengeneza ajira kwa Warundi.
Share:

TANZANIA, BURUNDI NA DRC ZAANZA MCHAKATO WA KUTAFUTA MSIMAMIZI UJENZI WA RELI YA KISASA UVINZA,MSONGATI NA GITEGA

Nchi za Tanzania Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zimeanza mchakato wa kumtafuta mtaalamu atakayesimamia ujenzi wa reli ya kisasa kwa vipande vya Uvinza Msongati na Gitega.

Hii inakuja siku chache tangu nchi hizi zisaini makubaliano ya awali kuhusu kuanza mchakato wa kutafuta fedha kwa wahisani zitakazofanikisha ujenzi huo.

Haya yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Ushoroba wa Kati Kapteini Dioudone Dukundane wakati wa mahojiano maalum na wanahabari.
Share:

Tuesday, 5 April 2022

BEI MPYA ZA MAFUTA KUANZA KUTUMIKA KESHO...IMEONGEZEKA

 

Mkurugenzi wa Petroli nchini Gerald Maganga akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu bei Kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia Jumatano,2 Machi 2022 .


Na Dotto Kwilasa-Malunde 1 blog-DODOMA

MAMLAKA ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA)imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini kuwa zitaanza kutumika kuanzia kesho ,Jumatano,tarehe 6 Aprili 2022. 


Mkurugenzi wa petroli nchini Gerald Maganga ameeleza hayo leo Jijini Dodoma wakati akiongea na Waandishi wa habari na kueleza kuwa Bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli ,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa Kupitia bandari ya Dar Es Salaam zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la 2 Machi ,2022.


Akiongea Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Geoffrey Chibulunje, Mkurugenzi huyo wa petroli nchini amefafanua kuwa kwa Aprili ,2022 bei  za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 321/Lita sawa na asilimia 21.45 mtawalia.


"Vilevile katika toleo lililopita bei za jumla za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeongezeka kwa shilingi 320.33/Lita  sawa na asilimia 13.29, Shilingi 288.50/Lita sawa na asilimia 12.69 na shilingi 472.41/Lita sawa na asilimia 22.72 mtawalia,"amefafanua


Akizungumzia mwezi Aprili,2022 Maganga amesema bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini ikihusisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa 2 Machi,2022.


"Kwa mwezi Machi mwaka huu,bandari ya Mtwara imepokea mafuta ya dizeli tu hivyo kwa Aprili 2022 bei za rejareja na jumla za mafuta ya petroli kwa mikoa ya Kusini yaani Lindi na Ruvuma zitakuwa sawa na zile zilizotangazwa tarehe 2 Machi,2022,


Kwa upande wa dizeli kwa mwezi Aprili 2022,Bei za rejareja na jumla za dizeli zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la mwezi uliopita ,bei ya rejareja ya dizeli imeongeza kwa shilingi 281/Lita sawa na asilimia 11.12 na bei ya jumla ya dizeli ikiwa imeongeza kwa shilingi 279.99/lita sawa na asilimia 11.67,"amefafanua.


Ameeleza kuwa kwa kuwa  hakuna matanki ya kuhifadhia mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka bandari ya Dar es Salaam na kwamba bei za rejareja za mafuta hayo katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa Kupitia bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.


"Mabadiliko haya ya rejareja yanachangiwa na kubadilika kwa bei za mafuta katika Soko la dunia, gharama za usafirishaji na thamani ya shilingi ukilinganisha na dola za Marekani,hivyo EWURA inaukumbusha Umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia Kupitia simu za mkononi Kwa kupiga namba *152*00#,"amefafanua


Licha ya hayo Maganga amefafanua kuwa Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ili mradi bei hizo zisivuke bei kikomo au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa kama ilivyokokotolewa Kwa kutumia formula na kanuni za EWURA zinazopanga Bei za mafuta za mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia gazeti la Serikali namba.57 la tarehe 28Januari mwaka huu.

Share:

KAMA UNA MATATIZO NA MBEGU ZA KIUME ANZA KUFANYA HILI LEO


Sasa nina umri wa miaka arobaini na miwili na nilioa yapata miaka sita iliyopita na kwa wakati huo wote sikufanikiwa kupata mtoto yeyote. Imekuwa uchungu kwangu! Ndoa sio mchezo.

 Tumekuwa na malumbano ya kila mara nyumbani mwetu huku bibi yangu akinifokea kwa kuwa sina uwezo wa kumpea mimba huku nami nikimlaumu kuwa ni tasa. Kila mmoja amekuwa akivuta ngozi upande wa kwake hadi pale tulipoenda kufanyiwa uchunguzi wa daktari ndipo ilipobainika wazi ya kwamba mbegu zangu ni hafifu haziwezi peana mke mimba. 

Kutoka siku hiyo nimekuwa nikisononeka hata sina amani kwangu na siwezi zungumza kamwe kama bwana mwenye nyumba maanake mimi ni dume bwege tu. Bahati mbaya, bibi yangu akaanza kuenda safari nyingi kila wiki na nilipomuuliza alinijibu kuwa anataka kutafuta mme wa kumtosheleza maanake mimi ni bure. 

Iliniuma siku hiyo aliponijibu hivyo lakini nisingeweza kumchapa. Kwa kweli siku hiyo alitoka akalala huko na nilipompigia simu aliniambia niachane naye ama asiwai rudi. Mke wangu aliendelea na hulka hizo hadi pale nilipotafutiwa suluhu ya kudumu na nyanyaangu ambaye alinipeleka kwa Daktari mmoja wa kienyeji aliyeitwa Kiwanga ambaye alinishugulikia kwa muda wa siku tatu na kwa kweli, kutoka siku hiyo mambo yakawa sambamba.

 Juzi nilikuwa na usiku wa kukata na shoka na bibi yangu kwani niliyomfanyia usiku kwa kitanda Mungu ndiye anayejua. Alibaki akihema na kusema nitamuua na nguvu nyingi. Hakuamini kamwe! Simba ni Simba! Nashukuru Kiwanga sababu mimi ni Jogoo sasa.

 Vile vile nawe kama unajuwa una matatizio na mambo ya mapenzi kwa nyumba yako tafadhali nakusihi pigia matabibu wa Kiwanga. Kiwanga Doctors ni shujaa wa mambo yote.

 Kwa mara nyingine, natoa wito kwa wenye shida za magonjwa, mapenzi, kazi, ndoa, biashara na afya kuharakisha kuwatembelea madaktari was Kiwanga. Tuvuti au Website yao ni: www.kiwangadoctors.com; Simu: +254 769404965 au wasiliana kwa barua pepe yaani Email: kiwangadoctors@gmail.com. Kumbuka sio lazima usafiri hadi ofisi zao. Ongea nao kwa njia ya simu na utasaidika kwa haraka kama vile watu wengine wanavyopata usaidizi.
Share:

NDEGE KUBWA ZAIDI YA ABIRIA DUNIANI YAPASUA ANGA SAA TATU IKITUMIA MAFUTA YA KUPIKIA

Ndege ya Airbus A380, imekamilisha safari ya majaribio ya kutumia mafuta ya kupikia kusafiri.

Ndege hiyo ya majaribio ilikamilisha safari ya saa tatu kutoka Uwanja wa Ndege wa Blagnac huko Toulouse hadi makao makuu ya Airbus ya Ufaransa mnamo Machi 25.

 Iliendeshwa na mafuta aina ya Sustainable Aviation Fuel au SAF ambayo mara nyingi hutengenezwa kwa mafuta ya kupikia yaliyotumika na takataka na inafanya kazi kwa injini moja ya Rolls-Royce Trent 900.

Airbus kisha ikafuatisha safari ya pili ya A380, ikitumia mafuta yale yale ya kupikia, mnamo Machi 29, ikiruka kutoka Toulouse hadi Nice. Ndege ya pili ilikuwa kufuatilia matumizi ya SAF wakati wa kupaa na kutua.

Mafuta yaliyotumika yalitolewa na TotalEnergies, kampuni iliyoko katika eneo la Normandy nchini Ufaransa. Airbus imekuwa ikifanya majaribio ya matumizi ya safari za ndege zinazotumia SAF kwa kipindi cha mwaka mmoja, huku A350 ikijaribiwa Machi 2021, na ndege ya njia moja ya A319neo ikiruka kutumia mafuta ya kupikia mnamo Oktoba. Kampuni hiyo inatarajia kupata kibali cha ndege yake kuruka kwenye SAF ifikapo mwishoni mwa muongo huu.

Hivi sasa, ndege za Airbus zinaweza kuendeshwa na hadi 50% ya SAF, iliyochanganywa na mafuta ya taa ya asili. Kampuni hiyo inadai kuwa ndege zinazoruka kwenye SAF zinaweza kufikia kati ya 53% hadi 71% ya upunguzaji wa kaboni unaohitajika kufikia lengo hilo. Airbus inapanga kuzindua ndege ya kwanza duniani isiyotoa hewa chafu sokoni ifikapo mwaka wa 2035. Ndege kubwa zaidi ya abiria duniani za A380 imekuwa ikipungua katika miaka ya hivi karibuni huku mashirika kadhaa ya ndege yakitaka kumalizwa kwa muda wa matumizi yao, kwa misingi ya utumizi wa mafuta ikilinganishwa na ndege za kisasa za masafa marefu.

Airbus iliwasilisha ndege ya mwisho ya A380 kwa shirika la ndege la Dubai Emirates mwishoni mwa 2021.
Share:

MAMA AFARIKI BAADA YA POLISI KUMPOKONYA POCHI YAKE

Scolastica Marada enzi za uhai wake
**
Familia moja katika kaunti ya Trans Nzoia inaomboleza kufuatia kifo cha jamaa yao kilichotokea baada ya afisa wa polisi kuripotiwa kumpokonya pochi lake lililokuwa na KSh 30,000 sawa na shilingi Laki sita za Tanzania.

Scolastica Marada, mama wa watoto watano, alizirai na kufariki baada ya maafisa kutoka Kituo cha Polisi cha Kiminini kuvamia nyumba yake na kupora pesa zilizokusanywa kutoka kwa chama.

 Marehemu alikuwa mfanyabiashara wa chang'aa. 

Kwa mujibu wa Daily Nation, siku hiyo ya mauti, marehemu aliripotiwa kukataa kuwapa polisi hongo ya KSh 1,000 kama 'ada za ulinzi', na kumchochea mmoja wao kumpokonya pochi lake.

"Kwa hiyo mmoja wa askari alinyakua mkoba uliokuwa na pesa ambazo dada yangu alipokea kutoka kwa kikundi chake cha merry-go-round kabla ya kuondoka nyumbani," dada mdogo wa Scolastica, aliyejulikana kwa jina la Brenda, alidai. 

Kulingana na dada yake Emily Nekesa, marehemu mwenye umri wa miaka 36, alikuwa akiugua ugonjwa wa moyo, na alipoanguka, alikimbizwa katika kituo cha afya kilicho karibu lakini akatangazwa kuwa amefariki alipofika “Nilipoingia ndani ya nyumba hiyo, nilimkuta dada yangu akiwa katika hali mbaya akiwa amelala chini, mara moja niliwataarifu majirani zetu waliosaidia kutoa huduma ya kwanza, tukamkimbiza katika Kituo cha Afya cha Solona kwa ajili ya matibabu,” alisimulia. 

Kulingana na Nekesa, dadake alipata fahamu akiwa njiani kuelekea kituo cha afya na kusema kuwa mmoja wa maafisa waliokuwa wamevalia miwani ‘alimuua’ kwa kuchukua pesa zake. "Macho nne amenimaliza, macho nne amebeba pesa zangu elfu thelathini nimepata kwa muganda, macho nne leo ameniua," alisema marehemu.

Chanzo - Tuko News
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger