Friday, 6 August 2021

Simbachawene Aagiza Waliowadhalilisha wapenzi wakiwa faragha Wakamatwe..."Huwezi Kumfumania Hawara"


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watuhumiwa wanaoonekana kwenye video clip mitandaoni wakiwashambulia wapenzi wakiwa kwenye faragha kwa madai ya kwamba wamewafumania.

Simbachawene ametoa agizo hilo leo Agosti 6, 2021 Jijini Dar es Salaama mara baada ya kuiona video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ikionesha kundi la watu wakiwavamia wapenzi hao na kuwadhalilisha kwa kuwapiga na kuwarushia maneno.

“Tabia hii imeshamiri sasa kama ambavyo video nyingi zinarushwa rushwa mitandaoni, leo nitumie fursa hii kutoa msingi wa kisheria lakini kukemea tabia hii ambayo imeanza kuonekana inaota mizizi. Ni kinyume cha sheria kabisa kuwaingilia watu walio kwenye faragha.

“Wakati mwingine watu wanafanya hivyo kwa kisingizo kuwa wamefumania, hakuna fumanizi ambalo linaweza kupangwa na kikundi cha watu, wanawake na wanaume wanapanga kwenda kuwavamia na kuwaingilia uhuru wao waliopo faraghani, kitendo hicho ni kinyume cha sheria .

Amesema hata kama ni fumanizi litakuwa pale ambapo si jambo la kupangwa na huyo anayefumania awe na ndoa halali na cheti halali cha ndoa lakini sio kwa mtu ambaye ulikuwa naye tu “Huwezi kusema umemfumania hawala yako, mahusiano ya hawala ni ya kupita”.



Share:

Waziri Ummy Mwalimu Aagiza Waliofanya igizo katika zoezi la uchomaji wa chanjo ya COVID-19 Wasimamishwe Kazi



Share:

Rais Samia awaongoza Viongozi mbalimbali na Wananchi kuaga Mwili wa Hayati Kwandikwa



Share:

Magavana Wa Afrika Wa Benki Ya Dunia Na Imf Waazimia Kupaza Sauti Ya Pamoja Kuhusu Mifumo Ya Kidigitali


Na Benny Mwaipaja, Bujumbura
MKUTANO wa 58 wa Magavana wa Afrika wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF umemalizika Mjini Bujumbura nchini Burundi kwa kutoa msimamo wa pamoja wa kuziomba Taasisi hizo za fedha kuzijengea uwezo wa miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchi za Afrika kwa ajili ya kuchochea uchumi wa nchi hizo.

Makubaliano mengine ya Magavana hao ni kuyaomba mashirika hayo ya fedha ya kimataifa kuzipatia nchi zao rasilimali fedha kwa ajili ya kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia hususan katika suala la biashara ya mtandao, uchumi wa kidigitali na ujenzi wa miundombuni ya kidijitali ili kuifikia sehemu kubwa ya wananchi mijini na vijijini

Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, alisema kuwa msimamo huo wa pamoja umelenga kuwawezesha wananchi kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia ya kidijitali katika kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii hususan katika kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Uviko-19.

“Kizazi kilichoelimika kuhusu matumizi ya kidigitali, kinachangia maendeleo na kubuni nyenzo zinazosaidia kutekeleza kazi za ubunifu ili kukuza ajira na kuboresha maisha ya wananchi” Alisema Mhe. Masauni

Alizungumzia pia suala la umuhimu wa nchi za Afrika zenye vyanzo vya uhakika vya nishati ya umeme kujengewa uwezo na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha  Duniani (IMF) kufua umeme kutokana na vyanzo vya gharama nafuu kama maji na gesi asilia pamoja na kuhakikisha kuwa huduma hiyo ya umeme inawafikia wananchi wengi ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za kidigitali.

“Takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wanaopata huduma ya nishati ya umeme barani Afrika imefikia chini ya asilimia mbili hivyo kuna umuhimu mkubwa wa Taasisi hizo za Fedha duniani kuzipatia nchi za Afrika rasilimali fedha kwa ajili ya miradi hiyo” Alisistiza Mhe. Masauni.

Mheshimiwa Masauni pia alisema kuwa, kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo ya umeme na miundombinu ya kidigitali, robo tatu ya wakazi bilioni 1.3 Barani Afrika hawatumii intaneti jambo linalokwaza wananchi kutumia fursa za kidijitali katika kuendesha maisha yao.

“Katika suala la umeme Tanzania tumepiga hatua kubwa ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia Mradi wa REA lakini tunahitaji fedha zaidi kwa ajili ya kutekeleza miradi itakayochochea ukuaji wa uchuni na maendeleo ya watu katika nyanja ya matumizi ya dijitali, sekta ambayo hivi sasa ina ajiri idadi kubwa ya watu wakiwemo vijana na ni lazima miradi hiyo iwe ni ile yenye tija” Aliongeza Mhe. Masauni

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Kundi la Kwanza la Afrika Dkt. Taufila Nyamadzabo, alisema kuwa mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa na kuahidi kuwa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF litayafanyiakazi kikamilifu maazimio yaliyofikiwa wakati wa Mikutano ya Taasisi hizo iliyopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka 2021, Washington, Marekani

“Kimsingi naamini Benki ya Dunia na IMF zitatoa fedha kwa nchi za Afrika katika kutimiza malengo yao ya kuwa na uwezo wa matumizi ya mifumo ya kidijiti, mifumo ya biashara ya mtandao pamoja na kuboresha nishati ya umeme lakini fedha hizo zitatolewa kwa kila nchi kivyake kadri zitakavyoomba kulingana na mahitaji na vigezo vinavyotakiwa” alisema Dkt. Nyamadzabo

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt. Jilly Maleko alieleza kuwa Mkutano huo umefanyika muda muafaka kwa ajili ya mustakabali wa nchi za Afrika ambazo zimeathiriwa kwa kiasi kikubwa kiuchumi kutokana na kusimama kwa shughuli nyingi za uzalishaji kwa sababu ya ugonjwa wa UVIKO-19.

“Wito wangu kwa Watanzania hasa vijana ni kuchangamkia fursa zitakazopatikana baada ya makubaliano yaliyofikiwa hapa kwa sababu katika kipindi hiki mifumo ya kidigitali kwa kutumia simu na kompyuta ndiyo inayotumika kwa kasi katika fursa mbalimbali za kujiletea maendeleo hivyo ni muhimu wakajifunza kikamilifu matumizi ya teknolojia hiyo” Alisema Dkt. Maleko

Mkutano wa 58 wa Magavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Dunia – IMF umezishirikisha nchi 54 za Bara la Afrika ambazo baadhi ya wajumbe walikuwepo katika Ukumbi wa Bunge la Burundi (Kigobe) mjini Bujumbura na wengine walishiriki kwa njia ya mtandao.


Share:

MKUTANO MKUU WA UCHAGUZI TFF KUFANYIKA KESHO JIJINI TANGA ,WAGENI KUTOKA CAF,FIFA KUHUDHURIA

 

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau akizungumza na waandishi wa Habari leo kuhusu kuelekea mkutano huo
MGOMBEA Urais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia akizungumza na Waandishi wa Habari leo

NA OSCAR ASSENGA, TANGA

KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau amesema mkutano mkuu wa Kawaida wa Shirikisho ambapo moja ya  agenda kubwa ni Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Jijini Tanga kesho

Ambapo maandalizi yake yakiwa yamekamilika kwa asilimia 95 ya wageni mbalimbali wakiwemo wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Africa CAF na Shirikisho la Soka Duniani FIFA wakitarajiwa kuhudhuria mkutano huo

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Jijini hapa huku asilimia 5 ya wajumbe iliyobakia ikitarajiwa kuwasili leo kuungana na wenzao kwa ajili ushiriki wao.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Tanga Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Wilfred Kidau alisema kwamba maandalizi yamekamilia huku wageni mbalimbali wakiwasili ikiwemo Rais wa Shirikisho la Soka nchini Somalia ambaye pia vilevile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF.

Alisema pia walikuwa na kamati ua uchaguzi wa TFF kuhakikisha maandalizi ya muhimu yanakamilika wao kama sekretarieti ni wajibu wao kuhakikisha kamati ya uchaguzi ili iweze kufanya mambo yake kwa asilimia mia moja.

Alisema wapo wageni wengine mbalimbali wameanza kuwasilia Jijini Tanga ambapo wegine wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) wakiwemo wajumbe wawili wawili wapo njiani tayari kutua Jijini Tanga.

Awali akizungumza na waandishi wa Habari Mgombea Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema kikatiba kila baada ya miaka minne wanafanya uchaguzi na wa mwisho ulifanyika mwaka 2017 na safari hii wanafanya AgostI 7 wanafanya uchaguzi huo hapa jijini Tanga huku akiwaomba watanzania wawaombee kwa ajili ya mkutano huo.

Alisema kwamba  mkutano huo utajadili taarifa zao za utekelezaji za mwaka na yeye atatoa taarifa yake ya miaka minne ya uongozi wake na wajumbe watajadili na baadae ya hapo wataenda kwenye uchaguzi huo anamshukuru Mwenyezi Mungu kwenye mkutano huo mgombea wa Urais atakuwa pekee yake na uthibitisho utafanyika kwenye mkutano huo hivyo anaomba wajumbe waweze kunithibitisha.

Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya Biashara United ya Mara Selemani Mataso alisema uchaguzi huo ni muhimu sana hasa wao viongozi wa vilabu wanahitaji kupata watu ambao watawasaidia kuhakikisha wanaenda kutengeneza muonekano wa mpira ambayo haiwezi kuwa na shida na kuweka usawa wa vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza.

Alisema wakipatikana viongozi namna hiyo wakuangalia maslahi ya mpira inakwenda kutengeneza safu ya kuonyesha kwamba soka linakuwa linakwenda kujipambanua kuendesha soka la kisasa.


Share:

Shahidi kesi ya Ole Sabaya aangua kilio mahakamani.

 Shahidi namba nane upande wa Jamhuri katika kesi ya jinai Namba 105 ya unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili Mwalimu Magdalena (Zulfa) Mallya ameangua kilio mahakamani wakati akiielezea mahakama mazingira aliyokutana nayo wakati akimfuatilia mumewe shahidi namba sita Bakari Msangi aliyekuwa ametekwa na Sabaya na kundi lake.

Shahidi huyo ameieleza mahakama kuwa siku ya tukio Februari 9, 2021 akiwa nyumbani ambapo alidai alikuwa anaumwa yeye pamoja na mtoto wake, alikuwa akiwasiliana na mume wake kwa njia ya simu ila ilipofika kuanzia majira ya saa moja jioni mume wake hakuwa anapokea simu na baadaye hakuwa anapatikana kabisa jambo lililoanza kumpa wasiwasi kwani siyo kawaida ya mume wake kufanya hivyo.

Alidai ilipofika saa tano usiku simu yake iliita na alipoangalia alikuwa akipigiwa na mume wake ambaye alizungumza kwa sauti ya chini kama vile mtu aliyejificha mahali na kumwambia ameshikwa na Sabaya tangu saa 11 amepigwa na hali yake ni mbaya hivyo amfuate.

"Nikiwa pale hoteli ya Tulia jirani alienda kuulizia mume wangu akaambiwa hayupo tukageuza gari tukawa tunataka kutoka nje ili tuone tunapataje msaada hata wa polisi wakati anageuza ghafla simu yangu iliita mume wangu aliongea kwa maumivu makali sana akasema usiindoke nikamwambia si ushuke akaniambia amefungwa pingu miguuni....kwa kweli niliumia sana,"alisimulia shahidi huyo huku akilia .

Shahidi huyo aliendelea kueleza mahakama hiyo  kuwa walibaki ndani ya eneo hilo ambapo baada ya muda alimuona Sabaya akitoka ndani ya hoteli hiyo akiwa ameshika bastola na bahasha ya kaki na alipoingia kwenye gari na vijana wake kwenye magari mengine magari yaliwashwa kwa ajili ya kuondoka.

"Nikakimbilia getini nikapiga magoti na nilikuwa nimenyoosha mikono nikaita mheshimiwa naomba usimuue mume wangu tuna watoto wadogo na mimi ni mgonjwa, ninakuomba mheshimiwa muachie mume wangu na Mungu atakubariki nilipiga kelele sana gari yake ikashika breki pale nilipopiga magoti,"aliendelea huku akilia.



Share:

MSIGWA AWAFUNDA MAAFISA UHUSIANO,MAWASILIANO SERIKALINI ....."MSIPUUZE VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII"


Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa


Na  Dotto Kwilasa, Dodoma.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewataka Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini,Wizara, Mashirika na Taasisi kuwa vinara katika kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa sahihi  ili kuondoa  changamoto ya upotoshaji inayoendelea katika jamii na kuleta hofu.

Msigwa ameyasema hayo leo Jijini Dodoma kwenye kikao kazi kati yake  Maafisa hao huku akiwataka kuwa wepesi kuisemea Serikali kwenye maeneo yao na kuepusha taarifa za upotoshaji.

Amesema, licha ya tatizo la upotoshaji wa taarifa kuwepo tangu mwanzo,kwa sasa  limezidi na kupelekea kukwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo hivyo kuwataka Maafisa uhusiano kufanya kazi kwa weledi na wakati ili kuondoa changamoto hiyo.
 
"Lazima tutimize majukumu yetu kwa kuwa vinara kuhakikisha watu wanapata taarifa sahihi kuihusu Serikali,linapotokea tatizo kama hilo sisi ndiyo tunaopaswa kuwajibika kuisemea Serikali,tusisubiri mambo yaharibike,"amesema.

Mbali na hayo aliwataka pia kuongeza juhudi katika utendaji kazi na kamwe wasiruhusu wananchi kupotoshwa.

"Katika utendaji kazi wenu msikubali kuruhusu kutolewa taarifa za uongo,kumbukeni kuwa vyanzo vya taarifa ni nyinyi naomba hili jambo mlifanyie kazi kwa weledi na  nguvu zote,"amesisitiza.

ATAKA  KIPAUMBELE VYOMBO VYA HA BARI ZA KIJAMII.

Katika hili, Msemaji huyo wa Serikali ametaka Maafisa Uhusiano na  Mawasiliano Serikalini kutopuuza vyombo vya habari vya Kijamii na kusema kuwa haipendezi kuvibagua kwa kuwa navyo vina umuhimu sawa na vyombo vingine.

"Msivipuuze vyombo vya habari za kijamii lazima  tushirikiane navyo haipendezi wewe ni Afisa habari wa Taasisi flani halafu unabagua vyombo hivi kana kwamba havifai ,"amesema na kuongeza;

"Lazima mtambue kuwa vyombo hivi vimesajiliwa  ili vitumiwe kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii,vilevile vyombo hivi hivi mnavyovidharau endapo mtavitumia  vitawapa muda wa kutosha kukanusha masuala ya upotoshaji kwa jamii kwa Kuwa ndiyo vipo karibu zaidi na jamii,"

MITANDAO YA KIJAMII

Kuhusu mitandao ya kijamii Msigwa amewataka Maafisa hao kutumia Mitandao vizuri linapokuja suala la akauti za Wizara huku alisisitiza kuwa kuna ulazima wa kuzofanyia kazi Mara kwa  mara akaunti hizo na kuleta maana iliyokusudiwa.

"Siamini kwamba siku inaweza kuisha bila kuwa na jambo  la kuitaarifu jamii ,wewe usipotumia mtu mwingine ataitumia nafasi hiyo kupotosha,Tovuti za Serikali lazima ziwe hai  kufikia lengo la kuhakikisha watanzania wanapata taarifa sahihi,"alisema na kuongeza;

"Tunapotekeleza majukumu yetu kuna njia nyingi za kufikisha taarifa,nitoe wito kwa vyombo vya habari za kijamii kuzingatia masuala ya utoaji wa taarifa sahihi,"amesisitiza.

Msigwa pia aliweka sawa kwenye tatizo la upotoshaji na kusema kwamba sio vyombo vya habari ndivyo vinafanya upotoshaji huo bali ni Mitandao ya kijamii hivyo jamii inapaswa kuwa macho kuelewa usahihi wa habari.
Share:

MWALIMU ATUHUMIWA KUBAKA MWANAFUNZI WAKE WA DARASA LA 6 AKIMUAHIDI KUMUOA

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella Mutabihirwa

Na Edina Malekela - Singida.
Mwalimu wa shule ya Msingi Misuna iliyopo katika Manispaa ya Singida anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumbaka Mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka (13) anayesoma darasa la sita katika shule hiyo.

Akitoa taarifa kuhusu  tukio hilo kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Stella Mutabihirwa amesema tukio hilo limetokea usiku waAgosti 1,2021.

"Baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa za kuhusu tukio hilo lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa mtoto huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alibakwa na mwalimu wake anayeitwa Alphonce Festo mwenye umri wa miaka (26) Mnyaturu ambapo usiku huo akiwa nyumbani kwake huko katika Mtaa wa Salimini alifanya tukio hilo",amesema.

Kamanda alisema mbinu aliyotumia mtuhumiwa kufanya tukio hilo ni kumhadaa binti huyo kwa kumuahidi kuwa atamuoa ambapo atakuwa na maisha mazuri jambo lililopelekea kufanya kitendo hicho.

Jeshi la Polisi bado linamshikilia Mwalimu huyo wakati taratibu za kumfikisha Mahakamani zinaendelea na tayari jalada la kesi hiyo limefikishwa kwa mwanasheria na hali ya afya ya mwanafunzi huyo inaendelea vizuri na anaendelea na masomo.

Aidha Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Singida kuachana na vitendo vya ubakaji kwani vitendo hivyo ni vya kikatili ambapo husababisha madhara mbalimbali kwa mtu kama vile magonjwa na kuathirika kisaikolojia ama kufa kabisa.
Share:

Cashier (Internal Candidates only) at U.S. Embassy Dar es Salaam

Cashier (Internal Candidates only)   Overview Hiring Path: • Open to the public Who May Apply/Clarification From the Agency: Current Employees of the Mission – This includes U.S. Citizen Eligible Family Members (USEFMs); Eligible Family Members (EFMs); Declared Members of Household (MOHs), dependents of U.S. Personal Services Contract (USPSC) who are assigned under COM – All […]

This post Cashier (Internal Candidates only) at U.S. Embassy Dar es Salaam has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Kesi ya Mbowe na Wenzake Yaahirishwa hadi 13 Agosti 2021


Kesi ya ugaidi inayomkabili  Freeman Mbowe na wenzake 3 katika Mahakama ya Kisutu imeahirishwa hadi 13 Agosti 2021, baada ya upande wa Serikali kudai taratibu za kuifungua kesi hiyo katika Mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza kutokamlika.

Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo  leo Ijumaa, Agosti 6, 2021  asubuhi wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama. Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.



Share:

Serikali Kusitisha Vibali Vya Uagizaji Wa Sukari Ifikapo 2022-Waziri Mkenda


 Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Serikali imesema ifikapo Mwaka 2022 itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi kwa makampuni ambayo ndio wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo.

Upungufu wa bidhaa hiyo nchini hautokani na uhaba wa miwa bali unasababishwa na makampuni kushindwa kuongeza uchakataji wa miwa kutoka kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo jana tarehe 5 Agosti 2021 katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma aliposhiriki katika kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini.

“Baada ya mwaka huu Serikali haitotoa vibali kwa wawekezaji waliopewa viwanda vya sukari kuagiza sukari nje kwani tayari watakuwa wamefikia uwezo wa kuzalisha sukari toshelevu ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa uanzishwaji wa viwanda vipya vya sukari hapa nchini”

Waziri Mkenda amesema kuwa zaidi ya Tani 350,000 za miwa ya wakulima katika Bonde la Kilombero mkoani Morogoro zinateketezwa kwa moto kutokana na kukosa soko la uhakika lakini viwanda haviongezi uwezo wa kuchakata miwa ili kuzalisha sukari ya kutosha.

Amesema kuwa zaidi ya Tani 40,000 zinaagizwa kutoka nje ya nchi jambo ambalo sio sahihi kwani viwanda vya sukari vilivyopo nchini vinapaswa kuongeza uwezo wao ili kuimarisha soko la wakulima jambo litakalopelekea nchi kutoagiza sukari.

Waziri Mkenda amesema kuwa mtu yeyote atakayeingiza sukari kiholela ni wasaliti wa nchi hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kuwa kuna wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana lakini viwanda vimeshindwa kuongeza uwezo wake wa kuzalisha sukari ili kuimarisha sekta ya ajira kwa wananchi.

Katika mkutano huo Waziri Mkenda ameipongeza serikali na mawaziri waliotangulia kuiongoza Wizara ya Kilimo kwa kusimamia vyema sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kufanikisha kupunguza wimbi kubwa la uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.


Share:

Tanzania Na Kenya Wakubaliana Kuzipatia Ufumbuzi Changamoto Za Kupima Corona Wasafiri


 Na.WAMJW-Nairobi
Tanzania na Kenya wamekubaliana ndani ya  wiki nne zijazo kufanyia kazi changamoto kubwa nne katika eneo la kupima wasafiri UVIKO 19.
 
Makubaliano hayo yamefanyika jana kwenye mkutano wa pamoja baina ya Mawaziri wa Afya wa Tanzania Dkt. Dorothy Gwajima na Waziri wa afya nchini Kenya Sen. Mutahi Kagwe mjini Nairobi.
 
Moja ya makubaliano ya kufanyia kazi changamoto hizo ni pamoja na kushusha gharama za upimaji wa UVIKO-19 kwa wasafiri wanaoingia na kutoka katika nchi hizo mbili ili kuchochea masuala ya biashara na utalii baina na nchi hizo mbili.
 
Nchi hizo pia zimekubaliana kufanyia kazi changamoto ya kulipisha fedha kipimo cha haraka cha Corona (PCR) kwa wasafiri wanaotumia njia ya barabara ikiwemo kuona uwezekano wa kushusha kwa kiasi kikubwa gharama hizo kwa wasafiri  wanaotumia ndege.
 
Kwa upande wa madereva wanaosafirisha mizigo na bidhaa muhimu  wamekubaliana kufanyia kazi uwezekano wa kutokutozwa gharama kwa kipimo cha Corona ili kupunguza mzigo kwa wasafirishaji ikiwa ni njia ya kuchochea uchumi kwa nchi hizo mbili.
 
Aidha Tanzania na Kenya wamekubaliana kuona uwezekano wa kutumia mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya kufuatilia afya za wasafiri pamoja na  kudhibiti wasafiri wasio kuwa waaminifu kwa  kugushi vyeti hivyo wanapopita mipakani.
 
Hata hivyo katika mkutano huo Mawaziri hao wamekubaliana kufanyia kazi mpango wa kuvitambua vyeti vya  upimaji vinavyotolewa na mamlaka za afya za nchi hizo mbili, pamoja na kubadilishana taarifa zinazohusu masuala ya afya ili kuimarisha udhibiti wa magonjwa mbalimbali yanayowaathiri wananchi wa pande hizo mbili ikiwemo Malaria, Polio na Corona.
 
Akiongea wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari Waziri wa Afya Dkt. Gwajima amesema kuwa tatizo la ugonjwa wa Corona ni la dunia nzima hivyo lazima  kuangalia ni namna gani halitowadhuru sana ili uchumi na ustawi wa jamii na nchi uendelee kwa kuweka makubaliano ya kuishi kwa Amani kama watu wanaoishi katika kijiji kimoja cha afrika mashariki.
 
Dkt. Gwajima amesema ugonjwa huo uliowafika hauwezi kuwaacha iwapo kutakuwa hakuna suluhu ya pamoja ya kuudhibiti kwani hadi sasa ugonjwa huu umetufundisha mengi na viongozi wa nchi zote mbili wamekuwa wakitoa maono mengi. Hivyo, kama Mawaziri wenye dhamana kwa kushirikiana na wataalam watahakikisha wanatafsiri dhamira ya viongozi wakuu wa nchi ili kuja na uhalisia.
 
Aliongeza kuwa janga hilo ni kubwa hivyo ni lazima kuendelea kushirikiana katika kudhibiti  na kuzuia anuai mpya za ugonjwa wa Corona kwa pamoja kwani miundombinu ya uchumi inashuka katika nchi zetu na kwa jamii pia.
 
“Baada ya kutokea janga hilo wasafiri na madereva walikua wanatakiwa kuendelea kusafirisha abiria,mizigo na bidhaa muhimu hivyo kubwa ni lazima kuweka jitihada ili kuwarahisishia wananchi kuendelea na shughuli za uchumi na maisha kwa usalama kwa ushirikiano baina ya nchi zetu hizi”.
 
Naye Waziri wa Afya nchini Kenya Sen.Mutuhi Kagwe  amesema kwamba Tanzania na Kenya ni majirani wa muda mrefu  hivyo vyovyote watakacho fanya hawawezi  kuwaacha majirani zao ambao ni Tanzania.
 
Katika kukabiliana na Corona Waziri Kagwe amesema lazima kujifunza kuishi nao  hivyo ni jambo la kuelewa kwamba hakuna nchi itakayokuwa na nguvu bila kushirikiana.
 
 “Sisi ni wamoja lazima tuendelee kujisaidia wenyewe Katika mapambano haya na vile vile kwenye Malaria,Polio kwa wananchi wetu mipakani” Alisisitiza.
 
Aliongeza kwamba nchi hizo mbili zina mashirikiano ya muda mrefu  katika maeneo  na sio tu masuala ya afya tu, hivyo wataimarisha ushirikiano hata katika maeneo mengine.


Share:

TBS Yakusanya Bilioni 3.9 Katika Zoezi La Ukaguzi Wa Magari Bandarini Yanayotoka Nje Kwa Mwezi Aprili Mpaka Agosti.

 Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amesema Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekusanya takribani Shilingi Bilioni 3.9 katika zoezi la ukaguzi wa magari bandarini yanayotoka nje ya nchi katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Agosti 03, 2021 na kuokoa kiasi cha shilingi Bilioni 2.7 ambayo kwa utaratibu wa zamani, TBS kwa niaba ya Serikali tungepata asilimia 30 pekee ya fedha hizi na asilimia 70 ingebaki nje ya nchi.

Prof. Mkumbo ameeleza hayo  Agosti 05, 2021 wakati alipoambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah kutembelea Bandari kuu ya Dar es salaam kwenye kitengo cha ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini unaofanywa na TBS na kujionea shughuli zinavyoendelea.

Aidha, Prof Mkumbo amesema TBS inaendelea kuboresha zoezi na utaratibu wa ukaguzi wa magari yanayoingizwa hapa nchini ambapo mpaka agosti 03, 2021 yamekaguliwa magari 11,079, kati ya m hayo 7,700 yalikidhi ubora na magari yaliyobaki yalikwenda kutengenezwa na kati yake magari 1,890 yaliweza kukidhi ubora baada ya matengenezo na mengine yaliyobaki yapo gereji yakiendelea kurekebishwa.

 “Kwa kuamua kutekeleza mpango huu, Serikali inaokoa fedha nyingi ambazo zingebaki nje hivyo kwa kipindi cha miezi minne tumekusanya takribani Bilioni 3.9 na fedha hii inaingia katika mfuko mkuu wa Serikali”. Amesema Prof.Mkumbo.

Pamoja na haya Prof. Kitila Mkumbo ametoa wito kwa wananchi wanaoagiza magari na wafanyabishara wanaofanya biashara hiyo kuendelea kuunga mkono utaratibu huo mzuri na kutoa ushirikiano kwa TBS na pale ambapo kuna upungufu waendelee kutoa maoni kama ambavyo wamekuwa wakifanya na Serikali kupitia TBS iweze kuyafanyia kazi, wakati huo huo ameipongeza TBS na wafanyakazi wote kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya hapo bandarini.

“Mapema mwaka huu Serikali ilianzisha utaratibu wa kukagua magari yote yanayoingizwa nchini yakaguliwe hapa na TBS ndio iliyokabidhiwa majukumu hayo, leo nimepata nafasi ya kukagua na kujionea kazi inavyoendelea katika vituo vyetu viwili na nimefurahi kuona zoezi hili linaendelea kuimarika” ameleza Waziri Prof. Kitila Mkumbo.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukaguzi wa Bidhaa kutoka Nje ya Nchi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mhandisi Said Mkwakwa amesema, lengo la ukaguzi wa magari yaingiayo nchini unaofanywa na TBS ni kuhakikisha magari yote yaliyotumika yanakaguliwa ili kubaini ubora wake na kazi hiyo waliianza tangu tarehe 15 Aprili, mwaka huu.

Kuanzia tarehe 01 Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi ulianza kufanyika baada ya magari hayo kuwasili nchini (Destination Inspection) ambapo waagizaji wote walitakiwa kupeleka maombi TBS na si kwa mawakala kama ilivyokuwa hapo awali.



Share:

Dr. Gwajima: Tulihimiza Matumizi Ya Tiba Asili Kwa Sababu Hapakuwa Na Njia Nyingine Ya Kupambana Dhidi Ya Corona

 Na WAMJW- Nairobi

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania ilihimiza matumizi ya tiba asili wakati wa mlipuko wa wimbi la kwanza la Corona kwa kuwa zilionesha kuwasaidia watu wengi kwenye kipindi hicho ambapo Dunia haikuwa na njia mbadala yoyote ya kupambana dhidi ya Corona ukilinganisha na uwepo wa chanjo katika kipindi hiki.

Dkt. Gwajima amesema hayo wakati akiongea na Waandishi wa habari wa nchini Kenya ambapo wamefanya mkutano wa pamoja wa kujadili changamoto zinazowakabili nchi hizo mbili ikiwemo ya UVIKO-19 kwa upande wa mipakani.

“Ugonjwa huu uliingia Wuhan nchini China Disemba 2019, wakati Dunia ilikuwa haielewi ifanye nini, Dunia nzima ilikuwa haina chanjo, haina formula ya dawa, haielewi ifanye nini kwa mfano; wakati huo nyoka ameshaingia ndani na wewe ndio mama na Watoto wamekuzunguka na nyoka yupo mlangoni, inatakiwa unapigana kwa mwiko kwa kummwagia uji au kwa chochote na ndivyo ilivyokuwa ” alisema

Aliendelea kusema kuwa, Tiba asili Kwa upande wa Tanzania lipo Baraza la kitaalamu kisheria ambayo imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kiasi kikubwa zimeonesha kusaidia watu wenye matatizo ya kifua kwa kuona umuhimu katika mapambano hayo ilikuwa ni muhimu kutumia tiba hizo ili kunusuru maisha ya Watanzania.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema kuwa, Tiba asili zilikuwepo toka zamani kabla ya dawa nyingine hazijaja, na zilisaidia kutibu magonjwa mengi, hata katika vita dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona kwenye wimbi la kwanza tiba asili ilionesha mafanikio makubwa sana.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa, licha ya kutumia tiba asili katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona, Serikali ilihimiza wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga nyingine ikiwemo kufanya mazoezi, kula chakula bora (lishe bora), kuvaa Barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuepuka misongamano isiyo yalazima.




Share:

Mbowe na Wenzake Wafikishwa Mahakamani


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukiwa na ulinzi mkali.

Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo saa leo Ijumaa, Agosti 6, 2021  wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.


Share:

Administrative Assistant at IRMCT

Administrative Assistant, FS-4   Org. Setting and Reporting This position is located in the Office of the Prosecutor of the International Residual Mechanism for Criminal Tribunals (IRMCT), Arusha Branch. The incumbent will work under the supervision of the Senior Trial Attorneys. *Appointment of the successful candidate to this position will be subject to budgetary approval. […]

This post Administrative Assistant at IRMCT has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Production Scheduler at Diageo

Production Scheduler     Job Description : About Us Diageo’s performance ambition is to become the most trusted and respected CPG; our “must dos” set out where we aim to win in order to achieve this aspiration. Within Supply Chain this translates into goals that aim to deliver world class performance at best cost, drive value […]

This post Production Scheduler at Diageo has been posted by Udahiliportaldaily

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger