Monday, 26 July 2021

United African University of Tanzania UAUT Prospectus 2021/2022

United African University of Tanzania UAUT Prospectus 2021/2022: Prospective students at the United African University of Tanzania – UAUT have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details […]

This post United African University of Tanzania UAUT Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

St. Joseph University In Tanzania SJUIT Prospectus 2021/2022

St. Joseph University In Tanzania SJUIT Prospectus 2021/2022: Prospective students at the St. Joseph University In Tanzania – SJUIT have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details […]

This post St. Joseph University In Tanzania SJUIT Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

St John’s University of Tanzania SJUT Prospectus 2021/2022

St John’s University of Tanzania SJUT Prospectus 2021/2022: Prospective students at the St John’s University of Tanzania – SJUT have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details […]

This post St John’s University of Tanzania SJUT Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Muslim University of Morogoro MUM Prospectus 2021/2022

Muslim University of Morogoro MUM Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Muslim University of Morogoro – MUM have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about MUM […]

This post Muslim University of Morogoro MUM Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

University of Arusha UOA Prospectus 2021/2022

University of Arusha UOA Prospectus 2021/2022: Prospective students at the University of Arusha – UOA have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about UOA Prospectus 2021/2022, […]

This post University of Arusha UOA Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Mwalimu Julius K. Nyerere University of Agriculture and Technology MJNUAT Prospectus 2021/2022

Mwalimu Julius K. Nyerere University of Agriculture and Technology MJNUAT Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Mwalimu Julius K. Nyerere University of Agriculture and Technology – MJNUAT have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the […]

This post Mwalimu Julius K. Nyerere University of Agriculture and Technology MJNUAT Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Tumaini University Makumira TUMA Prospectus 2021/2022

Tumaini University Makumira TUMA Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Tumaini University Makumira – TUMA have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about TUMA Prospectus 2021/2022, […]

This post Tumaini University Makumira TUMA Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Sokoine University of Agriculture SUA Prospectus 2021/2022

Sokoine University of Agriculture SUA Prospectus 2021/2022: Prospective students at the Sokoine University of Agriculture – SUA have been very anxious to search for information about the respective college, such as information on the courses they are going to study in each semester of the year. Knowing this we have prepared full details about SUA […]

This post Sokoine University of Agriculture SUA Prospectus 2021/2022 has been posted by Udahiliportal

Get more post by visiting Udahiliportal.com

know more details about Udahiliportal.com by visiting Udahiliportal.com - Find Jobs & Ajira mpya leo, ajira portal Tanzania, ajira yako, brighter Monday, mabumbe, mwananchi ajira, secretariet ya ajira, tamisemi ajira za afya, wizara ya afya, ajira Tanzania - selection za vyuo , selection, second selection vyuo, second selection, tamisemi selection, selection form one 2020/2021

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

Share:

Simbachawene: Tutadhibiti Vipenyo Vya Kupitisha Magendo Mipakani

 Na Felix Mwagara, MOHA, Moshi.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema serikali itavidhibiti vipenyo zaidi ya 300 vilivyopo katika Mpaka wa Tanzania na Kenya, katika maeneo ya Holili na Tarakea Wilayani Rombo, Mkoa wa Kilimanjaro.

Amasema uwepo wa vipenyo hivyo kumesababisha Serikali kupoteza mapato mengi kwasababu wanaopitisha magendo utumia njia hizo zisizo halali kupitisha bidhaa mbalimbali kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Waziri Simbachawene ameyazungumza hayo jana, katika kikao na Maafisa wa Taasisi mbalimbali wanaofanya kazi katika mipaka hiyo, baada ya kumaliza kukagua na kusikiliza taarifa zao kutoka kwa Taasisi zote katika mipaka hiyo.

“Hili jambo halikubaliki, lazima lifanyiwe kazi, nimelipokea ila naomba mjue kuwa kati ya mambo ya msingi kama nchi ni kudhibiti mipaka, huwezi kuwa na nchi alafu watu wanaingia na kutoka wanavyotaka, haiwezekani, lazima nikae na Mawaziei wenzangu pamoja na Makatibu Wakuu tuone jambo hili tunalidhibiti vipi,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa uwepo wa vipenyo zaidi ya 300, ni vingi sana ila lazima vidhibitiwe kwa kuharibiwa kwasababu Serikali inapoteza mapato mengi na kamwe jambo hilo halitapuuzwa.

“Suala hili ni la msingi katika maendeleo ya nchi, hivyo siwezi fanya maamuzi peke yangu, naomba niseme kuwa hii taarifa nimeipokea, na nitaipeleka kwa viongozi ili tuone tunafanyaje katika kudhibiti hivi vipenyo, ili watu wapite katika njia halali na zinazoeleweka na kwa hatua hiyo Serikali iweze kupata mapato.”Alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Mfawidhi wa Uhamiaji Kituo cha Holili, Eliaichi Marandu, alimwambia Waziri Simbachawene kuwa, Mpaka huo unakabiliwa na changamoto ya uwepo wa vipenyo vingi visivyo rasmi hali ambayo inawafanya kushindwa kudhibiti suala la magendo mpakani licha ya kuwa wanajitahidi mara kwa mara kufanya doria.

“Mheshimiwa Waziri, vipenyo hivi ambavyo vipo katika maeneo mbalimbali, yakiwemo ya Kamwanga, Rongai hadi mpaka wa Holili, vipo zaidi ya 300 na ni vikubwa hata magari makubwa yanaweza kupishana, hivyo kuwepo na vipenyo hivi kuna kuwa vigumu kudhibiti licha ya kuwa tunajitahidi kufanya dori.,"Alisema Eliaichi.

Hata hivyo, licha ya changamoto katika mipaka hiyo, lakini kwa upande wa Mpaka wa Tarakea wamevuka kiwango cha ukusanyaji wa mapato ambapo kuanzia mwezi Julai mwaka 2020,

kituo cha Tarakea kilitarajiwa kukusanya shilingi bilioni 13 lakini ilipofika mwezu Juni mwaka huu 2021, kituo hicho kilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 15.

Waziri Simbachawene amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kilimanjaro, na Jumatatu Julai 26, 2021 anatarajia kuanza ziara ya Mkoani Arusha ya kukagua utendaji kazi wa Taasisi zake pamoja na miradi mbalimbali.



Share:

Viwanja 594 Vyapimwa Kuzunguka Hospitali Ya Kanda Ya Kusini

 


Na Munir Shemweta, MTWARA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amesema Wizara yake imepima viwanja 594 katika eneo linalozunguka hospitali ya Rufaa ya Kanda ya kusini na kumilikishwa kwa wananchi.


Akizungumza wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika hospitali ya Kanda ya Kusini uliofanywa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango leo tarehe 26 Julai 2021, Dkt Mabula alisema, pamoja na ujenzi wa Hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa huduma za kitabibu, wizara ya Ardhi  iliona umuhimu wa kupima viwanja eneo hilo na kumilikisha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi na shughuli nyingine.


“Mhe Makamu wa Rais pamoja na ujenzi wa hospitali hii uliofanywa na Shirika letu la  nyumba la Taifa, wizara imepima na kumilikisha jumla ya viwanja 594 kuzunguka hospitali hii ili kuwezesha wananchi kujenga nyumba za makazi na shughuli nyingine” alisema Dkt Mabula.


Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, NHC imekuwa ikifanya kazi nzuri katika miradi mbalimbali na ujenzi wa hospitali ya Kanda ya kusini itakayohudumia mikoa ya Mtwara, Ruvuma na Lindi ni moja ya miradi mikubwa ya kimkakati iliyotekelezwa na shirika hilo.
Dkt Mabula alisema, mradi mwingine wa kimkakati unaojengwa na shirika la NHC ni ule wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara iliyopo eneo la Kwangwa sambamba na miradi ya ujenzi wa  nyumba na ofisi za Wakala wa huduma za misitu (TFS).


Aidha, Naibu Waziri Mabula alimuomba Makamu wa Rais kulisaidia Shirika kupatiwa miradi ya ujenzi na Taasisi za Serikali kwa kuwa Shirika hilo kwa sasa liko imara na linao uwezo wa kujenga miradi ya ujenzi iliyo na ubora wa hali ya juu.


Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango  alilipongeza Shirika la Nyumba la Taifa kwa ujenzi wa jengo hilo alilolieleza kuwa lina ubora usio na mashaka.


Alizitaka Taasisi za Serikali zenye miradi ya ujenzi kutoa kupaumbele kwa NHC katika ujenzi wa miradi yake na kulitaka Shirika la Nyumba la Taifa kuzingatia ubora wakati wa utekelezaji miradi sambamba na  kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na vifaa vya ujenzi kwenye miradi hiyo vinatoka nchini Tanzania.


Alilitaka shirika la Nyumba kukamilisha ujenzi wa mradi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini kwa wakati kama lilivyoahidi na kusisitiza kuwa, ujenzi wa hospirali hiyo ukamilike kwa wakati na kufikia Oktoba mwaka huu wananchi waanze kupata huduma.



Share:

JAMAA ANAYEDAIWA KUTAKA KUMCHOMA KISU RAIS WA MALI AFARIKI DUNIA

Mwanaume anayetuhumiwa kujaribu kumdunga kisu rais wa mpito wa Mali, Assimi Goïta, wiki iliyopita msikitini amekufa hospitalini akiwa chini ya ulinzi, serikali inasema.

Mshambuliaji huyo, ambaye hajatambuliwa, alikamatwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio lake, ambalo lilifanyika wakati Bwana Goïta akihudhuria sala katika msikiti.

Taarifa ya serikali ilisema afya ya mtu huyo ilikuwa imezorota akiwa chini ya ulinzi na alipelekwa hospitalini, ambako alikufa.Sababu ya kifo chake inachunguzwa .Bwana Goïta ameongoza mapinduzi mawili nchini Mali katika mwaka uliopita.


Share:

PROF. MANYA ATEMBELEA BANDA LA EXIM BANK MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA


Kaimu Meneja  wa Benki ya Exim (T) Ltd Tawi la Shinyanga, Bi. Sarah Paul Tito (kulia) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa katika Benki ya Exim kwa Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa kwanza kushoto)  alipotembelea banda la Exim Bank wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumapili Julai 25,2021.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Kaimu Meneja  wa Benki ya Exim (T) Ltd Tawi la Shinyanga, Bi. Sarah Paul Tito (kulia) akitoa maelezo ya huduma zinazotolewa katika Benki ya Exim kwa Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (wa kwanza kushoto) alipotembelea banda la Exim Bank wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumapili Julai 25,2021.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Soma pia:
Share:

KEVELA AVITAKA VYAMA VYA UPINZANIA KUACHA CHOKOCHOKO, WATULIE


Mwenyekiti  wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe (UWT) Scolastika Kevela.
***
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe (UWT) Scolastika Kevela amevitaka vyama vya upinzani kuacha kuleta chokochoko nchini kwa kigezo cha kutaka katiba mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kevela ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, alisema Rais Samia Suluhu Hassan alishatolea ufafanuzi suala hilo kwa kusema kuwa apewe muda hivyo wanapaswa kutulia. 

Alisema kauli hiyo ya Samia ilipaswa kuheshimiwa na kupokelewa kwa mtazamo chanya na wananchi wote hususani wale  wanaoleta chokochoko hususani wapinzani hao ambao muda mwingi wamekuwa wakianzisha wakitafuta sababu za kuanzisha chokochoko.

"Rais Samia aachwe afanye kazi yake tuliyomtuma wananchi wananchi kwa mujibu wa katiba, ndiyo kwanza uongozi wake una miezi minne madarakani, hizi kelele za wanaotaka katiba zinatolewa kwa lengo la kutaka kumtoa katika reli ya kuwatumikia watanzania", alisema Scolastika.

Aidha alisema anashangazwa na wapiga kelele hao kuanza kujitokeza kwa wingi na kuleta chokochoko hizo ndani kipindi hilo kifupi cha uongozi wa Rais Samia tofauti  hali ya kuwa kabla yake kulikuwa na kiongozi mwingine katika nafasi hiyo lakini hawakuthubutu kufanya hivyo.

"Mimi kama Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Njombe nalaani chokochoko hizo na zaidi nawaomba watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii kuendelea kuunga mkono juhudi anazozifanya Rais wetu kutuletea maendeleo Watanzania wote" ,alisema Scolastika.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huo amempongeza Rais Samia  kwa juhudi mbalimbali anazoendelea kuzichukua katika kuhimarisha mahusiano ya kidiplomasia na mataifa mengine duniani 

Alisema kitendo cha Rais huyo kukutana na viongozi kutoka mataifa mbalimbali na wakati mwingine kufanya ziara katika mataifa hayo, kunaonyesha dhamira yake ya kushirikiana na mataifa hayo katika masuala mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa uchumi. 
Share:

FISI ASABABISHA KIFO CHA MTOTO, AJERUHI WATATU


 Na Lucas Raphael Tabora
Katika hali isiyokuwa ya kawaida fisi aliingia ndani ya nyumba na kumnyakua mtoto  wa mwaka mmoja na kisha kukimbia naye na kumjeruhi vibaya kisha  kumsabishia kifo huku akiwajeruhi watu watatu na mmoja amelezwa katika hospital ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tabora kamishna Msadizi Safia Jongo Akizungumzia tukio hilo alisema lilitokea julai 25 mwaka huu majra ya saa 9 usiku katika kijiji cha kangeme kata ya Zungimlole wilaya ya Kaliua Mkoa Tabora

Alisema kwamba Tukio hilo limetokea katika hifadhi ya Luganzo Tongwe Kijiji cha Kangeme kata ya Zugimlole wilaya ya kaliua mkoani hapa ambapo  fisi huyo alitoka hifadhini na kuingia ndani ya nyumba ya Nhganya Mayala (45) muda wa majira ya saa 9 usiku na kumchukua Mtoto na kumjeruhi vibaya jambo lililosababisha kifo chake.

Alisema kwamba  watu watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto hiyo walijeruhiwa walipojaribu kumshambulia fisi huyo.

“Baadhi ya wananchi waliposikia lile tukio na katika hali ya kupambana na yule fisi aliweza kuwajeruhi watu watatu na wamejeruhiwa vibaya na mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora kitete kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi”alisema  

Aliongeza kuwa baadae askari polisi wakishirikiana na maafisa wanyamapori walienda kukagua tukio na kuona hali ikoje fisi huyo tena aliibuka na kuanza kuwashambulia askari na watu waliokuwa wakitoa taarifa kwa askari

“Askari walipambana na kufanikisha kumuua huyo fisi lakini katika mapambano hayo risasi 49 zimepotea kwa kumpiga tu ”aliongeza kamanda jongo

Kwa upande wao baadhi wa wananchi wa kijiji cha Kangeme kata ya Zugimlole walisema kuna idadi kubwa ya fisi katika eneo la hifadhi hiyo .

Waliendelea  kusema kwamba wameingiwa na  hofu kutoka na hali ya hatari kuanza kujitokeza na kuwaomba maafisa wanyamapori kufanya dolia za mara kwa mara kuzungukia katika hifadhi hiyo.

Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi safia jongo aliwataja watu waliojeruhiwa ni baba wa mtoto huyo ni Nganya Mayala 45 ambaye kang’atwa kingaja cha mkono wa kulia,Ngezi Lega 25 kang’atwa mkono wa kushoto na paja na Tule Malongo miaka 45 aliyevunjwa taya na kung’atwa mkono wa kushoto ambaye amelazwa katika hospitali Rufaa ya mkoa wa Tabora kitete.

mwisho

Share:

BENKI MPYA YA TCB YASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA...WAANIKA HUDUMA ZAO KABAMBE


Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso akielezea huduma zinazotolewa na Benki ya TCB kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso (katikati), Afisa Masoko wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Lupiana David (kulia) na Afisa wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga, Theodat Mahuvi wakionesha vipeperushi vinavyoelezea huduma zinazotolewa na Benki ya TCB.
Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso (katikati), Afisa Masoko wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Lupiana David (kulia) na Afisa wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga, Theodat Mahuvi wakionesha vipeperushi vinavyoelezea huduma zinazotolewa na Benki ya TCB.
Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso (katikati), Afisa Masoko wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Lupiana David (kulia) na Afisa wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga, Theodat Mahuvi wakionesha kwa ishara kauli mbiu ya Benki ya TCB 'Tanzania Commercial Bank Growing Stronger Together'.
Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso (katikati), Afisa Masoko wa Benki ya TCB Tawi la Shinyanga Lupiana David (kulia) na Afisa wa Benki ya TCB tawi la Shinyanga, Theodat Mahuvi wakionesha kwa ishara kauli mbiu ya Benki ya TCB 'Tanzania Commercial Bank Growing Stronger Together'

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Benki Mpya ya Serikali ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC) tawi la Shinyanga imeshiriki Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kutangaza muonekano wao mpya kutoka iliyokuwa Benki ya TPB na sasa Benki ya TCB.

Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayoongozwa na kauli mbiu “Uwekezaji wa Madini na Viwanda Shinyanga kwa Uchumi Endelevu” yameanza tarehe 23 Julai, yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 1 Agosti, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Meneja wa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC), Tawi la Shinyanga Julius Mataso amesema wanashiriki maonesho hayo kama wadau wa biashara na taasisi ya fedha wezeshi ya biashara katika mkoa wa Shinyanga.

“Tumeshiriki maonesho haya kwa ajili ya kujitangaza muonekano wetu mpya kutoka iliyokuwa Benki ya TPB na kuwa Benki ya Biashara ya Tanzania (Tanzania Commercial Bank- TCB PLC”,amesema Mataso.

“Kufuatia mabadiliko haya tunapenda kuwataarifu wateja wetu na Watanzania kwa ujumla kuwa tumebadilisha muonekano wa Nembo na jina la Benki. Mabadiliko haya yanaenda sambamba na kuboresha huduma zetu ili kukidhi kiu ya Wateja wetu na Watanzania kwa ujumla na kwa kutoa huduma za viwango vya hali ya juu",amesema Mataso.

“Miongoni mwa huduma tunazozitoa na tulizozifanya kuwa rafiki zaidi kwa wateja ni pamoja na huduma ya bima ya maisha ambapo kila mteja wetu aliye na akaunti kwenye benki ya TCB anakuwa na sifa ya kupata huduma ya bima ya maisha ambapo tunatoa mkono wa pole kwa mteja anapofiwa na mtegemezi (mme, mke au watoto wasiozidi  umri wa miaka 18) au yeye mwenyewe anapofariki dunia. Hii faraja tunaitoa kwa kiasi cha shilingi milioni 2”,amesema.

Ameeleza kuwa ili kupata bima ya maisha kupitia Benki ya TCB hakuna haja ya kujaza fomu ya kujiunga kwani ukishakuwa tu akaunti ya TCB basi unakuwa tayari na sifa za kupata huduma hiyo.

Ameongeza kuwa bima hiyo ya maisha pia wanaitoa kwa wanachama walio ndani ya vikundi mbalimbali vilivyojiunga kwa ajili ya kusaidiana katika masuala ya kijamii.

“Lakini pia katika Benki ya TCB tunatoa huduma za bima za mali kama vile magari, nyumba n.k”,amesema.

Aidha amewaomba Watanzania kuchangamkia huduma ya Akaunti ya Muda Maalumu ‘Fixed Depost Account’ inayotolewa katika Benki ya TCB ambayo wanatoa riba ya asilimia 11 kwa mwaka.

Amezitaja huduma zingine ni pamoja na huduma ya mikopo ya aina mbalimbali kama vile mikopo ya watumishi, wastaafu, wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa. Huduma zingine ni huduma ya kutuma na kupokea fedha ya Western Union.

“Tunawakaribisha Wana Shinyanga na Watanzania kwa ujumla kuja kupata huduma za kifedha katika benki yetu kwenye matawi yetu yaliyotapakaa nchi nzima. Tunawaahidi kuendelea kutoa huduma nzuri na bora”,amesema Mataso.

Soma pia:
Share:

Mwongozo Wa Udhibiti Wa Ugonjwa Wa Korona (Uviko-19) Kupitia Afua Ya Kuthibiti Misongamano Katika Jamii Bila Kuathiri Shughuli Za Kiuchumi


1. Utangulizi

Kutokana na mwenendo wa ugonjwa wa corona (UVIKO-19) nchini, Kamati ya Wataalamu imeainisha maeneo mahususi yanayohitaji kutiliwa mkazo kupitia afua za kupunguza msongamano katika jamii. 

Lengo ni kukata mnyororo wa maambukizi katika ngazi ya kaya na jamii. Mwongozo huu utawawezesha Wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi na kijamii sambamba na kubadili tabia zao huku wakizingatia mbinu za kujikinga na ugonjwa, kwa kupata elimu ya kutosha, na kujiwekea utaratibu wa kudhibiti ugonjwa kutokusambaa kwenye jamii. Wananchi tayari wamepokea mbinu hizi kwa mtazamo chanya lakini zinahitaji kuimarishwa bila kulega lega ili jamii iweze kujikinga, kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa UVIKO-19.


2. Kusitisha mikusanyiko mikubwa isiyokuwa ya lazima.
Mwongozo huu unasitisha mikusanyiko yote mikubwa ya kijamii, kidini na kisiasa mpaka ugonjwa utakapo dhibitiwa na kutolewa taarifa rasmi na Wizara ya Afya. Pale ambapo patakapohitajika ulazima wa kufanyika shughuli ya Mikusanyiko, kibali kiombwe kuanzia ofisi za serikali za mitaa, kupitia Halmashauri na idhini itolewa na Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa husika, kwa kuzingatia vigezo vyote vya kinga na usalama wa afya kwa wananchi.


3. Udhibiti wa mikusanyiko katika maeneo mbalimbali.

Maeneo yanayoleta mikusanyiko ni yale ya huduma za Kijamii, Kibiashara, Kiuchumi, Kiofisi n.k ambayo ni mojawapo ya vyanzo vya kusambaa kwa maambukizi katika jamii. Mwongozo huu unalenga kudhibiti ugonjwa huu bila kuathiri shughuli za kiuchumi na maisha ya kawaida ya kijamii ya wananchi. Baadhi ya maeneo hayo ni kama ifuatavyo: -


3.1.1 Vyombo vya Usafiri na Stendi za Mabasi/Daladala/Bodaboda
Ugonjwa wa Corona (UVIKO-19) unaweza kusambazwa kupitia vyombo vya usafiri hivyo hatua zifuatazo hazina budi kuendelea kuchukuliwa;


a) Kuhamasisha na kusimamia kuepuka msongamano na kuzingatia kukaa umbali wa zaidi ya mita moja kati ya mtu na mtu kama kuna uwezekano huo.

i. Wasafiri wawezeshwe kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka kabla ya kuingia kwenye vyombo vya usafiri hivyo, viongozi wa mtaa husika wahakikishe kuna vyombo vya kuhifadhia maji na sabuni vya kutosha katika kila kituo. Aidha, uongozi wa vituo vya mabasi usimamie uwepo wa vifaa vya kunawia kwa maji tiririka na kuhakikisha abiria wote wananawa mikono.
ii. Wamiliki wa vyombo vya usafiri wahakikishe wanaweka vipukusi vya kutakasa mikono katika vyombo vya usafiri.
iii. Kila msafiri anayeingia kwenye chombo cha usafiri wa umma lazima awe amevaa barakoa kama ilivyoelekezwa kwenye mwongozo isipokuwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 8.
iv. Abiria wote waendelee kuelimishwa kuhusu umuhimu wa kutosongamana ndani ya vituo vya Mabasi kupitia walinzi getini, wahudumu wa mabasi na askari wa usalama wa barabarani.
v. Bodaboda wabebe kwa idadi sahihi (1-2) (siyo mishikaki) na wavae barakoa
vi. Stendi zihakikishe zinatoa ujumbe wa kuelimisha jamii ya wasafiri mara kwa mara kupitia vipaza sauti, na wanapokuwa safarini, madereva na wahudumu wa vyombo vya usafiri wahakikishe ujumbe wa kuelimisha unatolewa kwenye chombo mara kwa mara.
vii. Wananchi wakae au kuongozana kwa umbali wa zaidi ya mita moja katika maeneo yote wanayokuwepo kabla ya kuingia kwenye chombo cha usafiri.
viii. Vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe magari ya usafiri wa umma wanapakia abiria kulingana na idadi ya viti pasipo kusimama; kwa magari maalumu yenye nafasi kubwa kama mwendokasi, inapolazimika kusimama basi kila abairia avae Barakoa na kuachiana angalau umbali wa nusu mita.


b) Upimaji wa dalili za ugonjwa wa Korona (UVIKO-19) na taratibu getini wakati wa kuingia /kutoka ndani ya Mabasi.
i. kupima joto mwili kwa kutumia ‘thermoscanners’ ufanyike getini na kwenye mabasi.
ii. Halmashauri zisimamie maeneo yote ya mabasi yaendayo Mikoani yaanzishe utaratibu wa uchunguzi wa wasafiri, na wale watakaoonesha dalili (ambazo zimeainishwa na Wizara ya Afya) wasiruhusiwe kuendelea na safari badala yake washauriwe kwenda kuonana na wahudumu wa afya.
iii. Magari yote yabandikwe namba ya simu ya dharura (199) itakayosaidia wasafiri wenye dalili za UVIKO-19 kupatiwa msaada muda wowote na mahali popote.
iv. Maafisa wa Usalama Barabarani wafanye ukaguzi wa kushtukiza kuhakikisha uzingatiaji wa maagizo haya ikiwemo utoaji wa jumbe za UVIKO-19.


c) Utaratibu Katika Nyumba za Ibada
Nyumba za ibada zikaguliwe mara kwa mara na kuhakikisha zinazingatia yafuatayo;
i. Ziweke vifaa vya kunawia mikono (maji safi tiririka na sabuni au Vitakasa mikono-Sanitizers) na muumini atakaye simamia unawaji kwa wote.
ii. Waumini wavae Barakoa
iii. Waumini wakae umbali unaozidi mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine pande zote.
iv. Taratibu za kufanya usafi na utakasaji wa viti, meza na maeneo wanapokaa kabla na baada ya ibada ufanyike. Alama katika viti ziwekwe kuonyesha umbali wa mita moja.
v. Wazee, Watoto na wale wote wenye matatizo ya kiafya yanayotambulika (Mfano. Kisukari, Shinikizo la Damu, Kansa n.k), wanashauriwa kujiepusha na ibada zenye mikusanyiko ya Watu wengi na wachukue tahadhari zote muda wote
vi. Kama nyumba ya ibada ni ndogo uanzishwe utaratibu wa kusalia nje/maeneo ya wazi au kuongeza idadi ya vipindi vya ibada na kuruhusu idadi ya watu wachache kuingia ibadani na kuzingatia uvaaji wa Barakoa.
vii. Ibada ziwe za muda mfupi usiozidi masaa mawili.
viii. Huduma zinazohusisha kugusana ziepukwe
ix. Kuwepo na ujumbe wa mara kwa mara kwa ajili ya kuwakumbusha waumini kuhusu namna ya kujikinga na UVIKO-19 na namba za kuwasiliana na huduma za afya iwapo atapatikana mgonjwa.


d. Maeneo ya Baa, Migahawa, Hoteli, Kumbi za Starehe, Mikutano, Harusi na Sherehe mbalimbali
Kimsingi baadhi ya shughuli za kundi hili zinafaa kuangaliwa iwapo ni muhimu? Lazima au zisubiri hali itengamae. Iwapo ni muhimu na lazima mambo yafuatayo hayana budi na ni lazima yazingatiwe;
i. Kuwe na kipima joto kwa wote wanaoingia kupata huduma kwenye eneo husika.
ii. Wamiliki au Waandaaji wa mikutano waweke vifaa vya kunawia mikono maji tiririka na sabuni vinavyotosheleza mahitaji au kutumia vipukusi
iii. Wateja /washiriki wakae umbali wa mita moja kutoka mteja hadi mteja.
iv. Ili kupunguza msongamano usio wa lazima, wateja washauriwe kununua vinywaji na kunywea nyumbani.
v. Sherehe zote za harusi kufanyika nje ya kumbi (open air) au kama zinafanyika ukumbini, ziwe za muda fupi, wageni waalikwa wawe wachache kuruhusu ukaaji wa mita moja au zaidi.
vi. Washiriki wote wa sherehe za harusi/Mikutano wavae barakoa.
vii. Wamiliki wahakikishe wanaweka walinzi na kuhakikisha kila anayeingia kwenye maeneo haya anavaa barakoa na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
viii. Kwenye mikutano ya ofisi za Umma, waraka/barua toka wizara ya utumishi ya 15 Mei, 2020, iendelee kuratibu utendaji wa watuimIshi katika kujikinga na UVIKO-19.
ix. Wamiliki wa Baa/Kumbi za Starehe au Harusi wahakikishe Wahudumu wanavaa Barakoa.
x. Kuwepo na utaratibu katika maeneo haya wa kupunguza watu kuchangamana.
xi. Maeneo haya yakaguliwe na Wataalamu wa Afya na Kamati za Ulinzi na Usalama kuhakikisha maelekezo yanazingatiwa.


a. Maeneo ya Vituo vya Kutolea Huduma za Afya
Vituo vya kutolea huduma za afya vinatakiwa kutekeleza hatua zifuatazo: -
i. Kuweka bango getini linalohimiza uvaaji wa barakoa na kuepuka misongamano wakati wote wa huduma.
ii. Wagonjwa wa nje wasio na dharura waonwe kwa kupangiwa tarehe maalumu (Appointments) ili kuzuia mlundikano kwa wagonjwa kwa wakati mmoja.
iii. Kwenye maeneo ya kusubiria huduma kwa wagonjwa viwekwe viti vya kutosha na vipangwe kwa kuzingatia umbali wa mita moja au zaidi kila pande ikiwezekana alama ziwekwe kudhibiti msongamano. Penye eneo finyu sehemu za kusubiria ziwekwe hata nje ya jengo la kituo cha kutolea huduma za afya.

iv. Ndugu wa kuona/kuleta mgonjwa wasizidi wawili (2) kwa wakati mmoja na wote watatakiwa kuvaa barakoa na watumie kwa muda usiozidi nusu saa kumuona mgonjwa.
v. Kudhibiti watu wasiohusika kwenye maeneo mbalimbali ya kituo cha afya kutembelea maeneo hayo.
vi. Kuruhusu wagonjwa kwenye kliniki za ufuatiliaji wa kawaida, kuwapigia simu Madaktari Bingwa wakati wa masaa ya kazi hususan kwa wale wanougua magonjwa yasiyohitaji kumwona daktari uso kwa uso ili wapewe ushauri.
vii. Kuwapima joto la mwili watu wote wanaoingia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.
viii. Wagonjwa wenye magonjwa sugu wapewe dawa za angalau miezi miwili.
ix. Wagonjwa na wateja wanaohitaji huduma za afya wenye umri wa miaka sitini au zaidi (wazee) wapewe kipaumbele kwenye huduma ili wasichangamane muda mrefu na watu wengine.
x. Vituo vyote vihakikishe vinaweka vifaa madhubuti (Visivyoshikwa kwa mkono-foot/pedal/elbow operated) vyenye maji tiririka na sabuni au vitakasa mikono (hand sanitizers) katika maeneo yote ya kutolea huduma (every Point of Care).


b. Vituo vya Polisi, Magereza na Mahakama
Vituo vya Polisi vitatakiwa kufanya yafuatayo: -
i. Kuweka maeneo ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni
ii. Watumishi na watu wote wanaoingia katika vituo vya polisi wavae barakoa muda wote.
iii. Kutoa kipaumbele cha dhamana kwa Mahabusu wenye makosa yanayodhaminika kisheria ili kupunguza msongamano.
iv. Kufanya kipimo cha haraka cha UVIKO -19 kwa mahabusu wote wanaofikishwa gerezani kwa mara ya kwanza.
v. Kuwapima joto la mwili watu wote kabla ya kuingia kituoni na chumba cha Mahabusu.
vi. Kuruhusu ndugu mmoja tu kumtembelea mfungwa, kumuona mahabusu katika siku iliyotengwa na kuhakikisha wafungwa na ndugu wote wanavaa barakoa na wanakuwa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu.
vii. Wasikilizaji wa kesi mahakamani wazingatie kuvaa barakoa na kukaa umbali wa mita moja kati ya mtu na mtu


c. Saluni pamoja na Vinyozi.
Maeneo ya Saluni na vinyozi ni lazima yakaguliwe mara kwa mara na maafisa afya wa Halmashauri na kuhakikisha mambo yafuatayo yanazingatiwa; -
i. Wamiliki wa Saluni na Vinyozi wanatakiwa kuwa na vifaa vya kutosha vya kuwezesha unawaji wa mikono nje ya saluni ambapo kila atakayeingia katika eneo hilo atahitajika kunawa mikono au kutakatisha mikono kwa kutumia vitakasa mikono vyenye kiwango cha alcohol asilimia isiyopungua 70%.
ii. Kuhakikisha upimaji wa joto la mwili kwa wateja kabla ya kuingia saluni na kwa vinyozi pale inapowezekana.
iii. Kuhakikisha uwepo wa taulo zilizofuliwa, kukauka na kupasiwa za kutosha kulingana na wingi wa wateja. Kila mteja atumie taulo lake lililo safi. Pale ambapo wateja huvishwa joho la kufunika mwili, mhudumu ahakikishe mteja amezungushiwa tissue shingoni kabla ya kumvika joho hilo. ‘Tissue’ isitumike zaidi ya mara moja.
iv. Kuhakikisha hakuna msongamano wa watu na kwamba kila kiti kiwe katika umbali wa mita moja na kuendelea na pale inaposhindikana wateja wasubiri nje.

v. Utakasaji wa vifaa vinavyotumika katika maeneo hayo ufanyike kila wanapomhudumia mteja kwa kutumia vitakasa vyenye alcohol asilimia 70 kama spirit.
vi. Kuhakikisha Saluni zinakuwa safi wakati wote.
vii. Kuhakikisha uvaaji wa barakoa muda wote kwa watoa huduma na wateja.
viii. Barakoa hizi ziwe zinatumika mara moja kila baada ya masaa 4 na ivaliwe barabara kuhakikisha inafunika mdomo na pua.


ix. Kuhakikisha wateja wenye joto kali la mwili, mafua na kikohozi hawaingii saluni (Weka Tangazo), waelekezwe kwenda kupata matibabu kwenye vituo vya afya.
x. Endapo Saluni/Vinyozi wanahuduma ya massage au kuosha, watoa huduma wahakikishe uvaaji wa gloves pamoja na barakoa muda wote wanapotoa huduma.
xi. Kusimamia utaratibu wa kunawa mikono kwa kila mteja anayeingia.
xii. Weka chombo cha kuhifadhia taka na hakikisha taka za barakoa na tissue zinachomwa.


d. Masoko, Magulio, Minada, Maduka makubwa na Maeneo mengine ya biashara

Mambo yafuatayo yanahitaji kuzingatiwa;
i. Halmashauri ziandae timu za kukagua maeneo haya inayojumuisha viongozi wa ngazi za jamii ili kupunguza misongamano katika maeneo husika.
ii. Halmashauri iainishe maeneo zaidi na kuangalia namna ya kupunguza msongamano ikiwa ni pamoja na kutumia viwanja vya mipira wa miguu au maeneo yoyote yaliyo wazi kwa ajili ya huduma za masoko au kushushia bidhaa. Lengo ni kuwawezesha wafanyabiashara na wateja kuwa kwenye umbali unaokubalika na kuweka utaratibu kwa wateja kukaa umbali wa mita moja au zaidi wakati wa kupata huduma

iii. Kuweka utaratibu kwenye maeneo ya kuingilia ili kuhakikisha kila mteja na mfanyabiashara anayeingia kupata huduma katika maeneo hayo awe amevaa barakoa au aelekezwe kununua barakoa bila shuruti
iv. Kila mwenye biashara aweke chombo chenye maji tiririka na sabuni na kila mara awaelekeze wateja wake kunawa kabla hawajaingia sokoni au dukani kupata huduma.
v. Watu wasiokuwa na kazi maalumu wasiruhusiwe kukaa katika maeneo hayo ili kupugunguza msongamano.
vi. Watu waelimishwe ikiwezekana wanunue mahitaji ya kuwawezesha kukaa muda mrefu ili kupunguza uwezekano wa kwenda kwenye maeneo hayo mara kwa mara
vii. Minada iepuke shughuli zinazofanya watu kukaa muda mrefu na kuchangamana zaidi kama uchomaji wa nyama (watu wanunue na kupeleka nyumbani) au unywaji wa pombe.
viii. Kuweka au kutumia vipaza sauti kwa ajili ya kuhimiza kanuni za afya na matangazo mbalimbali.
ix. Kuwashauri wazee, watoto na watu wenye magonjwa ya muda mrefu kuepuka kwenda kwenye mikusanyiko ikiwezekana wawaombe vijana kuwasaidia kuwanunulia mahitaji.
x. Iwapo kwenye maeneo haya kuna biashara mbalimbali zilizotajwa awali, utaratibu wake uzingatiwe kama ilivyokushaelezwa mfano Baa, Kumbi za Harusi, Saluni nk


e. Shughuli za Michezo na Matamasha ya Muziki
Mazoezi na shughuli zote za michezo ni sehemu muhimu katika kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa mbalimbali. Hata hivyo shughuli hizi zinatakiwa kufuata mwongozo wa kuzingatiwa kuendesha shughuli za michezo katika kipindi cha Mlipuko wa covid 19 nchi kwa lengo la kudhibiti maambukizi ambao uliytolewa na Wizara ya Afya Mei 2020. Hata hivyo kwa matamasha ya muziki, burudani na sanaa nyingine na ambayo yameidhinishwa na BASATA waandaaaji watahakikisha kuwa matamasha hayo yanafanyika zaidi kwenye maeneo ya wazi (viwanjani), ambapo kabla ya kuingia uwanjani waandaaji watahakikisha kuwa washiriki wananawa mikono kwa maji tiririka/kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa uwanjani. Kamati za ulinzi na usalama za Mikoa katika kuridhia matamasha haya, zitajiridhisha kwanza na uzingatiaji wa masharti haya. Aidha, kwa shughuli zote za sanaa zinazolazimika kufanyika ndani ya kumbi waandaaji watahakikisha zitazingatia Kanuni zote hizi na ile ya kuhakikisha watu wanakaa umbali wa mita moja.


Kuimarisha na kuongeza mbinu za utoaji wa elimu ya UVIKO-19 kwenye Mikusanyiko
Utoaji wa elimu ya afya kwa umma utaendelezwa kila siku kwa kuhusisha mbinu mbalimbali na wadau mbalimbali kwa kufanya yafuatayo;
i. Kuendelea kutumia vyombo mbalimbali vya habari katika utoaji wa elimu ya afya kwa umma.
ii. Kuhamasisha wananchi kuhusu tahadhari na namna ya kuendeleza jitihada za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kuhusisha makundi mbalimbali ya kijamii.
iii. Kutumia magari ya matangazo (PA system) na vipaza sauti (megaphones) katika kufikisha jumbe mbalimbali kwa jamii
iv. Kutumia vikundi vya Jamii/Jadi, Sanaa kufikisha jumbe na pia kutumia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) na pia kutumia wataalam wa maendeleo na ustawii wa jamii katika kutoa elimu ya afya kwa jamii kwa kutembelea kaya pamoja na kuwafuatilia watu wanaohisiwa au kuthibitishwa kuwa na ugonjwa wa UVIKO-19 kwa aijili ya kuwapa elimu ya kupata huduma na kuwakinga wengine wasipate ugonjwa.
v. Kutumia lugha ya Alama na maandishi ya nukta nundu kwa watu wenye ulemavu iliwawezekupata elimu stahiki
vi. Katika kupokezana Microphone, tahadhari zichukuliwe za kutumia vipukusi pale inapolazimu watumiaji zaidi ya mmoja


Matumizi ya Barakoa katika Misongamano
Matumizi ya Barakoa kwa wananchi wote kwenye sehemu zenye mikusanyiko (Mass Masking) ni hatua muhimu ya kukata mnyororo wa maambukizi katika jamii. Aidha, matokeo ni makubwa sana pale ambapo uvaaji barakoa unaenda sambamba na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na au kutumia vitakasa mikono. Pamoja na jitihada za kudhibiti misongamo kufanyika ni vyema pia wananchi waendelee kuhamasishwa kuvaa barakoa wanapotoka majumbani kwao pamoja na wale wote wenye dalili. Ni muhimu kwa mtu yoyote ambaye hataweza kuwa mbali na mtu mwingine kwa zaidi ya mita moja, ahakikishe anavaa barakoa muda wote anapokuwa na mtu ambaye hakai naye nyumba moja. Uvaaji wa barakoa utasaidia kupunguza maambukizi mengine ya mfumo wa hewa;


Hivyo tunapendekeza kuwa; -
i. Serikali kupitia Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Kata, Vijiji na Mitaa, ihakikishe wananchi wanaelimishwa namna sahihi ya kuvaa, kuvua, kufua, kupasi na kutunza barakoa.
ii. Mamlaka za Wilaya/Halmashauri Kata na Serikali za Mitaa zihakikishe zinaelimisha na kufanya ufuatiliaji zaidi wa uvaaji wa barakoa za aina zote katika maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko kama ifuatavyo:
iii. Kwenye daladala, mabasi na magari mengine ya abiria, lazima kila dereva na kila abiria avae barakoa;
iv. Kwenye maeneo yote ya mikusanyiko kama sokoni, dukani, stendi, saluni, hospitali, viwanja vya ndege, kwenye meli/mtumbwi, gengeni, kanisani, mashuleni/vyuoni, mabaa, harusi, sherehe au mikutanoni, kila mmoja avae barakoa.
v. Elimu itolewe ya kutosha kuhusiana na utengenezaji, matumizi sahihi na utupatikanaji wa Barakoa.
vi. Elimu juu uandaaji, uuzaji, Uvaaji na utumiaji sahihi wa Barakoa utolewe kwa umma kuanzia ngazi ya Kaya na Mitaa.


Mwisho, Wakuu wa Mikoa. Wilaya na Vyombo vya Ulinzi na Usalama, viwasaidie Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika kutekeleza Sheria ya Afya ya Jamii (Public Health Act 2009) kipengele cha 15 na 16 inayawapa mamlaka ya kuthibiti kusambaa kwa magonjwa katika maeneo yao kwa kusimamia mbinu mbalimbali za uthibiti kwa jinsi watakavyoshauri.


Imetolewa na.
Prof.Dr. Abel N. Makubi
KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
25 July 2021, Dar es Salaam



Share:

VIDEO: Krantz Mwantepele Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa Young CEO Club

 VIDEO:  Krantz Mwantepele Achaguliwa Kuwa Mwenyekiti Wa Young CEO Club



Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger