Saturday, 29 May 2021

JAMAA ACHOMA MOTO NYUMBA YA MAMA MKWE BAADA YA MKE KUTOROKA

Maafisa wa polisi eneo la Kiminini kaunti ya Trans Nzoia nchini Kenya wanamsaka jamaa mmoja mwenye umri wa makamo aitwaye Amos Wanjala ambaye anadaiwa kuvamia makazi ya mamake mkwe na kuchoma malazi yake.

Inaelezwa kuwa Amos Wanjala alitekeleza kitendo hicho baada ya mkewe kumtoroka.

Akiwa mwenye ghadhabu, Wanjala alivamia boma la Mercyline Wanyama Alhamisi, Mei 28,2021 mwendo wa saa tano usiku, alimuasha mama mkwe na kisha kuchoma malazi na baadhi ya nguo zake.

Mama huyo alisema alipoteza mali inayogharimu zaidi ya KSh 6,000 kwenye mkasa huo na hadi kwa sasa anashangaa ni nini kilichomfanya mkwe wake kumvamia.

Mshukiwa anasemekana kumtishia maisha mama huyo, hii ni kulingana na OCPD wa Kiminini Francis Tumbo.

Tumbo alisema mshukiwa akikamatwa, atashtakiwa kwa uharibifu wa mali na pia kumtishia maisha mama huyo.

"Akishakamatwa, atashtakiwa kwa kosa la kuharibu mali," OCPD huyo alisema.

Kwa mujibu wa taarifa za The Standard, mkaaji mmoja aliyetambulika kama Juma Barasa ametaka mshukiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa ajili ya kukiuka mila.

"Ni kinyume na ukoo wa Wabukusu kwa mtu yeyote kuwashambulia wakwe zake ama kuharibu mali yao," Barasa alisema.

Mmoja wa majirani amesema kwamba Wanjala atapigwa faini ya mbuzi ambayo itachinjwa kwenye sherehe ya utakaso.
Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 29



Share:

50 Job TAMISEMI & Wizara Ya Afya

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Opportunities TAMISEMI & Wizara Ya Afya. The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service. Public Service Recruitment Secretariat was established by the Public Service Act No. 8 0f 2002 as amended by Act […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 29,2021
















Share:

Friday, 28 May 2021

CCM Yalaani alichokifanya Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimelaani kitendo kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa UWT mkoa wa Arusha wakiongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Catherine Magige, baada ya kwenda kuvunja geti na kuingia kwenye makaburi ya familia mahali ambapo amezikwa Kuzula Madoda anayedaiwa kuwa mchumba wake.

Taarifa ya kulaani kitendo hicho imetolewa leo Mei 28, 2021, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka, na kusema kuwa CCM inaamini katika kujenga uimara wa familia, kuheshimiana ndani ya jamii na kuendeleza upendo katika familia halali, badala ya mivutano na uvurugaji usiokuwa na sababu.

"Chama kinatafakari kwa undani kwa mujibu wa kanuni za maadili na Katiba ya CCM, na kuchunguza kwa kina ili kuchukua hatua za kimaadili kwa wote watakaothibitika kuwa sehemu ya matukio yaliyojenga kukiuka kwa Katiba, kanuni na utamaduni wa kuheshimu na kuheshimiana uliojengeka ndani ya CCM," imeeleza taarifa hiyo.

Haya yote yanajiri baada ya video kusambaa mitandaoni zikimuonesha Mbunge huyo pamoja na watu wengine wakitumia nguvu kushiriki katika mazishi ya mfanyabishara huyo mkoani Arusha




Share:

Rais Samia akutana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Wanawake (UN-Women) Dkt. Phumzile Mlambo-Ngcuka



Share:

WAZIRI UMMY AWASIMAMISHA KAZI WATUMISHI WANNE UBADHIRIFU UJENZI MACHINJIO MANISPAA YA SHINYANGA


 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu akiwa kwenye ujenzi wa mradi wa machinjio ya kisasa Shinyanga.

Na Mwandishi wa  Malunde 1 blog

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Rais Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ummy Mwalimu amewasimamisha kazi wiki mbili watumishi Wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupisha uchunguzi tuhuma ubadhirifu ujenzi wa machinjio ya mifugo ya kisasa.


Watumishi walio simamishwa kazi ni Mchumi Gwakisa Mwakyeba, Mkuu wa idara ya Mifugo Tito Kagize, Mhandisi wa ujenzi Kasimu Thadei, pamoja na Mkuu wa idara ya manunuzi Godfrey Mwangairo.


Waziri Ummy akizungumza jana kwenye ujenzi wa mradi wa machinjio hiyo ya mifugo ya kisasa, mara baada ya kupewa taarifa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi na kuonekana kuna ubadhilifu wa fedha, ndipo akaamua kuwa simamishwa kazi watumishi hao ili kupisha uchunguzi.


Alisema Taarifa za mradi huo anazo kutoka kwa Mkukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuwa kuna ubadhirifu wa fedha kwenye machinjio hiyo, hivyo anashaghaa watu ambao waliohusika kutochukuliwa hatua.


"Mkurugenzi wewe ni mteule wa Rais hivyo sitakugusa kwenye suala hili, saizi yangu ni hawa watumishi, hivyo kuanzia sasa na wasimamisha kazi wiki mbili ili kupisha uchunguzi juu ya ubadhirifu wa ujenzi wa machinjio hii ya kisasa," alisema Mwalimu.


"Kuna watumishi wengine najua wameshahamishwa hapa Shinyanga, hivyo naagiza waletwe hapa ili kujibu  ubadhirifu wa ujenzi wa machinjio hii ya mifugo ya kisasa, pamoja na Wakandarasi wachukuliwe hatua,"aliongeza.


Aidha alisema gharama za ujenzi wa machinjio hiyo anazifahamu ni Sh. bilioni 5.7 na zimeshatumika bilioni 5.1 na kuhoji juu ya Sh. milioni 600 mahari zilipo, huku mradi huo ukiwa bado haujakamilika na kutakiwa tena kuongezwa Sh. 172 kutoka kwenye mapato ya ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Godfrey Mwangulumbi, akitoa taarifa ya ujenzi wa machinjio hiyo, alisema gharama za mradi huo awali ilikuwa ni Sh. bilioni 5.9, lakini zikapungua hadi Sh. bilioni 5.5 na zimeshatumika Bilio 5.1 huku akibainisha fedha Milioni 600 zipo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemoni Sengati, alisema suala la watumishi hao atalifanyia kazi na watatoa taarifa ndani ya wiki mbili ambazo zimetolewa.

Share:

Picha : DC MACHA ATEMBELEA MABANDA YA WAJASIRIAMALI WANAOSHIRIKI MAONESHO KAHAMA

Share:

Majaliwa: Nacte Visaidieni Vyuo Kutoa Elimu yenye Kukidhi Mahitaji


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameliagiza Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) liimarishe usimamizi na kuvisaidia vyuo kutoa elimu inayozingatia viwango vya ubora na vyenye kukidhi mahitaji ya soko ya ajira la sasa na lijalo.

Amesema kuwa ni wajibu wa vyuo hivyo kuhakikisha vinatoa elimu bora ili kuwafanya wahitimu wake wawe mahiri na kukidhi mahitaji ya nchi na pia kuwawezesha kujiajiri wao wenyewe.

Ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Mei 28, 2021) wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Amesema kuwa vyuo vya elimu na mafunzo ya ufundi vinapaswa kutumia fursa ya maonesho hayo kujitathmini na kujipima ili kuona ni kwa namna gani vinaweza kutoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi bora yanayokidhi mahitaji ya sasa ya soko la ajira na kutoa fursa kwa vijana kujiajiri.

“Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025 imeweka wazi kuwa elimu ni kipaumbele cha juu kwani ndiyo kitovu cha kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwenye jamii”.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa ulimwenguni kote elimu na mafunzo ya ufundi na ufundi stadi hujulikana kwa mchango wake mkubwa katika ukuaji wa maendeleo ya viwanda, uchumi na ustawi wa jamii. “Vyuo na taasisi zinazotoa elimu hii ni lazima vihakikishe vinatoa elimu bora inayokidhi viwango na mahitaji ya soko la sasa la ajira”


Kadhalika, Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kuweka sera ambazo zinatoa fursa kwa wadau mbalimbali kuwekeza katika sekta ya elimu na hivyo, kuunga mkono juhudi za kuliletea Taifa maendeleo.


“Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na taasisi za umma na binafsi ambazo zinatoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi hapa nchini. Hivyo, natoa wito kwa wadau wote kuungana na Serikali kuwekeza katika utoaji wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika fani mbalimbali”

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Wizara itaendelea kuhakikisha inatoa elimu ya mafunzo ya ufundi kwa kuzigatia mahitaji ya soko ya kipindi husika na kuwaandaa vijana kwa siku zijazo.

Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uongozi NACTE Prof. John Kondoro amesema kuwa watashirikiana na vyuo, taasisi za elimu ya mafunzo ya ufundi na wadau wengine kusimamia utoaji wa mafunzo na kuhakikisha elimu ya ufundi na mafunzo inatolewa kwa ubora ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira la ndani na nje.

 (Mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU



Share:

VIDEO: Barnaba Ft. Alikiba – Cheketua


VIDEO:  Barnaba Ft. Alikiba – Cheketua


Share:

Diamond platinumz kuwania tuzo za BET nchini Marekani


Wasanii watatu wa Afrika wameteuliwa kuwania tuzo za BET nchini Marekani.Wasanii hao ni Diamond Platinumz , Wizkid na Burnaboy kutoka Nigeria pamoja na wasanii wa Ufaransa .

Burnaboy aliibuka mshindi wa orodha hiyo mwaka uliopita . Wasanii hao watawania tuzo ya mwanamuziki bora wa kimataifa.

Tuzo za BET zitafanyika tarehe 27 mwezi Juni na watu watahudhuria tamasha lake baada ya kufanyika kwa video mwaka uliopita kwasababu ya mlipuko wa virusi vya corona.


Share:

SHINDANO LA MISS KAHAMA 2021 KUFANYIKA JUNE 6...WAREMBO 12 KUCHUANA


Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex akizungumzia kuhusu maandalizi ya Shindano la Miss Kahama 2021. Kushoto ni Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata.

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shindano la Urembo kutafuta mlimbwende wa Kahama ‘Miss Kahama 2021’ yanatarajia kufanika June 6,2021 katika ukumbi wa African Lounge Mjini Kahama yakishirikisha warembo 12 huku Msanii Mr. Blue akinogesha mashindano hayo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa Mei 28,2021, Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners ambao ni waandaaji wa Shindano la Urembo la Miss Kahama, Peter Frank Alex amesema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika.

Amesema shindano la Miss Kahama litafanyika June 6, 2021 African Lounge. Washiriki wapo 12 ambao ni mabinti warembo kutoka Kahama ambao sasa wapo kambini wanaendelea na mazoezi.

“Maandalizi ya shindano la Miss Kahama ni makubwa hivyo wananchi wategemee mambo makubwa siku hiyo kuanzia saa moja usiku. Tiketi zinaendelea kutolewa maeneo mbalimbali ikiwemo Huheso FM kwa Zakazi, BSL College, African Lounge na tunasambaza mtaa kwa mtaa na siku ya shindano tiketi zitapatikana getini”,amesema.

“Sisi kama waandaaji wa Miss Kahama tumekaa na Waandaaji Wakuu wa Miss Tanzania na tumepewa taratibu na vigezo mbalimbali hivyo. zile sintofahamu ambazo zilikuwa zinaendelea mtandaoni tumeshazirekebisha hivyo Shindano la Miss Kahama lipo kama kawaida tarehe 6 Mwezi wa Sita”,ameongeza Alex.

Ameeleza kuwa wameandaa zawadi na fursa mbalimbali kwa washiriki wa shindano la Miss Kahama ambazo zitawasaidia katika maisha yao huku akiwaomba wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani kujitokeza kushuhudia shindano hilo.

Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata amesema mwaandaaji wa shindano la Miss Kahama amekamilisha taratibu zote hivyo ana Baraka zote za kuendesha shindano hilo June 6, 2021.

“Waandaji wa shindano la Miss Kahama wameshakamilisha taratibu zote zilizokuwa zinatakiwa hivyo Mkurugenzi wa Br.Black Social Partners ,Peter Frank Alex ni mtu rasmi kwa ajili ya kuandaa shindano hilo Kahama kwa ajili ya kunyanyua vipaji vya watoto wa kike pamoja na vipaji vingine ndani ya Kahama”,amesema Mwata.

“Mwenzetu ameweza kuandaa maandalizi ya Miss Kahama. Kwa hiyo mimi kama Mwakilishi wa Miss Tanzania Organisation napenda kuwataarifu kuwa tumemruhusu Mkurugenzi wa Br.Black Social Partners ,Peter Frank Alex kufanya shindano la Miss Kahama kama chini ya Miss wilaya na utaratibu mwingine utafuata wa kuandaa Miss Mkoa na Kanda kama alivyoelekezwa”,amesema.

Amesema Taasisi ya Miss Tanzania inamchukulia Mkurugenzi wa Br.Black Social Partners ,Peter Frank Alex kama mdau anayeandaa kwa watoto kwa ajili ya kuonesha vipaji vyao katika jamii na kutumia kutangaza utalii na uwekezaji.
Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata akizungumzia shindano la Miss Kahama 2021. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex ambaye ni Mwandaaji wa Shindano la Miss Kahama 2021.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Br.Black Social Partners , Peter Frank Alex akizungumzia kuhusu maandalizi ya Shindano la Miss Kahama 2021.Kushoto ni Katibu wa Taasisi ya Urembo ya Miss Tanzania (Miss Tanzania Organization) na The Look Company Limited, Benard Mwata.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Share:

RC MALIMA AWATUMIA SALAMU WANAOSAFIRISHA WAHAMIAJI HARAMU, WANAOPITISHA DAWA ZA KULEVYA AWAAMBIA WASIJARIBU

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari


MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amewatumia salamu mawakala wa wahamiaji haramu ambao wanatumia mkoa huo kuwapitisha na wale wanaopitisha dawa za kulevya kwamba wasijaribu kufanya hivyo maana watakachokutana nacho kitakuwa historia kwao.

RC Malima aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga ambapo alisema mkoa huo hautakuwa dezo ya kupitisha wahamiaji haramu na kama kuna watu wanadhani anatania wafanye hivyo waone watakumbana na jambo gani.

Alisema kwamba mkoa huo hautakuwa sehemu ya watu kupitisha mauzauza yao na wasijaribu kutokana na kwamba wamejipanga vilivyo kuhakikisha vitendo vya namna hiyo havifanyika kwenye mkoa huo huku akitoa onyo kwa wanaodhani wanaweza kujaribu.

“Ndani ya wiki mbili wahamiaji haramu wameongezeka naomba wasiufanye mkoa wa Tanga kuwa ni dezo ya wao kupitia na niwaambie kwamba Tanga hautakuwa mkoa wa kupitisha mauzauza yao na hata wale ambao wanafikiria kwamba wanaweza kupitisha dawa za kulevya wasijaribu zari kwani tumejipanga kuwashughulikia”Alisema

Alisema wahamiaji haramu hao wanapitia mkoa wa Tanga kwenda mikoa ya Pwani ,Dar,Bagamoyo kwa hiyo aliwataka waandishi wa habari kufikisha salama kwa wananchi kwa wale wanaojua wazi kwamba watu wanao wanashirikiana kwenye kusafirisha binadamu wanaowatoa mkinga wanawasafarisha usiku kwa usiku.

“Hao watu ambao wanao wanashiriikiana kusafrisha binadamu wanawatoa wilaya ya Mkinga kuwasafirisha usiku kwa usiku  wengine wanapita Korogwe wanatoka Kilindi wanachana Korogwe hadi Handeni wanapitia Mkata wanaingia Pwani wengine wanatokea Mvomero pia eneo la Gairo hilo ni tatizo kubwa na hawawezi kufanikiwa kama hawana watu ambao wana shirikishiana nao”Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka waandishi wa habari mkoa wa Tanga wafikishe ujumbe kwamba wale wanaotumika kuwasafirisha huenda dhambi ya kusafirisha ni kubwa sana kuliko kusafirishwa.

Share:

Waziri Mhagama: Tatizo la ajira nchini, Tafiti mbili kwenye nguvu kazi na Rasilimali watu kufanyika mwaka huu.


Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), imepanga mwaka huu kufanya tafiti mbili kubwa ambazo zitajikita kwenye kubaini nguvu kazi pamoja na rasilimali watu.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo  tarehe 27 Mei, 2021, Jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wanaendelea kushirikiana ambapo Wizara hiyo inapitia sera ya elimu na huku Ofisi hiyo ikifanya tafiti.

“Mwaka huu tumeamua kufanya tafiti mbili kubwa ambapo tafiti moja tunaendelea nayo ambayo ni hali ya nguvu kazi nchini. Utafiti huo utatausaidia kujua ni asilimia ngapi ya vijana wanaofundishwa ndani ya  nchi na  wanaweza kuajirika nchini  na kama hawajaajiriki ni kwa nini. Aidha Utafiti huo utatusaidia kuelewa sekta ipi yenye fursa nyingi kuliko sekta nyingine ya ajira hii itasaidia mafunzo ya ufundi yaendane na mahitaji yetu ya ajira” Amesisitiza Mhagama

Aidha, Mhe. Mhagama amefafanua kuwa serikali imeshakamilisha utaratibu wa kufanya utafiti wa Hali ya rasilimali watu nchini. Utafiti huo utasaidia kuelewa juu ya watanzania waliopo nchini na waliopo nje ya nchi kama wanaendana na mahitaji ya ajira kwa sasa.

Ameongeza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa ikisimamia vibali vya ajira kwa wageni, hivyo wataelewa sababu ambazo hupelekea wawekezaji kuhitaji kuwaleta watu wao wenye ujuzi ile hali wenye ujuzi wa viwango hivyo wapo hapa Tanzania, lakini pia itaeleweka maeneo gani ambayo nchi haina ujuzi na wangependa ujuzi huo upatikane hapa nchini.

Mhe. Mhagama amewataka wadau wa elimu ya Ufundi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha changamoto za ajira zinashughulikiwa ipasavyo nchini. Amesisitiza kuwa ili kuweza kuwa na uchumi wa kati endelevu hadi kufikia uchumi wa juu tunahitaji kuwa na mfumo rasmi wa kuwandaa vijana katika viwango vya juu vya maarifa, ujuzi, na stadi za kutenda.

Mhe. Mhagama amefafanua kuwa kwa sasa serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati kwenye sekta ya nishati ya umeme, Reli ya kisasa, kwenye Sekta ya Afya na Elimu pamoja na Barabara na hivi karibuni utatekelzwa mradi wa Bomba la mafuta kutoka Tanzania hadi nchini Uganda. Ameeleza kuwa miradi hiyo ili iwe endelevu ipo haja ya kuwa na wataalamu wenye ujuzi wa kuendeleza uangalizi wa miradi hiyo.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la (NACTE), Prof. John Kondoro na Katibu Mtendaji (NACTE) Dkt. Adolf Rutayuga,wamefafanua kuwa  Kongamano hilo litalisaidia Baraza hilo kuwa na mipango ya kuunganisha nguvu ili kuwekeza kiasi cha kutosha katika Elimu ya Ufundi.

Aidha, wamefafanua kuwa wataweza kuwa na suluhisho kwenye masuala ya kupata maeneo ya kutosha ya mafunzo ya vitendo, Upatikanaji wa Takwimu sahihi za wataalamu kwenye sekta za ajira, Kuimarisha uhusiano kati ya Taasissi za Mafunzo na soko la ajira, na hatimaye Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaweza kutoa mchango mkubwa katika Maendeleo ya sekta zote za kiuchumi hapa nchini.

Pia, Mkurugenzi Idara ya Wanachama, Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Zachy Mbenna ameiomba serikali kushirikiana na sekta Binafsi katika juhudi za kuendeleza kukuza ujuzi kwa kusimamia tozo inayotozwa ya kukuza ujuzi  kwa kuelekezwa kwenye kukuza ujuzi moja kwa moja  kwa kuishirikisha sekta Binafsi kwenye maoni ya matumizi yake.

Ameomba kiwepo chombo cha kitaifa kitakacho ratibu juhudi za kukuza ujuzi kwa kuwaunganisha wanaotoa mafunzo ya kukuza ujuzi. Aidha, ameomba kuwapa motisha waajiri wenye utaratibu wa kukuza ujuzi katika maeneo yao ya kazi kwa kupewa utambuzi wakati wa kulipa kodi, ameomba wadau hao wa sekta Binafsi wanaochangia masuala ya ujuzi kupewa mazingira ya kipaumbele wakati wa uwekezaji. Utekelzaji wa masuala hayo yatasaidia kuongeza idadi ya wadau wanaotekeleza masuala ya kukuza nchini.

Kauli Mbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni “Kuimarisha Ushirikiano wa Wadau katika Kukuza Ujuzi kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda” Wadau hao ni Serikali, Taasisi zinazotoa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na Waajiri. Kongamano hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa ushirikiano na Taasisi ya Sekta Binafsi.

MWISHO.


Share:

Jeshi la Polisi Shinyanga lakamata Dawa za Kulevya


 SALVATORY NTANDU
Masunga Nindwa (36)mkazi wa Lunzwe mkoani Geita na Peter Matiko mkazi wa nyakato mkoani Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kilogramu 20 na mirungi kilogramu 25.

Akizungumza waandishi wa habari  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo (ACP) Debora Magiligimba alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika matukio mawili tofauti baada ya kufanyika kwa msako mkali wa jeshi hilo ambao umefanikisha kukamatwa kwa dawa hizo.

Katika tukio la kwanza Masunga Nindwa alikamatwa na jeshi la polisi wilayani kahama mei 21 mwaka huu katika nyumba ya kulala wageni ya kalunde iliyopo katika mtaa wa nyasubi akiwa na debe mbili za bangi zenye uzito wa kilogramu 20 huku akijua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.

Kamanda Magiligimba alisema kuwa katika tukio la pili mei 21 mwaka huu majira ya asubuhi katika kata ya Ibinzamata Peter Matiko alikamawa na jeshi hilo akiwa na mirungi kilogramu 25 iliyokuwa imewekwa kwenye mabegi aliyokuwa anaisafirisha kwenda mkoani Singida.

“Jeshi la polisi lilipata  taarifa za kiintelijensia kutoka kwa wasamaria wema na kuanza kuafuatilia na kisha kufanikiwa kuwakamata na dawa hizo za kulevya,mtuhumiwa wa mirugi alikiri kutumia na kuuza dawa hizo upelelezi ukikamilika tutawafiksha mahakamani,”alisema Magiligimba.

Sambamba na hilo Magiligimba alisema kuwa jeshi hilo pia linamshikilia Elida Zakaria (19)mkazi wa kagongwa kwa tuhuma za kukutwa na kete 111 za dawa za kulevya aina ya bangi zilizokuwa zimefungwa kwenye magazeti  nyumbani kwa Lucia Luhende ambaye ndiye mmiliki wa dawa hizo

“Tunatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote upelelezi ukikamilika na tunatoa rai kwa wananchi kuwafichua watu wanaouza na kusafirisha dawa za kulevya ambazo zimekuwa zileta athari kwenye jamii”,alisema Magiligimba.

Mwisho.


Share:

HEALTH LABORATORY ASSISTANT – 14 POST at Ministry Of Health (MOH)

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST HEALTH LABORATORY ASSISTANT – 14 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER Ministry Of Health (MOH) APPLICATION TIMELINE: 2021-05-27 2021-06-09 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To maintain cleanliness of the laboratory , glassware and equipment; ii. To perform Phlebotomy duties; iii. To keep records of received specimens, laboratory investigations and procedures under […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

LABORATORY TECHNOLOGIST II – 9 POST at Ministry Of Health (MOH)

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

POST LABORATORY TECHNOLOGIST II – 9 POST POST CATEGORY(S) HEALTHCARE AND PHARMACEUTICAL EMPLOYER Ministry Of Health (MOH) APPLICATION TIMELINE: 2021-05-27 2021-06-09 JOB SUMMARY NA DUTIES AND RESPONSIBILITIES i. To rreceive, extract and record samples for laboratory examination; ii. To prepare laboratory equipment and chemical tests and examinations; iii. To inspect and store laboratory reagents, equipment […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger