Sunday, 24 January 2021

MWENYEKITI HALMASHAURI TARIME NA MKEWE WATEMBELEA WAFUNGWA MAHABUSU GEREZA LA TARIME … WATOA MSAADA WA NGUO,VYAKULA NA FEDHA



Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyakonga Simion Samwel akimkabidhi kaimu mkuu wa gereza la wilaya ya Tarime aliyevaa (kofia) Francis Makelemo gunia za mchele,sabuni,mafuta kwa ajili ya wafungwa na mahabusu.
Ester Simion mke wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime Simion Samwel akitoa kanga kwa ajili ya wafungwa gereza la Tarime

Na Dinna Maningo, Tarime
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyakonga Simion Samwel  akiwa ameambatana na mke wa mke Ester Simion wamewatembelea wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Tarime na kutumia nafasi hiyo kuwaomba wadau mbalimbali kutoa msaada wa huduma za kiroho na kimwili.

Akiwa ameambatana pia na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka na Katibu Mwenezi wa CCM wilaya hiyo Marema Sollo leo Jumapili Januari 24,2021 , Simion amemkabidhi Kaimu Mkuu wa gereza wilaya ya Tarime, Francis Makelemo mchele kilo 480, sabuni za miche maboksi 10, sabuni za unga mifuko 22, mafuta ya kula ndoo 5 na kanga pea 40, pesa taslimu sh. 620,000/= kwa ajili ya watu wanaoletewa chakula nje vyote vikighalimu  jumla ya sh.Milioni tatu.

"Mimi ni muumini wa kanisa la Wasabato la Turwa na huwa tunatoa msaada kwa wahitaji,kutembelea wagonjwa,wafungwa na wengine wenye uhitaji,mimi na mke wangu tumewiwa kutoa fedha zetu za mfukoni ili wafungwa na mahabusu wapate huduma ya kimwili. Nawaomba na wengine wasaidie", alisema Simion.

Ester Simion alisema kuwa kwa kuwa yeye ni mama ameguswa kuwasaidia wanawake walioko gerezani kwa kuwanunulia kanga pea 40 zenye thamani ya sh.320,000/= na kuwaasa akina mama kusaidia wahitaji kwa chochote walicho nacho hata kama ni kidogo.

Mchungaji wa kanisa la Waandventista wasabato Turwa Joseph Iteremi alisema katika maandiko ya biblia Mathayo 25 inazungumzia kuwajali na kuwatembelea wahitaji na kanisa hilo pamoja na waumini wake huwatembelea wahitaji na kuwasaidia kwakuwa ni sehemu ya utume.

"Nimshukuru Mwenyekiti wa halmashauri kwa moyo wake wa kuwasaidia  wahitaji na kuwakumbuka wafungwa gerezani ,na niwashukuru askari wa gereza wamekuwa wakiwahudumia vizuri wafungwa lakini kutoa nafasi ya watu kuwatembelea na kuwaona wafungwa na mahabusu tuendelee na moyo huohuo wa kusaidia", alisema Iteremi.

Katibu wa CCM wilaya ya Tarime Hamis Mkaruka alisema kuwa kufungwa ni sehemu ya adhabu kwa ajili ya kujirekebisha hivyo wafungwa wana haki ya kupata huduma sawa na wengine huku akimpongeza mwenyekiti huyo kwa msaada alioutoa na kusema kuwa Chama Cha Mapinduzi kinampongeza kwa kuwa matendo mazuri ukifanya chama kizidi kuaminiwa.

Kaimu mkuu wa Gereza wilaya ya Tarime Francis Makelemo alisema kuwa gereza hilo lina jumla ya wafungwa na mahabusu wapatao 532 kati ya hao wafungwa ni 117 na mahabusu ni 415,alimshukuru mwenyekiti Simion kwa moyo wake wa kuwajali mahabusu na wafungwa na msaada alioitoa.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tarime ambaye pia ni Diwani wa kata ya Nyakonga Simion Samwel akimkabidhi kaimu mkuu wa gereza la wilaya ya Tarime aliyevaa (kofia) Francis Makelemo gunia za mchele,sabuni,mafuta kwa ajili ya wafungwa na mahabusu.

Share:

SERIKALI YA TANZANIA, KENYA YAOMBWA KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UHALIFU..MBUNGE WAITARA ACHANGIA MIL.5 UJENZI KITUO CHA POLISI

Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara akizungumza na wananchi kata ya Itiryo. Picha na Dinna Maningo

Mbunge Waitara akisalimiana na wazee kata ya Itiryo

Na Dinna Maningo,Tarime
Wananchi kata ya Itiryo wilayani Tarime mkoani Mara kwa kushirikiana na Mbunge wao wa jaimbo la Tarime vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mwita Waitara wameamua kuchanga fedha na nguvu kazi ili kujenga kituo cha polisi kufuatia kuwepo kwa vitendo vya mauaji na uhalifu vinavyodaiwa kusababishwa na watu kutoka nchi jirani ya Kenya kwa kushirikiana na baadhi ya Watanzania waishio mpakani.

Mbunge huyo amedai kuchukizwa na vitendo vya mauaji na uhalifu vikiwemo vya watumishi wa serikali kuvamiwa na kuporwa fedha na mali na kudai kuwa vinamchukiza ambapo aliwataka wananchi kushirikiana na serikali kuwafichua waovu ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

"Tukio la mwalimu kuuwawa liliteta taswira mbaya na nilitumia nguvu nyingi kulishughulikia lakini bado watu hawasikii wanaendelea kuua na kuchukua mali za watu,kuna mwananchi wakijiji cha Itiryo alipigwa risasi akafa, na inaelezwa kuwa majambazi wanatoka nchi jirani ya Kenya na wanashirikiana na waharifu kutoka kata ya Itiryo",alisema Waitara.

Waitara alisema kuwa kuwepo kwa matukio hayo yamewapa hofu watumishi wa serikali wakiweo waalimu wa shule ya msingi Itiryo kuomba uhamisho ili kunusuru maisha yao jambo ambalo linaweza kurudisha nyuma taaluma ya wanafunzi.

"Nimeambiwa kuwa kuna walimu wanataka kuhama matukio kama haya yanashusha heshima ya kabila letu la wakurya na ndiyo maana tunachukuliwa kama ni watu wakorofi,kwanini tuwafiche wahalifu lazima tuwataje kwa njia zozote hata kama ni kwa siri ili wakamatwe,tukiyaacha haya maovu watu watahama kata na uchumi utashuka, kwakuwa mmekubali kituo kijengwe nachangia milioni tano ya ujenzi",alisema Waitara.

Marwa Chacha alisema kuwa tukio la mauaji lililotokea Januari, 1/2021 na wananchi kupigwa na kunyang'anywa fedha liliondoa imani kwa wananchi na kwamba licha ya mkutano kufanyika na wananchi kuwataja waharifu lakini hawajachukuliwa hatua.

Nchagwa Matare alisema kuwa suala la kujengwa kituo cha polisi lilishazungumzwa na kuna maeneo yapo ambayo yanaweza kutumika kujenga kituo kikubwa cha polisi na kuwaomba viongozi wa serikali za vijiji kuhamasisha wananchi kuchangia fedha na nguvu kazi ili kujenga kwakuwa kitasaidia kuhimarisha usalama na kudhibiti matukio ya uhalifu.

Mwenyekiti wa kijiji cha Itiryo Chacha Paulo aliwataka wananchi kuwa wavumilivu kwa kuwa suala la watuhumiwa wa uhalifu linashughulikiwa na serikali nakwamba kuna siri zingine si mpaka wananchi kuharifiwa bali ni za kiuchunguzi.

"Kata yetu imepakana na kijiji cha Gwitembe na Ntimaro ambavyo viko nchi jirani ya Kenya, tukio la siku ya mwaka mpya usiku saa tano majambazi wanaodaiwa kutoka Kenya kwa kushirikiana na wa hapa kwetu walivamia sehemu nyingi wakamuua Mohono Gasaya akiwa kwenye grosari ya mwalimu Chris na kupora fedha kwa watu wengine waliokuwa kwenye Grosari hiyo kisha wakaondoka na kuvamia nyumba ya Wankyo Meko ambako watumishi ambao ni walimu wamepanga.

"Wakiwa na lengo la kupora fedha kwa mama huyo wakachukua fedha zake laki tatu na kuchukua simu ya mwalimu Lazaro,wakaondoka na kuvamia grosari ya Mseti Magabe wakapora fedha shilingi 380,000/= na kuwapiga wateja kwa ubapa wa panga,kisha wakaelekea barabara ya inayokwenda Kenya wakakuta duka la dawa la mtumishi wakavamia n akuwaweka chini watu waliokuwepo wakachukua dawa na mteja mwingine wakamtoa simu inayotumika kusajili watu wa bima NHF na wakaondoka kwenda Kenya"alisema Paulo.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa polisi walifika lakini hawakufanikiwa kuwakamata na kwamba anaiomba serikali ya Tanzania na Kenya kushirikiana ili kuwakaabili waharifu ambao wamekuwa wakifanya matukio na kukimbilia kwenye maficho ya Kenyamang'ari-Ntimaro,migodi midogo midogo ya Kehancha,Nairobi na Mombasa nchini Kenya na kwa upande wa Tanzania wanakimbilia katika maficho ya misitu mkoani Morogoro.
Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara akizungumza na wananchi kata ya Itiryo
Mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara akizungumza na wananchi kata ya Itiryo
Wananchi wa kata ya Itiryo wakimsikiliza mbunge wao Mwita Waitara
Wananchi wa Itiryo wakinyoosha mikono juu kuunga ushirikiano kati yao na serikali kuwafichua wahalifu
Wananchi wa kata ya Itiryo wakimsikiliza mbunge wao Mwita Waitara
Mwananchi akitoa kero zao juu ya matukio ya uhalifu yanayofanyika kwenye kata hiyo


Share:

RAIS WA ETHIOPIA BI. SAHLE - WORK ZEWDE KUFANYA ZIARA CHATO KESHO


Rais wa Ethiopia Bi. Sahle-Work Zewde.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa kesho Januari 25,2021 Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Ethiopia Bi. Sahle-Work Zewde kwa ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Chato mkoani Geita.

Prof. Kabudi ameyasema hayo leo huko Chato wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ujio huo wa rais wa Ethiopia ambapo amesema kuwa mahusiano ya Tanzania na Ethiopia yamekuwa ya shida na raha.

“Uhusiano wetu na Ethiopia umekuwa katika hali zote na ni mahusiano ambayo yalitengenezwa na waasisi wa mataifa haya mawili ambayo yamekuwa na manufaa kibiashara,” amesema Prof. Kabudi.

Mhe. Sahle-Work Zewde ni rais wa kwanza mwanamke nchini Ethiopia.

Via- EATV
Share:

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU KULA NYAMA YA NGURUWE 'KITIMOTO' KANDA YA ZIWA


Picha ya mnyama Nguruwe.
Serikali imepiga marufuku wananchi wa Kanda ya Ziwa kula nyama ya Nguruwe ikiwa ni hatua za kukabiliana na mlipuko wa homa ya nguruwe uliotokea hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dodoma Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema taarifa zilizopo zinaonyesha Homa ya Nguruwe ilianzia kwenye Halmashauri sita za Kanda ya Ziwa.

Aidha, imewaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu karantini zilizowekwa kwa ajili ya kutibu nguruwe ambao tayari wameathirika na ugonjwa huo.

“Kutokana na uwepo wa Homa ya Nguruwe tumewataka wananchi wa kanda ya ziwa kuacha kula nyama ya nguruwe ilikukabiliana na ugonjwa huu hatari ambao hauna tiba wala kinga, nawaagiza viongozi mnaohusika mikoani na wilayani kuhakikisha mnasiamia karantini zilizowekwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa ugonjwa huu hausambai kwenda maeneo mengine na kuleta madhara,”amesema Waziri Ndaki.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki.

Waziri Ndaki amezitaja halmashauri ambazo hazitaruhusiwa kula nyama ya Nguruwe kuwa ni Mbogwe, Sengerema, Geita, Misungwi, Kyerwa na Kahama ambazo kwa kiasi kikubwa zimeathirika na ugonjwa huo.

Amesema hadi kufikia Januari 22, 2020 zaidi ya nguruwe 1,500 sawa na asilimia 10 ya nguruwe wote nchini wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mifugo Prof. Ezron Nonga amesema lengo la kuzuia wananchi kula nyama ya nguruwe ambayo imeathirika na ugonjwa huo ni kudhibiti usienee kwa kasi katika maeneo mengine ambayo bado hayajaathirika.

CHANZO - EATV
Share:

COCA-COLA KWANZA BACKS GOVERNMENT EFFORTS TO IMPROVE LEARNING ENVIRONMENT BY DONATING DESKS WORTH 10M/-


Coca-Cola Kwanza Director of Public Affairs and Communications Salum Nassor (left) hands over part of 100 desks to Kibiti District Commissioner Gullamhussein S. Kifu. Coca-Cola Kwanza donated the desks to three primary schools in Kibiti District, Coast Region. The donation, worth 10m/-, is an initiative intended to support government efforts towards improvement of learning.
Coca-Cola Kwanza Director of Public Affairs and Communications Salum Nassor (left) hands over part of 100 desks to Kibiti District Commissioner Gullamhussein S. Kifu. Coca-Cola Kwanza donated the desks to three primary schools in Kibiti District, Coast Region. The donation, worth 10m/-, is an initiative intended to support government efforts towards improvement of learning.
Pupils of Kigunguli Primary School and Bungu Primary School enjoys some part of 100 desks donated by Coca-Cola Kwanza Ltd to three primary schools in Kibiti District, Coast Region. The donation, worth 10m/-, is an initiative intended to support government efforts towards improvement of learning. (Photo Courtesy of Coca-Cola Kwanza Ltd).






Kibiti, Coast Region Sunday 24 January 2021.


… Coca Cola Kwanza has donated 100 desks to Kibiti District in the Coast Region, an initiative intended to support government efforts towards improvement of learning.


The beverage firm’s donation worth 10m/- that was received by Kibiti District Commissioner Mr Gullamhussein Kifu is aimed at addressing the challenges of the shortage of school desks in primary schools in the area.During the handover event held in Kibiti District, it was unveiled that the donation will benefit three primary schools in the area with high shortage of desks.


Speaking at the event, Coca Cola Kwanza Director of Public Affairs, Communication and Sustainable Growth, Mr Salum Nassor said the company’s donation aimed at bringing back to the community part of the gains.“Coca Cola Kwanza objective is to Refresh and improve lives of Tanzanians in various sectors including education and this is one of reasons for donating desks to Kibiti District,” he said.


He said the community that benefits from the Coca Cola Kwanza donation makes an integral part of the company’s customers for its varied beverage products.Mr Nassor added, “The desks donated here at Kibiti were made from the timbers used to carry raw materials for making the Coca Cola Kwanza soft drinks. This shows how the company is making efficient use of the resources available for the benefit of the community,”


The Coca Cola Kwanza Director urged other institutions, stakeholders and non-government organisations work together and support the government efforts find solution to community problems.Speaking at the event, Kibiti Member of Parliament, Twaha Mpembenwe said the donation of desks has come at the right time at the commencement of the new semester with huge number of students’ registration due to free education initiative by the fifth phase government.


On his part, Kibiti DC Mr Kifu said the donation of desks from Coca cola Kwanza demonstrate the good and healthy relations between the government and the private sector which is benefitting the community.Mr Kifu insisted that the desks donated to schools in Kibiti District will be an incentive for students to raise their performance in their examination.


Coca Cola Kwanza is a subsidiary of Coca-Cola Beverages Africa from South Africa has been one of the leading companies in making desks and supporting schools with acute shortage to improve learning environment.Since when they launched the initiative of making desks as part of its corporate social responsibility, Coca-Cola has made and distributed over 3,000 desks to various schools.
Share:

WIZARA YA AFYA YATOA TAMKO SAKATA LA ANAYEUGUZA MGONJWA KUPIGWA NA MLINZI WA SUMA JKT HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi 

Na WAMJW- Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na kitendo askari wa ulinzi (SUMA - JKT) kumpiga ndugu wa mgonjwa aliyefika kumjulia hali mama yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 

Hayo yamesemwa leo na Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi pindi akiongea na Maafisa habari wa Wizara ya Afya katika Ofisi za Wizara hiyo katika jengo la Bima ya Afya Jijini Dodoma. 

"Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na inalaani sana kitendo hicho kilichofanywa na mlinzi wa SUMA - JKT" amesema Prof. Makubi. 

Akielezea juu ya tukio hilo Prof. Makubi amesema kuwa, Mnamo Januari 22, 2021 Ijumaa jioni askari wa kujenga taifa (SUMA-JKT) alionekana akimpiga ndugu wa mgonjwa katika maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga jambo ambalo ni kinyume na maadili na taratibu za kazi.

Aidha, Prof. Makubi amesema kuwa, Wizara kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Mkuu wa Wilaya imeelekeza mlinzi huyo atolewe kwenye kituo hicho cha kazi na kurudishwa makao makuu ya kanda ya jeshi hilo kwaajili ya hatua za kinidhamu kulingana na taratibu za jeshi hilo. 

Hata hivyo, Prof. Makubi ameeleza kuwa, Katibu Mkuu (Afya) Prof. Mabula Mchembe ameelekeza kupata maelezo kutoka kwa uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga wa jinsi tukio hilo lilivotokea, mazingira yake na hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Hospitali hiyo. 

Pia, ufanyike uchunguzi kama kulikuwa na uzembe wa utekelezaji wa mfumo na mwongozo wa utoaji huduma kwa mteja (customer care) ambao ulitolewa na Wizara kwa vituo vyote vya kutolea huduma za Afya ili kuona kama kulikuwa na udhaifu mpaka tukio hili kutozuilika, huku akisisitiza baada ya uchunguzi huo hatua stahiki zitachukuliwa. 

Mbali na hayo, Prof. Makubi ametoa rai kwa wananchi kuwa watulivu wakati hatua zikiendelea kuchukuliwa, huku akiwaasa wananchi kuendelea kupata huduma za Afya bila wasiwasi kwani Serikali imejipanga kuhakikisha suala hili halijirudii tena.

"Rai ya Wizara, tunaomba wananchi wawe watulivu wakati suala hili linafanyiwa kazi, na Jamii iendelee kupata huduma katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini bila wasiwasi wowote, kwani Serikali imejipanga kuhakikisha suala hili halijirudii" amesema Prof. Makubi. 

Wakati huo huo, Prof. Makubi ametoa wito kwa wananchi kufuata na kuzingatia taratibu zilizowekwa za muda wa kuingia na kuona wagonjwa katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya nchini. 

Pamoja na hilo, Prof. Makubi amewataka wananchi kutumia vizuri mifumo ya Mawasiliano ambayo imewekwa sehemu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupiga namba 199 bila malipo na za viongozi ili kuwasilisha malalamiko ili kufikia maamuzi sahihi ya migogoro. 

Pia, amewataka Viongozi na Watumishi wote kuendelea kusimamia vizuri huduma bora za afya kwa wananchi wanaowahudumia, kisha kuwakumbusha kusimamia vizuri miongozo ya huduma kwa wateja ambayo ilishatolewa na Wizara. 

Share:

🔴 KAMPUNI YA GVEN WEAR & GVENSALES AGENCY YATANGAZA NAFASI ZA KAZI

Kampuni ya Ushonaji Nguo na Mitindo Gven Wear ya Mkoani Shinyanga ikishirikiana na Gvensales Agency  inatangaza nafasi 20 za kazi za masoko.

SIFA
👉Vijana wa kiume na kike wenye umri kati ya miaka 18 hadi 25
👉Waliomaliza elimu ya kidato cha nne
👉Wenye uelewa na wanaojitambua katika kufanya kazi za masoko

USAHILI
Vijana wenye sifa wafike katika Ofisi za Gven Wear zilizopo karibu na NMB Bank Manonga Mjini Shinyanga kwa ajili ya usahili kuanzia siku ya Jumatatu Januari 25 hadi Jumatano Januari 27,2021.

Kwa Mawasiliano zaidi piga simu 0767926671 

GVEN Wear :  Your look is our priority



Share:

SIMBA SC YAMTAMBULISHA RASMI KOCHA WAKE MPYA...NI MWAMBA HASA WA SOKA!


Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez akimkabadhi jezi ya mabingwa wa nchi Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa
Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa wakisaini mkataba

Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Kocha Mkuu mpya Didier Gomes Da Rosa wakionesha mkataba mbele ya waandishi wa habari 
Na Damian Masyenene
BAADA ya kimya cha muda mrefu na usiri mkubwa, hatimaye Wekundu wa Msimbazi Simba SC wamemtambulisha rasmi Kocha wao Mkuu atakayekinoa kikosi hicho kinachokabiliwa na mashindano mbalimbali makubwa ikiwemo kuutetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha huyo mpya wa Simba atakayerithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ni Didier Gomes Da Rosa raia wa Ufaransa.

Wakimtambulisha leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mabingwa hao watetezi wa Tanzania wamesema

"Ni Mwamba hasa wa soka la Afrika akiwa na uzoefu mkubwa wa mashindano makubwa katika bara hili, huku akiwa ameshinda mataji kadha wa kadha.

"Mwalimu huyu ana leseni A ya Uefa inayomfanya awe kocha wa daraja la juu duniani. Karibu Simba Kocha Didier na utapata ushirikiano kutoka kwa klabu na Wanasimba wote kwa ujumla. #NguvuMoja,"

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa, kocha huyo mpya amesema “Nina furaha sana kuwa hapa na tuna nafasi ya kufanya mengi pamoja mbeleni.”- Kocha Didier baada ya kutambulishwa. Timu niliyoondoka niliamua mwenyewe. Nataka kuwepo Simba kwa muda mrefu.”- Kocha Mkuu mpya, Didier Gomes Da Rosa

Katika hatua nyingine, jana Klabu hiyo ilimtambulisha kocha wao mpya wa makipa kutoka nchini Brazil, Milton Nienov, ambaye amewahi kuwa kocha wa makipa katika klabu za Polokwane City, Lamontville Golden Arrows FC, Super Eagles FC, Free State Stars FC za Afrika Kusini na Club de Regatas Vasco da Gama, Sport Club Recifie na Figueirense FC za Brazil.

CHANZO- SHINYANGA PRESS CLUB BLOG

Share:

TANGA UWASA YAANDAA MRADI MKUBWA WA KUONGEZA UZALISHAJI WA MAJI KUTOKA LITA ZA UJAZO 30,000 HADI 45,000 KWA SIKU

 

Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Mamlaka Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)Mhandisi Salum Ngumbi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga  wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga.
Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Mamlaka Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa)Mhandisi Salum Ngumbi akizungumza na wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga. kulia wa kwanza ni  na anayefuatilia ni Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla
Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akieleza jambo wakati wa mkutano huo
Wananchi wa Mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni wakiwasikiliza wataalamu kutoka Tanga Uwasa
Mkazi wa Mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Seba akiuliza swali katika mkutano huo
 

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira  Tanga (Tanga Uwasa )imeandaa mradi mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita za ujazo 30,000 kwa siku  hadi  kufikia lita 45,000 kwa siku.


Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ujenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Salum Ngumbi wakati akizungumza wakati akitoa elimu kwa wananchi wa mtaa wa Kange Kasera Kata ya Maweni Jijini Tanga.

Elimu hiyo ambayo ilitolewa wakati wa mkutano huo imekuwa endelevu kuweza kukutana na wananchi kusikiliza kero zao na namna ya kuweza kuzipatia ufumbuzi ambao ulifanyika shule ya Msingi Kasera.

Alisema kwa sasa Tanga Uwasa wanazalisha maji mita za ujazo elfu 30 kwa siku lakini mahitaji ya wananchi kwa siku ni mita za ujazo elfu 35 kwa siku.

“Kutokana na hilo ndio maana tumepanga kufanya mradi wa  kuongeza miuondombinu ya kuzalisha maji kutoka mita za ujazo elfu 30 mpaka elfu 45 kwa siku na mradi huo utaanza mwezi Aprili mwaka huu”Alisema

Mhandisi Salum alisema mradi huo utakuwa wa miezi 12 na utakuwa na manufaa makubwa mawili katika mji wa Tanga la kwanza wananchi upatikanaji wa  maji ya uhakika ambayo hayakatikikatiki na maji yatapatikana maeneo yote masaa 24.

Alisema pia wakati wa utekelezaji mradi vijana watanufaika  kwa sababu watakwenda kuongeza machujio mawili kwenye mtambo wa kusafishia maji uliopo mowe Pande.

Aidha alisema hivyo kazi ya ujenzi kubwa itafanyika na kuna tenki la kuhifadhi maji lenye ujazo wa lita milioni 1 na watakwenda kujenga jengine lenye ujazo wa lita milioni 1 eneo la Pande .

Mhandisi huyo alisema pia watalaza bomba kubwa lenye kipenyo cha milimita 600 kwa urefu wa kilomita 12.5 kutoka mowe mpaka Kange Jeshini na kwenye tenki  hilo bomba litakuwa na kazi ya kusafirisha maji wanayoyazalisha na watakiwa na mabomba mawili makubwa ya kupelekea maji Tanga.

“ Hivyo vijana watanufaika kwenye kazi za ujenzi kuchimba mitaro kwani kwenye mikataba ambayo wataingia na wakandarasi  kwamba kazi yoyote ambayo haihitaji wataalamu maalumu inatakiwa itoke sehemu ya mradi kata ya maweni inaguswa kwa eneo la Mkurumuzi mpaka kange Jeshini"Alisema 
 
Aliwataka vijana wajitokeza kwa wingi kupata hiyo ajira ya muda hivyo tunawaomba wananchi kuwa tayari kupokea mradi na kutoa ushirikiana na mradi mkubwa una thaman i ya Bilioni 8.4 na wanasoimamia wenywe wataalamu wa Tanga Uwasa

Awali akizungumza katika mkutano Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala hivi sasa wamekuwa wakijitahaidi kadri wawezavyo kuboresha huduma zao  na sasa hawana utaratibu mpaka mteja kufika ofisini kwao  wanatumia simu zao wanapata huduma.

Alisema walichokwenda kuzungumza nao leo ni kutambulisha mradi mkubwa wa kutanua mtambo wa kuzalisha na kutibu maji wa Mowe ambapo maeneo yote ya kata za Maweni na Kiomoni yataguswa moja kwa moja na huo mradi.
Share:

MTANGAZAJI MAARUFU LARRY KING AFARIKI DUNIA


Mtangazaji maarufu nchini Marekani Larry King enzi za uhai wake

Mtangazaji maarufu nchini Marekani Larry King amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87 huko Los Angeles.

Larry King alikuwa maarufu kote duniani kwa kipindi chake cha mahojiano

King ameaga dunia Jumamosi katika kituo cha matibabu cha Cedars-Sinai kulingana na Ora Media, kampuni ambayo yeye pia ni mshikiri wa uanzilishi wake.

Wakati wa taaluma yake ya miaka 60, ambayo ni pamoja na miaka 25 ya kuwa mtangazaji wa kipindi chake mwenyewe katika Shirika la CNN, King alihoji viongozi wengi maarufu wakiwemo wanasiasa, wasanii na hata wanamichezo.

Mwezi huu, alitibiwa ugonjwa wa virusi vya corona, vyombo vya habari vya Marekani vimesema.

Miaka ya hivi karibuni mtangazaji huyo amekuwa na matatizo kadhaa ya kiafya ikiwemo mshtuko wa moyo.

King alianza kuwa maarufu miaka ya 1970 kwa kipindi chake cha redio kwa jina 'The Larry King Show', katika uliokuwa mtandao wa redio wa kibiashara wa 'Mutual Broadcasting System'.

Pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha 'Larry King Live' cha CNN kati ya mwaka 1985 na 2010, akihoji watu tofauti tofauti.

Pia aliandikia makala gazeti la USA Today kwa zaidi ya miaka 20.

Hivi karibuni, King alipeperusha kipindi kingine cha, Larry King Now, kupitia mtandao wa Hulu pamoja na kituo cha Televisheni cha kimataifa cha RT kinachomilikiwa na serikali ya Urusi.

CHANZO - BBC SWAHILI

Share:

NAIBU WAZIRI SILINDE AZIAGIZA HALMASHAURI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WOTE WANAKAA KWENYE MADAWATI DARASANI


Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde ameagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha hakuna mwanafunzi anayekaa chini kwa kukosa madawati au kusoma chini ya miti kwa upungufu wa madarasa na kuagiza ujenzi wa madarasa katika wilaya zote uanze mara moja kwa yale maeneo yenye upungufu wa madarasa.

Hayo ameyasema alipotembelea shule ya msingi King'ongo iliyopo wilaya ya Ubungo mkoa wa Dar es salaam kufuatia agizo la Rais wa Tanzania Dr. John Magufuli la kutaka ujenzi wa madarasa hayo ukamilike kwa haraka.

Naibu Waziri Silinde amesema serikali ilitoa fedha kwa ajili ya ujenziwa madarasa maeneo mengi ya nchi katika mradi wa lipa kwa matokeo EP4R tangu mwezi wa Sita mwaka jana lakini madarasa bado hayajakamilika katika baadhi ya maeneo lakini ujenzi wa madarasa katika shule ya King'ongo yanakamilika kwa wiki zisizozidi tatu na kutaka watendaji katika wilaya zote kukamilisha ujenzi bila kusukumwa na viongozi wakubwa wa nchi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic amemwambia Naibu waziri wa TAMISEMI kuwa ujenzi wa madarasa huo utakamilika tarehe 31 mwezi huu na mpaka tarehe tano wanafunzi wataanza kuyatumia madarasa hayo na mpaka kukamilika yatatumia zaidi ya milion 205 ujenzi wa vyumba tisa ambavyo vitakua na madawati yake pamoja ujenzi wa choo chenye matundu 12.
Share:

MWEKEZAJI AOMBA SERIKALI KUPUNGUZA KODI YA VIFAA VYA KUANZISHIA MIRADI

Baadhi ya majengo ya Katala High School iliyopo mjini Kiomboi wilayani Iramba mkoani Singida
Mmiliki wa Katala High School ya mjini Kiomboi wilayani Iramba, Jumbe Katala akitambulisha shule hiyo kwa Umma kupitia Waandishi wa habari.

***


Na Abby Nkungu, Singida

SERIKALI imeombwa kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi ya vifaa mbalimbali vinavyoingizwa nchini na wawekezaji wa ndani kwa ajili ya kutaka kuanzisha miradi inayolenga kuboresha huduma za jamii.

Rai hiyo imetolewa na Mmiliki wa Katala High School iliyopo mjini Kiomboi Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Jumbe Katala wakati wa hafla maalum kwa ajili ya kutambulisha shule hiyo kwa umma.

Alisema kuwa licha ya Watanzania  wengi  waliopo nje ya nchi kutaka  kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha  huduma za kijamii kwa kuwekeza miradi mbalimbali nyumbani, hatua  hiyo imekuwa ikikwamishwa na utitiri wa kodi kwa vifaa wanavyoingiza  kwa ajili ya shughuli husika.

Alitolea mfano wa moja ya shehena zake za mizigo iliyokuwa imebeba vifaa mbalimbali ambavyo alikuwa ameagiza kutoka nje ya nchi kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo ambayo anadai ilitozwa kodi kubwa.

"Ushauri wangu kwa Serikali, Wawekezaji wa ndani wapewe upendeleo wa kutozwa kodi nafuu wanapoingiza vifaa mbalimbali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi yao inayohusu huduma za kijamii" alisema na kuongeza;

Hali ilivyo hivi sasa, kodi iko juu sana kiasi cha kumvunja moyo mwekezaji yeyote; hasa sisi tunaoishi nje ya nchi tukija na vifaa tunatozwa kodi asilimia 100 ya gharama hali inayoweza kusababisha baadhi yetu kukata tamaa ya kuendelea na miradi tunayokusudia kuanzisha.

Alisema kuwa wale ambao walipewa fursa ya kufutiwa au kupunguziwa kodi wakavunja uaminifu, wanaweza kushughulikiwa kama wahalifu wengine na kwamba hiyo isiwe sababu ya kuwanyima unafuu wa kodi Wawekezaji  wengine walio waaminifu na wenye nia njema ya kuisadia Serikali katika kuleta maendeleo ya nchi.

"Tunapoamua kuja kuwekeza nchini tunakusudia, mbali na kuiunga mkono Serikali yetu katika suala la maendeleo, lakini pia tunaleta fursa za ajira kwa wananchi wetu; hivyo kuipunguzia Serikali mzigo wa watu wasio na ajira. Kodi kubwa imekuwa ni changamoto kwetu" alisema na kufafanua;

Sisi tunaoishi nje ya nchi tunaona ni bora kununua vifaa huko tulipo ili kukwepa kudhulumiwa na ndugu zetu iwapo utadiriki kutuma fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo hapa nchini. Kodi inapokuwa mara mbili ya gharama ya vifaa ulivyonunua, hakika inakatisha sana tamaa"

Alisema kuwa wazo la kujenga shule hiyo mwaka 2015 lilikuja baada ya kuona kumekuwa na idadi kubwa ya shule za Sekondari zenye kidato cha nne wakati hakuna hata shule moja yenye kidato cha tano wilayani humo; hivyo kukamilika kwa ujenzi wa shule hii kutaziba pengo lililopo.

Alisema shule hiyo ambayo itagharimu zaidi ya Sh bilioni 1.5 itakapokamika na kuchukua wanafunzi 500 wa kidato cha Tano na Sita, itaanza rasmi July mwaka huu ambapo kwa kuanzia wanafunzi 100 tu wa kidato cha tano watadahiliwa.

 

"Nia yetu ni kuwa Kituo cha Umahiri wa kitaaluma ambapo wanafunzi watakaohitimu masomo yao hapa watakuwa wameiva barabara ili kuweza kuchangia kwenye soko la Viwanda. Baada ya kukamilisha ujenzi wa A level tuna mpango wa kujenga Chuo Kikuu kisha shule ya Sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne huko kijiji cha Ruruma wilayani humu" alieleza.

 

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa eneo hilo licha ya kumpongeza Mwekezaji huyo kwa  kuona  umuhimu wa kuanzisha shule ya kidato cha tano na sita, wamekuwa na maoni tofauti juu ya suala la kodi.

Wengi walisema kuwa suala la kodi halina mbadala kutokana na ukweli kwamba hiyo ni moja ya njia kuu za kuiingizia mapato Serikali ili iweze kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake mbalimbali huku baadhi wakiunga mkono hoja ya kupunguziwa kodi wawekezaji wa sekta ya elimu na nyingine zinazohusu huduma za jamii.

Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO



Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50


⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4


⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.



Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama



Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger