Thursday, 21 January 2021

Post write off Recoveries Officer at Absa

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Post write off Recoveries Officer    Bring your possibility to life! Define your career with us With over 100 years of rich history and strongly positioned as a local bank with regional and international expertise, a career with our family offers the opportunity to be part of this exciting growth journey, to reset our future […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Regional Senior Technical Officer at FHI 360

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Regional Senior Technical Officer     FHI 360 is a nonprofit human development organization dedicated to improving lives in lasting ways by advancing integrated, locally driven solutions. Our staff include experts in Health, Education, Nutrition, Environment, Economic Development, Civil Society, Gender, Youth, Research and Technology; creating a unique mix of capabilities to address today’s interrelated development […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Senior Trainer/Mentor at BBC Media Action

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Title: Senior Trainer/Mentor Reports to: Partnership Development Manager (PDM) Location: Tanzania Contract: 12 months (with possible extension) Special requirements: Legal right to live and work in Tanzania. Fluent in spoken and written English and Swahili Closing date: 31 January 2021 BBC Media Action: We are the BBC’s international charity, and we believe in the power […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Mentor/Producer-Presenter at BBC Media Action

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Job Title: Mentor/Producer-Presenter Reports to: Senior Trainer Mentor Locatin: Tanzania. The post holder will be required to spend at least 80% of their time in the field, working with radio producers at partner stations throughout Tanzania. Special requirements: Legal right to live and work in Tanzania. Fluent in spoken and written English and Swahili Contract: February […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Senior Exploration Geologist at Barrick Gold Corporation

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Senior Exploration Geologist     Barrick Gold Corporation seeks to employ a Geologist to work with the Exploration Department across our operations in Tanzania. This role reports to the Exploration Manager. The role holder will be accountable to execute the exploration programs, provide leadership, strategy and systems that delivers optimal evaluation and development of potential resources […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Research Scientists at Ifakara Health Institute

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Positions: Research Scientists (3 Posts) Reports to:   Principal Investigator Work station: Dar es Salaam Apply by:   January 29th 2021 Project: Developing and Strengthening Data Science Capacity Institute overview  Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Research Officers at Ifakara Health Institute

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Positions: Research Officers (3 Posts) Reports to:  Principal Investigator Work station:  Dar es Salaam Apply by:  January 29th 2021 Project:   Developing and Strengthening Data Science Capacity Institute overview  Ifakara Health Institute (IHI) is a leading research organization in Africa with a strong track record in developing, testing and validating innovations for health. Driven by a core strategic mandate for research, […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Grants Coordinator at Norwegian Refugee Council

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Grants Coordinator   Kibondo Job Description The purpose of the Grants Coordinator position is to provide essential grant management support to HoP and AM in delivering quality programmes in line with the NRC COs strategy and PoA for Tanzania. Adherence to NRC policies, guidance and procedures   Develop and maintain overview of all grants, donor […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Data Entry Officer at Norwegian Refugee Council

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Data Entry Officer    Job Description The WASH Data entry Officer  will be based in GOAL’s office in NRC supporting the WASH Team in managing all the program data. This position will support the WASH team in data collection and analysis, designing and managing a WASH database and the provision of analyzed data for donor […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

Various Posts UTUMISHI at MUHAS

This this content has been copied from Udahiliportal , please kindly visit udahiliportal.com to access full content

Overview:   The Public Service Recruitment Secretariat (PSRS) is a government organ with a status of independent Department established specifically to facilitate the recruitment process of employees to the Public Service. Public Service Recruitment Secretariat was established by the Public Service Act No. 8 0f 2002 as amended by Act No. 18 of 2007, section […]

This this content has been copied from udahiliportal.com , please kindly visit Udahiliportalto access full original content content or click here for more details

 

 

Share:

MWANAUME MWINGINE AFARIKI DUNIA AKIWA GESTI NA MPENZI WAKE MWANZA


Picha ya kitanda

Na Mgongo Kaitira - Mwananchi
Mtu mmoja ambaye jina lake halijatambulika amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni akiwa na mwanamke anayehisiwa kuwa ni mpenzi wake.

Tukio hilo limetokea Januari 18, 2021 katika nyumba ya kulala wageni ya Fimbo Lodge iliyopo mtaa wa Kilimahewa Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.

Mmiliki wa nyumba hiyo, Christopher Lyang’ombe akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Januari 21, 2021 amekiri kutokea kwa tukio hilo akisisitiza watafutwe polisi kwa kuwa ndio wanaoendelea na uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba wanamshikilia kwa mahojiano mwanamke mmoja (jina linahifadhiwa) anayedaiwa kuwa mtu wa karibu wa marehemu na ndiyo alikuwa naye katika nyumba hiyo.

“Mtu anayetuhumiwa inadaiwa ni mtu wake wa siku nyingi tunamhoji tu ila upo ushahidi wa awali unaoonyesha alikuwa na matatizo ya presha,” amesema Muliro.

Tukio hilo limetokea ikiwa zimepita siku tano tangu kutokea kwa tukio kama hilo ambapo mkazi wa Goba jijini Dar es Salaam, David Makerege (80) alifariki dunia katika hoteli ya Mbezi Garden alipokuwa na Neema Kibaya (33).

CHANZO - MWANANCHI

Share:

SERIKALI YAWATAKA WACHIMBAJI WALIOVAMIA MGODI WA AL-HILAL KISHAPU WAONDOKE MARA MOJA


Wachimbaji wadogo wakimsikiliza Naibu Waziri, Prof. Shukrani Manya wakati akitoa maagizo ya serikali juu ya sakata la kuvamia eneo la mwekezaji

Na Suzy Luhende, Shinyanga 
WACHIMBAJI wadogo wa madini ya Almasi waliovamia na kuanza kuchimba katika kijiji cha Mwanh'olo kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wamepewa siku mbili wawe wameshaondoka eneo hilo kwa hiari ili kumpisha mwekezaji mkubwa mwenye leseni aendelee kufanya shughuli zake katika eneo hilo.

Agizo hilo limetolewa leo Januari 21,2021 na Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya, akiwa kwenye ziara yake ya siku moja mkoani Shinyanga, ambapo alizungumza na wanunuzi wa madini viongozi wa ChamaCcha wachimbaji (SHIREMA) pamoja na wachimbaji wadogo wanaochimba katika kijiji cha Mwanh"olo kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. 

Manya amesema serikali ya awamu ya tano inawapenda wananchi wake na inataka waweze kupata maendeleo wao wenyewe na Taifa kwa ujumla, hivyo inawaomba wachimbaji hao waweze kuondoka katika eneo hilo kwa sababu ni eneo la mwekezaji Al-Hilal ambaye tayari ana leseni yake na kwamba wao watatafutiwa eneo jingine ili waweze kuendelea kuchimba.

"Nawaombeni sana muwe wasikivu na muweze kuelewa vizuri huu ujumbe wa serikali niliouleta kwenu, kwa sababu serikali inawapenda, hivyo inawapa siku mbili mkusanye mchanga wenu mliouandaa halafu mujiunge vikundi muwe na leseni yenu, serikali itawatafutia eneo zuri ambalo mtaendelea kuchimba bila bughuza yeyote, kinachotakiwa muwe waaminifu mnapopata mali muuzie katika soko letu na serikali iweze kuingiza kipato," amesema Manya.

"Msikubali kudanganywa na mtu awanunulie madini yenu tukikuta unauza kwa mtu tunakutaifisha hiyo mali yako na usafiri ulionao, hivyo tunatakiwa kuuzia kwenye mfumo ulioandaliwa na serikali, na serikali haihitaji faida kubwa inahitaji faida kidogo tu na na mtajulishwa sehemu mtakayopelekwa baada ya kutii kuondoka hapa," ameongeza.

Naibu Waziri Manya amesema eneo hilo siyo shamba la mtu kama wanavyojua bali ni mali ya serikali ambayo imeshakatiwa leseni na mwekezaji Hamad Hilal, hivyo wanatakiwa watoke kwa hiari kwani watatafutiwa eneo jingine la kuchimba ili mwenye leseni yake aendelee kufanya shughuli zake za uchimbaji.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wanaochimba katika eneo hilo Zainab Said na Leonard Daudi wamesema wamekubali kuondoka pale ila wapewe muda wa wiki moja ili waweze kuosha mchanga wao na waweze kujiandaa kuondoka na mchanga wao kwa sababu muda waliopewa ni mdogo sana na waambiwe watapelekwa sehemu gani ili wakaendelee na kazi zao za uchimbaji. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akitoa taarifa kwa naibu waziri Manya amesema anashukuru kwa kufika naibu waziri huyo, hivyo anaamini atasaidia kuondoa mgogoro wa wachimbaji wadogo na mwekezaji Al-Hilal, maana tayari nae alikuwa na mpango wa kuwapa siku chache wawe wameshaondoka eneo hilo

"Mimi na kamati yangu ya usalama wa madini tulishaenda katika kijiji hicho na tumejitahidi na tayari wachimbaji hao tulikuwa tumeshawatoa na sasa wameanza kurudi tena, lakini tunasikia wanaowafadhili ni hawa viongozi wao na baadhi ya wanunuzi tuliwataka wawaondoe watu wao katika eneo hilo," amesema Telack

Naye Afisa Madini wa mkoa wa Shinyanga Joseph Kumburu amesema tayari ofisi ya madini April 20, 2020 ilishawatoa wachimbaji 400 ambao walivamia eneo hilo lakini wakaja kurudi tena na sasa lina wachimbaji zaidi ya 1000 ivyo ofisi ya madini ilikuwa inajiandaa jinsi ya kuwaondoa na kuwakamata wachimbaji wanaovamia katika eneo la muwekezaji Al-Hilal, na kuwakamata wale wanaojimilikisha maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya akizungumza na wanunuzi wa madini na viongozi wa Chama cha Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga (SHIREMA) katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, mapema wakati wa ziara yake mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (katikati) akizungumza katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya
Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya Almasi katika Kijiji cha Mwanh'olo wilayani Kishapu ambao wanaodaiwa kuvamia eneo la mwekezaji, Mgodi wa Al-Hilal
Maeneo ya uchimbaji wa madini ya Almasi katika Kijiji cha Mwanh'olo wilayani Kishapu yanayodaiwa kuwa ya Mwekezaji Kampuni ya Al-Hilal ambayo yamevamiwa na wachimbaji wadogo
Share:

BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA TADB YATOA MIKOPO YA ZAIDI YA BILIONI 200 KWA WAKULIMA NCHINI

Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Derick Lugemala akizungumza wakati akitoa salamu kutoka Taasisi mbalimbali za Fedha wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mkoani Tanga.


Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Derick Lugemala wakati akitoa salamu kutoka Taasisi mbalimbali za Fedha wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mkoani Tanga wa kwanza kulia ni Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na anayefuatia kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

WAZIRI Mkuu Kasim Majaliwa kulia akigawa mbegu ya Mkonge kwa mmoja wa wakulima za zao hilo mkoani Tanga Elizaberth Marandu wakati alipozindua zoezi la ugawaji wa Mbegu katika Kituo cha Taasisi ya Utafiti Tari Mlingano wilayani Muheza Mkoani Tanga wakati wa ziara yake

 

BENKI ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa mikopo yenye zaidi ya thamani ya Bilioni 200 kwenye sekta ya kilimo hapa nchini ili kuongeza tija na maendeleo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao mbalimbali nchini.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Derick Lugemala wakati akitoa salamu kutoka Taasisi mbalimbali za Fedha wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Mkoani Tanga.

Akizungumzia TADB katika zao la Mkonge, Alisema kwamba wanaamini zao  la mkonge na mazao mengine ya kimkakati  ni muhimu kwa maendeleo ya viwanda na uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa.  

"TADB ipo kwaajili yakuhakikisha wakulima wanawezeshwa ilikubadili kilimo chetu kuwa kilimo biashara".

Aidha alisema katika mikopo hiyo walioitoa  kwa mkoa wa Tanga pekee wametoa mikopo yenye thamani ya Bilioni 12 huku vyama vya msingi AMCOs na wakulima wa mkonge wakipata mikopo yenye thamani ya zaidi ya billioni 1 katika juhudi zakuwezesha kilimo cha Mkonge nchini.  .

“Kwa mara ya kwanza wakati  tunaliongelea zao la mkonge tulikuwa tunafikiria tutapata wapi mbegu kwa sababu ilikuwa ni shauku yetu kubwa kuongeza uwekezaji kwenye zao hilo na tulipofika tulikwenda moja kwa moja kuwatembelea watu wa TARI. 

Katika hatua za awali za ushirikiano wa TARI na TADB, kwanza ilibidi tuwezesha TARI kwa kuwajengea kitalu kwa ajili ya kutengeneza mbegu na miche bora”Alisema

Nia ya TADB katika ushirikiano huu ilikuwa kuhakikisha wakulima wanapata mbegu bora zitakazowawezesha kupata mazao bora zaidi. 

"Shauku yetu ilikuwa tukienda kwa wakulima tukiwaambia waendelee kulima mkonge tayari tulinajua wapi watapata mbegu kipekee tunawapongeza TARI kwa uwekezaji mkubwa walioufanya hapa". Alisema.

Mkurugenzi huyo wa fedha alisema wanaamini mbegu ambazo zimezalishwa wao watakuwa sehemu kubwa ya kwenda kuwakopesha wakulima waweze kununua mbegu na kuweza kupanua mashamba yao.

 

“Labda kwa kulipokea hilo Mh Waziri Mkuu niweze kutoa hamasa hata kwa wale ambao wanatarajia kutengeneza kitalu cha  kulima mbegu hizo waweze kuona namna kuwasaliana nasi waweze kupata mikopo kutokana na kwamba bado kuna uhitaji mkubwa wa mbegu”Alisema

Hata hivyo alisema benki hiyo imeweza kuwekeza mikopo mingi kwenye sekta ya kilimo ili kuweza kuhakikisha wakulima wanalima kwa tija kubwa na kuweza kunufaika kupitia kilimo.

“Tokea tumeanza kazi ya kuchochea  upatikanaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo mwaka 2016 mikopo iliyokwenda kwenye sekta ya Kilimo ilikuwa kwa asilimia 85 ilikuwa ni ongezeko kubwa sana”Alisema

Aliongeza kuwa TADB  kwa kuona wakulima wengi hawakopesheki kwenye taasisi nyingi za kifedha kupitia mfuko wa dhamana kwa wakulima wadogo, TADB imeingia ushirika na taasisi za kifedha 11 na kutoa dhamana kwa wakulima. 

Katika zao la Mkonge tumewezesha vyama vya msingi, kampuni na wakulima binafsi kupata mikopo kwenye taasisi zingine za kifedha kupitia mfuko huo wa dhamana. 

“Tunamshukuru Rais Dkt John Magufuli na wewe Mhe. Waziri Mkuu, Wizara zote na wadau mbalimbali ambao tumekuwa tukifanya kazi pamoja kuchochea uwekezaji endelevu kwenye sekta ya kilimo nchini”Alisema

Ambapo Jumla ya Tsh  Bilioni 1 za dhamana zimetolewa na TADB kupitia benki Washirika kama vile TPB,CRDB na NMB.

Share:

JIPATIE TIKETI YAKO SASA KUSHIRIKI TUKIO LA KIHISTORIA "USIKU WA WADAU SHINYANGA"


Share:

RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MBUNGE MARTHA UMBULLA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla (pichani) ambaye amefariki dunia katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Share:

Tanzia : MBUNGE WA CCM AFARIKI DUNIA


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla amefariki dunia katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kifo cha mbunge huyo aliyezaliwa Novemba 10, 1955 kimetangazwa leo Alhamisi Januari 21, 2021 na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ambaye amesema mbunge huyo amefariki dunia jana Jumatano Januari 20, 2021 

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina,” amesema Ndugai.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mjini Babati Feisal Dauda pia amethibitisha kutokea kwa kifo cha Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Martha Umbura amefariki dunia.

Taarifa hiyo ambayo katibu wa CCM Mjini Babati ameipakia katika ukurasa wake binafsi wa Facebook, haijaeleza chanzo cha kifo chake.

Martha Umbura amekuwa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara zaidi ya miaka kumi ambapo hadi anafariki alikuwa Mbunge wa viti maalum katika mkoa huo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.
Share:

WATOTO WANING'INIZWA JUU YA MTI KUPIMWA UZITO,WAJAWAZITO WALAZWA KWENYE MADAWATI, SAKAFUNI KUPATA HUDUMA


Na Dinna Maningo,Tarime

Wananchi katika kijiji cha Nyagisya kata ya Kiore wilayani Tarime mkoani Mara wamelazimika watoto wao kupewa huduma ya Kliniki chini ya mti wa muembe huku wakining'inizwa juu ya mti kupimwa uzito na wajawazito nao wakilazwa juu ya meza,madawati,sakafuni ili kupata huduma za afya.

Malunde 1 blog imefika katika kijiji hicho ili kufahamu sababu za huduma ya Kliniki kutolewa chini ya mti ambapo akina mama wakiwa wamebeba watoto wao pamoja na wajawazito walisema kuwa wanalazimika kufanya hivyo kwa kuwa kijiji hakina zahanati na kwamba huduma hiyo ya kliniki hutolewa mara moja kwa kila mwezi.

Pia walisema kuwa wanaepuka umbali wa kilomita 4 kwenda kupata huduma ya Kliniki katika zahanati ya Mtana kata ya Manga,umbali wa km 12 kwenda zahanati ya Gamasara kata ya Nyandoto na hospitali ya wilaya ya Tarime iliyopo umbali wa km14.

Furaha Joseph mkazi wa kijiji hicho alisema,"mimi ni mmoja wa akina mama tunaoteseka kuitafuta huduma ya afya hatuna zahanati ukiugua,au kwenda kupata huduma ya clinic mpaka ujipange uwe na nauli elfu 3,000 ya pikipiki kwenda Mtana,na 5000 kwenda hospitali ya wilaya kama hauna inabidi utembee kwa miguu inachosha".

Happines Johanes alisema kuwa wanapokwenda kwenye zahanati hizo baadhi ya watoa huduma hukataa kuwapa huduma na kuwataka kwenda zahanati ya Gamasara au hospitali ya wilaya jambo ambalo liliwalazimu kuomba kupewa huduma ya kliniki katika kijiji chao ili kuepuka usumbufu.

"Tukienda Mtana nesi wanatuambia nyie nao mnatusumbua si mjenge zahanati yenu? mnakuja tu kurundikana hapa,ukiwa unaanza kliniki wanakusukuma kwenda hospitali ya wilaya. Tunashukuru serikali yetu ya kijiji ilikaa ikaona ni kwanini tuendelee kuteseka tukaona ni bora huduma ya kliniki tuifanye hapa kwetu hata kama ni chini ya mti inatusaidia kupunguza umbali na gharama za nauli na kauli mbalimbali za kukatisha tamaa", alisema Johanes.

Kutolewa huduma hiyo ya kliniki chini ya mti bado ni changamoto kwa akina mama wenye watoto na wajawazito kwa kuwa mvua ikinyesha hutangatanga kutafuta mahali pakufanyia huduma na kujikinga mvua hali ambayo wakati mwingine watoto kupimwa uzito huku nguo ikifungwa juu ya kenchi kwenye madarasa shule ya msingi Nyagisya na Wajawazito kulala juu ya madawati,meza na sakafuni kupata huduma ya cliniki.

"Mwandishi bahati nzuri umekuja siku ya kliniki na umeshuhudia mwenyewe kwa macho yako,huwa tunapima hapa chini ya mti,mvua ikinyesha tunahangaika pakupima na kujikinga ikinyesha tunaenda ofisi ya kijiji nako wakiwa na vikao vyao tunaondoka tena tunaenda shuleni tunaomba tunapewa darasa lakini sasa hivi wanafunzi wamejaa hakuna madarasa inabidi tusubiri wanafunzi wakienda kupata chakula ndiyo tunaingia kama hakuna mvua tunakaa chini ya mti",alisema.

"Nesi anafunga kikoi juu ya kenchi watoto wanapimwa uzito,kwa wajawazito  wanaunganisha madawati au juu ya meza analala anapimwa kuangalia kimo cha mtoto,mlalo,mapigo,kama anacheza huduma anapata zote isipokuwa uzito na wingi wa damu hatupimwi,ofisi ikiwa wazi kuna godoro wananchi tulinunua linawekwa chini ya sakafu mjamzito unalala nesi anapiga magoti chini anakupima,tukiwa nje wanaweka meza mjamzito unalala juu ya meza unapimwa meza tunaazima shuleni",alisema Ester Mwita.

Rhobina Meng'anyi alisema kuwa huduma hiyo wanayoipata chini ya mti ni huruma ya serikali ya kijiji na halmashauri ya wilaya ya Tarime baada ya kuona wajawazito na watoto wanavyoteseka kupata huduma ya Kliniki ambapo Mariam Wambura aliwashukuru wauguzi kuwasogezea huduma karibu licha ya changamoto nyingi wanazozipata lakini hawajakata tamaa kuwasaidia.

Wananchi walisema kuwa adha ya mama na mtoto itapungua endapo ikijengwa zahanati kwani bado kuna huduma hawazipati kiwemo ya mjamzito kutopimwa uzito,baadhi ya vipimo kukosekana ,huduma ya kujifungua na matibabu ya ugonjwa hivyo bado hulazimika kuchapa mwendo kuitafuta huduma ya afya.

Ester Simon alisema"Mama mkwe wangu alikufa njiani akiwa anaenda kujifungua alivuja damu nyingi kutokana na mitikiso ya pikipiki barabara mbuvu alafu umbali mrefu,aliacha watoto sita na mke mwenzangu alipofika hospitali ya wilaya alijifungua lakini mtoto alifariki alizaliwa akiwa kachoka,mama mkewe wangu alifia njiani akienda kujifungua aliacha watoto sita na mimi nawatoto sita wakiugua napata shida sana hakuna zahanati".

Anna Ryoba alisema kuwa ni miongoni mwa wanawake waliojifungulia njiani kutokana na umbali mrefu na kwamba kutokuwepo kwa zahanati bado wanatembea umbali mrefu ambao usababisha baadhi ya wajawazito kujifungulia njiani,naye akiwa miongoni waliojifungulia njiani na wengine kujifungua wakiwa nyumbani jambo linalosababisha wengine kufa na watoto wanauzaliwa kufa kwa kwa kukosa huduma za kitaalamu au wakunga wenye utaalamu wa kuzalisha.

Wanaume nao hawakuwa nyuma kueleza kero zao,Athanas Machera alisema kuwa umbali mrefu wa kwenda kufuata huduma ya afya umekuwa kero kwa watoto wanaoachwa majumbani na wazazi wao kwakuwa ushida njaa bila kula chakula wakisubiri wazazi kufika kuwahudumia,wakati mwingine watoto wadogo wanalazimika kuwasha moto ili kupika chakula jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao.

Thomas Wambura ambaye ni mwendesha pikipiki alisema kuwa wajawazito wengi wanajifungua usiku hivyo wakati mwingine waendesha pikipiki hukataa kuwasafirisha usiku na wale wanaokubali huwatoza gharama kubwa na wengine kucheleweshwa kufikishwa hospitali na hivyo kujifungua njiani na nyumbani na wengine kufariki dunia kwa kukosa huduma.

"Ikiwa usiku gharama ni 30,000/= huku ni porini na ni mbali kuna fisi wengi,unakuta unakaa mbali na umelala na mke wako unapigiwa simu wakati mwingine saa saba za usiku au saa nane,hali hii inawashinda mabodaboda wengi mwingine akikupigia simu unaacha kupokea na wakati huo mgonjwa ana hali mbaya anakosa msaada anazidiwa anaamua kuzaa nyumbani wengine wanakufa,au uchungu unazidi anazalia njiani", alisema Wambura.

Rebeka Samson ni miomgoni mwa wauguzi katika zahanati ya Mtana anayetoa huduma ya kliniki chini ya mti kwenye kijiji cha Nyagiswa alisema kuwa ameamua kutoa huduma hiyo kwa kuwa ni sehemu yake ya kazi licha ya kukutana na changamoto nyingi wakati wa utoaji huduma.

"Huwa tunakuja wauguzi watatu leo niko mwenyewe mmoja anaumwa mwingine yuko masomoni,tunatoa huduma ya kliniki tu kwa watoto na wajawazito inayotolewa mara moja kwa mwezi na tunahudumia wagonjwa zaidi ya 50 kama unavyoona niko peke yangu kila kitu nafanya mimi,napima watoto,wajawazito na huduma ya chanjo.

"Isipokuwa uzito wajawazito hatuwapimi mzani wa kuwapimia ni mkubwa kuusafirisha kutoka zahanati ya Mtana ni mbali unaweza kuharibika,huwa tunawashauri waende kupima Mtana,mazingira si rafiki huwezi jua juu ya mti kuna wadudu gani wabaya,wakati mwingine sisimizi wanatusumbua lakini siwezi kukata tamaa maana naipenda kazi yangu na nijukumu langu kutoa huduma,nikiwa sina nauli ya usafiri inanibidi nikope baadae ofisi yangu unilipa", alisema Samson.

Muuguzi huyo alisema kuwa wakati wa mvua anapata shida kuhamahama kutafuta mahali pakutolea huduma  na maeneo ya kutolea huduma siyo mazingira salama lakini hulazimika kufanya hivyo ili kuhakikisha huduma ya kliniki inapatikana kijijini kama njia ya kuwapunguzia umbali lakini wajawazito na watoto hufika kwa wingi kupata huduma.

Kutokana na changamoto ya ukosefu wa zahanati wanakijiji wameamua kuchangishana fedha na nguvu zao kujenga zahanati ambapo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Tarime vijijini Mwita Waitara aliwaahidi kuwachangia milioni 5 ya kununua Saruji na baadhi ya vifaa vya ujenzi.

Mkuu wa shule ya msingi Nyagisya Egid Kamala alisema kuwa shule ina eneo zaidi ya ekari 50,kutokana na changamoto ya zahanati ilitoa eneo ekari 6 kujengwa zahanati na ekari 13 kujenga shule ya Sekondari.

Athanas Wambura alimpongeza Diwani wa Kata ya Kiore Rhobi John ambaye ni mwanamke kwa madai kuwa tangu kijiji hicho kianzishwe mwaka 1974 licha ya kuongozwa na viongozi mbalimbali wa serikali ya kijiji na Madiwani wa kata hawakuwahi kuhamasisha ujenzi wa zahanati lakini yeye amekuwa Diwani wa kwanza kuhamasisha ujenzi wa zahanati na ujenzi umeanza.

Mjumbe wa Serikali ya kijiji hicho Bruno Maswi alisema kuwa wameamua kusitisha ujenzi wa sekondari kwa kuwa kata hiyo ina sekondari mbili na kugeukia kwenye zahanati kutokana na kero nyingi ikiwemo wajawazito kufukuzwa zahanati ya Mtana na baadhi ya wagonjwa kunyima huduma.

Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha Nyagisya ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Senta Ghati John alisema kuwa sababu za wajawazito na watoto kupata huduma chini ya mti ni kutokana na kuwepo mgogoro kati ya kata yao ya Kiore na kata jirani ya Manga kuliko na zahanati ya Mtana kuwataka kujenga zahanati yao nasiyo kwenda kusongamana kwenye zahanati ya Mtana.

"Tukiwa hatuna vikao na hakuna watu wengi tunaowahudumia tunawaachia ofisi wanawahudumia wajawazito,nawapongeza wananchi kwa kujitolea kuhakikisha tunajenga zahanati wagonjwa na Wajawazito wanateseka sana uongozi wa kijiji tulikaa na uongozi wa shule tukashauriana eneo likapatikana la kujenga zahanati nawaomba wadau mbalimbali waguswe watusaidie tukamilishe ujenzi tumechoka kutukanwa na watu wa Mtana", alisema.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyagisya Waitara Kemo ambaye ana miezi minne tangu ahamishiwe kwenye kijiji hicho alisema kuwa tayali wananchi wamechimba msingi kwa nguvu zao,wamechanga fedha na tripu 5 za mawe zimenunuliwa,matofali 3,500,tripu nne za mchanga,mifuko 30 ya saruji na kuna kiasi cha milioni 1 na vitatumika kuanzia ujenzi na kwamba lazima ujenzi utakamilika ili kusogeza karibu huduma ya afya.

Diwani wa kata ya Kiore Rhobi John alisema kuwa kwakuwa wajawazito na watoto wanateseka sana akiwa kama Diwani wa kwanza mwanamke kuchagulia ndani ya kata hiyo atazidi kuhamasisha ujenzi wa zahanati baada ya kuona wagonjwa,wajawazito na watoto wanavyoteseka nakwamba Zahanati itakamilika mwaka huu na atashirikiana na wananchi wa kata yake katika maendeleo.





Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger