Sunday, 3 January 2021
Saturday, 2 January 2021
KATAMBI ARIDHISHWA KASI UJENZI VYUMBA VYA MADARASA, AMWAGA MAMILIONI YA FEDHA
Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi, (katikati) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, akishiriki kwenye ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika shule ya Msingi Mlimani Old Shinyanga.
Awali Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, katikati mwenye mavazi ya njano, akiwa kwenye ziara ya kukagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Mwangulumbi iliyopo Chibe Manispaa ya Shinyanga.
JESHI LA POLISI SHINYANGA LAKANUSHA TAARIFA ZA DEREVA WA LORI ALIYEPIGWA NA ABIRIA WA BASI LA FRESTER KUFARIKI DUNIA
KAMATI YA FEDHA,UONGOZI NA MIPANGO YAANZA KUCHUNGUZA MAGARI YA HALMASHAURI
JIKO LA MKAA LAUA WATU WATANO WA FAMILIA MOJA
MLEZI WA SKAUTI MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI AFANYA ZIARA MKOANI MBEYA
Mjumbe wa Bodi wa Skauti, Christopher Mwasambili (kulia) akizungumza kwenye kikao cha bodi.
Na Dotto Mwaibale, Mbeya
KAMISHNA Mkuu Msaidizi wa Skauti Tanzania anayeshughulikia makambi na mazingira ambaye pia ni mlezi wa mikoa ya Mbeya, Ruvuma na Iringa, Mary Anyitike amefanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa juzi, Anyitike alisema kuwa lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kuangalia utendaji kazi na kutembelea Uwanja wa Skauti wa Ally Hassan Mwinyi uliopo mkoani humo.
" Lengo la ziara hii ya siku moja ilikuwa ni kuangalia utendaji kazi na kutembelea uwanja wetu ambapo pia nilipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wajumbe wa bodi ya skauti mkoani hapa na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Skauti, Dkt.Julius Kaijage." alisema Anyitike.
Aidha Anyitike alisema kuwa katika ziara hiyo alipata fursa ya kuzungumza na wananchi wanaoishi jirani na uwanja huo na wafanya biashara ndogo ndogo kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi na kudumisha ujirani mwema.
Kamishna wa Skauti Mkoa wa Mbeya, Sadock Ntole alisema ziara hiyo ya kikazi ya Anyitike imewapa mori zaidi wa kazi na kuwa ujumbe walioupata ataufikisha katika wilaya zote za mkoa huo.
"Tumefarijika sana na ziara ya mlezi wetu na yote aliyotuelekeza tutayafanyia kazi" alisema Ntole.
AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II at Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu
POST AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II – 1 POST POST CATEGORY(S) SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu APPLICATION TIMELINE: 2020-12-31 2021-01-13 JOB SUMMARY NA The deadline for submitting the application is 13 January, 2021 CLICK HERE TO APPLY
The post AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II at Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu appeared first on Udahiliportal.com.
AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA II at Halmashauri ya Wilaya ya Igunga
POST AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA II – 1 POST POST CATEGORY(S) SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT EMPLOYER Halmashauri ya Wilaya ya Igunga APPLICATION TIMELINE: 2020-12-31 2021-01-13 JOB SUMMARY NA The deadline for submitting the application is 13 January, 2021 CLICK HERE TO APPLY
The post AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA II at Halmashauri ya Wilaya ya Igunga appeared first on Udahiliportal.com.
AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II at Halmashauri ya Manispaa ya Musoma
POST AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II – 1 POST POST CATEGORY(S) SOCIOLOGY, POLITICAL SCIENCE, COMMUNITY AND SOCIAL DEVELOPMENT EMPLOYER Halmashauri ya Manispaa ya Musoma APPLICATION TIMELINE: 2020-12-31 2021-01-13 JOB SUMMARY NA The deadline for submitting the application is 13 January, 2021 CLICK HERE TO APPLY
The post AFISA MAENDELEO YA JAMII MSAIDIZI DARAJA LA II at Halmashauri ya Manispaa ya Musoma appeared first on Udahiliportal.com.
PROCUREMENT & STORES MANAGER at TADB
BACKGROUND OF TADB Tanzania Agricultural Development Bank Limited (TADB) is a Government Institution established under the Companies Act, 2002 and licensed under the provisions of the Banking and Financial Institutions Act No 5 of 2006 and the Banking and Financial Institutions (Development Finance) Regulations, 2012. The bank has the following key objectives: To catalyze credit […]
The post PROCUREMENT & STORES MANAGER at TADB appeared first on Udahiliportal.com.
11 Teachers and Other Job Opportunities at Helasita Secondary School
History Helasita Secondary School was established under Company’s Act, Cap.16 of 2002 with mandate to provide education services. The school philosophy is to train students holistically by promoting such skills as; critical and independent thinking, creativity, innovation, communication, rational decision making, team work and adaptability to different environmental contexts just to mention a few. Join […]
The post 11 Teachers and Other Job Opportunities at Helasita Secondary School appeared first on Udahiliportal.com.
Professional Cleaners at Blue Sapphire Hall
ABOUT US Blue Sapphire Hall located at Jangwani Beach (opp. Ramada Resort) is a one stop events venue with modern facilities that hosts various events ranging from conference hall, wedding services, exhibitions (Local & International) and corporate events. IDEAL FOR: WEDDINGS | SEND OFF | CORPORATE EVENTS | EXHIBITION Posts available : 2 Gender […]
The post Professional Cleaners at Blue Sapphire Hall appeared first on Udahiliportal.com.
55 Government Job Opportunities at The University of Dar es Salaam (UDSM) – Various Posts
Overview: The University of Dar es Salaam is the oldest and biggest public university in Tanzania. It is situated on the western side of the city of Dar es Salaam, occupying 1,625 acres on the observation hill, 13 kilometers from the city centre. It was established on 1st July 1970, through parliament act no. 12 […]
The post 55 Government Job Opportunities at The University of Dar es Salaam (UDSM) – Various Posts appeared first on Udahiliportal.com.
Uingereza sasa rasmi iko nje ya umoja wa Ulaya
Nchi ya Uingereza, imeanza ukurasa mpya wa kujitegemea kutoka umoja wa Ulaya, baada ya usiku wa kuamkia jana kukamilisha rasmi safari ya kujitoa kwenye umoja huo.
Uingereza, iliacha kufuata sheria za umoja wa Ulaya kuanzia saa sita usiku kuamkia Ijumaa, ambapo sasa itakuwa na sheria zake za kusafiri, biashara, uhamiaji na usalama.
Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, amesema "uhuru uko mikononi mwao" na kuwa na uwezo wa "kufanya vitu tofauti na kwa namna bora", akisema mchakato wa muda mrefu wa kujitoa umekamilika.
Licha ya hatua hii, wanasiasa na watu waliopinga nchi hiyo kujitoa umoja wa Ulaya, wanasema hali itakuwa mbaya zaidi.
Waziri wa kwanza wa Uscotishi, Nicola Sturgeon, ambaye mara zote amekuwa akitaka nchi yake kubaki kwenye umoja wa Ulaya, amesema kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter "Scotland itarejea karibuni kwenye umoja wa Ulaya, kuweni na imani".
Mawaziri wa Uingereza, wameonya kuhusu uwezekano wa kushuhudiwa sintofahamu katika baadhi ya mambo, wakati huu taifa hilo likitekeleza sheria zake tofauti na zile za umoja wa Ulaya.
-RFI
Benard Membe Atangaza Kung'atuka ACT- Wazalendo
Aliyekuwa mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe ametangaza rasmi kujiuzulu uanachama na nafasi ya mshauri mkuu wa chama hicho.
Amesema kwa sasa, atabakia kuwa mshauri kitaifa na kimataifa wa kushughulikia na kupigia debe masuala ya demokrasia kwa taifa lake.
Hatua ya kujiuzulu ameitangaza kijiji kwao Rondo- Chiponda Mkoani Lindi, nchini Tanzania jana Ijumaa tarehe 01 Januari 2021, wakati akizungumza na DW.
Hata hivyo, hakutoa ufafanuzi zaidi juu ya sababu ya kuchukua maamuzi hayo.
Membe amesema,tayari ameandika barua ya kujiuzulu kwa kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kama utaratibu unavyotaka.
Hata hivyo, waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje wa Tanzania katika utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Mrisho Kikwete amesema, kwa sasa ni mapema kubainisha mwelekeo wake unaofuata katika vyama vya siasa.
Membe aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania kati ya 2007 hadi 2015 ametangaza uamuzi huo leo akiwa nyumbani kwake kijijini Rondo Chiponda, Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi ambapo amesema hajafanya uamuzi huo kwa shinikizo lolote na kwamba kwa sasa atakuwa mshauri wa masuala mbalimbali yanayoihusu nchi ya Tanzania na kupigania demokrasia ya kweli.
Mwanadiplomasia huyo alitangaza kuhamia Chama cha ACT Wazalendo miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 baada ya kufukuzwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tarehe 28 Februari 2020 na Kamati Kuu ya chama hicho, kisha uamuzi huo kubarikiwa na Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), tarehe 10 Julai 2020.
Membe alifukuzwa kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili ya CCM, pamoja na kuonywa mara kadhaa, pasina kubadilika.
Baada ya kuhamia ACT Wazalengo, Membe alitangaza kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho.
Taarifa Ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya Makusanyo Ya Kodi Mwezi Desemba 2020
Akitoa taarifa hiyo jijini Dar es salaam, Kamishna Mkuu wa TRA Dkt Edwin Mhede amesema, kiwango hicho cha ukusanyaji.mapato kimevuka lengo walilojiwekea la kukusanya Shilingi Trilioni 2.072.
Amewaambia Waandishi wa habari kuwa, ongezèko hilo la ukusanya mapato kwa kiasi kikubwa limechangiwa na mwamko wa Walipa kodi ambao wamekuwa wakilipa kodi zao kwa hiari.
Kwa mujibu wa Dkt Mhede, Idara ya walipa kodi wakubwa kwa mwezi Desemba mwaka 2020 pekee ilikusanya takribani Shilingi Trilioni Moja, Idara ya forodha ilikusanya mapato ya asilimia 97 ikikuatiwa na Idara ya walipa kodi.
NFRA Wajipange kununua Mahindi mengi kwa Wakulima – RC Wangabo
Wakati Utekelezaji wa lengo la Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) la kuweka mfumo wa kisasa wa kutunza mazao kufikia asilimia 80. Wakala hao wameshauriwa kujiandaa kununua mahindi mengi Zaidi ili kuwahakikishia wakulima soko la mazao yao katika kipindi cha msimu wa 2020/2021
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema kuwa ni vyema NFRA wakaongeza fedha za kununua mahindi na kisha kutafuta soko nje ya nchi hasa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Pamoja na nchi nyingine ili kuwapa fursa wakulima nchini kufanya biashara na NFRA ili kuepuka kuhangaika kutafuta soko la mazao yao.
“Mkoa wa Rukwa tumezalisha tani za mahindi tani 585,000 na matumizi yetu ya ndani ni tani 291,000 kwahiyo tulikuwa tuna ziada ya tani 294,000, sasa ukiangalia kwamba tani 294,000 halafu mahindi yananunuliwa tani 11,000 kwahiyo mahindi mengi yalibaki ndio kikawa kilio cha wakulima wa mkoa wetu wa Rukwa kwahiyo nategemea kwamba ukamilishwaji wa vihenge hivi NFRA itakuwa na uwezo wa kuchukua tani 58,500, hii kwa sisi mkoa wa Rukwa ni sawa na kuingiza na kutoa ili wawauzie watu wengine.”
“Kwahiyo niwaombe NFRA ndio wamekuwa mkombozi sasa kwa wakulima, mjipange vizuri ili kuongeza fedha muweze kununua mahindi mengi kwa wakulima vinginevyo wakulima watakata tamaa na sasa wanaendelea kuzalisha baada ya kuona kwamba hivi vihenge hapa vinakwenda kukamilika kwahiyo uwezo wa NFRA utakuwa mkubwa Zaidi wa kununua mahindi kwa wakulima, ninyi mnao uwezo wa kuona wapi muyapeleke hayo mahindi, ninyi mfanye biashara na nje na sisi tufanye biashara na nyie,” Alisema.
Kwa upande wake Mhandisi Mkazi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mhandisi Haruna Kalunga amesema kuwa hadi tarehe 28.12.2020mkandarasi ameshatumia muda wake wa miezi 15 sawa na asilimia 83 ya muda aliopewa kwenye mkataba huku utekelezaji ukiwa ni asilimia 80 na hivyo kuufanya mradi kuwa nyuma kwa asilimia 3 na kuongeza kuwa ucheleweshwaji huo umechangiwa na kucheleweshwa kwa msamaha wa kodi wa vifaa vinavyotoka nje ya Tanzania.
Kwa mkoa wa Rukwa mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Unia Araj kutoka Poland ikisaidiana na Mkandarasi Mzawa Elerai kutokea Arusha kwa thamani ya Dola za marekani 6,019,399.00 ambayo ni asilimia 30 ya mradi mzima unaotekelezwa katika mikoa mitatu Pamoja na Mkoa wa Katavi na Manyara wenye jumla ya thamani yad ola za marekani 20,280,906.00.