Tuesday, 1 December 2020

SERIKALI YAGUSWA NA JUHUDI ZA HUAWEI KUKUZA TEHAMA NCHINI

 Group-photo-1024x593 Speaker-1024x475


NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dk.Jim Yonazi amepongeza juhudi za Huawei za kuboresha ubora wa elimu ya ICT ili kuongeza ujuzi wa kuajiriwa kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini Tanzania.

Dk Yonazi alitoa pongezi hizo wakati wa Sherehe za Ufunguzi wa msimu wa tano wa programu ya "Seeds for the Future" ambao ulifanyika mtandaoni mapema wiki hii.

Kwa mara ya kwanza hapa nchini, programu ya "Seeds for the Future" ilizinduliwa mnamo 2016 kwa msaada wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Programu hiyo ilihusisha Vyuo Vikuu 4 wakati ikizinduliwa na sasa inajumuisha Vyuo Vikuu 7 ambavyo ni Chuo Kikuu ya Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbeya (MUST), Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT ) na Chuo Kikuu cha Elimu cha Dar es Salaam (DUCE)

"Nimearifiwa kuwa katika kuchangia ukuzaji wa vipaji vya TEHAMA nchini Tanzania na kuendana na mipango ya kimkakati ya nchi, Huawei imeongeza kwa kiasi kikubwa shughuli na ushirikiano na Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu hapa nchini. Hizi ni juhudi za kupongezwa kwa kwa kuwawezesha vijana wa kitanzania. ” Dkt. Yonazi wakati akitoa hotuba yake kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Zainab Chaula.

Pia, Dk Yonazi amewataka wanafunzi kutumia maarifa wanayopata kwenye programu hiyo kufundisha wengine ili kufaidisha idadi kubwa ya watu haswa wale ambao hawakuwa na bahati kama wao.

“Nawapongeza wanafunzi wote ambao wameshiriki katika program ya Seeds for the Future mwaka huu. Nawashauri watumie fursa hii ipasavyo kukuza maarifa yao na kupata uzoefu wa vitendo katika TEHAMA. Ninawahimiza pia kushiriki uzoefu waliopata na wenzao ili kuendeleza na kunoa maarifa waliyoyapata.” Aliongeza

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania, Frank Zhou aliangazia mipango ya Huawei ya kuiwezesha Tanzania kukabiliana na mahitaji ya teknolojia kidijiti ambayo yanabadilika mara kwa mara.

"Tunafahamu kuwa maendeleo ya dijiti yanahitaji mipango madhubuti ili kuiwezesha Tanzania kiuchumi kwa siku zijazo. Katika zama hii mpya, ujuzi wa TEHAMA utakuwa muhimu kwa jamii, kwa mashirika, na muhimu zaidi kwa vijana. Ndio maana tumewekeza kwa kina katika mipango kadhaa haswa ukuzaji wa vipaji zna ujuzi." Alisema.

Mwaka huu, ili kufikia vijana wengi zaidi nchini Tanzania, Programu ya “Seeds for the Futrure” itafanyika mtandaoni ili iweze kuchukua idadi kubwa ya wanafunzi kutoka mikoa tofauti na ili wanafunzi wenye mahitaji maalum pia washiriki. Ikilinganishwa na miaka ya nyuma, Huawei imeweza kuongeza idadi ya nafasi za mafunzo kutoka wanafunzi 10 hadi 47.

“Ninajivunia kuwatangazia kwamba baadhi ya washiriki hao ni wanawake, ambao wana nafasi muhimu sana katika tasnia ya TEHAMA. Ninapenda kuhamasisha wanafunzi wengi wachanga wanaohudhuria kozi hiyo kuangalia na kuijikita zaidi katika tasnia ya Mawasiliano." Aliongezea

Kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Habari, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Leonard aliisifia program ya "Seeds for the Future" na nafasi yake katika kuwawezesha vijana na kukuza uwezo wa kuajiriwa.

"Programu hii ni mfano madhubuti wa ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Huawei Tanzania katika kujenga mazingira yenye afya na endelevu ya rasilimali watu katika TEHAMA. Programu ya “Seeds for the Future” inafanya kazi kama daraja ambalo linaunganisha pengo lililopo kati ya mafunzo ya kinadharia na mahitaji ya vitendo katika soko la ajira. ”Alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha teknolojia wa Airtel, Bwana Prosper Mafole aliwahimiza wanafunzi kutumia fursa za kujifunza zinazotolewa na Huawei na akawakaribisha kwa msaada wowote endapo watahitaji.

Bwana Yuan Lin, Mshauri wa Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Tanzania, ameipongeza kampuni ya Huawei kwa kuonesha mfano mzuri katika kukuza vipaji vya TEHAMA nchini Tanzania kwa kuwajengea uwezo vijana wa shahada ya kwanza ambao watakuwa msukumo wa mabadiliko ya TEHAMA nchini Tanzania katika siku za usoni.

"Ubalozi wa China nchini Tanzania unahimiza makampuni mengine ya China kuwa na mipango kama hii ili kusaidia katika kuandaa wataalamu ambao wanasimama imara katika kutimiza malengo ya Tanzania ya uchumi wa viwanda na kuwa nchi ya kipato cha kati." Alisema.

Sherehe ya ufunguzi wa "Seeds for the Future" ilihudhuriwa na maafisa wa Serikali mashuhuri wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na Mshauri wa Uchumi na Biashara wa Ubalozi wa China nchini Tanzania Bwana Yuan Lin.

Share:

Fahamu Kwanini INFINIX Note 8 Ni Simu Pendwa Kwa Mwaka Huu Wa 2020.


Toleo jipya la simu ya Infinix 8 Note iliyozinduliwa hivi karibuni imebeba processor aina ya Helio G80 ikiwa ndio sifa kuu kwa simu hiyo na kupelekea kuvunja rekodi yake yenyewe kwa kuja na simu janja yenye mfumo wa kukidhi mahitaji ya wadau wenye matumizi makubwa ya simu. 


Infinix NOTE 8 imekuja na sifa nyengine zenye kuifanya simu hiyo kuwa ya kipekee kama vile 64MP Ultra HD 6, Battery mAh 5200, kioo cha nchi 6.95, Android 10.


Processor
MediaTek Helio G80 processor ikichagizwa na MediaTek HyperEngine Game Technology ambayo inaipa nguvu simu hiyo na kuiwezesha kufanya kazi kwa haraka na kuhakikisha kuwa simu hiyo inagusa maeneo mengine yote ya kimsingi kwa ufanisi. Chipset yenye sifa ya kufanya kazi vizuri imefungwa katika simu hiyo si tu kuifanya iwe nyepesi wakati wa matumizi bali inaifanya kuwa imara zaidi.


Inarahisisha games zinazochukua muda mrefu kufunguka kwa haraka na kucheza kwa ufanisi, zinatumika katika maeneo maalum na games zenye ukubwa. Simu hii imeongezewa ufanisi wa hali ya juu na maboresho ya uunganishwaji kwa minajili ya kuwezesha mtu kucheza game bila bughudha. 


Battery
Infinix NOTE 8 imebeba ujazo wa battery yenye mAh 5200M lengo ni kuona mtumiaji wa Infinix Note 8 anaifurahiya simu yake kwa muda mrefu pasipo hofu ya kuzima chaji lakini pia hujaa chaji kwa haraka. hii inapewa nguvu na teknolojia ya hali ya juu (power marathon) iliyomo ndani ya simu janja ambayo hata kama chaji inakwisha inaiwezesha kutunza chaji kwa muda fulani. Kwa wapenzi wa games, hii itawahakikishia wanakuwa na muda mrefu wa kucheza au kutazama na Kwa mfanyabiashara au mjasiriamali aliyefanikiwa, Note 8 inakupa uhakika wa haya yafuatayo kwa urahisi kama vile kutuma barua pepe, kutumia apps zinazohusu shughuli za kiofisi, kutumia apps za kufanya mikutano kupitia video na mengine zaidi.


Vile vile simu hii ina teknolojia ya injini mbili. Jambo hili linaifanya Infinix Note 8 kuwa ya baridi, ikipunguza joto kwa jotoridi 8 wakati inachajiwa.


Kamera
Moja ya sifa kubwa zinazoitofautisha simu hii na simu nyingine ni kuwa na kamera kubwa mbili 64MP Ultra HD 6nyuma na 16MP mbele. Kioo chake kikiwa na uwiano wa 20.5:9 ambacho kina kamera ndogo mbili ambapo inakiwezesha kioo cha simu hiyo kuzunguka kufikia eneo la kamera kiasi cha kutoleta usumbufu ukiitumia kuangalia video kwenye simu.


Simu hiyo yenye kioo chake cha kisasa (6.95" Dual Infinity-O Display) kinasaidia kamera kuchukua picha zenye ubora kwa kuhakikisha hakuna vizuizi vyovyote vitakavyoharibu ubora wa picha.


Infinix pia imepata suluhisho la kukabiliana na mazingira ya mwanga mdogo ambalo limekuwa likiwasumbua watumiaji wakati wakichukua video. Kwa kutumia zaidi ya siku 180 (usiku na mchana) kufanya utafiti na maboresho kukabiliana na suala hili, simu hii ina mfumo maalumu wa kuiwezesha simu kufanya kazi katika mazingira ya giza (Note 8’s Ultra Night Mode 2.0) inakupa matokeo mazuri katika mazingira yenye mwanga hafifu.


Muonekano
Muonekano wake utaweza kuwavutia watu mbalimbali na kwa namna simu hii ilivyo umuhimu wake utaongezeka maradufu kama ambavyo ilivyo muhimu kwa mtu kuvaa nguo mwilini mwake. Simu hii ina muundo mwepesi sambamba na GEM CUT ambayo imebuniwa kwa kuangalia mitindo inavyokwenda na hadhi yake. Uumbaji wa simu hii ambao bado ni mfano wa kuigwa umebebwa na mistari ya kipekee na uhalisia wa teknolojia. Muundo wake wa Gem Cut ni mahususi kwa ajili ya kubadili muonekano wa mtumiaji. 


Mapokezi
Ukipitapita madukani na kwenye mitandao ya kijamii utagundua ni simu iliyopokelewa vizuri sana na hii ni huenda na wanachokipromoti ndicho wateja wanachokutana nacho baada ya ununuzi, Infinix NOTE 8 imepokelewa vizuri na watu wa rika lote hasa wale wenye kuitumia simu kama chombo muhimu katika shughuli za kila siku za kujipatia kipato.


Upatikanaji
Infinix NOTE 8 inapatikana kwa bei isiyozidi sh. 540,000 katika maduka yote ya simu nchini Tanzania ikiwa na ofa ya GB 96 kutoka Vodacom lakini pia unaweza tembelea https://www.infinixmobility.com/tz/ .

MAWASILIANO;
0744606222




Share:

Utayari Wa Wafugaji Kushirikishwa Kwenye Miradi, Hufanya Miradi Hiyo Kudumu


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugp na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wafugaji wanaposhirikishwa katika uchangiaji wa miradi mbalimbali kwa ajili ya mifugo yao wamekuwa wakionyesha utayari na kufanya miradi hiyo kudumu kwa kuwa wanajisikia kuwa sehemu miundombinu hiyo.

Akizungumza (31.11.2020) katika bwawa la kunyweshea mifugo maji la Elwaniolera lililopo kijiji cha Eluwai, Kata ya Monduli Juu, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, Prof. Gabriel amesema wakazi katika eneo hilo wameonesha utayari wa kulifanyia ukarabati bwawa hilo linalohudumia zaidi ya wafugaji 2,000 katika vijiji vya Eluwai, Emairete na Enguiki kutokana na kina cha bwawa hilo kupungua kutokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ikiwemo ya kilimo.

“Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli umenieleza kuwa wakazi wa Kata ya Monduli Juu wako tayari kushiriki kwa kiwango kikubwa katika kulifanyia maboresho bwawa hili, wafugaji wanaposhirikishwa nao wako tayari kushiriki na faida yake kubwa hakutakuwa na haja ya serikali kugharamia kila kitu lakini pia wanaposhirikishwa mara zote miundombinu hiyo huwa inadumu kwa kuwa nao watajisikia sehemu ya miundombinu hiyo.” Amesema Prof. Gabriel

Ameongeza kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo tayari kulikarabati Bwawa la Elwaniolera kwa kujenga mabirika kwa ajili ya mifugo kunywea maji kwa kuwa hali ilivyo sasa ni hatari kwa mifugo, wachungaji pamoja na usalama wa bwawa lenyewe.

Aidha, Prof. Gabriel amesema wizara itaangalia namna ya kuboresha masuala ya majosho katika vijiji vya Eluwai, Emairete na Enguiki ili kuhakikisha kwamba dhana nzima ya kuboresha afya ya mifugo inafanikiwa.    

Pia, amesema wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akizindua Bunge la 12 alifafanua kuwa angependa kuona Sekta ya Mifugo inachangia zaidi katika uchumi.

Amebainisha kuwa kwa sasa Sekta ya Mifugo inachangia kwa asilimia 7.64 na inakuwa kwa asilimia tano ambapo lengo la wizara ni kuhakikisha sekta hiyo ifikie kuchangia kwa zaidi ya asilimia 15.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema Kata ya Monduli Juu ina mifugo mingi hivyo masuala ya malisho na afya ya mnyama ni muhimu kwa kuwa na mifugo mingi na bora ni muhimu kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli ili wafugaji waweze kunufaika kupitia Bwawa la Elwaniolera ili maji yake yaweze pia kutumika katika shughuli nyingine za kilimo cha umwagiliaji.

Kwa upande wake Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli Dkt. Yandru Marmo amemueleza Prof. Gabriel kuwa Bwawa la Elwaniolera limeanza kupungua kina chake kutokana na shughuli za kibinadamu zinazoendelea katika chanzo cha maji ya bwawa hilo, hali inayosababisha udongo kusafirishwa hadi kwenye bwawa na kusababisha kina chake kuzidi kupungua na kuhofia madhara makubwa kwa wafugaji wanaolitegemea kunyweshea mifugo maji.

Dkt. Marmo ameongeza kuwa ni muhimu kwa bwawa hilo kufanyiwa ukarabati kwa kuwepo kwa mabirika ya kunyweshea mifugo maji ili mifugo isiingie ndani ya bwawa kwa kuwa inachangia pia udongo kuingia ndani ya bwawa pamoja na shughuli za kibinadamu ikiwemo ya kilimo zisifanywe karibu na chanzo cha maji ya bwawa hilo ili kuzuia pia udongo kusafirishwa hadi kwenye bwawa na kusababisha kina chake kupungua.

Bwawa la Elwaniolera lililopo Kata ya Monduli Juu, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, lilijengwa mwishoni mwa miaka ya 1970 kwa jitihada za serikali wakati Hayati Edward Moringe Sokoine akiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MWISHO.


Share:

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Yatoa Awamu Ya Tatu Ya Mikopo Ya Tzs Bilioni 11.04 Kwa Wanafunzi Wapya 3,544


Na Mwandishi Wetu,HESLB,
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya Awamu ya tatu yenye jumla ya wanafunzi wapya 3,544 waliopangiwa mikopo kwa mara ya kwanza katika mwaka wa masomo 2020/2021 yenye thamani ya TZS 11.04 bilioni.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumanne Desemba Mosi, 2020 na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru ilisema ili kupata taarifa za kina kuhusu mikopo waliyopangiwa, wanafunzi hao 3,544 wanashauriwa kutembelea akaunti zao walizotumia kuomba mikopo kwa njia ya mtandao maarufu kama SIPA – Student’s Individual Permanent Account (SIPA).

“Kufuatia kutolewa kwa awamu hii ya tatu, hadi sasa jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo ni 53,364 yenye thamani ya TZS 173.29 bilioni. Aidha, jumla ya wanafunzi 69,625 wanaoendelea na masomo wamepangiwa TZS 247.5 bilioni baada ya kufaulu mitihani yao ya mwaka 2019/2020” alisema Badru.

Kufunguliwa kwa dirisha la rufaa
Badru alisema baada ya kutangazwa kwa awamu ya tatu za upangaji mikopo, hatua inayofuata ni kufunguliwa kwa dirisha la rufaa kwa siku saba (07) kuanzia kesho (Jumatano, Desemba 2, 2020) ili kuwawezesha waombaji ambao hawajapangiwa mikopo au hawajaridhika na viwango walivyopangiwa kuambatisha nyaraka za ziada kuthibitisha uhitaji wao.

Kwa mujibu wa Badru alisema Katika kipindi cha rufaa, wanafunzi watahitajika kutembelea mfumo wa olas.heslb.go.tz, kufuata maelekezo na kuwasilisha rufaa zao kutoka popote walipo BILA MALIPO YOYOTE kwa HESLB” alisema Badru.

“HESLB inatoa wito kwa wanafunzi ambao bado hawajapangiwa mikopo na ni wahitaji, kutumia muda wa siku saba (07) za rufaa kuwasilisha nyaraka sahihi ili hatimaye wapangiwe mikopo ya kuwawezesha kulipia gharama za masomo” alisema Badru.

HESLB ilianzishwa na sheria mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi Julai, 2005 ili kuwawezesha watanzania kupata elimu ya juu na kukusanya fedha za mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika.

MWISHO


Share:

Halima Mdee, Wenzake Kukata Rufaa Ndani ya Chadema


Aliyekuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima James Mdee amesema, yeye pamoja na wenzake 18 hawatoondoka ndani ya chama hicho na wanaendelea na utaratibu wa kukata rufaa kupinga kufukuzwa.


Mdee amesema hayo leo Jumanne tarehe 1 Desemba 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kutoa msimamo wao baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema.
 

Mdee na wenzake 18 walituhumiwa kwa “usaliti, kughushi na uasi” wa chama hicho kwa kujipeleka kuapishwa tarehe 24 Novemba 2020 na Spika Job Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum, wakijua chama hicho, hakijapendekeza majina yao Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Uamuzi wa kamati kuu, ulitolewa mbele ya waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe tarehe 27 Novemba 2020 akisema, Mdee na wenzake wamekisaliti chama na kama hawaridhiki na uamuzi huo, wanaweza kukata rufaa baraza kuu ndani ya siku 30 au kuomba radhi.

“Nimejitokeza hapa kuja kutuliza haya mambo maana yanaonekana ni makubwa ila nimekuja kuyaweka yanavyotakiwa yawe, mimi na wenzangu tumekuja hapa kuzungumza nanyi, na niwaambie sisi ni CHADEMA kindakindaki,” amesema Mdee

Kuhusu tuhuma za kununuliwa, Mdee amesema hajawahi kuwaza kununuliwa na wala hatarajii kwani yeye ni miongoni mwa wabunge waliokuwa wanapinga rushwa ndani ya bunge.

“Kumekuwa na maneno mengi, kuna watu wanasema Halima nimenunuliwa, naomba niseme mimi sijanunuliwa, sinunuliwi na sitarajii kununuliwa.”

Pia amezungumzia madai ya wao kugomea wito wa kamati kuu kama mwenyekiti wa chama hicho alivyosema wakati wa kutoa maamuzi ya kamati hiyo, Mdee amesema waliiandikia barua kuomba wapewe muda ili waweze kwenda wakiwa na majibu ya busara.

“Hatukudharau kikao, tuliomba tu Wiki moja mbele, Mbowe amenijenga Mimi, ametujenga, inawezekana kuna Vijana wana ya kwao lakini kuna Viongozi tunawaheshimu sana kwasababu wana mchango mkubwa wa sisi kuwa hapa, lakini hatimaye tumevuliwa Uanachama

“Sisi tumefukuzwa ila tutakuwa Wanachama wa hiyari, ndio maana tumevaa gwanda za CHADEMA, mamlaka za rufaa zipo Baraza Kuu, jana jioni tumepata barua ya taarifa ya uamuzi, mchakato wetu wa rufaa tutaanza kuutafakari ili tuangalie namna ya kutatua tatizo

“Tunaipenda CHADEMA, tunaiheshimu CHADEMA, hatutoondoka CHADEMA, tutabaki Wanachama wa hiyari mpaka tutakapomaliza mchakato wa ndani ya Chama wa kumaliza matatizo yetu, naamini tutayajenga ndani kwetu, leo sizungumzi nje na kuongeza matatizo

“Tuna dhamira za kuchukua hatua za Kikatiba ndani ya Chama chetu na hatua nyingine kwa kadri ambavyo tutaona zina afya kwa pande zote mbili, na kwakweli nimetukanwa sana na hili limenisadia kujua Marafiki wa kweli na wale ambao walikuwa wananisikilizia” -Amesema Halima Mdee



Share:

Housegirl Mbaroni Kwa Kumchoma Kisu Mgeni


Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni ACP, Ramadhani Kingai amethibitisha kifo cha kijana aliyechomwa kisu na dada wa kazi.

Ezekiel Nyamko mkazi wa Kimara, alichomwa kisu mara mbili kwenye kifua na mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa rafiki yake, tukio lililopelekea kifo chake.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa Nyamko alienda kumtembelea rafiki yake Kelvin ambaye wazazi wao pia ni marafiki na alipofika aliomba chakula lakini mtuhumiwa alimnyima na kumwambia kuwa bado wenyeji hawajala hivyo asubiri. Nyamko alimjibu kuwa “una roho mbaya kama sura yako” na kuongeza kuwa ndiyo maana Kelvin hamuoi.

Maneno hayo yalimkera mtuhumiwa na kufikia hatua ya kumchoma kisu kifuani mara mbili marehemu.

Mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Hapiness ameshikiliwa na polisi huku mwili wa marehemu ukiendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi.


Share:

Madini Kuchangia Mabilioni Kwenye Pato La Taifa


Na Jonas Kamaleki, MAELEZO
Tanzania imejaliwa kuwa na maliasili nyingi zinazoweza kuifanya nchi hii kuondokana kabisa na umasikini na utegemezi, hivyo kujiendesha bila kutegemea misaada toka nje ya nchi.


Licha ya kuwa na hifadhi za taifa za wanyama, bahari, maziwa, mito na milima na mabonde, nchi hii imejaliwa pia kuwa na madini, bidhaa muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi.
Takriban madini aina zote yanayopatikana duniani yapo Tanzania ikiwemo Tanzanite inayopatikana nchini pekee. Huu ni utajiri kwa vizazi na vizazi endapo Yyataendelea kudhibitiwa, kusimamiwa,kulindwa na kutumiwa ipasavyo. Yataliingizia Taifa mabilioni ya shilingi.


Juhudi za makusudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kutumia vizuri rasilimali ya madini zimeifanya Tanzania kuingiza mabilioni ya fedha ambazo zinatumika katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya Afya, Elimu na Miondombinu ya barabara, reli na umeme.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ambaye ni muasisi wa mageuzi makubwa katika Sekta ya Madini, Dkt. John Pombe Magufuli anasema haya kuhusiana na madini: “Kwenye miaka mitano iliyopita tumepata mafanikio makubwa kwenye sekta ya madini. Mapato yameongezeka kutoka shilingi bilioni 168 mwaka 2014/2015 hadi shilingi bilioni 527 mwaka 2019/2020. Mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019.”


Aliongeza kwa kusema, “Zaidi ya hapo, kwa mara ya kwanza, katika historia ya nchi yetu, mwaka 2019, sekta ya madini iliongoza kwa kutuingizia fedha nyingi za kigeni, Dola za Marekani bilioni 2.7. Nitumie fursa hii kulipongeza Bunge la 11 kwa kutoa mchango mkubwa katika kupatikana kwa mafanikio haya.” 


Fedha iliyopatikana kutokana na madini yaani bilioni 527 inaweza kutoa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka na nusu, inaweza kujenga vituo vya afya 1,150 au inaweza kulipia gharama ya elimu ya awali hadi sekondari kwa kipindi cha miaka miwili (yaani miezi 24).


Sekta ya Madini ikiendelea kusimamiwa vyema maendeleo makubwa katika nchi yatapatikana na kuibadilisha Tanzania kiuchumi na kuingia uchumi wa kati wa juu hadi kufikia uchumi wa juu wa nchi zilizoendelea kama vile Marekani, Uingereza, Sweden Ujerumani, China na nyinginezo ndani ya kipindi kifupi.


Akionyesha dhamira yake ya dhati kuhusu mchango wa madini katika kukuza uchumi wa Taifa, Rais Magufuli aliongeza, “Kwenye miaka mitano ijayo, tutaendelea kuimarisha ulinzi na usimamizi wa madini yetu, (kama tulivyofanya kwa kujenga Ukuta Mirerani) kwa kuimarisha Sheria zetu ili madini yetu yasitoroshwe na Serikali kukoseshwa mapato. Aidha, tunakusudia kuendelea kufanya majadiliano na wawekezaji wakubwa kwa kuzingatia mfano wa Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Kampuni ya Barrick yaliyowezesha kuundwa kwa Kampuni ya Twiga Minerals Corporation.”


Ujenzi wa ukuta wa Mirerani umedhibiti kwa kiwango kikubwa utoroshwaji wa Tanzanite na kufanya nchi hii kupata mauzo makubwa ya madini hayo. Zaidi ya hayo amepatikana bilionea mzawa kutokana na udhibiti huo Bwana Saniniu Laizer ambaye amejipatia zaidi ya shilingi bilioni11kwa kuiuzia Serikali ya Tanzania madini ya Tanzanite.


Aliyekuwa Waziri wa Madini, Doto Biteko alisema,“Ujenzi wa ukuta kuzunguka machimbo ya madini eneo la Mirerani na kuweka vifaa vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kuwa madini yaTanzanite ambayo ni rasilimali ipatikanayo Tanzania pekee inalindwa. Kufuatia uwekezaji huo, sote tumeshuhudia kuongezeka mara dufu kwa mapato yatokanayo na madini ya Tanzaite katika eneo hilo hususan kutoka kwa wachimbaji  wadogo kutoka shilingi 166,094,043 kabla ya kujenga ukuta hadi shilingi 2,150,000,000 baada ya kujengwa kwa ukuta.”


Lilikuwa jambo la kushangaza kuona Tanzania haikuwa ya kwanza wala ya pili hata ya tatu kwa kuuza Tanzanite duniani wakati madini hayo yanapatikana Tanzania pekee katika dunia nzima. Uelekeo wa sasa utaifanya nchi hii kuwa kinara katika uuzaji madini hayo. Na kwa kufanya hivyo pato la Taifa litaongezeka.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alinukuliwa akisema haya kuhusu kudhibiti utoroshwaji wa madini, “Katika kukabiliana na utoroshwaji wa madini, Serikali iliamua kuanzisha masoko ya madini nchini kwa lengo la kuondoa mianya ya kuweza kufanya biashara ya madini kupitia njia zisizo rasmi. “Hadi sasa tuna jumla ya masoko ya madini 27 na vituo vidogo vya ununuzi wa madini 28 kote nchini.”


Aliongeza kuwa masoko hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha upatikanaji sahihi wa takwimu za madini tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya kuanzishwa kwake.
“Masoko haya yanafanya kazi katika misingi ya kiushindani na uwazi wa kibiashara. Pia, niwahakikishie kuwa masoko yetu yana ulinzi na usalama wa kutosha na sifa zote za kimataifa zinazohitajika katika kuendesha biashara hiyo. Hivyo, yatumieni vizuri masoko haya,”alisema Waziri Mkuu.


“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali, ikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite, chuma, bati, nickel, copper, n.k. Aidha, tuna gesi aina mbalimbali, kama vile ethane, helium, ambayo hivi karibuni zimepatikana futi za ujazo bilioni 138 kwenye Ziwa Rukwa, ambazo zinaweza kuhudumia dunia kwa miaka 20. Hii ndiyo sababu, kila siku nimekuwa nikisema, sisi sio masikini; sisi ni matajiri. Nchi yetu ni tajiri sana”,alisema Rais Magufuli hivi karibuni wakati akizindua Bunge la 12 jijini Dodoma.


Rais Magufuli alibainisha juhudi nyingine za Serikali kwa kusema:“Kuhusu madini pia, kwenye miaka mitano ijayo pia tutaendelea kuliimarisha Shirika letu la Taifa la Madini (STAMICO) ili lishiriki kikamilifu kwenye shughuli za madini; kuwawezesha wachimbaji wetu wadogo, ikiwa ni pamoja na kuwatengea maeneo ya uchimbaji, kuwapatia mafunzo, mikopo pamoja na vifaa. Na natambua kuwa, wapo baadhi ya watu wamepewa leseni za utafiti na uchimbaji lakini hawajazifanyia kazi; tutazifuta leseni zao, na maeneo hayo kuyagawa kwa wachimbaji wengine, hususan wachimbaji wadogo. Wachimbaji wadogo ni muhimu sana katika kukuza sekta ya madini.”


Serikali itaendelea kuimarisha masoko ya madini pamoja na kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya uchenjuaji, uyeyushaji, usafishaji na utengenezaji wa bidhaa za madini.


Haya yote yanalenga pia kuongeza thamani ya madini na kuongeza ajira hasa kwa vijana zitakazotokana na shughuli zinazohusu madini kama vile uchenjuaji na utengenezaji wa bidhaa za madini 


“Tunataka madini yachimbwe hapa Tanzania, yachenjuliwe, yayeyushwe na kisha bidhaa za bidhaa za madini zitengenezwe hapa hapa Tanzania; na ndipo ziuzwe nje ama watu kutoka nje waje kununua bidhaa za madini hapa nchini. Ni imani yetu kuwa, kutokana na hatua tulizopanga kuzichukua sekta ya madini itaweza kuchangia angalau asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025, alisisitiza Rais Magufuli.


Mchango wa asilimia 10 kwa Pato la Taifa utakuwa mchango wa maana ambao utasaidia katika kutekeleza miradi ya kimkakati ya maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi mkubwa utakaosaidia kuboresha maisha ya watanzania.




Share:

Ahukumiwa Jela miaka 2 kwa kumkata viwembe mtoto wa kambo


Mahakama ya Wilaya ya Kigoma imemtia hatiani Agnes Damian (40) mkazi wa Mji Mwema Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kosa la kumkata kwa wembe sehemu mbalimbali za mwili binti wa miaka 15 ambaye ni mtoto wa mume wake.

Katika hukumu hiyo iliyodumu kwa takribani dakika 18 ikisomwa na Hakimu Eva Mushi amesema adhabu hiyo inapaswa kuwa fundisho na onyo kwa wanatenda matukio ya kikatili hasa kwa watoto.

Hakimu Mushi ameongeza kuwa hukumu ya kesi namba 95/2020 imezingatia sheria ya adhabu kifungu 225 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisbo mwaka 2019.

Tukio hilo lilitokea Juni 18 mwaka usiku ambapo mtuhumiwa aliingia chumbani na kufanya ukatili huo akimtuhumu kuwa binti huyo alimpiga mwanae na kwamba lazima ampe onyo.

Imebainishwa kuwa binti huyo alijeruhiwa kwa wembe maeneo ya miguu, mapaja na mgongoni

Kesi hiyo ilikuwa chini ya mawakili wa serikali Happiness Mayunga na Crement Masua ambapo mara baada ya hukimu wakili Masua ameeleza kutoridhishwa na kifungo cha miaka miwili huku akioneshwa kuridhishwa na faini ya milioni 5.

Kabla ya adhabu hiyo, Agnes aliomba kupunguziwa adhabu kwa kuwa anatunza watoto wawili, ni yatima na hivi karibu amepona ugonjwa wa kupoza japo hajawa timamu asilimia mia moja.

Kwa kuzingatia ushahidi wa watu sita wakiwemo baba mzazi, majirani, daktari na askari, hakimu alimuhumuku kifungo cha miaka 2 jela na faini milini 5 na kwamba iwe fundisho kwa wengine.


Share:

Raia wa Burundi wakamatwa kwa kuishi nchini kinyemela


Raia wawili wa Burundi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai ya kuingia na kuishi nchini bila kuwa na vibali vinavyotambulika kisheria

Akisoma hati ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Yusto Ruboroga, Wakili wa Serikali Shija Sitta amedai kuwa washitakiwa hao Sindandugu John na Chekelo Aziz walikamatwa eneo la Msimbazi, jijini Dar es Salaam Novemba 24 mwaka huu kwa tuhuma ya kuingia nchini bila vibali na kuishi nchini bila kuwa na nyaraka zinazotambulika kisheria.

Aidha Wakili Sita amedai kuwa washitakiwa hao baada ya kuingia nchini walianza kufanya kazi ya kuendesha pikipiki maarufu bodaboda.

Hata hivyo washitakiwa hao wamekana shitaka lao na kesi hiyo imeahirisha hadi Disemba 14 mwaka huu kwa ajili ya washitakiwa kusomewa hoja za awali.

Akizungumza kwa niaba ya Idara ya Uhamiaji mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili Sitta amewataka wananchi kuepuka kutoa ajira kwa watu wanaoingia nchini bila kuwa na taarifa kamili za uraia wao kwa ajili ya usalama wa Taifa.


Share:

AFYA YA WAFANYAKAZI NCC NI THAMANI KWA KAZI ZETU-DKT MTURI

Na Mwandishi Wetu

WAKATI dunia ikiadhimisha Siku ya Mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi, Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limesema limefikia malengo yake ya kuhakikisha wafanyakazi wanaelimishwa kuhusu Ukimwi na maambukizi ya virusi visababishavyo ugonjwa huo, kwa mwaka huu.

Limesema litahakisha zana muhimu zinazohitajiwa na wafanyakazi kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya VVU na Ukimwi (Kondomu) zinaendelea kupatikana kwa urahisi katika maeneo yote ambako zinapaswa kuwepo ndani ya ofisi hiyo, kwa ajili ya wahusika kuchukua na kwenda kuzitumia pindi wanapokuwa wakizihitaji.

Mtendaji Mkuu wa Baraza hilo, Dk Matiko Mturi alisema Dar es Salaam jana kuwa, mpango wa kulinda wafanyakazi wake dhidi ya maambukizi ya magonjwa hasa Ukimwi ni endelevu na kwamba unatekelezwa kupitia mafunzo, ushauri nasaha na njia nyingine zinazotumika kufikisha ujumbe kwa wafanyakazi kuhusu namna bora ya kujikinga, kama vile semina na maandiko mbalimbali vikiwemo vipeperushi na ajenda maalumu kwenye vikao vyote vya wafanyakazi.

“Tunashukuru kwamba wafanyakazi wa NCC wamekuwa wakitoa ushirikiano wa hali ya juu kufanikisha utekelezaji wa mpango mkakati wetu wa kuwapa elimu kuhusu masuala ya afya hususan namna ya kujikinga na maambukizi ya VVU pamoja na mambo yote wanayopaswa kuyajua kuhusu Ukimwi,”alisema.

Kutokana na maelezo ya Dk Mturi, NCC ilifanikiwa kupima kwa hiyari wafanyakazi wake, baada ya kuwaandaa kisaikolojia na kufanikiwa kuwapa elimu iliyohitaji sit u kuhusu Ukimwi bali hata magonjwa mengine ambayo walipaswa kupata elimu kuyahusu.

Alisema lengo la kuweka mpango mkakati huo, pamoja na kutimizwa kwa matakwa ya Serikali ya kuhakikisha vita dhidi ya maambukizi ya VVU na Ukimwi vinapiganwa hata katika maeneo ya kazi kwa wafanyakazi kupewa elimu ya kujikinga na maradhi, ni kuhakikisha usalama wa afya za wafanyakazi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“NCC inajali na kuthamini afya ya wafanyakazi wake, kwa sababu ndio watenda kazi wanaotegemewa katika uzalishaji wa kila siku, hivyo kutokuwa na afya njema kwao ni tatizo pia kwa mlolongo mzima wa ut

Share:

Field Officer at Food For His Children Tanzania

Job Title: Field Officer Location: Karatu, Arusha, Tanzania JOB DESCRIPTION/RESPONSIBILITIES Discipleship: provide individual teaching of D4D principles and Biblical values to help individuals grow in their relationship with Jesus and to understand who they were created to be and how their role fits with the rest of their family and community. Demonstrate Christ-like behavior in all areas […]

The post Field Officer at Food For His Children Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Network Engineer at Computer Centre Tanzania Limited

Network Engineer Company Name Computer Centre Tanzania Ltd Company Location Dar es Salaam, Tanzania MINIMUM REQUIREMENTS: Qualifications: · Relevant IT Degree or Advanced Diploma – Information Systems · CCNP: Cisco Certified Network Professional – Routing and Switching or equivalent · Fortinet NSE3/4 or Sophos Certified Engineer – XG Firewalls or Yeastar will be an added advantage CERTIFICATIONS […]

The post Network Engineer at Computer Centre Tanzania Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Resident Operations Manager at SiSi Multibiz Limited

Resident Operations Manager Location: Dar es Salaam, Tanzania About the job Urgently looking for candidates on below positions for our small boutique resort property in Kigamboni, Dar es Salaam. Position: Resident Operations Manager F&B manager QUALIFICATION: Preferably Tanzanian, EA citizens may be considered… Must have at least 2yr similar position experience & 5yr hospitality work background Basic […]

The post Resident Operations Manager at SiSi Multibiz Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Immigration Consultant at Migratio Group Tanzania

ob Title: Immigration Consultant Location: Dar es Salaam, Tanzania A career as an Immigration Consultant at Migratio gives you the opportunity to work with a smart, motivated, and diverse peer group. Our exclusive focus on immigration means you will practice in an exciting, ever-changing, and challenging environment with people who are passionate about immigration. Migratio is […]

The post Immigration Consultant at Migratio Group Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Restaurant Manager at Andigo Tanzania

Job Title: Restaurant Manager   Location: Dar es Salaam, Tanzania Overview We are seeking a Restaurant Manager with a background of managing Zanzibar/Indian/Asian Food Menu. The ideal candidate must be a Tanzanian national comfortable working n an Indian and Zanzibar style restaurant setting, preferably speaking Hindi. We offer a basic salary and performance-based incentives. Responsibilities   […]

The post Restaurant Manager at Andigo Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Various Posts at Favorite HR Services Tanzania

Branch Manager Location: Dar es Salaam, Tanzania Overview Industry: Banking Location: Dar es Salaam Minimum Education: Bachelors Degree Required Experience: At least 5+ Years Job Purpose   Ensuring overall branch management; staff management, business growth and development, operational excellence Develop and implement business strategies to deliver performance and growth targets and maintain a good business […]

The post Various Posts at Favorite HR Services Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

IT Support Officer at AccessBank Tanzania (ABT)

Job Title: IT Support Officer Overview AccessBank Tanzania (ABT) is a commercial bank with a special focus on microfinance. With very strong international shareholders such as AccessHolding, International Finance Corporation, KfW, African Development Bank and MicroVest. ABT’s vision is to be committed to the development of financial systems that support social progress by rendering services to […]

The post IT Support Officer at AccessBank Tanzania (ABT) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger