Thursday, 19 November 2020

Rais wa Zanzibar Dr Mwinyi Atangaza Baraza la Mawaziri


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo November 19, 2020, aMEtangaza Baraza jipya la Mawaziri la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika hafla maalum inakayofanyika Ikulu.

Mwinyi amesema Katika Baraza hilo, zipo wizara mbili ambazo bado hajateua mawaziri (Wizara ya Afya na Wizara ya Biashara). Asema hajateua Naibu Waziri yeyote katika baraza hilo, atateua kama akiona kuna wizara inahitaji Naibu.

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI ZANZIBAR:

1. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uchumi na Uwekezaji – Mheshimiwa Mudrik Ramadhan Soraga.

2. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) – Mheshimiwa Masoud Ali Mohammed.

3. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba na Utawala Bora – Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman.

4. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango – Mheshimiwa Jamal Kassim Ali.

5. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi – Mheshimiwa Dokta Khalid Mohammed Salum.

6. Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji na Mifugo – Mheshimiwa Soud Nahoda Hassan.

7. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali – Mheshimiwa Simai Mohammed Said

8. Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni – Mheshimiwa Tabia Mwita Maulid.

9. Wizara ya Biashara ya Maendeleo ya Viwanda. Hakuna Waziri.

10. Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi – Mheshimiwa Riziki Pembe Juma.

11. Wizara ya Maji na Nishati – Mheshimiwa Suleiman Masoud Makame.

12. Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto. Hakuna Waziri.

13. Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale – Mheshimiwa Lela Mohammed Mussa.

14. Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Mheshimiwa Abdallah Hussein Kombo.

15. Wizara ya Ujenzi – Mheshimiwa Rahma Kassim Ali.



Share:

PRINCIPAL RECEIPTIONIST Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy

The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy. Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the Mwalimu […]

The post PRINCIPAL RECEIPTIONIST Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PRINCIPAL SUPPLIES OFFICER I Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy

The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy. Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the Mwalimu […]

The post PRINCIPAL SUPPLIES OFFICER I Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

MKURUGENZI WA MASHTAKA TANZANIA AWAONYA WANAOFICHA VIFAA VYA UJENZI 'SIMENTI 'NA MABATI'


Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini kuacha kuficha Vifaa hivyo.
**
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Biswalo Mganga amewaonya wauzaji wa vifaa vya Ujenzi kufuatia baadhi yao kuficha Simenti na Mabati kwa lengo la kuongeza bei ili kujipatia faida kubwa zaidi, na kusema kuwa kufanya hivyo ni kosa la Jinai.

Bw. Mganga ameeleza kuwa watu wote wanaofanya hivyo wanafanya kosa la uhujumu uchumi ambalo limeanishwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kutaifishwa mali kwa yeyote atakayekamatwa kwa kutenda kosa hilo.

Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo Jijini Dodoma leo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika yaliyokuwa na lengo la kufahamu mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tangu kuanzishwa kwake ambapo ameeleza kuwa imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake.

Aidha, amesema kuwa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kuhakikisha kuwa Haki, Amani na Usalama vinapatikana nchini kwa Maendeleo ya Taifa. Mwonekano wa nembo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma
 
 Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Biswalo Mganga akusoma Dira ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
Mwonekano wa mbele wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) lililoko Jijini Dodoma
Share:

FULL POWER, ZATI 50 NI KIBOKO YA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA UUME MDOGO

Zati 50
Full Power
Sababu za upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume:


⇒Ngiri,

⇒Henia

⇒Kisukari

⇒Tumbo kujaa gesi

⇒Kutopata choo vizuri

⇒Utumiaji madawa kwa muda mrefu

⇒Unywaji wa pombe kupita kiasi

⇒Msongo wa mawazo 



⇮⇒Haya yote hupelekea mwili kutokuzalisha homoni ya gesrtogine au kuwa chache na kushindwa kupata mzunguko mzuri wa damu na vichocheo vingine kama madini ya zinki ambayo hukufanya kuwa na msisimko  na kufanya kuwa na muda  mrefu na nguvu za kutosha.



FULL POWER



⇨Ni dawa ya vidonge ya miti shamba inaongeza nguvu za kiume na kutibu kabisa tatizo hilo.



⇨Inaongeza hamu ya tendo la ndoa

⇨Inakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya Dakika 30 na kurudia tendo zaidi ya mara nne na zaidi.

Zati 50


⇨ Inarutubisha maumbile ya uume  na kunenepesha urefu nchi 6,unene sentimita 4


⇨Dawa hii ni ya kutibu kabisa tatizo hilo.



Pia tunatibu Magonjwa mengine Kama



Matatizo ya pumu,Bawasiri, vidonga vya tumbo,Kisukari,Magonjwa sugu ya zinaa,Kaswende,U.T.I , kiuno,miguu kuwaka moto, Fangasi sehemu za Siri, kupunguza unene wa mwili,tumbo kuunguruma,kujaa gesi, matatizo ya uzazi kwa wanawake, kurutubisha mbegu za uzazi kwa akina baba, matatizo ya meno tunatibu bila kungoa

Kliniki yetu inapatikana Zanzibar, Dar es salaam na Shinyanga.

Wasiliana nasi kwa simu namba 071770 22 27
Share:

UZINDUZI WA MTANDAO WA WANAWAKE LAKI MOJA KUFANYIKA DESEMBA 5,2020

 

Share:

DED UKEREWE : KATAENI BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WATOTO


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ukerewe Bi Esther Chaula
****
Jamii wilayani ukerewe Mkoani Mwanza imetakiwa kuacha tabia ya kuwatoa watoto wao kwenda kufanya kazi za majumbani badala yake wawape elimu ili waweze kutimiza ndoto zao kwani ndiyo msingi wa maisha yao ya baadaye. 

Wito huo umetolewa Novemba 17 na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe Bi. Esther Chaula katika hotuba yake ya ufunguzi wa awamu ya pili ya mradi wa kupinga usafirishaji haramu wa watoto na uhamiaji usio salama kwa minajili ya kuwatumikisha kazi hatarishi unaotekelezwa wilayani humo na Shirika la KIWOHEDE kwa ufadhili wa terres des hommes-Netherlands (TDH-NL). 

Alisema kama jamii kila mmoja akitimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuchukizwa na vitendo vya usafirishwaji watoto ukimchukulia huyo mtoto anayefanyia vitendo hivyo kama mtoto wako inawezekana kabisa kumalizia tatizo hilo. 

"Mchukulie yule mzazi ambaye ni rahisi kurubuniwa kirahisi kwamba nipe mtoto ebu jiangalie kwamba yule mzazi ungekuwa ni wewe ndiyo ukawa unarubuniwa wewe ili mtoto wako aende kufanyishwa kazi na kuteseka ungejisikiaje?" alisema.

Aidha aliwataka watendaji wa wilaya na mamlaka za serikali za mitaa kushirikiana na kiwohede katika kutekeleza awamu ya pili ya mradi huo kwani wamekuwa wakifanya shughuli hizi kwa kuinua ustawi wa jamii kwa kufuata misingi ya utekelezaji wa sera na afua zinazowekwa na serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kiwohede Bi Justa Mwaituka aliishukuru ofisi ya Mkurugenzi kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiupata kila mara wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

“Kwanza niipongeze ofisi yako kwa namna ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa maafisa wangu kila mara wanapokuja kwako kama unavyofahamu mradi huu una mashirikiano ya karibu na maafisa ustawi, maafisa maendeleo ya jamii, elimu, mipango na idara nyingine kwa kweli Kumekuwa na ushirikiano mkubwa”, alisema.

Aliongeza kuwa katika awamu ya kwanza ya mradi kwa kushirikiana na idara Mbalimbali kama maendeleo ya jamii, dawati la jinsia na watoto pamoja na ustawi wa jamii Wametoa ushauri nasaha, wamefanikiwa kutengeneza mifumo ya upatikanaji wa huduma za afya kwa watoto, wametoa mafunzo mbalimbali ya stadi za maisha, wametoa misaada ya kisheria na kuwarejesha baadhi yao mashuleni kuendelea na masomo. 

Kwa upande wake mratibu wa mradi Amos Juma aliyataja mafanikio yaliyopatikana katika awamu ya kwanza ni pamoja na watoto 6477 kufikiwa kupitia vipindi vya mafunzo kupitia vilabu mashuleni na mitaani huku watoto 165 wakipewa ushauri wa kisheria na ushauri nasaha pamoja na wazazi 200 kujengewa uwezo wa malezi bora. 

Afisa mradi kutoka Tdh-NL Valence Nkulanga alisema shirika lao linaendelea na shughuli za kuhakikisha hakuna mtoto anayenyonywa huku wakiendelea kutoa ufadhili kwa shirika la kiwohede kuhakikisha wanafanikiwa kudhibiti biashara haramu ya usafirishaji watoto kupitia mradi huo. 

Mradi huo unafanyika katika vijiji 36 vilivyopo katika Kata 8 ukitekelezwa na Shirika la kiwohede kupitia ufadhili kutoka shirika la kimataifa la terres des hommes - Netherlands(Tdh-Nl). 

Uzinduzi huo wa awamu ya pili ya mradi umefanyika wilayani ukerewe na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wilayani humo akiwemo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri (alikuwa mgeni rasmi) , maafisa maendeleo, maafisa elimu, mkuu wa polisi dawati la jinsia na watoto, viongozi wa dini, viongozi wa serikali ngazi ya kata na vijiji, walimu wa shule, waandishi wa habari na maafisa wa Kiwohede.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwohede Bi Justa Mwaituka akizungumza
Wp Bernadetha afisa wa polisi dawati la jinsia na watoto akitoa mada
Valence Nkulanga afisa mradi kutoka TDH-NL akitoa mada
Washiriki wa uzinduzi wakiwa ukumbini.
Mshiriki akichangia mada
Washiriki wa uzinduzi wakiwa katika picha ya pamoja
Share:

PRINCIPAL SUPPLIES OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy

The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy. Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the Mwalimu […]

The post PRINCIPAL SUPPLIES OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

PRINCIPAL PUBLIC RELATION OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy

The Mwalimu Nyerere Memorial Academy invites application from suitably qualified Public Servants who wish to transfer to the Mwalimu Nyerere Memorial Academy.   Establishment of the Academy The Mwalimu Nyerere Memorial Academy (MNMA) is a public higher learning institution which was established by an Act of Parliament No. 6 of 2005. The Origin of the […]

The post PRINCIPAL PUBLIC RELATION OFFICER II Transfer Vacancies at Mwalimu Nyerere Memorial Academy appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

RC SHINYANGA APIGA MARUFUKU SARUJI KUUZWA BEI JUU


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akikagua bei ya Saruji kwenye moja ya ghara mjini Shinyanga.
****

Na Marco Maduhu, Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amebaini sababu za wafanyabiashara kupandisha bei ya Saruji mkoani humo, na kupiga marufu kuuza bei ya juu.

Mfuko wa Saruji mkoani humo una oanzia pointi 32 na 42, unauzwa kwa bei moja kuanzia shilingi 20,000/= ,21,000/= hadi 22,000/=, kwa wafanyabiashara wa maduka, lakini wenye maghara wanauza tofauti mfuko wa pointi 32 ni Shilingi 17,500/=, na 42 ni 18,000/=.

Telack alibaini utofauti huo  jana alipofanya ziara ya kukagua bei ya Saruji kwenye maduka na maghara mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga, na kusema kuwa Saruji ipo ya kutosha, isipokuwa kuna ujanja ambao unafanyika kwa wafanyabishara kutaka faida kubwa.

"Nimebaini kuna ujanja ambao unafanyika wa kuuza Saruji, wafanyabiashara wa kawaida wananunua Saruji kwa wenye maghara bei ya kawaida shilingi 17,500/= na 18,000/=, lakini wao wanapandishia wananchi na kuuza zaidi ya 20,000/=," alisema Telack.

"Kuanzia sasa napiga marufuku kwa wafanyabiashara, hakuna kuuzia wananchi bei ya saruji kuanzia shilingi 20,000/= bali bei iwechini ,waache kutaka kupata faida kubwa na kuumiza wananchi," aliongeza.

Naye mmoja wa wafanyabiashara wa kuuza Saruji kwenye maduka John Ngalya, alikiri kupandisha bei ya saruji, kwa madai kuwa na wao wanauziwa bei ya juu kutoka kwa wanunuzi wakubwa wanaotoa Saruji moja kwa moja kutoka viwandani.

Kwa upande wake wakala wa kusambaza Saruji kwa wafanyabiashara kutoka  viwandani Shufaa Mabula, alisema bei ya Saruji imepanda kutokana na uzalishaji kuwa mdogo tena wa older, na kusababisha kuingia gharama ya kusubili mzigo.

Nao baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwamo Estormine Henry, waliipongeza Serikali kuingilia kati suala hilo la kupanda kwa Saruji ambalo lilisababisha kupanda kwa gharama za ujenzi.
Zoezi la ukaguzi bei ya Saruji likiendelea.
Mmoja wa mawakala wa usambazaji saruji kutoka viwandani Shufaa Mabula (kushoto),akielezea sababu za kupanda kwa bei ya Saruji, kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack.
Share:

Serikali yawaonya wamiliki wa maduka ya dawa


 SERIKALI imewataka wamiliki wa maduka ya dawa za binadamu kuacha kutoa dawa kwa mgonjwa ambaye hana cheti cha daktari/tabibu kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria zilizowekwa.
Pia imewaomba wananchi kuhakikisha wanatumia dawa kwa uangalifu na umakini zaidi ili kuweza kuepuka usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya Antibayotiki.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam jana na Mganga Mkuu wa serikali Profesa Abel Makubi alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya kuamasisha wananchi kuhusu uelewa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya Antibayotiki

Alisema baadhi ya maduka ya dawa yamekuwa yakifanya makosa kwa kumpatia mgonjwa dawa bila ya kuona cheti kilichotolewa na daktari.

“Cheti cha daktari ni muhimu kwa mgonjwa kuwanacho kabla kupewa dawa ya aina yoyote iwe katika kituo cha huduma ya afya au duka la dawa”alisema Profesa Makubi

Alisema kutolewa kwa dawa hizo kiolela bila ya kuona cheti cha daktari kinaweza kumsabisha mgonjwa usugu wa vimelea vya dawa.

Alisisitiza kuwa uwepo wa usugu wa vimelea vya katika dawa Antibayotiki unaweza kuliweka taifa katika kupoteza nguvu kazi pamoja na kutumia fedha nyingi kutumia kununua dawa

Profesa Makubi alisema kutokana na matumizi mabaya ya dawa hizo kwa tiba ya binadamu na wanyama madhara yake yamekuwa makubwa ya kutisha.

Alisema kwa mujibu wa tafiti zimeonesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa za matumizi ya dawa hizo kutumika isivyo sahihi.

” Asilimia 50 ya dawa zimekuwa zikitumika isivyo sahihi huku matumizi makubwa kutibia mifugo na kuchaganywa katika vyakula vya wanyama kinyume na taratibu za kitabibu”alisema Profesa Makubi

Aliongeza kuwa ripoti ya benki ya dunia ya mwaka 2017 inabainisha kuwa zaidi ya watu laki 7 wanafariki Kila mwaka kutokana na usugu wa dawa hizi.

Akizungumza kuhusu utumiaji wa dawa kwa mgonjwa alisema anapaswa kufuata maelekezo ya dawa sahihi ikiwa ni pamoja na kuepuka kukatisha dozi.

” Kila mtu anapaswa kufuata matumizi sahihi ya dawa ikiwa ni pamoja na kutozitumia kiolela ikiwa ni pamoja na kutokukatisha dozi “alisema Profesa Makubi

Kwa upande wake Mfamasia Mkuu wa serikali Daud Msasi alisema kwa sasa wanafanya utaratibu wa kupitia maduka yote Kama njia ya kujiridhisha katika utoaji wa dawa.

Aidha alitaka jamii kuacha kutumia dawa ambazo mtu tayari amezitumia kwani kufanya hivyo kinaweza kusababisha usugu wa dawa.

Pia alisema kupitia wiki hii wanaendelea kutoa elimu ya uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa aina ya Antibayotiki ili siweze kusababisha vimelea vya usugu dhidi ya dawa hizo.


Share:

Kuboreshwa kwa Vitambulisho vya Wajasiriamali Wadogo Kutawaongezea Wigo Wa Biashara


Na. Jovina Bujulu-MAELEZO
Hivi karibuni Rais John Pombe Magufuli amezindua Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia ushindi wa kishindo alioupata katika uchaguzi wa mwezi Oktoba, ambapo alichaguliwa kuiongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika hotuba yake ya uzinduzi, Rais Magufuli alionyesha dira, falsafa, mwelekeo na vipaumbele vya nchi katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano. Pamoja na mengi aliyozungumzia , Rais aliahidi kuboresha vitambulisho vya wajasiriamali ili waweze kutambulika rasmi na kuweza kupata mikopo katika taasisi za fedha hapa nchini.

Rais Magufuli alisema kuwa, kama alivyoahidi wakati wa kampeni kwamba katika kipindi cha uongozi wake wa miaka mitano ijayo, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa wajasiriamali wadogo, machinga, mama lishe, baba lishe waendesha boda boda na bajaji.

Tangu ilipoingia madarakani, Serikali ya Awamu ya Tano ilianza kuwatambua rasmi wajasiriamali wadogo nchini pote kwa kuwapatia vitambulisho ambavyo vilikuwa vinalipiwa shilingi 20,000 kwa mwaka. Utambuzi huo uliwapa uhuru wajasiriamali hao wadogo kufanya biashara zao bila kubugudhiwa na mtu au mamlaka yoyote hivyo kujiongezea kipato.

Vitambulisho hivyo vya awali vilitolewa na Rais Magufuli mwaka 2018, ambapo jumla ya vitambulisho 670,000 vilitolewa na kuwawezesha wafanyabiashara ndogo ndogo kutambulika nchini na kuhakikisha wanafanya shughuli zao bila kusumbuliwa na kama ilivyokuwa awali ambapo walikuwa wanasumbuliwa sana na mamlaka mbalimbali za miji na halmashauri.

Katika utaratibu wa awali, kila mkoa ulipewa vitambulisho 25,000, ambapo kila mjasiriamali aliyekihitaji alikilipia na pesa ilipelekwa TRA na vilikuwa vinatolewa kwa hiari. Utaratibu huo ulimwezesha kila Mkuu wa Mkoa kukusanya shilingi milioni 500 ambazo ni mchango wa sekta hiyo ya wafanyabiashara.

“Miaka mitano iliyopita tulianzisha utaratibu wa kutoa vitambulisha maalum kwa wajasiriamali wetu wadogo, tunakusudia kuviboresha vitambulisho hivyo kwa kuweka picha na taarifa nyingine muhimu kama ilivyo kwenye vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kwenye Hati za kusafiria(Pasipoti)”, alisema Rais Magufuli.

Kuboreshwa kwa vitambulisho hivyo kutakuwa ni fursa nyingine muhimu kwani wataweza kukua na kutajirika na kuondokana na dhana ya kuwa wafanyabiashara wadogo ambapo hii itawezekana kwa sababu wataweza kutambulika kwenye taasisi za fedha na kuweza kupata mikopo kwa ajili ya kukuza biashara.

Aidha, kutokana na maboresho hayo wajasiriamali hao wataweza kukuza mitaji yao kwa kuwa sasa watakuwa na uwezo wa kukopa na kuweza kupanua biashara zao nchi nzima. Hivyo ni wakati muafaka kwao kukuza na kupanua biashara zao kwa sababu ya uwezo wao wa kuongeza mtaji utakuwa umerahisishwa.

Endapo wajasiriamali hao wataitumia fursa hii ipasavyo  mbali na kuweza kupata mikopo ya biashara , wataweza pia kupata mikopo mikubwa ambayo itawanasua katika umaskini ikiwa ni pamoja na kubadilisha biashara zao kutoka kuwa ndogo ndogo na kuwa za kati hadi za juu.

Vitambulisho hivyo pia vitawafanya wajiamini zaidi ikiwa ni pamoja nakuongeza bidii  katika shughuli zao kwani sasa wataweza  kukopesheka kutokana na kuwa na vitambulisho hivyo vilivyoboreshwa. Hivyo wafanya biashara hawana budi kuchangamkia fursa hii kwa kuhakikisha kuwa wanavipata pale vitakapokuwa vimeanza kulipiwa.

Kufuatia kauli ya Rais kuhusu kuboresha vitambulisho hivyo wajasiriamali wameonesha kufurahishwa na hatua hiyo na kusema kuwa sasa ni wakati  wa kukuza mitaji yao na kuinuka kiuchumi. Mama Lishe, Mwajuma Salum wa soko la Mwananyamala amesema kuwa, “ Rais Magufuli kweli ni mkombozi wa wanyonge, miaka yake mitano ya mwanzo alitupatia vitambulisho na hivyo kutuwezesha kufanya biashara zetu kwa amani bila kusumbuliwa na mtu yeyote, sasa  amesema ataboresha vitambulisho hivyo ili tuweze kukopesheka,  Mungu amlinde”.

Naye muuza matunda katika eneo la Afrika Sana Sinza, Mary Zephania amesema, “ Vitambulisho vikiboreshwa na nikapata cha kwangu hatua ya kwanza nitakwenda kuomba mkopo ili nikuze mtaji wa biashara yangu ili ikiwezekana niweze kusafirisha matunda hata nje ya nchi”.

Baadhi ya wafanyabishara wadogo wadogo wa soko la Manzese wamesema kuwa wana imani na Serikali ya Rais Magufuli ambayo wakati wote ina dhamira ya kuwaondoa katika umaskini, maana tangu Rais aingie madarakani amekuwa akihimiza kuondolewa changamoto mbalimbali zinazowakabili wajasiriamali.

Tangu kuingia madarakani mwaka 2015, Rais Magufuli amechukua hatua mbalimbali za kuimarisha uchumi na kuwakomboa wananchi kutoka katika umaskini na kuwawezesha kufanya biashara bila kusumbuliwa ili kuwafanya wawe matajiri. Aidha katika hotuba yake kwa Bunge la 12, ameendelea kusema kuwa Serikali atakayoiunda itaendeleza jitihada za kukuza uchumi.


Share:

Wizara Ya Maji Yaanza Kutekeleza Ilani Ya CCM 2020-2025


 Na Mohamed Saif, Mara
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema Serikali kupitia Wizara ya Maji imeanza rasmi kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.

Mhandisi Sanga alisema hayo Mkoani Mara Novemba 17, 2020 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Bilioni 70.5 wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka katika maeneo ya Wilaya za Musoma Vijijini na Butiama.

Mkataba huo ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga na Mkandarasi Kampuni ya UNIK Construction Company ya Lesotho.

“Tupo hapa kutekeleza Ilani ya Chama Tawala cha  CCM ya Mwaka 2020 hadi 2025 yenye kurasa 303 ambayo imetuelekeza kuhakikisha tunafikisha maji kwa wananchi wa Butiama na Musoma Vijijini kutoka Ziwa Victoria,” alisema Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kupeleka fedha za kutekeleza mradi huo kama alivyokuwa ameahidi wakati wa Kampeni za uchaguzi Mkoani humo.

“Tunakila sababu ya kumshukuru Rais Dkt. Magufuli kwani mradi huu tunaosaini unatekelezwa kwa fedha za Serikali yake,” alisema Mhandisi Sanga.

Akizungumzia utekelezaji wa mradi, Mhandisi Sanga alisema utajengwa kwa miezi 24 na kwamba kwa awamu ya kwanza utaweza kuzalisha kiasi cha lita milioni 17 dhidi ya mahitaji ya sasa ambayo ni lita milioni 12 kwa siku.

Aliongeza kuwa awamu ya kwanza ya mradi itaanza kunufaisha vijiji 19 yaani Wilaya za Butiama na Musoma Vijijini lakini pia kijiji kimoja kutoka Wilaya ya Bunda.

Alitaja maeneo yakayonufaika na mradi kuwa ni Miji ya Mugango, Kiabakari, Butiama na vijiji vya Kwibara, Nyamisisye, Kiabakari, Singu, Mwanzaburiga, Kyawazaru, Kamugegi, Kyatungwe, Ryamugabo, Bumangi, Bisarye, Tiring’ati, Butiama, Rwamkoma, Buturu, Nyang’oma, Mayani, Katalyo na Tegeruka.

Mhandisi Sanga alibainisha kwamba eneo lenye mtandao wa majisafi litaongezeka kufikia asilimia mia moja kwa miji ya Mugango, Kiabakari na Butiama na kwamba zaidi ya wakazi 165,000 watapata huduma ya maji kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo, Mhandisi Sanga alibainisha kwamba lengo ni kuhakikisha zaidi ya vijiji 39 kutoka kwenye wilaya hizo vinanufaika pindi mradi utakapokamilika kwa asilimia mia moja ambapo alisema kwa wakati huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 35 kwa siku.  

Mradi unajengwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka kwa wadau wa maendeleo Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko wa. Maendeleo wa Saudia (SFD)

Utiaji saini wa mradi huo mkubwa wa maji ni wa kwanza kutekelezwa tangu kuanza kwa  kipindi cha pili cha Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.


Share:

Maabara Ya Kisasa Ya Utafiti Katika Sekta Ya Uvuvi Nchini Yajengwa Kupitia Mradi Wa SWIOFISH


 Na. Edward Kondela
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amesema serikali imetilia mkazo suala la utafiti katika sekta ya uvuvi nchini ili kuhakikisha inapata taarifa sahihi ya maeneo ya mavuvi, kuzalisha vifaranga bora vya samaki pamoja na chakula bora cha samaki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa maabara ya kisasa ya utafiti wa uvuvi itakayotumika na Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) inayojengwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), Dkt. Tamatamah amesema mradi huo unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi Bilioni 2.6 unalenga kukuza sekta ya uvuvi nchini.

“Kwenye uchumi wa bluu katika awamu hii tunategemea meli nane kwenye uvuvi wa bahari kuu hivyo unapofanya uvuvi wa bahari kuu haujiendei tu lazima watafiti kama TAFIRI waende baharini wajue chambo wanapata wapi kwa ajili ya kuvua samaki, pia tuna mpango wa kuongeza uzalishaji wa samaki kupitia ufugaji kwenye maeneo mawili ya chakula bora pamoja na vifaranga bora hivyo tafiti ni muhimu kupitia maabara hii.” Amesema Dkt. Tamatamah

Ameongeza kuwa katika miaka mitano ijayo serikali itapunguza au kuondoa kabisa changamoto ya upatikanaji wa vifaranga bora vya samaki na chakula bora cha samaki kutokana na watu wengi kujitokeza katika ufugaji wa samaki ambapo mahitaji ni vifaranga milioni 50 kwa mwaka lakini kwa sasa vifaranga vinavyozalishwa hapa nchini ni milioni 30 pekee.

Kwa upande wake mratibu wa mradi wa SWIOFISH Tanzania Bara Bw. Nichrous Mlalila amesema baada ya kukamilika kwa jengo hilo wataalamu watajikita katika kufanya utafiti ambapo kwa sasa sampuli za mazao ya samaki zimekuwa zikisafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya tafiti hali ambayo inahatarisha usalama wa nchi na rasilimali zake.

Aidha, amesema serikali inatarajia kujenga maabara nyingine kupitia mradi huo kwa ajili ya kuzalisha vifaranga bora vya samaki wa baharini pamoja na mbegu za zao la mwani katika kukuza sekta ya uvuvi hapa nchini.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei amesema taasisi hiyo ina mikakati mingi katika kukuza tafiti za uvuvi hapa nchini kwa kutumia teknolojia ya kisasa pamoja na kupunguza gharama za kutuma sampuli za uvuvi kwenda nchi za nje na hivyo sampuli zote kufanyiwa kazi katika maabara hiyo.

Mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia umeanza kazi hapa nchini mwezi Juni mwaka 2015 na unatarajia kukamilika mwezi Mei mwaka 2021, huku serikali ikiwa na matumaini makubwa ya mradi huo kuendelea kuwepo hapa nchini kutokana na matokeo chanya katika kukuza sekta ya uvuvi kupitia mradi huo, ambapo ujenzi wa maabara hiyo unatarajia kuwa umekamilika na kukabidhiwa kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi tarehe 8 mwezi Desemba mwaka 2020.


Share:

Rais Dkt. Mwinyi atengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya Afya, Dkt. Jamala Adam Taib kuanzia Novemba 18, 2020.

Aidha, Dkt. Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Dkt. Ali Salum Ali.

Dkt. Mwinyi amefikia uamuzi huo baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo ili kujionea mwenyewe hali ya utoaji wa huduma na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.

Kufuatia utenguzi huo, Dkt. Mwinyi amesema wote ambao uteuzi hao umetenguliwa watapangiwa kazi nyingine.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi Novemba 9



Share:

Wednesday, 18 November 2020

TFCG na MJUMITA WACHOCHEA KUWEPO USAWA WA KIJINSIA KATIKA JAMII KWENYE UHIFADHI SHIRIKISHI WA MISITU


Rasi wa Ndaki ya Misitu Wanyamapori na Utalii  SUA, Prof. Suzan Augustino akiwasilisha matokeo ya utafiti huo wa masuala ya kijinsia kwa wadau wa uhifadhi shirikishi wa misitu  nchini.
Prof. John Jackoniah ambaye ni mmoja wa watafiti kutoka Ndaki ya sayansi za jamii na Insia ya Chuo kikuu cha sokoine cha kilimo SUA  akiwasilisha sehemu ya utafiti huo wa mbele wa wadau hao wa misitu mjini Morogoro.
Mkurugenzi msaidizi wa Shirika la TFCG bwana Emmanuel Lyimo akieleza malengo ya utafiti huo uliofanywa na watafiti kutoka SUA kabla ya kuanza rasmi kusikiliza matokeo hayo ya utafiti.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.
Baadhi ya wadau kutoka TFCG,MJUMITA, Wizara ya Maliasili na utalii,Waandishi wa habari na maafisa Misitu kutoka halmashauri za wilaya wakifuatilia uwasilishwaji wa matokeo hayo.


Na Calvin Edward Gwabara, Morogoro


UTAFITI uliyofanywa na Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) umebainisha kuwa usawa wa kijinsia unaimarika na kuzingatiwa sana kwenye vijiji vinavyoshiriki miradi ya uhifadhi shirikishi wa Misitu kupitia Shirika la kuhifadhi Misitu ya asili Tanzania -TFCG.

Hayo yamebainika na Rasi wa Ndaki ya Misitu, Wanyama pori na utalii Profesa. Suzan Augustino  wakati wa  uwasilishwaji wa matokeo ya utafiti mbele ya wadau wa misitu mjini Morogoro na kusema kuwa jitihada kubwa zimefanywa na TFCG na Mtandao wa Jamii wa usimaizi wa Misitu Tanzania MJUMITA kwa kuhakikisha jamii yote inashirikishwa na inanufaika na rasilimali zitokanazo na misitu hiyo.

“ Kuna mabadiliko makubwa chanya kwenye vijiji ambavyo TFCG na MJUMITA wanatekeleza miradi yao hasa wa mkaa endelevu ikilinganishwa na vijiji vilivyo nje ya mradi ingawa wanaume wanaongoza kwenye kazi zinazohitaji nguvu” alibainisha Prof. Suzan.

Prof. Suzan alisema kuwa kwenye Mradi wa Mkaa Endelevu wanawake wanakuja juu katika kushiriki kwenye biashara hiyo ijapokuwa wao wanatumia fedha kulipa watu kufanya kazi zao kama vile kukata magogo, kuyakusanya na kupanga tanuri la mkaa kazi ambazo zinaonekana kuhitaji nguvu zaidi.

Aidha Suzan alisema kuwa baadhi ya vijiji vina ushiriki mdogo wa wanawake na hiyo kwa mujibu wa utafiti wao wamesema inasababishwa mila na  destuli Zao kwamba kazi za maporini hufanywa na wanaume tu na sio wanawake ingawa mitazamo hiyo imeanza kufutika taratibu baada ya jitihada za TFCG na MJUMITA za kutoa elimu.

Prof. Suzan alisema watu wengi wanajua usawa wa kijinsia kwenye ngazi za maamuzi ni kuwa na idadi sawa ya wanawake, wanaume na Makundi mengine lakini ukweli ni kwamba kinachotakiwa kuangaliwa ni nani kawakikisha kundi gani na sauti ya like na mchango wake kwenye kufanya maamuzi maana wanaweza kuwa idadi sawa lakini wote hawana sauti.

Kwa upande wake Prof. John Jackoniah Mtafiti kutoka Ndaki ya Sayansi za jamii na Insia - SUA alisema pamoja na mafanikio hayo ya kuongeza uwiano wa kijinsia kwenye jitihada za usimamizi shirikishi wa Misitu na matumizi ya mapato ya rasilimali hizo lakini wanaume ndio wameonekana kunufaika zaidi.

Alisema kupitia utafiti huo walioufanya kwenye vijiji 10 katika Wilaya za Kilosa, Mvonero na Morogoro wanaume ndio wameonekana kuwa na sauti zaidi kwenye maamuzi na hata kwenye kugawana rasilimali za misitu kwenye maeneo hayo.

“ Lakini utaona wanawake walioolewa ndio wasio na sauti zaidi lakini wale ambao hawajaolewa au waliopewa talaka wananufaika Kama wanaume na Pia wana sauti kwenye kutoa maamuzi na kwenye kugawana mapato ya rasilimali za Misitu” alifafanua Prof. Jackoniah.

Alisema kuwa ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kibiashara za rasilimali za Misitu umeongeza mzigo kwa wanawake kwakuwa kazi za nyumbani nazo zinawaangalia kwakuwa mgawanyo wa majukumu ya nyumbani haujabadilika umebaki palepale.

Akieleza lengo la Utafiti huo Mkurugenzi Msaidizi wa TFCG, Emmanuel Lyimo alisema masuala ya kijinsia yametengenezewa mkakati mahususi wa kuhakikisha yanazingatiwa kikamilifu kwakuwa ni swala mtambuka kwenye maendeleo.

Alisema baada ya kutekeleza Mradi kwa muda sasa wameona wafanye Utafiti huo ili kuona namna maswala hayo yanavyozingatiwa na kutafuta njia za kuboresha zaidi kama kuna vitu Vinakosekana kupitia mapendekezo ya watafiti hao kutoka SUA.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger