Friday, 6 November 2020

PICHA: Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli alivyoongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM jana tarehe 05 Novemba 2020

 


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jana  tarehe 05 Novemba 2020 mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi mara baada ya kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM jana tarehe 05 Novemba 2020 mkoani Dodoma.


Share:

Rais Magufuli amteua Prof. Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali


Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk. John Magufuli amemteua Prof. Adelardius Lubango Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali .

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imesema uteuzi wa Prof. Kilangi unaanza  tarehe 05,Novemba,2020. Prof. Kilangi ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada yakipindi cha kwanza kumalizika jana tarehe tano novemba 2020.


Share:

Waangalizi wa Kimataifa: Madai ya Trump Hayana Msingi


Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi wa Marekani amesema jana kwamba madai ya Rais Donald Trump hayana msingi, yanayosema kwamba kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi huo.

Michael Georg Link anayeongoza ujumbe wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) ameongeza kuwa madai ya Trump yanadhoofisha imani ya umma kwa taasisi za kidemokrasia nchini humo.

Katika ripoti ya awali, ujumbe huo pia ulionya kwamba matamshi ya Trump wakati wa kampeni zake, yaliangaliwa na wengi kuwa na uwezo wa kuchochea vurugu za kisiasa baada ya uchaguzi.



Share:

Ofisi ya Ardhi Rukwa yawatahadharisha waliovamia maeneo ya umma.


 Na Abdulrahman Salim, Rukwa RS
Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Rukwa inaendelea na zoezi la kufanya uhakiki wa maeneo ya wazi na maeneo ya umma yaliyoorodheshwa kwa mujibu wa ramani za mipango miji za halmashauri za mkoa huo ili kubaini endapo kuna uvamizi umefanyika katika maeneo hayo.

Akiongea kuhusiana na zoezi hilo Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Rukwa Swagile Msananga amesema kuwa lengo la kufanya zoezi hilo ni kupata orodha kamili ya meneo ya wazi ili yaweze kutambulika rasmi huku akiwaonya wananchi waliovamia katika maeneo hayo.

“Kwa maeneo ambayo yatakuwa yamevamiwa, kutakuwa hakuna namna ya kufanya isipokuwa wavamizi wataondolewa ili kupisha maeneo ya wazi kwasababu yanatakiwa yalindwe kwa nguvu zote, na maeneo ambayo yapo salama mpaka sasa hivi tutahakikisha mipaka yake inawekwa bayan ana wananchi watatakiwa waiheshimu,” Alisema.

Aidha aliongeza kuwa baada ya kupata orodha ya kamili ya maeneo hayo atakabidhiwa Mkurugenzi ili aweze kuyaandalia hati kwaajili ya ulinzi wa maeneo hayo kwa siku za usoni.


Share:

Mawasiliano Yarejeshwa Vijiji Vya Libobe Na Ming’wena Katika Halmashauri Ya Wilaya Ya Mtwara


Muonekano wa Barabara ya Libobe – Ming’wena kabla ya kujengwa na TARURA iliyopo Kata ya Libobe Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara ambayo iliharibiwa na mvua na kukata mawasiliano kati ya vijiji vya Libobe na Ming’wena.


Muonekano wa Barabara ya Libobe – Ming’wena yenye urefu wa kilomita 4.8 ikiwa imekamilika na kuanza kutumika.

************************************

Na. Thereza L. Chimagu
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umefanikiwa kufanya ukarabati wa barabara iliyoharibiwa na mvua na kupelekea kukatika kwa mawasiliano kati ya Vijiji vya Libobe na Ming’wena vilivyopo Kata ya Libobe katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara.

Akizungumzia ujenzi wa barabara hiyo Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Mhandisi Patrick Kanyagha alisema, baada ya kupata changamoto ya kukatika kwa barabara hiyo waliomba fedha za dharura kutoka TARURA Makao Makuu na kupatiwa kiasi cha Shilingi Milioni 185 ambazo zilitumika kutengeneza barabara iliyopo kati ya Kijiji cha Libobe hadi Ming’wena yenye urefu wa Kilomita 4.8. kwa kiwango cha Changarawe ili wananchi waendelee na shughuli zao za kiuchumi.

” Kipande hiki cha Km 4.8 ni sehemu ya barabara ya Libobe- Ming’wena- Likwidi- Mtama yenye jumla ya urefu wa Km 19, na tulichukua maamuzi ya kutengeneza baada ya mvua kuharibu miundombinu ya barabara pamoja na kuathiri makazi ya wananchi ili kurejesha mawasiliano na kuwezesha  wananchi kusafirisha bidhaa zao kama hapo awali”, alisema Mhandisi Kanyagha.

Meneja huyo alisema kuwa   baada ya kupatiwa fedha hizo kazi walizozipa kipaumbele zilikuwa ni kurejesha tuta, kujenga “box culvert” mpya ambapo zimejengwa 8, kujenga mtaro wa maji ya mvua na kurejesha tabaka la changarawe urefu wa Km 3.5. ambapo kazi zote zimekamilika na mawasiliano yamerejea katika vijiji hivyo.

Naye, Bw. Majid Rashid ambaye ni mkazi wa   Kijiji cha Ming’wena ameipongeza Serikali kwa kutengeneza barabara katika eneo hilo kwani imesaidia kupunguza kero ya usafiri na kufanya wananchi waendelee na shughuli zao kama hapo awali.

“Tunaishukuru TARURA kwa kutujali na kutufanyia ukarabati wa  haraka kwani  tulikuwa na changamoto ya usafiri kutoka hapa hadi kufika barabara kuu ya Mpapora kwani magari na hata pikipiki yalikuwa hayapiti kabisa lakini baada ya matengenezo ya barabara tumefaidika sana na imerahisisha mawasiliano”, alisema Bw. Rashid.

Naye, Somoe Kankunje Mkazi wa Kijiji cha Ming’wena alisema, upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika eneo hilo umerahisishwa na ukarabati wa barabara hiyo kwani hawapati shida ya usafiri na wanaendelea na biashara zao kama awali bila matatizo.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijni (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara unaendelea na kazi mbalimbali zikiwemo za matengenezo ya barabara na vivuko katika Wilaya hiyo ili kuwawezesha wananchi kusafiri na kusafirisha mazao Pamoja na bidhaa zao kwa urahisi.



Share:

Watatu kizimbani kwa tuhuma za kuchoma moto mabweni ya shule Kilimanjaro


Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imewafikisha mahakamani washtakiwa watatu wanaohusishwa na matukio ya kuchoma moto bweni la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Uchira na bweni la Shule ya Sekondari Ebeneza Sango zilizopo wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi, Mkurugenzi Utenganishaji wa Shughuli za Mashtaka na Upelelezi katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Oswald Tibabyekomya amesema katika tukio la kuchoma moto bweni la shule ya Sekondari ya  Wasichana  Uchira yupo mwalimu mmoja pamoja na mwanafunzi mmoja.

Ameeleza kuwa katika tukio la kuchoma moto bweni la Shule ya sekondari Ebeneza wamemfikisha mahakama mwanafunzi mmoja.

Aidha, amefafanua kuwa, kulingana na upelelezi uliofanyika wamebaini kichocheo kikubwa ni mahusiano mabaya na ushawishi wa vikundi rika visivyofaa shuleni.

Ofisi ya Taifa ya Mashtaka imesema upelelezi wa matukio hayo pamoja na mengine yanayofanana na haya bado yanaendelea. 

 

Credit:TBC



Share:

Marais wa Afrika wampongeza JPM kwa Ushindi wa Kishindo


Na Anitha Jonas – MAELEZO
Marais waliyohudhuria  sherehe za kuapishwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli  wampongeza kwa ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu uliyofanyika hivi karibuni pamoja na kuwapongeza watanzania  kwa kumaliza zoezi hilo kwa amani.

Akizungumza katika sherehe hizo, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni alisisitiza kuwa ushiriki  wa nchi mbalimbali za Afrika katika sherehe hiyo ni matunda ya msimamo thabiti wa Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere  na baadhi ya viongozi  wa Afrika ambao hawakukubali kuwa vibaraka wa mataifa ya nje.

“Napenda kutoa pongezi kwa watanzania kwa kufanya uchaguzi salama na kumaliza bila vurugu zozote pia na toa pongezi kwa Rais Magufuli kwa ushindi wa kishindo kwani ameshinda kwa kura nyingi pamoja na wabunge mbalimbali wa chama cha CCM nao nimewaona wameshinda kwa kura nyingi, nilikuwa nikifuatilia matangazo ya matokeo ya uchaguzi kupitia televisheni ya TBC 1,” alisema Museveni.

Pamoja na hayo naye Rais wa Comoro,  Azali Assoumani  alitoa pongezi kwa Rais Magufuli huku akisisitiza kumuombea katika majukumu yake  aliyopewa ya kuwatumikia na kuwaongoza Watanzania ili aweze kukamilisha  kazi hiyo kama ilivyo desturi  ya viongozi kutekeleza wajibu wao kwa ufanisi kwa msaada wa Mungu.

Naye  Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmaerson Mnangagwa  alitoa pongezi  kwa watanzania  na kutoa  salamu kutoka wananchi wa  Zimbambwe ambapo alisisitiza kuwa Zimbabwe wanaiangalia Tanzania kama baba na mama wa uhuru wa taifa lao kama alivyowasisi Hayati Mwl. Julius Nyerere.

“Tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa sababu katika kipindi alichokuwa Mwenyekiti wa SADC  alikuwa kinara wa kusimamia kuondolewa  kwa vikwazo  mbalimbali ambavyo Zimbabwe tulikuwa tumewekewa kwa kutangaza tarehe 25 Oktoba,2020 kuwa siku maalum ya kupinga vikwazo hivyo ikiwa ni  maamuzi ya Jumuiya ya SADC,” alisema Rais Mnanangwa.

Halikadhalika nae Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Botswana , Slumber Tsogwane alitoa salamu kwa niaba ya Rais wake Mokgweetsi Masisi kwa kumpongeza  Rais Magufuli  kwa ushindi wa kishindo  huku akieleza sababu mbalimbali zilizomfanya rais wake ashindwe kushiriki sherehe hiyo  kwa kubanwa na majukumu ya kitaifa, pamoja na hali ya   kuhitajika kukaa karantini mara baada ya kurejea nchini kwa siku kumi na nne atakapotoka nje ya nchi kutokana na hali ya ugongwa wa Corona .

Aidha, Katika sherehe hizo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli  aliwashukuru watanzania kwa kujitokeza kumpigia kura kwa wingi na kumpa ushindi wa kishindo na alisisitiza kuwa uchaguzi kwa sasa umekwisha na hivyo ni wakati wa kuchapa kazi na kulijenga taifa.

“Napenda kuwapongeza  viongozi wote wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusimamia zoezi la uchaguzi vyema na kuhakikisha  linaendeshwa kwa uwazi na haki, pia nawashukuru watanzania wote  kwa kuwa wazalendo na kulinda amani ya taifa na  mara baada ya uchaguzi,” alisema Rais Magufuli.

Akiendelea kuzungumza mara baada ya uapisho huo, Rais Magufuli aliahidi kuendelea kusimamia miradi mikubwa yote aliyoianzisha na kutekeleza mingine mipya pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali za taifa na kukuza uchumi, ikiwemo kutatua changamoto ya ajira kwa vijana pamoja na mapambano dhidi ya rushwa.

Sherehe hizo za uapisho zilihudhuriwa na Marais watatu, Mabalozi takribani themanini,  viongozi wa Jumuiya ya  Afrika Mashariki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar na viongozi mbalimbali kutoka nchi za Afrika wakiwemo mawaziri wa nchi mbalimbali na viongozi wa mashirika ya kimataifa.


Share:

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Novemba 6



Share:

Thursday, 5 November 2020

Workshop Foreman- After sales at Achyutam

Workshop Foreman- After sales Achyutam Dar es Salaam, Tanzania The ideal candidate will be having minimum 5 years of experience in a well-reputed workshop. Responsibilities Maintaining good shop floor efficiency HSSE Audit Report, CSI Score and maintaining other records and targets Training and development of other team members Proper communication, job flow and guidance for […]

The post Workshop Foreman- After sales at Achyutam appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Medical Supplies Officer at Tindwa Medical and Health Services(TMHS )

Male Medical Supplies Officer We are looking for a highly skilled male Medical Supplies Officer. Duties And Responsibilities.  Receiving of orders. Issuing of quotations. Planning and management of activities involved in sourcing and procurement. Research, Registration and Development of medicine, equipments and consumables. Managing of all incoming and deliveries. Ensure that all confirmed orders are […]

The post Medical Supplies Officer at Tindwa Medical and Health Services(TMHS ) appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Chief Finance Officer at DCB Commercial Bank

Chief Finance Officer  DCB Commercial Bank was formed following an outcry of Dares Salaam residents on the lack of capital as the major obstacle faced by micro entrepreneurs in their effort to improve their businesses. The bank was registered in 2001 as Dar es Salaam Community Bank Limited, the primary objective being carrying out micro […]

The post Chief Finance Officer at DCB Commercial Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Deputy Vice Chancellor at Ardhi University

Deputy Vice Chancellor  Advertisement for the Position of Deputy Vice Chancellor for Planning, Finance and Administration (DVC-PFA) of Ardhi University. Advertisement for the Position of Deputy Vice Chancellor for Planning, Finance and Administration (DVC-PFA) of Ardhi University Ardhi University is a Public University established under the Universities Act No. 7 of 2005 and the Ardhi […]

The post Deputy Vice Chancellor at Ardhi University appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Data Clerks at Humuliza Organization Tanzania

Data Clerks (20 Posts) Humuliza Organization Job Summary HUMULIZA is looking for a competent data clerks who can support in data entry of program activities. Roles and responsibilities: Directly enter data in the reporting systems as may be directed by M&E Officer Enter data in all organization designed systems including excel sheets, word power point Collate […]

The post Data Clerks at Humuliza Organization Tanzania appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Truck Driver at Kuehne+Nagel

Truck Driver Kuehne+Nagel Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania We deliver high quality solutions to our customers and we are leaders in the logistics industry. Join us and become a part of our great team. Your Role The purpose of the role is to ensure timely collection and delivery of cargo to and from […]

The post Truck Driver at Kuehne+Nagel appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Head of Internal Audit at Maendeleo Bank

Head of Internal Audit  Maendeleo Bank PLC is inviting applications from qualified and experienced candidates to fill the vacant position of Head of Internal Audit at its Head Office. The Bank seeks to recruit highly competent, self-motivated and professional individual to manage internal audit functions. Job Summary: Responsible for evaluating and contributing to the effectiveness […]

The post Head of Internal Audit at Maendeleo Bank appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Country Finance and Operations Officer at CBM

Country Finance and Operations Officer  Overall Mission: CBM is an international Christian development organization, committed to improving the quality of life of people with disabilities in the world. CBM addresses disability as a cause and consequence of poverty, and works in partnership to create an inclusive society for all. Job Holder: The job holder promotes, […]

The post Country Finance and Operations Officer at CBM appeared first on Udahiliportal.com.

Share:

Assistant Accountant at Mwananchi Communications Limited

Mwananchi Communications Limited, publishers of the leading Tanzania newspapers, Mwananchi, The Citizen and Mwanaspoti is looking for motivated and highly experienced individuals to fill the position. ASSISTANT ACCOUNTANT. Job Purpose: To enhance and improve the MCL’s cash flow through effective credit management. Main Responsibilities: Reviews adverts to run on credit and other mode of payment; […]

The post Assistant Accountant at Mwananchi Communications Limited appeared first on Udahiliportal.com.

Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger