Thursday, 3 September 2020

Angalia Picha : MAELFU WAJITOKEZA MKUTANO WA KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM MAGUFULI LEO SHINYANGA



Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiserebuka na msanii wa Bongo Fleva Chegge Chigunda wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi CCM katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo Alhamisi Septemba
3, 2020.
 (PICHA NA KADAMA MALUNDE NA IKULU)



Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiserebuka na msanii wa Bongo Fleva Chegge Chigunda wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo Alhamisi Septemba
3, 2020


Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho tawala Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiserebuka na msanii wa Bongo Fleva Chegge Chigunda wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo Alhamisi Septemba
3, 2020

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa ameishika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020-2025 katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo Septemba 3, 2020.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Shinyanga mjini katika Mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo Septemba 3, 2020
 
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wananchi wa Shinyanga mjini katika Mkutano wa Kampeni za Urais 
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza huku akiwa ameishika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa mwaka 2020-2025 katika mkutano wa Kampeni za Urais kwa upande wa CCM uliofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo Septemba 3, 2020.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwatambulisha wagombea ubunge majimbo mbalimbali mkoa wa Shinyanga
Mgombea ubunge Jimbo la Kishapu Boniface Butondo akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za Uchaguzi CCM katika uwanja wa CCM Kambarage leo.
Mgombea ubunge Jimbo la Solwa Ahmed Salum 'Jembe lisiloisha makali' akizungumza kwenye mkutano wa kampeni za Uchaguzi CCM katika uwanja wa CCM Kambarage leo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi na kumuombea kura kwa wananchi wa Shinyanga.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitambulisha wagombea udiwani Jimbo la Shinyanga Mjini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akiomba kura kwa wananchi wa Shinyanga.
Wagombea Ubunge Majimbo mbalimbali mkoa wa Shinyanga wakicheza muziki 
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM, Humprey Polepole akizungumza.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni za Uchaguzi CCM.
Viongozi mbalimbali mkoa wa Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga. Kushoto ni MNEC Gaspar Kileo
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Waandishi wa habari wakiendelea kuchukua matukio
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za CCM katika uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM
Wagombea udiwani Jimbo la Shinyanga Mjini wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za uchaguzi CCM.
Viongozi wa dini wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi CCM
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za uchaguzi CCM
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za uchaguzi CCM
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za Uchaguzi CCM
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Kampeni za Uchaguzi CCM


Msanii kutoka Shinyanga Nkunda Star akitoa burudani
Msanii Sholo Mwamba akitoa burudani
Makada wa CCM wakicheza muziki
Makada wa CCM wakicheza muziki.
Wakazi wa Shinyanga wakiwa kwenye Mkutano wa Kampeni za CCM.

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za Urais leo Septemba 3, 2020.
Picha zote na Kadama Malunde & Ikulu 
Share:

WAZIRI UMMY ATAKA MASHIRIKA YASIYOKUWA YA KISERIKALI NCHINI KUZINGATIA UWAZI NA UWAJIBIKAJI

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau wa asasi za kiraia (NGOs) zinazofanya kazi Halmashauri ya Jiji la Tanga na mkoa wa Tanga ambapo kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kushoto ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira kulia Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau wa asasi za kiraia (NGOs) zinazofanya kazi Halmashauri ya Jiji la Tanga na mkoa wa Tanga ambapo kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali kushoto ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira kulia Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa
Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni  Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa
Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu katikati akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kikao hicho kushoto ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira kulia ni Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa
KATIBU wa Taasisi ya Odo Ummy Foundation Khatibu Kilenga akizungumza jambo wakati wa mkutano huo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kikao hicho kushoto ni Mkurugenzi wa Asasi ya Tree of Hope ya Jijini Tanga Fortunata Manyeresa na wa pili kulia ni Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini kuzingatia uwazi na uwajibikaji kwenye shughuli zao ikiwemo fedha hasa wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu.


Ummy ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM)aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa asasi za kiraia (NGOs) zinazofanya kazi Halmashauri ya Jiji la Tanga na mkoa wa Tanga ambapo kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali.
 

Alisema hategemei kuona shirika lisilokuwa la kiserikali linapata fedha za kwa ajili ya kuchochea mpasuko na masuala yatakayoleta mfarakano kati ya watanzania kubwa waendelee kuheshimu sheria, kanuni zinazosimamia mashirika hayo.


Aidha alisema lazima wafanye kazi kwa malengo waliyoyaomba na sio kujiingiza kwenye masuala mengine yatakayohatarisha umoja na mshikamano kwenye nchi ambayo ni tunu kubwa.


Waziri Ummy aliyataka pia mashirika hayo kuhakikisha rasilimali fedha wanazozipata ambazo wanaziomba kwa jina la watanzania kuzitumia kikamilifu kwa ajili ya wananachi wanaoombea fedha hizozna sio kwa maslahi yao binafsi.


“Lakini kubwa amesisitiza uwazi na uwajibukaji kwa asasi za kiraia kwa wananchi na serikali na ndio maana mwaka 2019 tulitoa kanuni mpya za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yanazitaka kila asasi inayopokea fedha inayozidi milioni 20 kuhakikisha inatoa taarifa kila baada ya miwezi mitatu kwa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii namna zitakavyotumika na matokeo yanayotarajiwa”Alisema.


Awali akizungumza wakati wa mkutano huo Mgombea Ubunge Viti Maalumu kupitia kundi Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara (CCM) Neema Lugangira amewaambia viongozi wa asasi hizo mkoani Tanga huku akieleza kazi yake kubwa ni kuwa kiunganishi kati ya NGOs, Bunge, Serikali, CCM na wafadhili ili waweze kupata mafanikio.


Alisema dhamira ya kukutana na viongozi wa NGOs za Mkoa wa Tanga ni dhumuni kubwa likiwa ni kumwezesha kupata uelewa wa changamoto zao ili aweze kuandaa vipaumbele vyake.


Alisema kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kinatambua kazi kubwa inayofanywa na Asasi hizo hapa nchini na ndio maana katika vipaumbele vikuu vya CCM kwenye ilani ya mwaka 2025.


Neema aliwathibitishia viongozi wa (NGOs) mkoa wa Tanga kwamba CCM inatambua kazi kubwa inayofanywa na Asasi hizo nchini na ndio maana katika vipaumbele vyake vikuu kwenye ilani a 2020 -2025.


“Kuchukua hatua madhubuti za kujenga mazingira wenzeshi kwa asasi za kiraia, kidini na vyombo vya habari kulinda kustawi ili kuchangia maendeleo ya Taifa”Alisema Neema.


Aidha alisema maendeleo hayana chama wala dini hivyo kupitia nafasi hiyo atahakikisha anawaunganisha ili kuweza kuwa chachu kubwa ya maendeleo kwao.


“Lakini wana Tanga mtambue kwamba nyie ni asasi za kwanza za kiraia ambao tunakutana nanyi tokea nimetangazwa Agosti 20 mwaka huu naamini wadau wa asasi za kiraia hatuna mambo ya vyama.


“Ila mtanisamehe siku ya leo wakati narejea ilani ya CCM muone namna gani ilani inatambua NGOs kama wadau muhimu ambao wanashirikiana na serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii yetu”Alisema
Share:

Picha : MAGUFULI AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI SHINYANGA..AMFAGILIA KATAMBI, AAHIDI KUMPA KAZI MASELE


Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (kulia) wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Septemba 3,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za CCM mkoa wa Shinyanga leo .Wa kwanza kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko, Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba na Katibu Tawala wilaya ya Kahama, Timoth Ndanya
Mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akiomba kura
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akiwatambulisha wagombea ubunge mkoa wa Shinyanga wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dr John Magufuli akiwatambulisha wagombea udiwani Jimbo la Shinyanga Mjini wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM mkoa wa Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Magufuli, amewaomba wananchi wa Shinyanga kumpa kura mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi ambapo pia ameahidi kumtafutia kazi nyingine aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele.

Dk. Magufuli ameyasema hayo leo Alhamis  Septemba 03, 2020, wakati akizungumza na wananchi wa Shinyanga mjini katika mkutano wa kampeni za urais uliofanyika katika uwanja wa Kambarage.

“Yale mengine ya pembeni achaneni nayo, Katambi ni kijana nampenda mpeni kura, atawavusha, jana tu nimekutana na Masele aliyekuwa Mbunge wa hapa wala sina tatizo, mimi ni Rais nitamtafutia kazi nyingine, ukishakuwa Rais Makazi yapo mengi tu

“Masele nitamtafutia tu kazi ya kwenda kufanya, ukishakuwa Rais kazi ni nyingi, hata leo kuna nafasi ya Mtu mmoja anafanya hovyohovyo huko, Katambi ameacha Ukuu wa Wilaya Dodoma Makao Makuu kuja kuomba kura Shinyanga anawapenda, Katambi ukichaguliwa usibadilike kama wengine”,amesema Magufuli.

Pamoja na hayo Magufuli ameelezea mipango ambayo anatarajia kuikamilisha katika Mkoa wa Shinyanga iwapo atarejea madarakani baada ya uchaguzi.

“Hapa Shinyanga tumetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hospitali, zahanati na mradi mkubwa wa kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga ambapo itafika mahali tatizo la umeme litakuwa ni ndoto, kwani tumepeleka umeme katika vijiji 136 vya mkoa huu,” alisema huku akiahidi kukamilisha pia miradi mbalimbali ya barabara mkoani humo.

Mgombea ubunge wa Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi akiomba kura achaguliwe kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini

Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM Mkoa wa Shinyanga leo.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM Mkoa wa Shinyanga leo.
Maelfu ya wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi CCM Mkoa wa Shinyanga leo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog





Share:

Serikali Kusaini Hati Ya Utekelezaji Ya Shilingi Bilioni 125.69 Kwa Ajili Ya Kuimarisha Huduma Za Afya Ngazi Ya Msingi

Na. Catherine Sungura,WAMJW-Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendelo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo wanaochangia sekta ya afya kupitia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund imeridhia kuweka saini Hati ya Shilingi Bilioni 125.69 kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya katika ngazi ya msingi nchini

Akiongea wakati wa kuidhinisha makubaliano hayo,  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Mabula Mchembe amesema kuwa lengo kuu la Mfuko huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1999 ni Kuimarisha huduma za afya katika ngazi ya msingi (halmashauri) zote nchini.

Amesema katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2020/21  Wadau nane (8) watachangia jumla ya USD 53.84 sawa na Shilingi bilioni 125.69 kwa kipaumbele cha kuimarisha huduma za afya katika vituo vya afya kwenye halmashauri zote 184 nchini.

“Shilingi bilioni 105.32  zitatumika kwa ajili ya kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika vituo vya afya vipatavyo 5,533 kwenye halmashauri zote 184 nchini ikiwa ni pamoja na ununuzi wa dawa, vifaa na vifaa tiba, uendeshaji wa vituo, ukarabati mdogo na huduma za chanjo na vikoba. “Fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja vituoni kwa utaratibu wa ‘Direct Health Facility financing” Alisema Prof.. Mchembe.

Aidha, Prof Mchembe alisema Shilingi bilioni 4.29 zitatumika kwa ajili ya kuziwezesha Timu za Afya za Mikoa 26 kufanya ufuatiliaji na usimamizi shirikishi katika halmashauri zote nchini na Shilingi bilioni 2.09 zitawezesha Ofisi ya Rais– TAMISEMI kusimamia na kutoa msaada wa kitalaam katika halmashauri na mikoa yote nchini.

Aliongeza kuwa Shilingi bilioni 5.13 zitawezesha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutekeleza masuala ya sera, mikakati na miongozo kwa ajili ya kuhakikisha huduma za afya zinatolewa kwa kiwango na ubora stahiki na Shilingi bilioni 8.86 zitakuwa kwa ajili ya kutekeleza maeneo mengine ya kipaumbele katika sekta.

“Vipaumbele tulivyoidhinisha  na kamati ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wataalam 620 wa dawa za usingizi; kununua machine za kisasa za kutolea dawa za usingizi katika vituo vya afya ngazi ya halmashauri na kufanya ukarabati mkubwa katika vyuo vinne (4) vya kutolea mafunzo ya watalaam wa afya”.

Prof. Mchembe alitaja maeneo mengine ya kipaumbele yaliyoidhinishwa na Kamati Kuu ya Mfuko huo kuwa ni kuhuisha Mkataba wa Makubaliano (MOU) baina ya pande zote mbili kwa kipindi cha 2021 – 2026, kununua mashine za kutolea dawa za usingizi katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na kuvijengea uwezo vituo vya afya katika kusimamia na kutumia fedha kwa kuzingatia miongozo na taratibu mbalimbali.

Maazimio ya uwekaji saini Hati hiyo yamefanyika kwenye ofisi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto iliyoko mji wa Serikali Mtumba ambapo ulihudhuriwa na watalaam kutoka Wizara ya  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Fedha na Mipango, OR – TAMISEMI, Bohari ya Dawa na Wadau wa Maendeleo wanaochangia Mfuko huo kutoka Canada, Denmark, KOICA, Ireland, Switzerland UNICEF, UNFPA na Benki ya Dunia. walioshiriki kwa njia ya ‘video conference’.


Share:

Simiyu Wajipanga Kumpa Ushindi wa Kishindo Mgombea Urais wa CCM Dr John Magufuli

Na Samirah Yusuph
Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Simiyu imepewa jukumu la kuhakikisha kuwa Asilimia 97 ya kura za mgombea nafasi ya Rais kwa tiketi ya chama hicho zinapatIkana kutoka katika mkoa huu.

Jukumu hilo limetolewa na katibu wa mkoa wa Simiyu Haula Kachwamba alipokuwa akizungumza na vijana hao baada ya matembezi ya hamasa kwa ajili ya maandalizi ya kumpokea mgombea  wa ngazi ya Rais mkoani hapo tarehe nne mwezi wa nane 2020.

"Asilimia kubwa ya wapiga kura wetu ni vijana hivyo ni jukumu lenu kuhakikisha vijana wanatumika kura ili kuweza kufikia lengo la asilimia 97 ya kura za mheshimiwa rais " alisema Haula

Akiweka mkazo wa namna ambavyo wamejiandaa katika kutafuta kura hizo mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bariadi Mayiku, alisema kuwa wao wamejipanga katika kuhakikisha kura hizo zinapatikana.

 "Huu ni ujumbe kwa vyama vya upinzani na wajue kuwa tumejipanga na tunaomba wajitokeze kwa wingi ili tumwambie mheshimiwa raisi kuwa asilimia 100 ataipata Simiyu," Alisema Mayiku.

"Kiupekee ni washukuru kwa kushiriki matembezi haya ambayo yamefikisha taarifa kwa wapinzani sisi ni kina nani na ninawaomba kesho pia mjitokeze kwa ajili ya kumpokea mgombea wetu kiti cha rais,"  alisema Rucy John Sabu Mbunge mteule vijana mkoa wa Simiyu.

Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa ccm mkoa wa simiyu Lumeni mathias alisema kuwa matembezi hayo yalikuwa na zaidi ya vijana 300 ambayo yalilenga kuwataarifu vijana na wananchi kwa ujumla kuwa kesho kuna ujio wa mgombea wa nafasi ya Rais katika mkoa huo.



Share:

Marekani yamuwewekea vikwazo mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alitangaza jana kuwa Marekani imeweka vikwazo dhidi ya mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC Fatou Bensouda kwasababu ya ofisi yake kuendelea na uchunguzi wa watu wa Marekani. 

Pompeo alisema aliyeongezwa pia katika orodha ya vikwazo ni Phakiso Mochochoko mkuu wa idara ya sheria ya ICC, anayehusika na ushirikiano na hisani, kwa kutoa msaada kwa Bensouda za taarifa mbali mbali. 

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani ameiita mahakama hiyo ya uhalifu wa kivita, ambayo Marekani haihusiki nayo, kuwa ni taasisi iliyovurugika na yenye ufisadi wa hali ya juu. 

Mwezi Juni , rais wa Marekani Donald Trump alitoa amri ya rais inayoweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya maafisa wa ICC wanaohusika katika uchunguzi wa vikosi vya jeshi la Marekani kwa uwezekano wa uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.


Share:

Takukuru yarejesha fedha za wakulima wa zao la pamba.

Samirah Yusuph
Maswa. WAKULIMA wa zao la pamba katika kijiji cha Gula wilaya ya Maswa mkoani Simiyu wameipongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru)kwa kuweza kuokoa kiasi cha fedha sh Milioni 6.2 walizouza zao hilo kwa musimu huu wa kilimo 2019/2020

Wakulima hao ambao ni wanachama wa Kilimo hai cha pamba katika kijiji hicho chini ya Kampuni ya ununuzi wa zao hilo ya S.M Holiding ya Jijini Mwanza fedha zao hizo zilikuwa zimepotezwa na Mhasibu wa kampuni hiyo,Paul Simba baada ya kufanya udanganyifu.

Wametoa pongezi hizo wakati wakikabidhiwa pesa hizo na Mwenyekiti wa Kilimo Hai Maswa,Laurence Chonjo chini ya usimamizi wa  Afisa wa Takukuru wilaya ya Maswa,Greyson Chogo katika ghala la kuuzia zao hilo lililoko maeneo ya misheni katika kijiji hicho.

Walisema kuwa wao wanalima kilimo hai cha zao hilo chini ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikiwawezesha pembejeo kwa masharti ya kuwauzia pamba lakini walifanyiwa vitendo vya hujuma na kudhulumiwa pesa zao.

Walisema kuwa licha ya kufuata maelekezo ya serikali kuwa fedha zao watalipwa kupitia akaunti zao za benki au simu lakini walichobaini namba za simu zilizoandikwa hazikuwa zao bali ni za mhasibu huyo aliyekuwa akinunua pamba katika kituo hicho.

"Tulielezwa kwa musimu huu hakuna mkulima atakayelipwa pesa taslimu atakapouza pamba yake hivyo tulio wengi tuliandika namba za simu ili pesa iingie huko lakini cha kushangaza tulipoona muda mrefu umepita tuliona tufuatilie tuone malipo yetu yameishia wapi tukagundua mhasibu aliweka namba zake za simu na pesa zetu zikaingia kwake,"alisema Njile Waziri.

Waliendelea kueleza kuwa baada ya kubaini hali hiyo walitoa taarifa kwa uongozi wa serikali ya kijiji na baadaye walikwenda kutoa taarifa kwa taasisi hiyo na ndipo walipolifanyia kazi na hatimaye wameweza kupata fedha zao kwani awali walikuwa wamekata tamaa kuziipata.

“Niipongeze Takukuru katika wilaya yetu ya Maswa kwa kufanikisha kuipata fedha yetu ambayo tulifanyiwa mchezo mchafu na huyu mhasibu kwa kufanikisha  kuokoa pesa zetu ambazo tulishakata tamaa kuzipata lakini wamepambana hadi leo hii tumekabidhiwa,” alisema Peter Jinasa.

Naye Afisa wa Takukuru,Greyson aliyeshuhudia wakulima hao wakipokea fedha hizo alisema kuwa ni vizuri makampuni hayo ya ununuzi wa mazao ya wakulima wakaajili wafanyakazi ambao ni waaminifu sambamba na kuwafanyia ukaguzi wa mara kwa mara ili kuepusha wakulima kupoteza haki zao baada ya kuuza mazao yao.

"Takukuru tulipopata malalamiko haya ya wakulima wapatao 10 na tuliamua kuyafanyia kazi haraka ili kuhakikisha wakulima wanalipwa fedha zao hivyo ni vizuri haya makampuni yakatoa ajira kwa wafanyakazi waaminifu na wafanyiwe ukaguzi wa mara kwa mara ili kuondoa matatizo kama haya,"alisema.

MWISHO.


Share:

BABU JOHA AKAMATWA NA TAKUKURU

Na Mwandishi wetu, Babati 
MMILIKI wa kampuni ya JACO Service Group John Stepheni Kabelinde maarufu kama Babu Joha ambaye ni mkazi wa jiji la Dar es salaam anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kuwasilisha nyaraka za upotoshaji na kujipatia zabuni. 

Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza mjini Babati September 3 mwaka huu amesema Kabelinde anadaiwa kutoa nyaraka hizo na kufanikiwa kupata zabuni ya kufyeka majani yaliyo pembeni ya barabara ya Babati hadi Gehandu. 

Makungu amesema Babu Joha alifanikiwa kupata zabuni hiyo kupitia nyaraka za upotoshaji baada ya kuwashinda wazabuni wengine tisa walioomba nafasi hiyo. 

Amesema uchunguzi unaonyesha kupitia kampuni yake ya JACO Service Group amekuwa akikwepa kodi mbalimbali za serikali hivyo kuangukia kwenye makosa ya kuhujumu uchumi wa Taifa na anatarajia kufikishwa mahakamani September 4.

Ametumia nafasi hiyo kuvishukuru vyombo vya habari amabayo vimesambaza habari hizo hadi kufanikisha ukamatwaji wa Babu Joha ambaye amekamatwa jijini Dar es salaam. 

Awali, Julai 9 mwaka huu Makungu aliwaambia waandishi wa habari kuwa Babu Joha anatafutwa na TAKUKURU kwa kudaiwa kufanya kosa hilo hadi hivi sasa ametiwa mbaroni na kusubiri kufikishwa mahakamani. 

"Napenda kuwafahamisha watuhumiwa wa uhalifu kuwa serikali ina mikono mirefu hivyo kujificha hakuwezi kuwa suluhisho kwa wanaotafutwa," amesema Makungu. 
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu akizungumza mjini Babati na waandishi wa habari.


Share:

Katibu Mkuu Wa Mambo Ya Nje Afanya Mazungumzo Na Mratibu Mkazi Wa Umoja Wa Mataifa Nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Generali Wilbert A. Ibuge akizungumza na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini,
Bw. Zlatan Milišić alipomtembelea Ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 2 Septemba 2020.

Katika mazungumzo yao walijadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa ambapo Balozi Ibuge alitoa shukrani kwa Shirika hilo kwa ushirikiano uliopo kati yake na Serikali hususan kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

Kwa upande wake, Bw. Milišić aliipongeza Tanzania kwa kudumisha amani na utulivu ambao ni chanzo cha uchumi wa nchi kustawi.

 Pia aliipongeza kwa kuendelea kuchangia vikosi vya ulinzi wa amani kwenye mataifa mbalimbali  yenye  migogoro duniani na kuitakia Tanzania uchaguzi wa amani na utulivu hapo mwezi Oktoba 2020.


Share:

Balozi Wa Tanzania Nchini Kenya Awasilisha Hati Za Utambulisho Kwa Rais Kenyatta

Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.

Hafla ya kuwasilisha hati za utambulisho imefanyika Ikulu jijini Nairobi ambapo pamoja na mambo mengine, Rais Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Balozi Simbachawene. 

Balozi Simbachawene amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa ataendelea kuboresha mahusiano ya nchi hizo mbili za Tanzania na Kenya, kukuza biashara baina ya nchi hizo kwa kuboresha diplomasia ya uchumi kwa ujumla wake.


Share:

OPERESHENI ZA TAKUKURU MKOANI SINGIDA ZAOKOA SHILINGI 199,559,254/= IKIWEMO MIKOPO UMIZA

Na Mary Mwakapenda, Manyoni
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imefanikiwa kuokoa kiasi cha Tsh. 199,559,254/= kufuatia operesheni mbalimbali zilizofanywa ili kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa mkoani humo katika kipindi cha kuanzia Julai 2019 hadi Juni 2020.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George H. Mkuchika wakati akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

 Mkuchika ameyataja baadhi ya maeneo ambayo operesheni hiyo iliyalenga kuwa ni pamoja na mikopo umiza ambapo kiasi cha Tsh. 58,150,000/= kiliokolewa, kwa upande wa mapato yatokanayo na usimamizi wa madini, kiasi cha Tsh. 44,623,254/= kiliokolewa, sanjari na hayo, kiliokolewa kiasi cha Tsh. 11,456,500/= kutokana na mapato ya usimamizi wa minada, na kiasi cha Tsh. 85,329,500/= kilirudishwa kutoka kwa wanachama wa vyama vya ushirika.

 Mkuchika amefafanua kuwa, jitihahada zote hizi zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na TAKUKURU zinatokana na weledi, ujasiri na uzalendo uliopo katika kushughulikia tatizo la rushwa nchini, hivyo ameitaka TAKUKURU kuendelea na kasi hiyo ili kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi nchini.

Katika eneo la utoaji elimu dhidi ya vitendo vya rushwa, Mhe. Mkuchika ameanisha kuwa, TAKUKURU imefanikiwa kufungua na kuimarisha klabu 234 za Wapinga Rushwa mashuleni na vyuoni na kutoa semina pamoja na mikutano ya hadhara 225.

Aidha, Mhe. Mkuchika amemuahidi Mhe. Ndugai kujenga Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Kongwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa tarehe 22 Julai, 2020 wakati akifungua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chamwino na kuongeza kuwa, hatua hii inadhirisha nia ya dhati ya Serikali ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini.

Jengo la Ofisi ya TAKUKURU la Wilaya ya Manyoni ni mojawapo ya majengo saba ambayo Mhe. Rais Magufuli alitakiwa kuyafungua kwa pamoja tarehe 22 Julai, 2020 wakati akifungua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Chamwino, Dodoma. Hata hivyo, aliweka utaratibu wa kuyafungua kwa nyakati tofauti na kumuelekeza Mhe. Ndugai kulifungua jengo hilo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika akitoa maelezo kuhusu jengo la TAKUKURU Wilaya ya Manyoni kabla ya kumkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuzungumza na wananchi na kulizindua jengo hilo.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuzungumza na wananchi kabla ya kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wananchi wilayani Manyoni jana kabla ya kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akisoma kibao cha ufunguzi wa jengo baada ya kuzindua jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana. Wanaoshuhudia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Bibi Rahabu Magwisa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) George Mkuchika akiipongeza Klabu ya Wapinga Rushwa ya Shule ya Sekondari ya Mlewa Wilayani Manyoni wakati wakiimba wimbo wa mapambano dhidi ya rushwa kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo la Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana.


Share:

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KENYA AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS KENYATTA

RAIS wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. John Stephen Simbachawene.

Hafla ya kuwasilisha hati za utambulisho imefanyika Ikulu jijini Nairobi ambapo pamoja na mambo mengine, Rais Kenyatta amepokea hati za utambulisho za Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Balozi Simbachawene. 

Balozi Simbachawene amemhakikishia Rais Kenyatta kuwa ataendelea kuboresha mahusiano ya nchi hizo mbili za Tanzania na Kenya, kukuza biashara baina ya nchi hizo kwa kuboresha diplomasia ya uchumi kwa ujumla wake.
 Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiwa tayari kupokea hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Stephen Simbachawene.


Share:

MGOMBEA URAIS WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI UWANJA WA KAMBARAGE KWA AJILI YA MKUTANO WA KAMPENI ZA URAIS

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kwa ajili ya Mkutano wa Kampeni za Urais leo tarehe 03 Septemba 2020.



Share:

YANGA YABADILI KAMBI, ICHEKI KAMBI YAO MPYA KAMA ULAYA

Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

Hii sasa sifa!!! Kutokea Mikocheni hadi Kimbiji, kikosi cha timu ya Yanga kwa sasa wanatarajiwa kuhamia Kimbiji katika kambi mpya wakitokea Mikocheni.

Hatua hiyo inakuja baada ya mdhamini wao GSM kuamua kuwabadilishia kambi na kuwapeleka nje ya mji ili kupata muda zaidi wa kujifua na Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kambi hiyo mpya ya Yanga ina mahitaji yote ikiwemo Uwanja wa mazoezi wa mpira wa miguu, Kikapu na michezo mingine.

Mabadiliko hayo yanafanyika muda mfupi kabla ya kuanza kwa Ligi msimu 2020/21 siku ya Jumapili wakitokea katika kilele cha siku ya Mwananchi.

Yanga ilifanya kilele cha siku ya Mwananchi siku ya Jumapili Agosti 30, na kuweka historia ya kujaza uwanja pamoja na kuwa tamasha lililovutia na kufana likonogeshwa na Msanii Harmonize huku wakicheza Mchezo wa Kirafiki dhidhi Agle Noir.




Share:
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

Popular Posts

Unordered List

Pages

Blog Archive


Copyright © MASWAYETU BLOG | Powered by Blogger